Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiwatambulisha [600807]
1
2
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiwatambulisha
kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mgo mbea wa CCM wa Urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu John Pombe Magufuli (kushoto) na
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamh uri ya Muungano wa Tanzania Ndugu
Samia Suluh Hassan (kulia) watakopeperusha bendera ya CCM katika
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2015.
3
ILANI YA CCM KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015
Utangulizi
1. Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili y a Uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2015 wa ku wachagua Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, Wabunge, Wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi na Madiwani imeandaliwa ikiwa ni mk ataba kati ya CCM na
wananchi. Ilani hii imeandikwa kwa kuzingatia Dira ya Maendeleo ya
Taifa ya 2025 na Mwelekeo wa Sera za CCM zenye lengo na nia ya
kuendelea kuwatumikia wananchi kwa kipindi cha miaka mitano ijayo
(2015 -2020).
2. Ilani hii ni tamko maalum u kwa wapiga kura kuhusu nia ya CCM ya
kuendelea kushika dola na kuwaongoza Watanzania kwa njia ya
kidemokrasia, na hasa kuendelea kudumisha amani, umoja wa Kitaifa,
usawa, ustawi wa wananchi, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
3. Nia na uwezo wa CCM wa kuendelea kuongoza Taifa hili unajidhihirisha
katika uzoefu ambao tumeupata kwa miaka 38 tangu kuanzishwa kwake
na kuwa madarakani, ambapo katika kipindi chote hiki kimeiwezesha
nchi yetu kupata mafanikio makubwa katika nyanja za kiuchumi, kisiasa
na kijamii.
4. Katika miaka mitano ijayo (2015 -2020) , CCM ikiwa madarakani ,
itazielekeza Serikali zake kutumia nguvu zake zote kuendelea
kupambana na changamoto kubwa nne :- Kwanza kuondoa umaskini ;
pili kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana ; tatu
kuendeleza vit a dhidi ya adui rushw a na ubadhirifu wa mali ya umma ;
na nne kuendelea kudumisha amani, ulinzi na usalama wa maisha ya
wananchi na mali zao.
Kupambana na Umas ikini
5. Pamoja na mafanikio ya kukua kwa uchumi na ongezeko la huduma za
kijamii yaliyopatikana kat ika kipindi hiki, bado ipo changamoto kubwa ya
umas ikini wa kipato na usio wa kipato . Takwimu zinaonesha kwamba
asilimia 28.2 ya Watanzania ni mas ikini. Wengi wa wananchi hao
wanaishi vijijini (asilimia 75) na wanategemea kilimo katika maisha yao.
4
Wapo pia wananchi mas ikini wanaoishi mijini ambao wanaendesha
maisha yao kupitia shughuli za biashara ndogo ndogo zisizo rasmi.
6. Katika kupambana na changamoto hii, CCM ita zielekeza Serikali zake
kuboresha maisha ya wananchi wote na hususan wa vijijini , kwa
kuchuku a hatua zifuatazo: –
(a) Kuhamasisha kilimo kupitia kauli mbiu ya Kilimo Kwanza kwa
kuwawezesha wakulima kupata mafunzo ya kilimo cha kisasa,
pembejeo, zana za kisasa na wataalam u wa ugani pamoja na
mbinu za kuyafikia masoko ya uhakika ya mazao yao ;
(b) Kuongeza ka si ya kupima ardhi yao na kuwapatia hati miliki za
kimila ambazo wata zitumia kama dhamana ya kuwawezesha
kupata mikopo ya kuendeleza s hughuli zao za kilimo , ufugaji na
uvuvi;
(c) Kuendeleza juhudi za kuimarisha huduma za ki jamii ikiwemo
elimu, afya, maji , ume me na ujenzi wa nyu mba bora ; na
(d) Kuongeza kasi ya kurasimisha biashara na kuwapatia
wafanyabiashara wadogo maeneo ya kufany ia biashara , leseni na
fursa za kupata mikopo yenye masharti nafuu.
7. Mafanikio ya utekelezaji wa mas uala haya yote kwa pamoja
yanatara jiwa kuleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo mijini na
vijinini , na hivyo kupunguza kwa kiwango kikubwa hali ya umasiki ni
nchini.
Ajira kwa Vijana
8. Suala la ukosefu wa ajira kwa vijana ni moja ya changamoto
zinazolikabili Taifa letu na dunia yote kwa ujuml a. Katika kipindi cha
miaka mitano iliyopita yapo mafanikio yaliyop atikana katika kuongeza
ajira. Hata hivyo , mafanikio katika upanuzi wa elimu ya Sekondari na
Vyuo yameongeza mahitaji ya ajira ya vijana wasomi kila mwaka
ikilinganishwa na nafasi zinazokuw epo.
9. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo jitihada za ku lipatia ufumbuzi
tatizo la ajira nchini zitaendelezwa . Kipaumbele kitakuwa katika kukuza
na kuanzisha viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vilivyo na uwezo wa
kuajiri watu wengi na vyenye kuzalisha bi dhaa zinazotumiwa na watu
wengi wa ndani ya nchi na zile za kuuza nchi za nje. Aidha, kwa upande
5
wa Tanzania Zanzibar, mikakati ya kuongeza ajira kwa vijana itazingatia
mazingira maalamu ya fursa za uchumi wa visiwa.
10. Katika kipindi cha 2015 -2020, sekta za uzalishaji mali kama kilimo,
ufugaji, uvuvi, viwanda vikubwa na vidogo na huduma za kiuchumi
kama vile miundombinu ya nishati, uchukuzi na ujenzi zitaelekeza
mipango yao katika kupunguza umas ikini na ku anzisha ajira hususan
kwa vijana. Aidha, huduma za ja mii za elimu, afya na maji zitajielekeza
kusaidia kuondoa umas ikini na kuongeza ajira.
Vita dhidi ya Rushwa
11. Jitihada za kuinua uchumi na kuongeza huduma za jamii hazitaleta
manufaa kwa wananchi na kuondoa umas ikini iwapo adui rushwa
ataendelea kulitafuna T aifa letu. Rushwa ni adui wa haki pia ni adui wa
maendeleo na ustawi wa wananchi, hivyo ni moja ya changamoto
kubwa inayoikabili nchi yetu na dunia kwa ujumla.
12. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, CCM itazielekeza Serikali zake
kuendeleza mapambano dhidi ya adui rushwa kwa nguvu zake zote na
kuendelea kuziba mianya ya rushwa katika taasisi za umma ; kuchukua
hatua kali na za haraka kwa wale wote watakaobainika kuendeleza
rushwa Serikalini na katika sekta binafsi ; na kuimarisha vyombo na
taasisi zinazohusi ka na kuzuia na kupambana na rushwa ; ikiwa ni
pamoja na kuanzisha Mahakama Maalum u kwa ajili ya makosa ya
rushwa na uhujumu uchumi .
13. Sambamba na kupambana na tatizo la rushwa, Serikali pia zitatakiwa
kushughulikia kwa ukali zaidi tatizo la ubadhirifu na w izi wa mali ya
umma, matumizi mabaya ya madaraka, ukiukwaji wa maadili ya uongozi
na utumishi wa umma, kuchelewesha kutoa maamuzi yenye maslahi
kwa umma na kusimamia uwajibikaji katika kutekeleza masuala yenye
maslahi kwa umma.
Ulinzi na Usalama
14. Nchi yetu imepata mafanikio makubwa ya kuwa na amani na utulivu
tangu tupate uhuru mwaka 1961 na Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka
1964. Imekuwa kimbilio la wat u wa Mataifa ya jirani kila wa patapo
matatizo ya uvunjifu wa amani katika nchi zao. Hata hivyo , siku za
karibuni vimeanza kuonekana viashiria vinavyoleta hofu ya usalama wa
6
wananchi, hasa vitendo vya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi
(Albino), kuuawa kwa vikongwe, ukatili dhidi ya wanawake na watoto
na tishio la vitendo vy enye mwelekeo wa ki gaidi.
15. Katika kip indi cha miaka mitano ijayo, CCM ita zielekeza Serikali zake
kuendelea kuimarisha vyombo vyote vya ulinzi na usalama kwa
kuviongez ea raslimali fedha, raslimali watu, maslahi, zana za kisasa na
mafunzo. Aidha, elimu kwa umma itatolewa ili kukomesha imani po tofu
za kishirikina zinazosababisha mauaji ya albino na vikongwe na hatua
kali za kisheria zitachuku liwa dhidi ya wale wote watakaobainika
kujihusisha na vitendo vya mauaji ya makundi hay o.
Utekelezaji wa Ilani
16. Kazi kubwa ya Serikali z a CCM katika kipindi cha miaka mitano ijayo
itakuwa ni kuendele za mapambano dhidi ya uma sikini, ukosefu wa ajira,
rushwa; na kudumisha umoja, amani, ulinzi na usalama . Ili kutimiza
azma hiyo, CCM ita zielekeza Serikali zake zisiwe kubwa , zenye
watumishi weledi, waadilifu na wa wajibikaji . Serikali zisizo na urasimu
unaokwamisha na kuchelewesha maamuzi na utekelezaji . Serikali
zitakazongeza maradufu au hata zaidi ukusanya ji wa mapato ya ke ili
zijitegemee kadri inavyowezekana kwenye bajeti zake.
17. Vile vile katika kipindi cha Il ani hii, Chama Cha Mapinduzi ki taziagiza
Serikali zake kuendeleza na kuimarisha mfu mo wa Matokeo Makubwa
Sasa (BRN na BRP ) katika kutekeleza Ilani na kusimamia utekelezaji wa
miradi ya kimkakati na kipaumbele unaozingatia nidhamu ya utekelezaji
katika muda ul iopangwa, ufuatiliaji makini na wa kina, pamoja na
kupata ufumbuzi wa vikwazo na changamoto za utekelezaji.
7
SURA YA KWANZA
HALI YA UCHUMI – MWAKA 2010 – 2015
NA MALENGO YA MWAKA 2015 – 2020
18. Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 –2015, ililenga kati ka
kutekeleza kipindi cha kwanza cha Mwelekeo wa Sera za CCM katika
miaka ya 2010 –2020 na kutekelezwa katika kipindi cha pili na cha
mwisho cha Serikali ya Awamu ya Nne chini ya uongozi wa Mhe. Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tan zania.
Katika kipindi hiki, Serikali imetekeleza kwa mafanikio makubwa
Mwelekeo wa Sera za CCM katika miaka ya 2010 –2020 kwa kuzingatia
Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na Malengo ya Milenia. Aidha,
kutokana na mafanikio hayo, Serikali imeweza kuendeleza na
kuimarisha huduma za kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Hali ya Uchumi
19. Katika kipindi hiki, Serikali imeweza kutekeleza mipango yake kwa
ufanisi mkubwa licha ya changamoto zilizokuwa zikijitokeza na kuleta
mafanikio ya kiuchumi yafuatayo: –
(a) Ukuaji wa Pato la Taifa kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita,
umekua kwa wastani wa asilimia 7 kwa mwaka ;
(b) Ukusanyaji wa mapato ya ndani umeongezeka kutoka wastani wa
Shilingi bilioni 390 kwa mwezi mwaka 2010 na kufikia wastani wa
Shilingi bilioni 850 kwa mwezi , mwaka 201 4/15;
(c) Misaada na mikopo ya Washirika wa Maendeleo kwenye bajeti ya
Serikali imepungua kutoka asilimia 42 mwaka 2005 hadi asilimia 8
mwaka 2015 /2016;
(d) Mapato ya kodi yameongezeka kutoka Shilingi trilioni 5.74 mwaka
2010/11 na kufikia shilingi trilioni 7.42 mwaka 2014/ 15;
(e) Mfumko wa bei umeendelea kubakia tarakimu moja (single digit)
na umepungua kutoka wastani wa asilimia 19.8 Desemba, 2011
hadi kufikia asilimia 4.8 Desemba, 2014 na asilimia 4.3 Machi,
2015.
8
(f) Bajeti ya Serikali imeongezeka kutoka Shilingi tri lioni 4.18 mwaka
2010/2011 hadi Shilingi trilioni 2 2.49 mwaka 2015/2016 ; na
(g) Wastani wa p ato kwa kila mwananchi limeongezeka kutoka
Shilingi 770,000 mwaka 2010 hadi wastani wa S hilingi 1,675,232
mwaka 2014.
20. Sekta ya Fedha ndi o kipimo kinachoweza kuonesha viwango
vya uchumi wa nchi vilivyofikiwa katika vigezo mbalimbali
kama vile Pato la Taifa, Ukuaji wa Uchumi na Mfumko wa Bei.
Maendeleo ya haraka katika nyanja hizo ya tategemea uimara
na uwezeshaji wa sekta ya fedha.
Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilan i hii 2015 -2020, Chama
Cha Mapinduzi kitaielekeza Serikali kutekeleza yafuatayo na
kuhakikisha kwamba: –
(a) Uchumi unaendelea kukua kwa kasi ya wastani wa asilimia 8 au
zaidi na kuinua ustawi wa Watanzania kwa kuongeza mapato ya
wananchi kufikia kiwango cha wa stani wa nchi ya uchumi wa kati
na hivyo , kuongeza fursa za ajira na kupunguza umas ikini; na
(b) Kunakuwepo utulivu wa uchumi jumla ambao ni endelevu
(sustainable macroeconomic stability) kwa kufanya yafuatayo: –
(i) Kudhibiti mfum ko wa bei ili uendelee kubaki kwen ye
tarakimu moja na hivyo kuzuia kasi ya kupanda kwa
gharama za maisha ;
(ii) Kudhibiti nakisi ya bajeti ili iendelee kushuka na kufikia
kiwango kisichozidi asilimia 3 ya Pato la Taifa ili pamoja
na mambo mengine, Tanzani a iendelee kuwa kivutio
kwa wawekezaji na kupunguza gharama za kukopa kwa
ajili ya maendeleo ya nchi yetu ;
(iii) Kusimamia Deni la Taifa liendelee kuwa himilivu ili
lisiwe mzigo kwa uchumi wetu bali liendelee kuwa fursa
na kichocheo cha maendeleo ya nchi yetu ;
9
(iv) Kuhakikisha thamani ya S hilingi yetu inate ngamaa ili
kujenga imani ya uchumi wetu kwa lengo la kuongeza
shughuli za uwekezaji, uzalishaji na bia shara;
(v) Kuongeza mauzo ya bidhaa zetu nje ya nchi, kudhibiti
matumizi ya fedha za kigeni na kuepuka kuagiza bidhaa
zisizo za lazima kutoka nje ya nchi ; na
(vi) Kuendelea kuwa na mikakati itakayowezesha kuwa na
akiba ya fedha za kigeni zinazotosheleza kuagiza bidhaa
na huduma nje bila ya matatizo.
(c) Kuimarisha ukusanyaji wa mapato kwa kuongeza vyanzo vipya
vya mapato na kupanua wigo wa walipa kodi ili kuongeza
uwezo wa Serikali wa kugharimia huduma za kijamii na
kiuchumi ;
(d) Kusimamia kwa ufanisi matumizi ya fedha za umma kwa
kuzingatia sheria na miongozo ya ununuzi wa umma, ukaguzi
na kusimamia mali za Serikali ili Watanzania wote wanufaike na
rasilimali zilizopo ; na
(e) Kuimarisha Sekta ya Fedha kwa kuhakikisha wananchi
wananufaika kwa kufanya yafuatayo: –
(i) Kuendelea kupanua huduma za fedha hadi vijijini kwa
lengo la kuwafikia wananchi wengi ;
(ii) Kuhamasisha wananchi wajiunge na huduma za B ima
ya Afya, Bima ya Maisha na Mifuko y a Hifadhi za Jamii
ili kujihakikishia kinga dhidi ya majanga na maisha ya
uzeeni na baada ya kustaafu ; na
(iii) Kuweka mazingira yatakayowezesha kushuka kwa riba
ya mi kopo katika Taasisi za F edha ili kutoa fursa kwa
wananchi kupata mikopo ya muda mfupi na mrefu kwa
riba nafuu.
(f) Kutekeleza Sera na Sheria za kusimamia mapato yanayotokana
na gesi asilia na mafuta ili kuhakikisha fedha zinatumika kwa
manufaa ya Wananchi wa kizazi hiki na kijacho ;
(g) Kuwawezesha wananchi kumiliki na kuwekeza kwenye soko la
mitaji na dham ana kwa: –
10
(i) Kuongeza ufanisi wa shughuli za minada kwa njia ya
simu na mtandao wa intaneti;
(ii) Kuelimisha umma kuhus u fursa za kujiongezea kipato
kupitia masoko ya mitaji na uwekezaji; na
(iii) Kuendelea kutoa fursa kwa wajasiriamali wadogo na
wa kati ili waweze kunu faika na Soko la Hisa la Dar es
Salaam (DSE) kupitia dirisha maalum u la kukuza na
kuimarisha masoko ya wajasiriamali wadogo na wa
kati.
(h) Kuboresha mfumo wa kifedha kati ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar ( SMZ) kwa manufaa ya pande zote mbili za
Muungano kwa kutekeleza yafuatayo: –
(i) Kuimarisha asasi zinazohusika na masuala ya
uhusiano wa kifedha kati ya SMT na SMZ ;
(ii) Kukamilisha hatua za kuanzisha Akaunti ya Fedha
ya pamoja ili kuzidi kuimarisha mshikamano na
maelewano ; na
(iii) Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuweka
utaratibu wa kuoanisha viwango vya kodi ya
forodha kati ya pande mbili za Jamhuri ya
Muungano.
11
SURA YA PILI
MAFANIKIO NA MALENGO YA SEKTA ZA UZALISHAJI
Kilimo na Ushirika
21. Katika kipindi cha miaka mi tano iliyopita, Chama Cha Mapinduzi kiliweka
kipaumbele cha kuhakikisha kuwa kilimo nchini kinakuwa endelevu na
chenye tija ili kuliwezesha Taifa kujitosheleza kwa chakula; kuongeza
mapato ya wakulima; kuwa chanzo cha kuaminika cha malighafi ya
sekta ya vi wanda; na kuendelea kuwa chanzo kikuu cha ajira kwa
wananchi. Kwa kutekeleza azma hiyo, mafanikio yafuatayo
yamepatikana: –
(a) Bajeti ya S ekta ya kilimo imeongezeka kutoka Shilingi bi lioni 903.8
mwaka 2010/11 hadi S hilingi trilioni 1.08 mwaka 2014/15 ;
(b) Dirisha la kilimo limeanzishwa k atika B enki ya Rasilimali (TIB) kwa
lengo la kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wakulima ili
waweze k ununu a pembejeo na zana za kilimo . Aidha,
imeanzishwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo mahususi kwa ajili ya
kutoa mikopo kwa wakuli ma;
(c) Katika kuimarisha huduma za ugani, udahili katika vyuo vya kilimo
umeongez eka kutoka wanafunzi 1,246 mwaka 2010/11 hadi 2,5 00
mwaka 2013/14. Aidha, idadi ya maafisa ugani katika ngazi ya
Vijiji na Kata imeongezeka kutoka 5,184 mwaka 2010/11 hadi
9,558 mwaka 2013/14 ;
(d) Uzalishaji na usambazaji wa pembejeo bora za kilimo
umeimarishwa ambapo: –
(i) Uzalishaji wa mbegu bora umeongezeka kutoka tani
10,477.17 mwaka 2005 hadi tani 32,340 mwaka 20 14;
usambazaji umeongezeka kutoka tani 16,148.2 mwaka
2009/2010 hadi tan i 35,352 mwaka 2013/14 ; na
(ii) Usambazaji wa mbolea umeongezeka kutoka tani 302,200
mwaka 2009/2010 hadi tani 343,687 mwaka 2013/14.
(e) Matumizi ya matrekta madogo na makubwa yameongezeka
kutoka 11,223 mwaka 2010/11 hadi 16,412 mwaka 2013/14.
12
Ongezeko hili limech angia kuongozeka kwa eneo linalolimwa kwa
matrekta kutoka asilimia 12 mwaka 2010/11 hadi asilimia 14
mwaka 2013/14 ;
(f) Ruzuku ya mbolea na pembejeo imeongezeka kutoka Shilingi
bilioni 7.5 mwaka 2005/06 hadi Sh ilingi bilioni 299.3 mwaka 2014;
(g) Kiwango cha uzali shaji wa mazao ya chakula kimeendelea
kuongezeka kutoka tani milioni 12.83 mwaka 20 09/10 hadi tani
milioni 16.01 mwaka 20 14/15. Kwa ongezeko hilo Taifa lim eweza
kujitosheleza kwa chakula;
(h) Katika juhudi za kuhifadhi mazao kwa ubora unaostahili, jumla ya
maghala 30 yenye uwezo wa kuhifadhi kati ya tani 5,000 hadi
10,000 yamekarabatiwa. Aidha, ujenzi wa ghala lenye uwezo wa
kuhifadhi tani 5,000 umekamilika katika Wilaya ya Songea mwaka
2013/14 chini ya mpango wa SAGCOT ;
(i) Hatua za kuongeza thamani ya mazao ya k ilimo cha mboga
mboga na matunda zimechukuliwa kwa kujenga Maeneo ya
Hifadhi ya Mazao (Packhouse and refeer container) katika Wilaya
za Lushoto na Korogwe. Aidha, mashine za kusindika na kusafisha
mafuta ya alizeti zimesambazwa kwa vikundi vya wazalishaji na
wasindikaji wadogo katika mikoa inayolima alizeti nchini ;
(j) Mchakato wa k uanzish a Soko la Bidhaa (Commodity Exchange)
umeanza na imetungwa Sheria Na. 15 ya Mwaka 2015 . Soko hilo
litamwezesha mkulima kuwa na uhakika wa kuuza mazao yake na
kupata bei nzuri;
(k) Hatua za kuimarisha soko la nafaka zimechukuliwa kwa kuondoa
zuio la kuuza nafaka nje ya nchi; kuwezesha Wakala wa Taifa wa
Chakula kununua nafaka kutoka kwa wakulima kwa bei ya soko;
na kutafuta masoko ya ndani na nje ya nchi ;
(l) Hatua za kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa lengo
la kuondoa migogoro katika maeneo mbalimbali nchini
zimeendelea kuchukuliwa kwa kupima na kutoa ha ti miliki kwa
wakulima vijijini ; na kwa wawekezaji wakubwa na wadogo.
Jitihada hizo zimewezesha upimaji wa jumla ya ekari 44 4,663.2 za
mashamba ya wakulima ;
13
(m) Kilimo cha umwagiliaji kimepewa kipaumbele kwa kupanua eneo
la umwagiliaji ambapo Sheria ya Umwagiliaji Na. 5 ya mwaka
2013 imetungwa na kua nzisha Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.
Aidha, kutokana na utekeleza ji wa Sera na Mikakati mbalimbali,
kilimo cha umwagiliaji kimechangia asilimia 24 ya mahitaji ya
chakula nchini ; na
(n) Kwa muda mrefu Sekta ya U shirika ilikabiliwa na changamoto
kadhaa ambazo zilidumaza jitihada za kuendeleza ushirika. Ili
kuondokana na chan gamoto hizo, Sheria ya Vyama vya Ushirika
ilifanyiwa mabadiliko na kuanzisha Sheria mpya (Sheria Na. 6 ya
mwaka 2013) ambayo imeanzisha Tume Huru ya Maendeleo ya
Ushirika.
Kilimo cha Umwagiliaji kinachotumia zana bora kitaongeza tija kwa wakulima
ambao n dio wengi nchini.
22. Katika kipindi cha mwaka 2015 – 2020, Chama Cha Mapinduzi
kitaielekeza Serikali kut ilia mkazo utekelezaji wa Awamu ya
Pili ya Programu ya Kuendeleza Kilimo (Agricultural Sector
14
Development Programme – ASDP II) pamoja na miradi ya
Tekelez a kwa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ili kufikia
malengo makuu ya kukifanya kilimo kuwa cha kisasa na cha
kibiashara; chenye tija na ambacho mazao yake yatakuwa
yameongezewa thamani. Lengo ni kuhakikisha kuwa Taifa
linajitosheleza kwa chakula; kuimarisha uchum i; kuongeza
kipato cha wakulima; kuwa kichocheo cha kukua kwa viwanda;
na kuongeza ajira kwa kufanya yafuatayo: –
(a) Kuimarisha upatikanaji wa pembejeo na zana za kilimo ili
kuongeza tija na uzalishaji kwa kuzingatia matumizi ya teknolojia
ya kisasa hususan k atika kuboresha mifumo ya utoaji wa ruzuku
na pembejeo pamoja na ku waunganisha wakulima na Benki ya
Maendeleo ya Kilimo na taasisi nyingine za fedha ;
(b) Kutoa elimu kwa wakulima juu ya kanuni bora za kilimo kwa
kuongeza idadi ya maafisa ugani kutoka 9,558 wa liopo sasa hadi
kufikia 1 5,082 mwaka 2020; na kuanzisha V ituo vya Mafunzo ya
Kilimo na Mifugo katika kila Kata nchini ; na
(c) Kuimarisha kilimo cha umwagiliaji ili kupunguza utegemezi wa
mvua kwa kuongeza eneo la umwagiliaji kutoka hekta 461,326
mwaka 2014 ha di 1,000,000 mwaka 2020. Ili kufanikisha hilo,
Serikali itafanya mambo yafuatayo: –
(i) Kwa kushirikiana na sekta binafsi, k uwekeza katika
miundombinu ya umwagiliaji kwa kujenga mifereji mikuu,
mifereji ya kati na kujenga mabwawa ya kuhifadhia maji
kwenye maene o yenye u kame ;
(ii) Kuhamasisha wakulima kupitia vyama vyao vya
umwagiliaji kuchangia katika ujenzi wa mifereji midogo ya
kuingiza maji mashambani na kushiriki katika kutunza
mifereji hiyo ;
(iii) Kuwafundisha kulima kwa tija na ufanisi kwa kutumia
miundombinu iliyopo ikiwa ni pamoja na kulima zaidi ya
mara moja kwa mwaka ;
(iv) Kukamilisha ujenzi wa skimu zote za umwagiliaji
zilizoanza kujengwa miaka ya nyuma ;
15
(v) Kujenga, kukarabati na kuboresha skimu za umwagiliaji
za wakulima wadogo na wa kati ili kuongeza uzalishaji na
ufanisi wa matumizi bora ya rasilimali maji ;
(vi) Kujenga na kuimarisha mabwawa ya uvunaji wa maji ya
mvua kwa aj ili ya umwagiliaji wa kilimo cha mpunga ;
(vii) Kushirikisha sekta binafsi katika uwekezaji na uendel ezaji
wa kilimo cha umwagiliaji; na
(viii) Kuijengea uwezo Tume y a Taifa ya Umwagiliaji ili iongeze
kasi ya ujenzi wa miundombinu.
(d) Kuboresha mfumo wa utafiti wa kilimo nchini ili matokeo ya tafiti
hizo yawafikie wakulima kwa kufanya yafuatayo: –
(i) Kugundua na kutathmini aina za mbegu bora za mazao
mbalimbali zenye sifa ya kutoa mavuno mengi,
zinazostahi mili mabadiliko ya tabianchi na zenye viinilishe
vingi;
(ii) Kuzalisha mbegu za mazao mbalimbali kwa kushirikiana na
taasisi za umma na binafsi ili kutosheleza mahitaji ya
uzalishaji wa mbegu bora nchini ;
(iii) Kutafiti magonjwa na visu mbufu vya mimea vinavyoathiri
mazao hasa migomba, mihogo, minazi, mahindi, mpunga,
mboga na matunda ili kuongeza tija na uzalishaji wa mazao
nchini ;
(iv) Kuchambua mifumo ya kilimo, kutoa teknolojia za
kurutubisha udongo na matumizi bora ya mbolea na
kuandaa ra mani za ikolojia kwa kila Kanda; na
(v) Kuboresha miundombinu ya utafiti na kuwa jengea uwezo
watafiti ili kuong eza ufanisi wa utafiti nchini.
(e) Kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi ya kilimo kwa
kuendelea kupima mashamba ya wakulima na kutoa hati miliki za
kimila kwa wakulima wadogo kwa lengo la kuondoa migogoro ya
ardhi na kutumia hati hizo kama dhamana ya kupata mikopo ; na
(f) Kuwawezesha wakulima hususan vijana na wanawake
kujishughulisha katika kilimo kwa kufanya yafuatayo: –
16
(i) Kuainisha na kupima maeneo ya ard hi ya kilimo ili
kuwawezesha wakulima kujiajiri katika sekta ya kilimo
hususan kilimo cha mazao ya mboga mboga, matunda,
maua , mbegu za mafuta na nafaka ;
(ii) Kuendelea k upima maeneo na kuyapatia hati miliki ili
kuwawezesha wakulima kushiriki katika kuyaendelez a
maeneo hayo kwa kutumia hati miliki kama dhamana ya
kupata mikopo kutoka katika taasisi za fedha ;
(iii) Kuwaunganisha wakulima (V ijana na wanawake ) na asasi
za fedha kwa ajili ya kupata mikopo ya pembejeo, zana
bora na mashine za usindikaji kupitia vyama vyao vya
ushirika na vikundi vya uzalishaji mali ; na
(iv) Kuimarisha matumizi ya teknolojia zitakazorahisisha kazi ili
kuwapunguzia harubu wanawake na vijana katika kilimo.
(g) Kuwezesha upatikanaji wa Masoko ya Mazao ya Kilimo kwa
kufanya yafuatayo: –
(i) Kushirikisha sekta binafsi kujenga miundombinu ya
masoko na maghala bora ya kuhifadhia mazao mbalimbali
hususan vijijini kwa kutoa elimu na kuondoa vikwazo vya
utaratibu wa Stakabadhi ya Mazao Ghalani ;
(ii) Kuanzisha Soko la Bidhaa kwa mujibu wa Sheria ya Soko la
Bidhaa (Commodi ty Exchange Act) Namba 15 ya mwaka
2015;
(iii) Kujenga masoko ya kimkakati katika maeneo ya mipaka ya
nchi ili kuwapa wakulima fursa ya kuuza mazao yao nje ya
nchi;
(iv) Kuviimarisha na k uviwezesha vyama vya ushirika kuwa na
uwezo wa kutafuta masoko ya mazao ya waku lima ya
ndani na nje kwa kuweka mfumo madhubuti wa
ukusanyaji, uchambuzi na uenezaji wa taarifa za masoko
na kutoa elimu juu ya uongezaji thamani na biashara .
(h) Kuhamasisha sekta binafsi na vyama vya ushirika wa mazao
kuanzisha viwanda vya kusindika mazao y a kilimo hususan
kwenye maeneo ya uzalishaji wa mazao hayo kwa lengo la
17
kuongeza thamani na kuongeza ajira. Aidha, kuwawezesha
wakulima kupata majokofu ili kuhifadhi matunda na mazao ya
mboga mboga yanayoharibika haraka pamoja na vifungashio.
Mifugo na Uvuvi
23. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Sekta ya Mifugo na Uvuvi
imeimarishwa ili kuwaongezea wafugaji na wavuvi kipato pamoja na
kuchangia ukuaji wa Pato la Taifa.
Mifugo
24. Katika kipindi hicho, Sekta ya Mifugo imepata mafanikio yafuatayo: –
(a) Masham ba m atano yenye uwezo wa kuzalisha mitamba 5,000
kwa mwaka yameanzishwa. Aidha, Kituo cha Uhamilishaji cha
NAIC kilichopo Arusha kimeimarishwa na kinazalisha mbegu bora
za mifugo. Vituo vipya vya Uhamilishaji vimeanzishwa katika
Mikoa ya Pwani, Dodoma, Mbe ya, Katavi, Lindi na Mwanza. Sekta
binafsi imezalisha mitamba 10,000 mwaka 2013/14 na
kusambazwa kwa wafugaji ;
(b) Ruzuku ya dawa za kuogesh ea mifugo imetolewa ambapo lita
252,138 za dawa zenye thamani ya Shilingi bilioni 4.2
zimenunuliwa na kusambazwa katika Mikoa yote nchini ;
(c) Ujenzi na ukarabati wa Vyuo vya Mifugo vya Mabuki, Kikulula na
Rorya umefanyika na kuwezesha mafunzo kwa wafugaji 2,000
pamoja na kutoa mafunzo kwa Maafisa Mifugo 2,000 katika ngazi
ya Astashahada na Stashahada ;
(d) Dozi milioni 7.1 za Chan jo ya Homa ya Mapafu ya Ng’ombe, dozi
900 za chanjo ya Homa ya Bonde la Ufa (RVF) na dozi milioni
12.8 za chanjo ya Sotoka zimenunuliwa na kusambazwa katika
mikoa mbalimbali nchini ;
(e) Kituo cha Uchunguzi wa Magonjwa ya Mifugo (ZVC)
kimefunguliwa huko Sumbawa nga kwa ajili ya kuhudumia Eneo
Huru la Magonjwa ; na
(f) Jumla ya wataalam u 900 wamesajiliwa ikiwa ni pamoja na kusajili
vituo vya kutolea huduma za mifugo. Aidha, leseni 290 za
18
Wakaguzi wa Nyama, Wahamilishaji na Watalaam u wa Maabara
za Mifugo zimetolewa.
Ufugaji bora wenye tija kwa wafugaji ambao pia hupunguza uharibifu
wa mazingira.
25. Katika kipindi cha Ilani hii ya 2015 -2020, Chama Cha
Mapinduzi kit aielekeza Serikali yake kuiendeleza Sekta ya
Mifugo kwa kuchukua hatua zifuatazo: –
(a) Kuongeza uzalishaji wa mitamba kwenye mashamba
inakozalishwa na kuweka mazingira wezeshi kwa Sekta Binafsi
kuendelea kuzalisha mitamba ili kuhamasisha ufugaji wa kisasa ;
(b) Kutenga, kupima na kumilikisha wafugaji maeneo ya ufugaji
nchini ili kuongeza maeneo ya ufugaji yaliyopimwa k utoka hekta
milioni 1.4 za sasa hadi hekta milioni 5.0 mwaka 2020 ;
19
(c) Kujenga miundombinu ya mifugo kwa kuongeza idadi ya
malambo kutoka 1,378 yaliyopo sasa hadi 2,000; na kujenga
mabw awa katika mikoa yenye mifugo mi ngi. Aidha, vitajengwa
visima virefu 300, majosho 50 na kuanzisha minada 164 ya
mifugo katika maeneo yote yatakayotengwa kwa ajili ya ufugaji
ili kuzuia kuhamahama kwa wafugaji kunakosababisha migogoro ;
(d) Kutoa dhamana kwa vikundi vya wafugaji ili kupata mikopo
kwenye asasi za fedha, hususan vija na na wanawake
watakaokuwa kwenye vyama vya ushirika vya ufugaji wa
ng’ombe, kuku, mbuzi na uzalishaji malisho pamoja na usindikaji
wa mazao ya mifugo (nyama, maziwa na ngozi) ;
(e) Kuanzisha mashamba darasa ya malisho katika kila Halmashauri
ya Wilaya ili wafugaji wa asili wajifunze jinsi ya kuboresha na
kuhifadhi malisho (feed banks) hususan wakati wa kiangazi na
ukame ;
(f) Kueneza ufugaji wa mifugo bora kupitia mikopo ya mifugo kwa
wafugaji watakaojiunga ka tika vikundi kupitia miradi ya kopa
ng’ombe/mbuzi lip a ng’ombe/mbuzi au kopa ng’ombe /mbuzi lipa
maziwa ;
(g) Kuendelea kutoa elimu kwa wafugaji wanaomiliki na
watakaomilikishwa ardhi ili kutumia hati zao kama dhamana ya
kupata mikopo kutoka asasi za fedha ;
(h) Kuendelea kutoa elimu kuhusu matumizi ya teknolojia ya
uhamilishaji katika kuboresha koosafu za mifugo nchini kwa
kutoa huduma za uhamilishaji kwa wafugaji kwa gharama nafuu
kupitia ruzuku itakayowekwa katika mbegu za uhamilishaji ;
(i) Kuboresha huduma za uhamilishaji kwa kuimarisha vituo vya
uhamilishaji vya Taifa vya NAIC – Usa River (Arusha) na Sao Hill
(Iringa); na vituo vya Kanda vya Kibaha (Mashariki), Lindi
(Kusini), Mbeya (Nyanda za Juu Kusini), Dodoma (Kati), Mwanza
(Ziwa) na Mpanda (Kusini Magharibi) ili kusogeza karibu huduma
ya uhamilishaji kwa wafugaj i na kujenga vituo vipya vya
uhamilishaji vya Kanda vya Tabora (Magharibi) na Tanga
(Mashariki) ;
20
(j) Kuendelea kukuza na kuendeleza masoko ya mifugo na mazao
yake yanayozalishwa na wafugaji na kujenga viwanda viwili (2)
vya ngozi katika mikoa ya Singida na Dod oma;
(k) Kuendelea kutoa ruzuku ya dawa za kuogesha mifugo kiasi cha
lita milioni 1.0 ili kuhakikisha kuwa majosho 2,428 yaliyopo
nchini yanatumika kudhibiti kupe na magonjwa wayaenezayo
hususan ugonjwa hatari wa Ndigana kali. Aidha, Serikali itatoa
ruzuku ya Chanjo ya Ndigana kali (ECF) na kushirikisha sekta
binafsi na wadau wengine kufufua majosho 150 na kujenga
majosho mapya 200 katika mikoa yenye mifugo mingi ;
(l) Kuendelea kununua na kutoa chanjo za magonjwa ya mlipuko
yanayoathiri afya ya mifugo na binadamu na kuwezesha biashara
ya mifugo katika soko la kimataifa, hususan Ugonjwa wa Homa
ya Mapafu ya Ng’ombe (CBPP), Homa ya Bonde la Ufa (RVF) na
Sotoka ya Mbuzi na Kondoo (PPR) ;
(m) Kuendelea kuimarisha eneo huru la magonjwa ya mifugo katika
Kanda ya Kusini Maghar ibi na kuanzisha vitalu huru vipya viwili
(2) vya magonjwa katika ranchi za Kongwa na Ruvu ili kukidhi
matakwa ya soko la kimataifa hivyo kuongeza ajira na Pato la
Taifa; na kuongeza thamani ya mifugo na mazao yake ;
(n) Kuendelea kuzalisha chanjo za magonjwa y a mifugo katika kituo
cha Uzalishaji wa chanjo cha Kibaha (Tanzania Vaccine
Institute) ;
(o) Kuimarisha huduma za ugani na mafunzo kwa kuongeza udahili
wa maafisa ugani kutoka 1,800 hadi 2,500 kwa mwaka katika
vyuo vinane (8) vya Serikali na kushirikisha vyuo 2 1 vya sekta
binafsi kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa maafisa ug ani
katika ngazi za vijiji na K ata ili kuimarisha huduma za mifugo ;
(p) Kuhamasisha sekta binafsi kuanzisha viwanda vya nyama na
mazao mengine yatokanayo na mifugo ikiwemo jibini na ngozi
hususan katika maeneo yenye mi fugo mingi ili kuongeza
thamani; na
(q) Kuitafutia ufumbuzi wa kudumu migogoro ya wakulima na
wafugaji.
21
Uvuvi
26. Kwa kuzingatia ukubwa wa maeneo na wingi wa rasilimali za uvuvi
tulizonazo, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, ya mepatikana
mafanikio yafuatayo: –
(a) Usimamizi wa rasilimali za uvuvi Tanzania Bara umeimarishwa
ambapo vituo 25 vya doria vimeanzishwa na kupewa zana za
kisasa kwa lengo la kudhibiti uvuvi haramu katika maeneo
mbalimbali nchini ;
(b) Vikundi vya usimamizi shirikis hi wa rasilimali za uvuvi 226
vimeanzishwa na kufanya idadi ya vikundi hivyo kufikia 749, kati
ya hivyo 511 vimesajiliwa na vinatekeleza majukumu yake kwa
kuzingatia sheria ndogo ya mipango kazi yake ;
(c) Ujenzi na uboreshaji wa mialo ya kisasa ya kupokelea m azao ya
uvuvi umetekelezwa katika Kanda ya Pwani ya Bahari ya Hindi
(3), Ziwa Tanganyika (4) na Ziwa Victoria (6). Aidha, mialo 19 ya
ukanda wa Ziwa Victoria imekarabatiwa ;
(d) Vituo vya kuzalisha vifaranga wa samaki wa maji baridi
vimeanzishwa katika Mikoa ya Lindi, Kigoma, Ruvuma, Tanga,
Pwani, Geita na Morogoro. Vituo hivyo kwa ujumla vina uwezo
wa kuzalisha vifaranga 10,000,000 kwa mwaka ;
(e) Sekta binafsi imeendelea kuhamasishwa kushiriki katika uvuvi
ikiwemo kuanzisha viwanda vya kuchakata samaki. Hadi sasa
kuna viwanda 48 vya kuchakata samaki na maghala 84 ya
kuhifadhi a mazao ya uvuvi ; na
(f) Jumla ya vikundi 208 vya Kuweka na Kukopa (VICOBA)
vimeanzishwa ambapo wananchi 5,573 wamenufaika na hivyo
kuwawe zesha kuendesha shughuli ndogo ndogo za uvuvi.
27. Katika kipin di cha Ilani hii ya 2015 –2020, Chama Cha
Mapinduzi kitaielekeza Serikali kuiendeleza Sekta ya Uvuvi kwa
kuchukua hatua zifuatazo: –
(a) Kuanzisha na kuimarisha vikundi na vyama vya ushirika vya
msingi vya wavuvi wadogo wadogo kwa lengo la kuwakopesh a
22
vifaa viki wemo zana za uvuvi katika maeneo ya mwambao wa
Bahari ya Hindi, maziwa na mito kwa kupunguza kodi na
kuviwezesha vikundi hivyo vikopesheke ;
(b) Serikali kwa kushirikiana na Sekta B inafsi na Vyama vya Ushirika
itanunua meli tano za uvuvi zenye uwezo wa kuvua sa maki
Bahari Kuu ambapo ajira zaidi ya 15,000 kwa mwaka
zitapatikana ;
(c) Kujenga bandari ya uvuvi katika ukanda wa Pwani ambayo
itawezesha meli zinazovua Bahari Kuu kutia nanga kwa lengo la
kuhaulisha samaki, kuuza samaki, kutoa takwimu sahihi na
huduma nyingi ne. Zaidi ya ajira 30,000 zita patikana na
kuongeza pato kwa jamii na Taifa ;
(d) Kuimarisha miundombinu ya uvuvi kwa kujenga mialo mitatu
(Ziwa Victoria), minne (Ziwa Tanganyika) na miwili (Ziwa
Nyasa) na hivyo kuongeza idadi ya mialo kutoka 39 hadi 48 na
kuimarisha masoko ya samaki ya Feri (Dar es Salaam), Kirumba
(Mwanza) na Muganza (Kagera) ili kuongeza thamani na ubora
wa samaki pamoja na kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi
kabla ya kumfikia mtumiaji ;
(e) Kuimarisha hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu 18 pamo ja na
kuanzisha maeneo mengine sita (6) na hifadhi katika maziwa
makuu, hususan Victoria, Tanganyika na Nyasa ili kuhakikisha
kuwa mazalia na makulia ya samaki yaliyoharibika
yanarejeshwa katika hali yake ya awali ;
(f) Kurejesha mazalia na makulia ya samaki ya liyoharibika
kutokana na mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mazingira
kwa kuweka matumbawe bandia na kupanda mikoko katika
bahari ;
(g) Kushirikiana na Mashirika ya Umma yenye dhamana ya uvuvi
nchini, k uwavutia wawekezaji kuanzisha viwanda vya kusindika
na kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi, vyombo na zana za
uvuvi;
(h) Kuboresha maeneo ya uvuvi kwa kutumia teknolojia rafiki ya
mazingira kwa kuweka vifaa vya kuvutia samaki (Fish
23
Aggregating Devices) baharini ili kuwawezesha wavuvi wadogo
kuyafikia maeneo yenye samaki wengi na hivyo kuongeza
upatikanaji wa samaki ;
(i) Kuimarisha huduma za ugani na mafunzo kwa kuongeza udahili
wa maafisa ugani wa uvuvi kutoka 1,200 hadi 2,500 kwa
mwaka na kuwezesha upatikanaji wa M aafisa Ugani katika
ngazi ya Kata ili kuimarisha h uduma za uvuvi na ufugaji wa
samaki ;
(j) Kuendeleza utafiti wa kurudishia samaki na kupandikiza samaki
ili kuongeza wingi katika maziwa, mito na mabwawa, hususan
Ziwa Victoria ;
(k) Kuanzisha na kuimarisha vikundi na vyama vya ushirika vya
wafugaji wa samaki kwa l engo la k ukuza ufugaji wa samaki
nchini;
(l) Kushirikiana na wadau wa ufugaji samaki ili kuongeza uzalishaji
wa samaki kwa kujenga mabwawa ya kufugia samaki na
kuongeza uzalishaji kutoka tani 10,000 hadi 50,000 kwa mwaka
na kupanua wigo wa ajira kwa vijana ;
(m) Kuwawezesha wakulima wa mwani, hususan vikundi vya akina
mama na vijana wa mwambao wa pwani katika kuongeza
uzalishaji kutoka tani 12,000 hadi tani 20,000 kwa mwaka,
uzalishaji wa chaza wa lulu, kaa, kamba na viumbe wengine wa
baharini kwa kuwapatia nyenzo na utaalamu ;
(n) Kuwawezesha wavuvi wadogo wadogo kupata vifaa vya uvuvi
kwa bei nafuu ;
(o) Kuhamasisha uchimbaji wa mabwawa na ufugaji wa samaki
katika maeneo yenye ukame kwa lengo la kuongeza lishe bora
pamoj a na kuongeza ajira kwa vijana; na
(p) Kuendelea kupamba na na uvuvi haramu ili uvuvi uwe endelevu
na wenye tija.
Utalii
28. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali imeendelea
kuhakikisha k wamba Sekta ya Utalii inaimarishwa na kuendelezwa kwa
24
kuwa ni moja ya sekta zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika Pato la
Taifa na ajira kwa wananchi. Katika kipindi hicho, mambo yafuatayo
yamefanyika: –
(a) Ujenzi wa Chuo Kipya cha Utalii , Kampasi ya Bustani
umekamilika mwaka 2011 na kuwezesha idadi ya udahili wa
wanafunzi kuongezeka kutoka 138 mwaka 2005 hadi wanafunzi
289 mwaka 2014. Ili kuongeza wataalam wa fani hii, Serikali
imeruhusu taasisi binafsi na wakala kutoa mafunzo ya utalii na
ukarimu katika ngazi ya Astashahada na Stashahada ;
(b) Tanzania imefanikiwa kuviingiza vivutio vya utalii kwenye soko la
Kimataifa ambavyo ni Mlima Kilimanjaro, Mbuga ya Serengeti na
Bonde la Hifadhi la Ngorongoro kuwa kati ya Maajabu Saba ya
Asili ya Afrika ( New Wonders of Africa ); na
(c) Makusanyo yatokanayo na shughuli za utalii yameongezeka
kutoka wastani wa Shilingi trilioni 2.98 mwaka 2012 /13 hadi
Shilingi trilioni 3.94 mwaka 2013/14.
29. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Chama Cha Mapinduzi
kitasimamia utekelezaji wa mikakati ya kukuza utalii nchini
kwa kuhakikisha kwamba, Serikali inatekeleza mambo
yafuatayo: –
(a) Kuongeza idadi ya watalii wanaoingia nchini kutoka 1,102,026
mwaka 2015 hadi 2,00 0,000 mwaka 2020 kwa kuwezesha Sekta
Binafsi kuwekeza katika huduma za miundombinu ya utalii
pamoja na kuendeleza Mkakati wa Kimataifa wa Utangazaji wa
Utalii ili kuwavutia watalii wengi zaidi ;
(b) Kuongez a msukumo katika utalii wa kihistoria kwa kuboresha
miundombinu kwenye maeneo ya malikale na kuyatangaza
maeneo hayo;
(c) Kuongeza bajeti ya Sekta ya Utalii ili kuutangaza utalii ndani na
nje ya nchi ;
(d) Kuimarisha mafunzo ya Hoteli na Utalii hususan katika ngazi ya
shahada ili kuongeza ubora wa watumishi wa huduma za
25
Ukarimu na Utalii kwa kukifanya Chuo cha Taifa cha Utalii kutoa
mafunzo ya ukufunzi ;
(e) Kuhamasisha wananchi kutembelea vivutio vya utalii wa ndani
na kuweka mazingira yatakayowezesha wawekezaji wa nda ni
kuendeleza biashara za utalii pamoja na kuwajengea uwezo
waongoza watalii ;
(f) Kufanya jitihada za kufungua fursa za utalii katika Kanda ya
Kusini pamoja na kutumia fukwe zake ;
(g) Kuendelea kujenga mazingira bora ya kuwawezesha vijana
kuanzisha kampuni za kute mbeza watalii katika maeneo
mbalimbali ya utalii ; na
(h) Kuhifadhi malikale kwa kuishirikisha jamii kutumia Malikale
kama chanzo cha kujipatia kipato kwa kutoa elimu ya
ujasiriamali, kutenga maeneo ya biashara, kuishirikisha sekta
binafsi na kutoa elimu ya uhi fadhi kwa umma.
Maliasili
30. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, pamoja na changamoto
mbalimbali zilizojitokeza katika Sekta ya M aliasili, Serikali imechukua
hatua za kuhakikisha kuwa sekta hii inapewa msukumo wa kutosha ili
iweze kuchangia kikamilifu katika kuboresha maisha ya wananchi.
Katika kutimiza azma hiyo, Serikali imetekeleza yafuatayo: –
(a) Hatua zimechukuliwa za kuimarisha m ahusiano mema baina ya
Mamlaka ya Hifadhi za Taifa na wananchi wanaoishi karibu na
hifadhi hizo kwa kufanya yafuatayo: –
(i) Maeneo 16 yaliyokosa sifa ya kuendelea kuwa maeneo ya
hifadhi yamer ejeshwa kwa mamlaka za wananchi;
(ii) Vijiji vinavyopakana na hifadhi vimepatiwa huduma
mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa,
nyumba za walimu, barabara na masoko ; na
(iii) Jumla ya wanaviji ji 7,320 wamepatiwa mizinga ya nyuki
24,076 na kupewa mafunzo ya mbinu za kisasa za ufugaji
nyuki na kutafuta masoko ya asali ikiwa ni pamoja
kuwawezesha kushiriki katika maonesho mbalimbali ndani
na nje ya nchi.
26
(b) Upandaji wa miti kwenye misitu ya jamii ume ongezeka ambapo
wastani wa miti milioni 200 kwa mwaka imepandwa katika kipindi
cha miaka mitano iliyopita ambapo asilimia 65 ya miti yote
iliyopandwa imeendelea kukua vizuri .
31. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Serikali itaendelea
kuchukua hatu a za kuh akikisha kwamba Sekta ya Maliasili
inazidi kuimarika ili kuyafanya mazao yatokanayo na malia sili
hususan misitu na nyuki yana endelea kuchangia katika ukuaji
wa uchumi, kuwaongezea wananchi kipato na kuongeza fursa
za ajira. Ili kufikia azma hiyo Chama Cha Mapinduzi
kitaielekeza Serikali kufanya yafuatayo: –
(a) Kuendelea kujenga mahusiano mema baina ya Mamlaka ya
Hifadhi za Taifa na wananchi wanaoishi karibu na hifadhi hizo
kwa namna ambayo wananchi hao watanufaika na uwepo wa
hifadhi hizo;
(b) Kutatua migogoro ya m ipaka kati ya wananchi na maeneo ya
jirani na hifadhi kwa kushirikisha wadau katika kuhakiki mipaka
ya maeneo ya hifadhi kwa kuweka alama za kudumu; kuandaa
mipango ya matumizi bora ya ardhi; na kuzingatia utawala wa
Sheria katika kusimamia rasilimali za m aliasili ;
(c) Kuboresha miundombinu ndani ya Mapori ya Akiba na Vikosi
dhidi ya ujangili na kuongeza vitendea kazi vya kisasa kwa ajili
ya doria na upelelezi nje na ndani ya maeneo ya hifadhi ;
(d) Kuendelea kutekeleza programu ya ufugaji nyuki ya mwaka
2007–2016 ili kuwajengea uwezo wadau wake kuzifahamu mbinu
bora za uzalishaji wa mazao ya nyuki na pia masoko ya asali na
nta ya ndani na nje ya nchi ;
(e) Kuendelea kuimarisha doria za ulinzi wa wananchi dhidi ya
wanyamapori kwa kuboresha mfumo wa utoaji taarifa za
wanyamapori waharibifu. Aidha, Serikali itaboresha na kutoa kwa
wakati kifuta machozi kwa watu au familia zitakazoathirika kwa
kiwango kinacholingana na athari zitakazotokea ;
27
(f) Kuongeza eneo la kupanda miti kutoka hekta 60,000 mwaka
2015 hadi hekta 130,000 mwaka 2020 na kuhakikisha kwamba
mbao zinazovunwa zinatumiwa kwa ajili ya kutengeneza samani
na matumizi mengine hapa nchini badala ya kusafirisha magogo
nje ya nchi ;
(g) Kuweka utaratibu wa wazi utakaowawezesha wananchi
wanaoishi jirani na hifadhi kufaidika na ras ilimali hizo ;
(h) Kuanzisha Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori ambayo
moja kati ya majukumu yake ni kuweka utaratibu utakaotumika
katika kutoa vibali vya uvu naji wa raslimali za maliasili ; na
(i) Kupambana na ujan gili wa wanyama pori wakiwemo Tembo na
Faru.
Viwanda na Biashara
32. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Ilani ya Uchaguzi iliweka
msukumo mkubwa zaidi katika kuimarisha uzalishaji katika viwanda
vilivyopo na kujenga viwanda vipya ili kuongeza uwezo wa uzalishaji na
michepuo ya bidhaa, kuhimiza mau zo ya bidhaa ndani na nje ya nchi na
kushirikiana na Sekta Binafsi katika kuendeleza viwanda vya kimkakati
kupitia mashirikia ya Umma ya NDC na EPZA. Katika kipindi hicho
mafanikio makubwa yamepatikana ambayo ni pamoja na: –
(a) Ukuaji wa Sekta ya Viwanda:
(i) Sekta ya Viwanda imekua kutoka asilimia 7.7 mwaka 2010
hadi asilimia 7.9 mwaka 2013. Ukuaji huo umechangiwa
kwa kiasi kikubwa kutokana na kuimarika kwa uzalishaji
viwandani, hususan viwanda vya vinywaji, saruji, bidhaa za
chuma; na usindikaji wa mazao ya kili mo;
(ii) Mwenendo wa mchango wa Sekta y a Viwanda katika Pato
la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 9.6 mwaka 2010 hadi
asilimia 9.9 mwaka 2013 ; na
(iii) Miradi mipya ya viwanda vilivyosajiliwa na ujenzi kuanza
katika kipindi husika imefikia 454.
(b) Ujenzi wa viwanda vi nane vya Saruji ambao uko katika hatu a za
mwisho za kukamilika ambavyo vitawezesha Taifa kuongeza
28
uzalishaji zaidi ya maradufu na hivyo nchi yetu kuijitosheleza kwa
saruji na nyingine kuuzwa nje. Aidha, k sukamilika kwa viwanda
hivi kutaifanya bei ya saruji kushuka na pia kuongeza ajira
mambo ambayo yataendelea kuboresha ustawi wa wananchi ;
(c) Katika Kanda ya Ziwa, ujenzi wa Kiwanda cha Nguo unaendelea.
Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kutumia kiwango kikubwa
cha pamba inayozalishwa katika ukanda huo hatua amb ayo
itahakikisha soko la uhakika la pamba na kuongeza ajira kwa
wakazi wa eneo hilo na kwa W atanzania kwa ujumla ;
(d) Ujenzi wa viwanda viwili vikubwa vya ngozi unaoendelea katika
mikoa ya Arusha na Shinyanga ambapo utakapokamilika utafanya
uuzaji wa ngozi gha fi nje ya nchi kuwa historia. Ngozi na bidhaa
za ngozi zitauzwa nje ya nchi zikiwa zimeongezewa thamani na
hivyo kuongeza ajira ; na
(e) Uzalishaji wa mbolea za NPK na MRP katika kiwanda cha Minjingu
umeongeza kutoka tani 75,000 hadi kufikia tani 100,000 kwa
mwaka.
(f) Mauzo ya Bidhaa za Viwandani:
(i) Mauzo kwenda soko la nchi wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki (EAC) yameongezeka kutoka dola za
Kimarekani milioni 419 mwaka 2010 hadi dola milioni
450 mwaka 2013 ;
(ii) Mauzo kwenda soko la Jumuiya ya Maendeleo Kusi ni
mwa Afrika (SADC) yameongezeka kutoka dola za
Marekani 625 mwaka 2010 hadi kufikia dola 1,209
mwaka 2013 ; na
(iii) Mauzo katika soko la Marekani kupitia Mpango wa AGOA
yameongezeka kutoka dola za Marekani milioni 51
mwaka 2010 hadi dola milioni 76 mwaka 2013.
(g) Maeneo Maalum u ya Uwekezaji :
(i) Mikoa 20 imetenga Maeneo Maalum u ya Uwekezaji ili
yawekewe miundombinu ya msingi itakayovutia Sekta
Binafsi kujenga viwanda na kufanya biashara katika
maeneo hayo ; na
29
(ii) Sheria za Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo Nje
(EPZ) na Maeneo Maalumu ya Uchumi (SEZ) zimepitiwa
ambapo vivutio mbalimbali ikiwa ni pamoja na nafuu ya
kodi vimebainishwa ili kuhamasisha ushiriki wa Sekta
Binafsi katika uwekezaji .
(h) Benki ya Rasilimali imeanzisha Dirisha Maalum u kwa ajili ya
kuwezesha wazali shaji wa bidhaa mbalimbali kupata mikopo
kwa riba nafuu kwa ajili ya ujenzi wa viwanda ;
(i) Jumla ya makampuni 130 yamewekeza mitaji yenye thamani ya
Shilingi bilioni 2,041.6 mwaka 201 4 ukilinganisha na Shilingi
bilioni 126.6 mwaka 201 0 na kutengeneza ajira z a moja kwa moja
zilizotokana na uwekezaji huo kufikia 31,923 ; na
(j) Ekari 107 zimepimwa katika Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kuanzisha
Vijiji vya Viwanda (Industrial Villages) na kupata hati miliki (Title
Deeds) ili kuanzisha viwanda vya kusindika na kutengenez a
bidhaa za ngozi.
(k) Muunganisho wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI):
Katika kipindi cha mwaka 2010 -2013, jumla ya mikopo 56,517
yenye thamani ya Shilingi bilioni 30.6 imetolewa na kuwezesha
upatikanaji wa ajira zipatazo 113,876 kupitia Mfuko wa
Kuendeleza Wafanyabiashara Wadogo (NEDF) .
30
Mradi wa Kiwanda cha kukamua mafuta ya Alizeti kinachojengwa nje
kidogo ya mji wa Dodoma .
33. Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2015 –2020,
Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza Serikali kuweka nguvu
kubwa katika kukamili sha utekelezaji wa Sera ya Maendeleo
Endelevu ya Viwanda Awamu ya Tatu (2010 –2020) ambayo
malengo yake ni kuiwezesha Sekta ya Viwanda kuchangia
katika kufikia malengo ya maendeleo ya muda mrefu kama
ilivyoanishwa katika Dira ya Maendele o ya Taifa 2025. Aidha,
Utekelezaji wa Ilani hii utakuwa ni sehemu ya Utekelezaji wa
Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka M itano (2015/16 –
2020/21 ) ambao lengo lake ni kuendelez a uchumi wa viwanda.
Katika kipindi hicho, utaanza ujenzi wa viwanda mama (basic
industries) na ku imarisha viwanda vilivyopo lengo likiwa ni
kuhakikisha kwamba: –
31
(a) Mchango wa Sekta ya Viwanda katika Pato la Taifa unaongezeka
kutoka asilimia 9.9 mwaka 2013 hadi asilimia 15 ifikapo mwaka
2020;
(b) Sekta ya Viwanda inaongeza ajira kufikia asilimia 40 ya ajira z ote
ifikapo 2020 kwa kuweka kipaumbele cha kujenga viwanda
vinavyotumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini kama vile
kilimo, mifugo, uvuvi na maliasili ; Viwanda hivyo ni pamoja na
viwanda vya nguo, sabuni, korosho, matunda n.k.
(c) Kuandaa mikakati thabiti ya kuhamasisha sekta binafsi kuanzisha
viwanda vikubwa na vya kati na ku weka utaratibu wa kuvi linda
dhidi ya viwanda vya nje ;
(d) Kujenga mazingira rafiki yatakayowezesha kupunguza gharama za
uwekezaji na uendeshaji wa viwanda;
(e) Kuanzisha viwanda vya msingi vina vyotumia malighafi ya chuma
katika maeneo ya Liganga na Mchuchuma ;
(f) Sekta ya Viwanda inaongeza fursa za masoko hususan yenye
upendeleo wa ushuru wa forodha kama Jumuiya ya Afrika
Mashariki, Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, Utatu wa
COMESA -EAC-SADC na Umoja wa Ulaya, nchi rafiki kama I ndia,
China, Japan na Marekani ; na
(g) Kuendeleza kasi ya ujenzi wa viwanda vidogo na vya kati hasa
vinavyosindika mazao.
(h) Kuhakikisha Benki ya Rasilimali (TIB) inapanua wigo wa Dirisha
Maalumu ili liweze kutoa huduma zak e kwenye maeneo yote
nchini ikiwemo Tanzania Zanzibar.
Madini
34. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali imeendeleza juhudi
katika kuhakikisha Sekta ya Madini inachangia kikamilifu katika kukuza
uchumi na ajira. Kutokana na juhudi hizo, mchango wa madini katika
Pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 3.3 mwaka 2010 hadi
asilimia 3.5 mwaka 2014. Kuimarika kwa sekta hii kumetokana na
kufanyika mambo yafuatayo: –
(a) Shirika la Madini la Taifa (STAMICO ) limewezeshwa kumiliki hisa
kwenye migodi ya STAMIGO LD (100%), Buchreef (45%),
32
Buhemba (100%), Kiwira (100%), Tanzanite one (50%),
Tulawaka (100%), NDC –Liganga (20%), Mchuchuma (20%),
Ngaka Coal Projects (30%) na Mgodi wa Almasi wa Mwadui
(25%) ;
(b) STAMICO imeanzisha Kampuni iitwayo Kyerwa Tin Company
Limited ( KTCL) ili kununua madini ya bati kutoka kwa wachimbaji
wadogo wa madini hayo huko Kyerwa. Hadi kufikia Machi, 2015
jumla ya tani 71.3 zimenunuliwa kwa gharama ya Shilingi
1,106,326,000. Aidha, tani 30 zimeuzwa kwa Dola za Marekani
201,000 ;
(c) STAMICO imefanik iwa kupata kandarasi nne (4) za uchorongaji
na utafiti wa madini yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.35
ambapo jumla ya ajira mpya 78 zimepatikana kutokana na
upatikanaji wa mashine za kisasa za uchorongaji ;
(d) Ofisi mbili za madini za Kanda zimeanzishwa; moj a katika Kanda
ya Ziwa Nyasa inayohudumia Mikoa ya Njombe na Ruvuma; na
nyingine kanda ya Ziwa ambayo inahudumia Mikoa ya Mara na
Simiyu ili kusimamia na kudhibiti biashara ya madini. Kuanzishwa
kwa ofisi hizo mpya kumeongeza idadi ya ofisi za Kanda kufiki a
kumi (10) na hivyo kuongeza ufanisi kwa wadau wa sekta hii ; na
(e) Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) umeendelea kuwezeshwa kwa
kupatiwa fedha na vitendea kazi ili kuimarisha utendaji kazi wake.
Katika kipindi hicho Wakala wa Jiolojia amepata mafanikio
yafuat ayo:-
(i) Mfumo wa utunzaji, uchakataji, na usambazaji/uuzaji wa
takwimu na taarifa za upatikanaji madini ili kuvutia
uwekezaji umeboreshwa ;
(ii) GST imejiunga na COSOTA ili kusajili machapisho yake na
kupewa haki miliki ( Copyright) ;
(iii) GST imejenga maabara ya kisas a ya kuchunguza miamba
na madini baada ya kununua vifaa muhimu na vya kisasa ;
na
33
(iv) GST imefanikiwa kufanya ugani na uchoraji wa ramani za
upatikanaji wa madini (geological and mineral occurrence
mapping) kwa asilimia 92 ya ardhi kavu ya Tanzania Bara.
(f) Idadi ya leseni za madini imeongezeka hadi kufikia 37,261
mwaka 2015 ambapo leseni za uchimbaji mkubwa ni 15;
uchimbaji wa kati ni 380; uchimbaji mdogo ni 33,131; na leseni
za utafutaji madini ni 3,735. Watanzania wanamiliki asilimia 70 ya
leseni hizo, wageni as ilimia 25 na asilimia 5 ya leseni hizo
zinamilikiwa kwa ubia kati ya Watanzania na Wageni ;
(g) Wachimbaji wadogo wametengewa maeneo 25 yenye ukubwa wa
kilometa za mraba 2,407 na jumla ya leseni 8,800 zimetolewa
kwenye maeneo hayo ;
(h) Wachimbaji wadogo 10,000 wam epatiwa mafunzo ya huduma za
ugani (extension services) katika nyanja za kutambua umbile na
tabia ya mashapo, masuala ya utunzaji wa mazingira, utambuzi
wa madini na uboreshaji wa uchenjuaji madini ;
(i) Jumla ya Shilingi milioni 909.5 zimetolewa kwa wachimbaji
wadogo kama ruzuku ;
(j) Mpango wa utunzaji mazingira katika maeneo ya uchimbaji wa
madini (Modern Environmental Protection Plan) umeanzishwa na
umewahamasisha wachimbaji wadogo kutunza mazingira na
kuepuka kuchafua vyanzo vya maji ;
(k) Mikataba ya madini imepitiw a kwa lengo la kulinda maslahi ya
nchi ambapo baadhi ya vipengele v imefanyiwa marekebisho ili
mrahaba ulipwe kwa kiwango cha asilimia 4 ya mauzo ghafi ya
dhahabu ( gross value ) badala ya asilimia 3 ya mauzo halisi ya
dhahabu ( Net Back Value ) iliyokuwa ikili pwa na wawekezaji hapo
awali;
(l) Migodi ya Bulyanhulu, North Mara, Buzwagi na Geita imeanza
kulipa ushuru wa huduma (service levy) kwa Halmashauri husika
kwa kiwango cha asilimia 0.3 ya mapato ghafi ya migodi hiyo
badala ya Dola za Kimarekani 200,000 zilizoku wa zinalipwa kwa
mwaka ;
34
(m) Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) imeanzisha
madawati ya ukaguzi kwenye viwanja vya ndege vya Kimataifa ili
kudhibiti vitendo vya utoroshaji wa madini nje ya nchi , hatua
iliyow ezesha kukamatwa madini yenye thamani ya Shili ngi bilioni
15; na
(n) Kamati Maalum u ya Kitaifa (National Local Content Committee)
imeundwa ili kusimamia mikakati iliyowekwa na wadau
kuhakikisha kuwa Makapuni ya Madini yanaongeza kiwango cha
manunuzi ya bidhaa na huduma hapa nchini kwa lengo la
kuongeza aj ira na soko la bidhaa za ndani.
35. Katika kipindi cha 2015 hadi 2020, Chama Cha Mapinduzi
kitaielekeza Serikali yake kutekeleza mambo yafuatayo ili
kuendelea kukuza Sekta ya Madini na kuongeza mchango wake
kwenye Pato la Taifa: –
(a) Kuweka na kusimamia mfumo th abiti wa kukagua shughuli za
migodi, kukusanya takwimu za madini na kufuatilia maduhuli
yatokanayo na madini kwa malengo mapana ya kuongeza
mapato ya Serikali ;
(b) Kuweka na kutekeleza mikakati madhubuti ya kuvu tia mitaji
ya uwekezaji katika Sekta ya Madini, h ususan kwenye madini
adimu (Rare Earth Elements – REE);
(c) Kuhamasisha uzalishaji na masoko ya madini ya viwandani ;
(d) Kuweka miundombinu muhimu (umeme, simu, maji,
barabara) kupitia ushirikiano wa Serikali na Sekta Binafsi
(PPP) kwenye maeneo yenye uwezekano wa kuanzishwa kwa
migodi mikubwa mipya ;
(e) Kuboresha mfumo wa utoaji na usimamizi wa leseni za
madini, na upatikanaji wa taarifa muhimu kwa wadau kuhusu
Sekta ya Madini;
(f) Kuimarisha udhibiti na usimamizi wa upatikanaji, utunzaji,
usafirishaji na matumizi ya baru ti katika shughuli za migodi ;
(g) Kuendelea kuliimarisha Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ili
liweze kushiriki kikamilif u kwenye shughuli za utafutaji,
35
uchimbaji na utoaji huduma katika Sekta ya Madini kwa niaba
ya Serikali na Watanzania wote ;
(h) Kuendelea ku ujengea uwezo wa kifedha na rasilimali watu
Wakala wa Jiolojia Tanzania ili uweze kufikia kiwango bora
zaidi katika ukusanyaji wa takwimu na taarifa muhimu za
kijiolojia na kijiofizikia zitakazosaidia katika kuchochea kasi ya
utafutaji na upatikanaji wa ma shapo ya madini hapa nchini
yanayoweza kuchimbwa kwa faida ;
(i) Kuendelea kuujengea uwezo Wakala wa Ukaguzi wa Madini
Tanzania na Ofisi za Madini Mikoani ili zijiimarishe katika
kukagua na kusimamia shughuli za uzalishaji na biashara ya
madini nchini, na hivyo kuongeza manufaa yatokanayo na
Sekta ya Madini kwenye uchumi ;
(j) Kusimamia na kuhamasisha uwekezaji katika shughuli za
uongezaji thamani madini ili kukuza mchango wa sekta hiyo
katika Pato la Taifa ;
(k) Kubuni na kutekeleza mikakati mahsusi itakayowezesha
kupung uza au kukomesha kabisa vitendo vya utoroshaji wa
madini kwenda nje ya nchi na biashara haramu ya madini
nchini ;
(l) Kuweka na kutekeleza mikakati maalum u itakayowezesha
soko la Tanzanite hapa nchini kuimarika zaidi na hivyo
kuongeza manufaa yatokanayo na mad ini hayo
yanayopatikana Tanzania pekee ;
(m) Kuwawezesha wachimbaji wadogo kujiajiri kupitia sekta hii
kwa kufanya yafuatayo: –
(i) Kuwatambua, kuwarasimisha na kuwapatia maeneo
ya uchimbaji m adini;
(ii) Kuwapatia ruzuku, mafunzo, teknolojia na maarifa ya
kisasa kwa ajil i ya k uendeleza shughuli za uchimbaji;
(iii) Serikali kupitia STAMICO kwa kushiriki ana na
wachimbaji wakubwa kuwaweze sha kupata mikopo
na masoko; na
36
(iv) Kuendelea kuongeza na kuwekeza mtaji wa Benki ya
Rasilimali (TIB) ili iweze kutoa mikopo kwa
wajasiriamali wadogo .
(n) Kuendelea kuimarisha ukaguzi wa migodi katika masuala ya
usalama, utunzaji wa mazingira na afya migodini ; na
(o) Kuhakikisha migodi yote mikubwa nchini inaendelea inanunua
huduma na bidhaa kutoka hapa nchini kwa kiwango cha
kuridhisha kwa kadri ya upatikanaj i wake.
37
SURA YA TATU
SEKTA ZA MIUNDOMBINU NA HUDUMA ZA KIUCHUMI
Ardhi
36. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, serikali imep ata mafanikio
yafuatayo katika Sekta ya Ardhi:-
(a) Utawala wa Ardhi :
(i) Jumla ya vijiji 1,619 katika Halmashauri za Wilaya 37
vimepi mwa;
(ii) Jumla ya vijiji 5,558 vimepatiwa vyeti vya Ardhi ya
Kijiji;
(iii) Jumla vijiji 509 vimeandaliwa mipango ya matumizi
bora ya ardhi katika wilaya 69 nchini ;
(iv) Jumla ya Hatimiliki za Kimila 348,000 zime tolewa ; na
(v) Ofisi za Ardhi za Kanda zimeanzishwa na
kuimarish wa.
(b) Mpango wa Taifa wa Matumizi ya Ardhi (2013 -2033)
umeandaliwa na utekelezaji wake umeanza ambapo Vijiji 509
vimeandaliwa mipango ya matumizi ya ardhi katika wilaya 69
nchini na kufanya vijiji vilivyoandaliwa mipango hiyo kufikia
1,560 .
(c) Mipango Miji:
(i) Programu ya Kurasimisha na Kuzuia Makazi H olela
imeandaliwa mwaka 2012 ;
(ii) Elimu ya Urasimishaji na Kuzuia Makazi H olela imetolewa
katika mikoa mbalimbali ;
(iii) Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Dar es Salaam zimetoa
leseni za makazi 35,362 na kutoa Hati 2,204 za kumi liki
Ardhi;
(iv) Huduma za upimaji na ramani zimepelek wa katika ofisi
mbalimbali za K anda;
(v) Ili kupunguza msongamano katika miji mikubwa nchini
hususan Dar es Salaam na Arusha, mipango kabambe ya
38
kujenga miji midogo ya Luguruni (ekari 156.53), Mji Mpya
wa Kiga mboni (ekari 16,047) na Kawe (ekari 267.71)
imekamilika. Aidha, miji midogo ya Burka/Matevesi (ekari
579.2) na eneo la Usa River (ekari 296) katika Jiji la
Arusha itajengwa ; na
(vi) Mpango wa kuanzisha mji mpya wa kisasa wa Kigamboni
ili kukabiliana na ukuaji w a kasi wa Jiji la Dar es Salaam
umekamilika. Hatua ambazo zimefikiwa katika uanzishwaji
wa mji huo wa kisasa ni: –
Wakala wa kusimamia utekelezaji na uendelezaji wa
Mpango wa Mji mpya wa Kigamboni (KDA)
umeundwa ;
Rasimu ya Mpango Kabambe wa Mji mpya wa
Kigamboni imeandaliwa (Kigamboni New City Master
Plan – 2011 – 2031) ;
Ujenzi wa daraja la Kigamboni na barabara
kiunganishi unaendelea chini ya usimamizi wa Wizara
ya Ujenzi ;
Eneo la upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam katika
Kata ya Vijibweni limebainishwa na kazi ya uthamini
inaendelea ; na
Utaratibu mpya wa uendelezaji wa Mji wa Kigamboni
umepitiwa na kuridhiwa na Kamati ya Wadau wa
Kigamboni ambapo Serikali itajihusisha zaidi na
uwekezaji katika kuweka/kujenga miundombinu kama
vile barabara, umeme na maji. W ananchi
wataruhusiwa kufanya yafuatayo: –
– Kuwa wae ndele zaji wenyewe katika eneo la
mradi kwa kuzingatia Mpango Kabambe wa
kuendeleza Mji wa Kigamboni; au
– Kuingia ubia na mwekezaji, ambapo thamani
ya ardhi ya mwananchi itakuwa ndio mtaji
wake; au
39
– Kulipwa fid ia/kuuza eneo lake kwa
wawekezaji/Serikali kwa bei ya soko.
(d) Kazi ya kuanzisha Benki ya Ardhi (Land B ank) kwa ajili ya
wawekezaji wa ndani na nje imeendelea kutekelezwa na
jumla ya Shilingi bilioni moja zimetengwa kwa ajili ya kianzio
cha Mfuko wa Fidia ya Ardhi (Land Compensation Fund).
Aidha, mashamba 66 mkoani Morogoro yameainishwa kwa
ajili ya kuingizwa kwenye Hazina ya Ardhi na mashamba 112
mkoani Arusha yamekaguliwa na kupendekezwa kuingizwa
kwenye Hazina ya Ardhi ;
(e) Baadhi ya Halmashauri za Miji na Wil aya nchini
zimewezeshwa kutumia mfumo wa teknolojia ya kompyuta
katika kutoa huduma za ardhi ;
(f) Halmashauri za Miji na Wilaya zimeendelea kujengewa uwezo
kupitia Mfuko wa Mzunguko (Plot Development Revolving
Fund) wa kupima viwanja na kuviuza kwa wananchi am bapo
jumla ya Halmashauri 14 zimeidhinishiwa mikopo ya jumla ya
Shilingi bilioni 2.67 ; na
(g) Hatua zifuatazo zimechukuliwa katika kuzijengea uwezo
Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji ili kuhakikisha majukumu
ya Sekta ya Ardhi yanatekelezwa ipasavyo: –
(i) Kompy uta 100 kwa ajili ya matumizi ya shughuli za
Sekta ya Ardhi katika Halmashauri 100 hapa nchini
zimenunuliwa na kusambazwa ;
(ii) Vifaa vya upimaji vim enunuliwa na kufikishwa katika
Halmashauri ya Manyoni (Total station 1), Jiji la
Mbeya (Total station 1), Ofisi ya Mkoa wa Mwanza
(GPS 1 na Total station 1) ; na
(h) Pamoja na changamoto zinazoyakabili Mabara za ya Ardhi na
Nyumba ya Wilaya , hatua zifuatazo zimechukuliwa katika
kushughulikia mashauri yahusuyo ardhi na nyumba: –
(i) Mabaraza 39 ya wilaya mbalimbali yamepatiwa
watumishi, samani na vitendea kazi ;
40
(ii) Mabaraza mapya 10 yameanzishwa katika wilaya za
Nzega, Manyoni, Kilosa, Tunduru, Mpanda, Kyela,
Muleba, Ngara, Karagwe na Ngorogoro hivyo kufanya
mabaraza yanayotoa huduma kufikia 49 ; na
(iii) Hatua za kinidhamu zimeendele a kuchukuliwa dhidi ya
wenyeviti wa mabaraza ya wilaya waliokiuka maadili ya
umma.
(i) Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) kwa kushirikiana na sekta
binafsi limeendelea kujenga nyumba kwa ajili ya makazi na
mafanikio yafuatayo yamepatikana: –
(i) Ujenzi wa majengo ya biashara 81 na nyumba za
makazi 5,900 umekamilika ;
(ii) Ujenzi wa majengo 50 ulioshirikisha sekta binafs i
umekamilika ; na
(iii) Ardhi yenye ukubwa wa ekari 4,642 katika maeneo
mbalimbali nchini imenunuliwa kwa ajili miradi
mbalimbali ya ujenzi wa nyumba.
(j) Wakala wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA)
umefanya yafuatayo :-
(i) Utafiti k uhusu mashine za kufungamana
(interlocking press machine), kofia, mashine za
“hydraform”, majaribio ya sampuli ya udongo,
ujenzi wa zege na kofia za vigae vya kuezekea
ulifanyika na m atokeo ya utafiti huo yameenezwa
katika Halmashauri za Wilaya za Namtumbo,
Karatu, Monduli, Simanjiro, Sumbawanga, Bariadi,
Kilombero, Rungwe na Halmashauri za Manispaa za
Temeke, Kinondoni, Ilala, Tabora, Iringa, Dodoma
na Halmashauri ya Jiji la Tanga; na
(ii) Jumla ya mashine za kufyatulia matofali 1,105
ziligawiwa kwa Halmashauri mbalimbali nchini.
(k) Uanzishwaji wa vyama vya Ushirika wa Nyumba umeendelea
kuhamasishwa ili kuwezesha wananchi wa kipato cha chini
kunufaika na mikopo ya nyumba ambapo: –
41
(i) Vijana 150 wamepewa mafunzo ya teknolojia ya
ujenzi wa nyumba bora na za gharama nafuu katika
ofisi za Wakala, katika Mkoa wa Kagera (vijana 55) na
Jiji la Dar es Salaam (vijana 95) ;
(ii) Mwongozo kuhusu kuanzisha na kusimamia vyama
vya Ushirika wa Nyumba umeandaliwa ; na
(iii) Jumla ya mashine 656 za kufyatulia matofali
yanayofun gamana zimetolewa kwa Halmashauri 163
ambapo kila H almashauri ilipatiwa wastani wa
mashine nne.
(l) Ujenzi wa mtandao wa upimaji nchini wenye alama 640 za
madaraja mbalimbali umekamilika kwa asilimia 98 ;
(m) Upimaji wa njia za kuingia katika bandari (port approaches)
za Dar es Salaam na Zanzibar umekamilika ;
(n) Kampuni ya Dhamana ya Mikopo ya Nyumba (The Tanzania
Mortgage Refinancing Company) imeanzishwa kwa lengo la
kutoa mikopo ya muda mrefu kwa benki za biasha ra ili nazo
zitoe mikopo ya nyumba ya muda mrefu kwa wananchi
ambapo mafanikio yafuatayo yamepatikana: –
i. Benki za biashara 20 zimetoa mikopo ya muda mrefu
yenye riba nafuu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba kwa
wananchi 3,598 ;
ii. Mfuko wa Mikopo Midogo Midogo ya Nyumba (Housing
Micro -finance Fund) umeanzishwa chini ya Benki Kuu ya
Tanzania (BOT) . Aidha, mtaji wa Shilingi bilioni 36
zimetengwa kwa ajili ya Mfuko wa Dhamana ya Mikopo
ya Nyumba (TMRC) ;
iii. Mwongozo kuhusu sifa za taasisi za fedha zinazostahili
kupata mkopo kutoka TMRC umeandaliwa ; na
iv. Mpango wa kutoa elimu kwa umma kuhusu Sheria,
Kanuni na Taratibu za mikopo ya nyumba umeandaliwa.
(o) Ujenzi wa Nyumba na Majengo ya Serikali :
42
Katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2015, Serikali kupitia
Wakala wa Majengo (TBA) imend elea na ujenzi wa ofisi
za Serikali, nyumba za viongozi na mradi wa nyumba
10,000 kwa ajili ya watumishi wa umma katika mikoa
mbalimbali nchini . Ujenzi wa majengo ya umma umekuwa
ukizingatia mahitaji maalum u ya watu wenye ulemavu.
37. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Chama Cha Mapinduzi
kitaielekeza Serikali kuendelea kutekeleza mipango ya
kuendeleza ardhi katika maeneo yafuatayo: –
(a) Utawala wa Ardhi
(i) Kujenga mfumo utakaorahisisha umilikishaji wa ardhi na
uhifadhi wa kumbukumbu za ardhi kwa kukamilisha ujen zi
wa Mfumo Unganishi wa Kuhifadhi Kumbukumbu za Ardhi
(Integrated Land Management Information System) ;
(ii) Kuimarisha huduma za ardhi katika Kanda kwa kujenga
majengo manane (8) ili kusogeza huduma za ardhi karibu
na wananchi katika Kanda za Nyanda za Juu Kus ini
(Mbeya), Ziwa (Mwanza), Kaskazini (Moshi), Magharibi
(Tabora), Kati (Dodoma), Kusini (Mtwara), Kanda ya
Mashariki, na Kanda ya Dar es Salaam inayohudumia mkoa
wa Dar es Salaam ;
(iii) Kuimarisha utoaji wa huduma za ardhi katika Kanda nane
(8) za Ardhi nchini kwa lengo la kuongeza kasi ya utoaji wa
Hatimiliki za Kimila nchini ;
(iv) Kuzijeng ea uwezo Halmashauri za Miji na Wilaya kwa
kuzipatia mafunzo, vifaa, rasilimali fedha na w ataalamu ili
ziweze kupima viwanja na mashamba nchini ;
(v) Kuendelea kuimarisha Mfuko wa Fid ia ya Ardhi ili uweze
kufidia ardhi itakayotwaliwa kwa matumizi ya umma na
uwekezaji ;
(vi) Kufanya uhakiki wa mashamba pori yasiyoendelezwa kwa
kipindi kirefu na kugawa upya kwa wananchi ;
43
(vii) Kuanzisha Baraza la Taifa la Ushauri la Ardhi ( National
Land Advisory Cou ncil) ili kuwezesha ardhi kutumika kwa
ufanisi ;
(viii) Kutoa elimu kwa umma juu ya Sheria za Ardhi, Sheria ya
Mipangomiji, Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi na
Sheria zingine zinazohusiana na utawala wa ardhi;
(ix) Kuimarisha huduma ya utatuzi wa migogoro ya ard hi kwa
kuanzisha Mabaraza mapya 100 ya Ardhi na Nyumb a
kwenye wilay a zenye migogoro mingi ya ardhi;
(x) Kuhakikisha maafisa ardhi wasio waaminifu
wanashughulikiwa; na
(xi) Kuanzisha akiba ya ardhi (land bank).
(b) Utayarishaji wa Mipango ya Matumizi Bora ya ardhi
nchini
(i) Kuendelea kutekeleza Mpango wa Taifa wa Matumizi ya
Ardhi;
(ii) Kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji 7,500 na
mipango ya matumizi ya ardhi ya Wilaya 25 ;
(iii) Kukamilisha upimaji wa mipaka ya vijiji vyote nchini ;
(iv) Kuwapatia wananchi hatimiliki za kimi la 2,500,000 pamoja
na kujenga masjala za ardhi 250 katika ngazi za Wilaya
na Vijiji ; na
(v) Kuwapatia wananchi hati miliki 2,000,000 pamoja na
kusaji li nyaraka nyingine za kisheria.
(c) Nyumba
(i) Kuboresha mazingira ya upatikanaji wa mikopo kwa ajili ya
ujenzi wa n yumba za gharama nafuu na kwa masharti
nafuu ;
(ii) Kuwaelimisha wananchi kuzielewa sheria za mikopo ya
nyumba ili wazitumie kupata mikopo ya muda mrefu kwa
ajili ya kujenga au kununua nyumba na kuhamasisha
mabenki na asasi nyingine za fedha z itoe mikopo ya
nyum ba kwa muda mrefu na yenye riba nafuu ;
44
(iii) Kuweka utaratibu utakaowezesha kuanzisha Benki ya
Nyumba ya Taifa ;
(iv) Asasi za Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi zitajenga
nyumba za gharama nafuu zisizopungua 50,000 ;
(v) Kuwawezesha wanavijiji kujiunga kwenye viku ndi vya
ujenzi vitakavyopatiwa elimu ya jinsi ya kujenga nyumba
bora vijijini ;
(vi) Kuliwezesha Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuwa
Mwendelezaji Miliki M kuu (Master Estate Developer );
(vii) Kupunguza kodi kwenye vifaa vya ujenzi wa nyumba za
gharama nafuu hususan v ijijini;
(viii) Kuanzisha na kuimarisha vyama vya ushirika vya ujenzi wa
nyumba zenye gharama nafuu ;
(ix) Kuelimisha na kuhamasisha wananchi kujenga nyumba
bora kwa kutumia vifaa vya ujenzi vya gharama nafuu ; na
(x) Kujenga nyumba za watumishi wa umma na majengo ya
serikali yenye kuzingatia mahitaji maalumu ya watu wenye
ulemavu kwa: –
Kuanza ujenzi wa majengo yatakayotumika kama
Ofisi kwa Taasisi za Serikali ili kuipunguz ia Serikali
gharama ya kodi kubwa ya pango katika soko huria;
Kuendelea na mradi wa ujenzi wa nyumba 10,000
kwa ajili ya watumishi wa umma ambapo asilimia 50
zitajengwa katika maeneo ya vijijini; na
Kuboresha karakana 6 za kutengeneza samani za ofisi
na nyumba za Serikali ili kupunguza gharama za
uagizaji wa samani kutoka nje ya nchi.
(xi) Kukamilisha utungaji wa Sera ya Taifa ya Nyumba
(Housing Policy ).
(xii) Kuanzisha Mamlaka ya Udhibiti na U endelezaji wa Miliki
(Real Estate Regulatory Authority ) ambayo pamoja na
majukumu mengine itasimamia udhibiti wa kodi za pango
kwa nyumba za makazi na biashara.
(d) Mipango Miji na Vijiji
45
(i) Kukamilisha uandaaji wa Mipango Kabambe ( Master Plans )
kwa miji mikuu yote ya mikoa ;
(ii) Kuhimiza ujenzi wa miji ya pembezeno (Satilite cities)
katika jiji la Dar es Salaam pamoja na miji mingine ili
kufanya miji hiyo ikue kwa kuzingatia mipango mi ji;
(iii) Kuendelea kujenga mji mpya wa Kigamboni ( Kigamboni
New City ) kwa kuzingatia matakwa, maslahi na ushiriki wa
wananchi wa Kigambon i;
(iv) Kuendelea kutekeleza Programu ya Taifa ya Kurasimisha
Makazi yaliyopo katika maeneo ambayo hayajapimwa kwa
lengo la kuya panga na kuyapima viwanja katika miji ya Dar
es Salaam, Mwanza, Arusha, Tanga, Morogoro na Mbeya.
Program hii itatoa hatimilki za Makazi ; na
(v) Kuendeleza maeneo yaliyoiva ( re-development scheme ) ya
Kipawa, Namanga, Vingunguti, Manzese, Buguruni,
Msasani Bond e la Mpunga na Kawe , Jijini Dar es Salaam.
(e) Upimaji na Ramani
Upimaji wa ardhi na utayarishaji wa ramani ni chanzo muhimu
cha taarifa zinazohitajika katika kubuni na kutayarisha mipango
ya matumizi ya ardhi kwa sekta mbalimbali. Hadi sasa ni sehemu
ndogo t u ya ardhi ya nchi imepimwa, hivyo ili kuifanya ardhi
kuchangia ka tika kukuza P ato la Taifa, kutoa fursa za ajira na
kuvutia uwekezaji ipo haja ya kuongeza kasi ya upimaji wa ardhi.
Katika kipindi hiki, Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza
Serikali kufanya yafuatayo: –
(i) Kuendeleza upimaji wa ardhi katika maeneo ya mipaka ya
nchi ili kuimarisha ulinzi na usalama ;
(ii) Kuimarisha alama za mipaka kati ya Tanzania na nchi jirani
za Kenya, Burundi, Zambia, Malawi, Uganda, Rwanda,
Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kong o;
(iii) Kujenga kituo cha kupokea picha za anga ( Satellite
Receiving Station ) kitakachojengwa katikati ya nchi (Chuo
Kikuu cha Dodoma) ambacho kitawezesha utayarishaji wa
46
ramani za msingi ( base maps ), kupanga na kuongeza kasi
ya kupima ardhi kwa ajili ya matum izi mbalimbali ; na
(iv) Kuzijengea uwezo wa rasilimali watu na fedha Halmashauri
za Wilaya, Miji na Majiji na kuzipatia zana za kisasa za
kupima ardhi na usanifu wa ramani na kuwapatia mafunzo
stahiki watalaam u wa ardhi.
Usafirishaji na Uchukuzi
38. Ujenzi na ukar abati wa miundombinu ya usafiri na usafirishaji
umechochea kukua kwa shughuli za kiuchumi ambazo zimewezesha pia
kuongeza ajira nchini. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali
imeendelea kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika ujenzi na ukarabati wa
miundombinu ya barabara, reli, madaraja, vivuko na viwanja vya ndege
ambao umekuwa msingi wa kukua kwa uchumi wetu na shughuli
nyingine za kijamii. Tanzania imepiga hatua kubwa katika sekta hii na
kuifanya kuwa moja kati ya nchi zenye mtandao mzuri wa miun dombinu
ya usafiri hususan barabara katika Bara la Afrika.
(a) Barabara
Nchi yetu ina mtandao wa barabara wenye jumla ya urefu wa
kilometa 35,000 zinazojumuisha kilometa 12,786 za barabara
kuu na kilometa 22,214 za barabara za mikoa.
Katika kipindi cha miaka kumi cha uongozi wa Serikali ya
Awamu ya Nne, barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa
13,753 zimekuwa katika h atua mbalimbali za ujenzi ambapo
jumla ya barabara zenye urefu wa kilometa 4,691
zimekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami na barabara
zenye u refu wa jumla ya kilometa 2,358 zimeendelea
kujengwa katika kiwango cha lami. Aidha, jumla ya barabara
zenye urefu wa kilometa 3,419 zimefanyiwa upembuzi na
usanifu kwa ajili ya ujenzi. Barabara hizo ni kama
zilivyoanishwa: –
(i) Barabara ambazo zimekamilika ku jengwa kwa
kiwango cha lami:
Korogwe – Handeni (km 65)
47
Dumila – Rudewa (km 45)
Lwanjilo – Chunya (km. 36)
Tanga – Horohoro (km 65)
Masasi – Mangaka (km 54)
Minjingu – Babati – Singida (km 222)
Mwandiga – Manyovu (km 60)
Handeni – Mkata (km 54)
Barabara y a Kilwa/Dsm (km 12)
Barabara ya Ma ndela/Dsm (km 16)
Msimba – Ikokoto – Mafinga (km 219)
Arusha – Namanga (km 105)
Chalinze – Segera –Tanga (km 245)
Isaka – Ushirombo (km 132)
Rau Madukani – Mawela – Uru Njari (km 12.5)
Tunduma – Sumbawanga (km 230)
Sehemu ya Bonga – Babati (km 19.2)
Dodoma – Iringa (km 260)
Puge – Tabora (km 56)
Manyoni – Itigi – Chaya (km 89.30)
Tabora – Ndono (km 42)
Uvinza – Kidahwe (km 77)
Daraja la Malagarasi na Barabara zake (km 48)
Namtumbo – Songea (km 70)
Peramiho – Mbinga (km 7 8)
Ujenzi kwa sehemu ya Mwenge – Tegeta (km
12.9)
Segera – Korogwe (km 20)
Korogwe – Mkumbara (km 76
Arusha – Minjingu (km 104)
Simiyu/Mara Border – Musoma (km 85)
Banana – Kitunda – Kivule – Msongola (km 3.2)
Msoga – Msolwa (Chalinze Bypass) Km 10)
Barab ara ya Mafia (Mafia Access Road) (km 14)
Barabara ya Dodoma University (km 12)
48
(ii) Barabara ambazo zipo katika hatua mbalimbali
za ujenzi :
Mziha – Turiani – Magole (km 84.6)
Dumila – Kilosa (km 63)
Dumila – Turiani – Handeni (km 174)
Bariadi – Lamadi (km 71. 8)
Mbeya – Chunya – Makongolosi (km 115)
Makofia – Msata (km 64)
Kisarawe – Maneromango (km 54)
Ushirombo – Lusahunga (km 110)
Kwa Sadala – Masama (km 12.2)
Kibosho Shine – Kwa Raphael – International
School (km 43)
Kirua Nduoni – Marangu Mtoni (km 31.5)
Kahama Mjini (km 5)
Bunda – Kisorya – Nansio (km 93)
Dodoma – Babati (km 261)
Sumbawanga – Kinyani – Nyakanazi (km 562)
Nzega – Tabora (km 116)
Manyoni – Itigi – Tabora (km 264)
Mangaka – Mtambaswala (km 65)
Mto wa Mbu – Loliondo – Mugumu – Nata-
Makutano (km 452)
Tunduru – Namtumbo (km 194)
Tabora – Urambo (km 90 )
Uyovu – Bwanga – Biharamulo (km 112)
Kisesa – Usagara (km 17)
Kyaka – Bugene (km 59)
Segera – Same – Himo (km 261)
Arusha – Moshi – Himo – Holili (km 140)
Nyanguge – Musoma – Sirari (km 262)
Katumba – Mbambo – Tukuyu (km 80)
Kaliua – Kazilambwa (km 56)
Barabara ya Kibamba – Monganzila (km 4.0)
49
Barabara ya KIA – Mererani (km 26)
Mafinga – Igawa (km 137.9)
Mwigumbi – Maswa – Bariadi (km 100)
KAMATA – Bendera Tatu (km 1.3)
Ardhi – Makongo – Goba (k m 9)
(iii) Barabara ambazo zimefanyiwa upembuzi na
usanifu na baadhi ya maeneo ujenzi kwa
kiwango cha lami unaendelea :
Makurunge – Saadan – Pangani – Tanga (km
178)
Rujewa – Madibira – Mafinga (km 151)
Matai – Kasesya (km 50)
Mbinga – Mbamba Bay (km 66)
Kamwanga – Sanya Juu (km 75)
Makambako – Songea (km 295)
Mtwara – Masasi (km 200)
Sanya Juu – Bomang’ombe (km 25)
Tabora – Mbambali – Bukene – Itobo – Kahama
(km 149)
Lupilo – Malinyi – Kilosa kwa Mpepo – Londo –
Kitanda (km 96)
Ifakara – Mahenge (km 67)
Kibondo – Mabamba (km 35)
Kolandoto – Lalago – Mwanhuzi – Matala –
Oldeani Jct (km 328)
Omugakorongo – Kigarama – Murongo (km 105)
Mpemba – Isongole (Tanzania/Malawi) (km 49)
Soni – Bumbuli – Dindira – Korogwe (km 74)
Makofia – Mlandizi – Vikumburu (km 148)
Kibaoni – Majimoto – Inyonga (km 162)
Mpanda – Ugala – Kaliua – Ulyankulu – Kahama
(km 428)
Makongolosi – Rungwa – Mkiwa (km 412)
Mtwara – Newala – Masasi (km 209)
50
Handeni – Kiberashi – Kondoa – Singida (km 460)
Kibaha – Mapinga (km 23)
Geita – Bukoli – Kahama (k m 107)
Mbande – Kongwa Jct – Mpwapwa (km 50)
Njombe – Makete (km 109)
Nata – Fort Ikoma (km 141)
Ipole – Koga – Mpanda (km 255)
Dsm (Port) – TAZARA – JNIA – Pugu (km 29)
Outer ring road (Pugu – Kinyerezi – Mbezi
(Morogoro) – Mpiji Magore – Bunju (km 34)
Barabara ya Dar es Salaam – Chalinze –
Morogoro (km 200)
Sehemu ya Dar es Salaam – Chalinze (km 100)
“Express way”
Musoma – Makojo – Busekela (km 92)
KAMATA – Bendera Tatu (km 1.3)
Ardhi – Makongo – Goba (km 9)
Daraja jipya la Selander (DSM)
Barabara ya Ar usha – Kibaya – Kongwa (km 430)
Barabara ya Nyamirembe Port – Katoke (km 50)
Barabara ya Murugarama – Rulenge – Nyakahura
(km 85)
Barabara ya Ipole – Rungwa (km 172)
Barabara ya Uongozi Institute (km 8.8)
Barabara ya Mwanangwa – Misasi – Salawe –
Kahama (k m 149)
(b) Madaraja
(i) Ujenzi wa daraja la Kilombero umeanza.
(ii) Ujenzi wa daraja la mto Mwatisi (Morogoro)
umekamilika.
(iii) Ujenzi wa daraja la mto Malagalasi Kigoma,
umekamilika.
51
(iv) Ujenzi wa daraja la Kigamboni ili kuunganisha
Kigamboni na Jiji la Dar es Salaam ume kamilika kwa
zaidi ya asilimia 80.
(v) Ujenzi wa daraja la Nangoo (M asasi), Ruhekei
(Mbinga) na Mbutu (Igunga) umekamilika.
(vi) Ujenzi wa d araja la Rusumo (Kagera) umekamilika .
(vii) Ujenzi wa d araja la waenda kwa miguu la Mabatini
(Mwanza) umekamilika.
(viii) Ujenzi wa daraja la Sibiti (Singida) unaendelea.
(ix) Upembuzi yakinifu na usanifu wa daraja la Ruhuhu
(Ruvuma) umekamilika.
(x) Ujenzi wa d araja la Kavuu (Katavi) unaendelea.
(c) Vivuko
Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA)
imenunua vivuko vinane kwa ajili ya kutoa huduma katika
maeneo mbalimbali Nchini.
(i) Msangamkuu (Mtwara)
(ii) Rusumo (Kagera) na
(iii) Ilagala (Kigoma)
(iv) Kahunda – Maisome
(v) Kahunda – Musoma – Kinesi
(vi) Kahunda – Kisorya – Rugezi
(vii) Dar es Salaam – Bagamoyo
(d) Kupunguza Msongamano katika Jiji la Dar es Salaam
Ili kupunguza mson gamano wa magari katika Jiji la Dar es
Salaam, Serikali imefanya mambo yafuatayo: –
(i) Usanifu wa kina umekamilika kwa makutano ya TAZARA
na Ubungo kwa ajili ya kujenga barabara za juu ; na
(ii) Serikali inaendelea kupanua mtandao wa barabara kwa
kujenga na kukara bati barabara zifuatazo: –
Mbezi (Morogoro road) – Malambamawili –
Kinyerezi – Banana (km 14.0)
Tegeta Kibaoni – Wazo – Goba – Mbezi mwisho
(km 20.0)
52
Tangi Bovu – Goba (km 9.0)
Kimara – Baruti – Msewe – Changanyikeni (km
2.6)
Kimara – Kilungule – External M andela road (km
9.0)
Ubungo Bus Terminal – Mabibo – Kigogo Round
about (km 6.4)
Kigogo Round about – Bonde la Msimbazi –
Twiga/Msimbazi (km 2.7)
Tabata Dampo – Kigogo – Ubungo Maziwa (km
2.25)
Old Bagamoyo – Garden Road (km 9.0) Usanifu
umekamilika
Jet Co rner – Vituka – Devis C orner (km 6) ujenzi
umekamilika
(iii) Ujenzi wa awamu ya kwanza ya miundombinu ya
mabasi yaendayo haraka (Bus Rapid Transit – BRT):
Kimara – Kivukoni, Fire -Kariakoo na Magomeni –
Morocco (km 20.9) unaendelea.
39. Katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2020, Chama Cha
Mapinduzi kitaielekeza Serikali kuendelea kutekeleza miradi ya
ujenzi wa barabara na madaraja, vivuko, nyumba na majengo
ya Serikali kwa lengo la kuongeza kasi ya maendeleo ya
kiuchumi na huduma za kijamii . Aidha, kipaumbele katika
ujenzi wa barabara ki tazingatia barabara zinazounganisha nchi
yetu na nchi jirani; barabara zinazounganisha mikoa; na
barabara zinazokwenda kwenye maeneo y enye fursa za
kiuchumi kama vile Liganga, Mchuchuma n.k. Ili kutimiza
azma hiyo Serikali itafanya mamb o yafuatayo: –
(a) Kuimarisha Mfuko wa Barabara (Tanzania Road Fund)
(i) Kubuni vyanzo vipya na kuimarisha ukusanyaji wa
mapato yatokanayo na vyanzo vya sasa ili kuongeza
mapato ;
53
(ii) Kubuni/kuboresha mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ili
kuhakikisha kwamba thamani na ubora wa kazi
unaendana na fedha zilizotumika (value for money) ; na
(iii) Kuanzisha wakala/taasisi itakayosimamia kazi za ujenzi
na matengenezo ya barabara za miji na majiji na
Halmashauri ambazo ziko chini ya TAMISEMI.
(b) Masuala ya Kisera
Ili kupunguza umas ikini, kuwawezesha wananchi kiuchumi na
kuongeza kasi ya maendeleo, Serikali itashughulikia masuala
yafuatayo: –
(i) Kuunganisha makao makuu ya mikoa ambayo bado
haijaunganishwa kwa barabara za lami na kujenga
barabara kuu zote zinazounganisha Tanzania na nchi
jirani kwa kiwango cha lami ;
(ii) Kuhakikisha kuwa makao makuu ya Wilaya ambaz o bado
barabara zake hazipitiki majira yote zinafanyiwa ukarabati
angalau kwa kiwango cha changarawe na kuzifanya
zipitike majira yote ya mwaka ;
(iii) Kupunguza umaskini kwa kushirikisha kikamil ifu vikundi
vya wananchi katika kazi za matengenezo madogo
madogo ya barabara kama vile kazi za kufyeka nyasi,
kuzibua mifereji na kufanya usafi wa barabara zinazopita
katika maeneo yao ; na
(iv) Makandarasi wazalendo wanaoonesha nia ya kushiriki
katika kazi kub wa za ujenzi wa barabara watapatiwa
dhamana na Serikali ili kuwajengea uwezo na kuwapatia
fursa za kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za sekta ya
ujenzi.
(c) Kukamilisha ukarabati wa barabara zote unaoendelea na
ujenzi kwa kiwango cha lami ambao umekwishaanz a
katika barabara kuu na barabara za mikoa: –
(i) Kukamilisha Ujenzi (km 2 ,439.35)
Sumbawanga – Matai – Kasanga (km 56 kati ya km
112)
54
Mziha – Turiani – Magole (km 75 kati ya km 84.6)
Dumila – Kilosa ( km 18 kati ya km 63)
Dumila – Turiani – Handeni (km 174)
Bariadi – Lamadi (km 13 kati ya km 71.8)
Mbeya – Chunya – Makongolosi (km 56 kati ya km
115)
Bagamoyo – Makofia – Msata (km 7 kati ya km 64)
Kisarawe – Maneromango (km 48 kati ya km 54)
Kibosho Shine – Kwa Raphael – International
School (km 24 kati ya km 4 3)
Kirua – Nduoni – Marangu Mtoni (km 16 kati ya km
31.5)
Nyamuswa – Bunda – Kisorya – Nansio (km 117 kati
ya km 117.5)
Babati – Dodoma (km 195.15 kati ya km 251)
Sumbawanga – Kanyani – Nyakanazi (km 483.7 kati
ya km 562)
Nzega – Tabora (Puge) (km 20.5 kat i ya km 116)
Manyoni – Itigi – Tabora (km 113 kati ya km 264)
Mangaka – Mtambaswala ( km 65)
Makutano – Nata – Mugumu (km 125)
Kyaka – Bugene (km 28 kati ya km 59)
Tunduru – Namtumbo (km 194)
Tunduru – Mangaka (km 137)
Mwigumbi – Maswa – Bariadi (100)
Tabora – Urambo (km 8.8 kati ya km 90)
Uyovu – Bwanga – Biharamulo (km 112)
Kisesa – Usagara (km 17)
Mganza – Kasenda (km 4.2)
Katumba – Mbambo – Tukuyu (km 80)
Kidahwe – Kasulu (Kanyani) (km 50)
Kikusya – Ipinda – Matema Beach (km 39.5)
KIA – Mererani (km 26 )
55
Mwanga – Kikweni – Lomo (km 7.5 kati ya km
22.5)
Kaliua – Kazilambwa (km 42 kati ya km 56)
Singida – Sepuka – Ndago – Kizaga (75 kati ya km
89)
Dodoma University Road (km 12)
(ii) Kukamilisha Ukarabati (km 517.2)
Ushirombo – Lusahunga ( km 67 kati ya km 110)
Kawawa Jct – Mwenge (km 4.3)
Segera – Same – Himo (km 131 kati ya 285)
Nyanguge – Musoma – Sirari (km 177 kati ya km
262)
Mafinga – Igawa (km 137.9)
(d) Kuanza ujenzi mpya na ukarabati wa barabara kwa
kiwango cha lami
(i) Kuanza ujenzi ( km 5 ,427.0 )
Njombe – Makete (km 109)
Nata – Fort Ikoma (km 30)
Mto wa Mbu – Loliondo (km 213)
Sanya Juu – Bomang’ombe (km 25)
Tabora – Ipole – Koga – Mpanda (km 359)
Matai – Kasesya (km 50)
Sanya Juu – Kamwanga (km 75)
Rujewa – Madibila – Mafinga(km 151)
Makurunge – Saadani – Pangani – Tanga (km 178)
Mbinga – Mbamba bay (km 66)
Mtwara – Mingoyo – Masasi (km 200)
Mpemba – Isongole (Tanzania/Malawi) (km 49)
Makongolosi – Rungwa – Mkiwa (km 412)
Mtwara – Newala – Masasi (km 209)
Kibaha – Mapinga (km 23)
Geita – Bukoli – Kahama (km 107)
Mbande – Kongwa Jct – Mpwapwa (km 50)
56
Ipole – Rungwa (km 172)
Njombe (Kibena) – Lupembe – Madeke (Mfuji)
Morogoro/Njombe Boarder (km 125)
Njombe – Ndulamo – Makete – Kitulo – Isyonje(km 205)
Itoni – Ludewa – Manda (km 211)
Dar e s Salaam – Chalinze – Morogoro express way (km
190)
Musoma – Makojo – Busekera (km 92)
Tabora – Mambali – Bukene – Itobo – Kahama (km 149)
Lupilo – Malinyi – Kilosa kwa Mpepo – Londo – Kitanda
(km 296)
Ifakara – Mahenge (km 67)
Kibondo – Mabamba (km 35)
Kolandoto – Lalago – Mwanhuzi – Matala – Oldeani Jct
(km 328)
Mugakorongo – Kigarama – Murongo (km 105)
Soni – Bumbuli – Dindira – Korogwe (km 74)
Makofia – Mlandizi – Vikumburu (km 148)
Handeni – Kiberashi – Kondoa – Singida (km 460)
Pugu – Kifuru – Mbezi M wisho – Mpiji Magoe – Bunju
(km 34)
Kisarawe – Mlandizi (km 52)
Kiboroloni – Tsuduni – Kidia (km 10.8)
TPC – Mabogini – Kahe (km 11.4)
Nyamirembe Port – Katoke (km 50)
Iringa – Ruaha National Park (km 104)
Njombe (Ramadhani) – Iyayi (km 74)
Mziha – Handen i (km 68)
Kilosa – Mikumi (km 72.8)
(ii) Kuanza Ukarabati (km 1055.12)
Arusha – Moshi – Himo-Holili (km 140)
Makambako – Songea (km 295)
Mtwara – Mingoyo – Masasi (km 200)
Lusahunga – Rusumo (km 92)
57
Nyakasanza – Kobero (km 60)
Mlandizi – Chalinze (km 53)
Mbeya -Tunduma (km 110)
Igawa – Uyole (km 105.12)
(e) Kuzifanyia upembuzi na usanifu wa kina km 6,530.7
barabara zifuatazo :-
Kibaoni – Majimoto – Inyonga (km 162)
Mpanda – Ugala – Kaliua – Ulyankulu – Kahama (km 428)
Arusha – Kibaya – Kongwa (km 430)
Bugene – Kasulo (BENACO) (km 124)
Mbeya – Igawa (km 116)
Mbeya – Tunduma (km104)
Murshaka – Murongo (km 125)
Kilindoni – Ras M kumbi (km 55) – Mafia
Morogoro – Dodoma (km 263)
Mwanza – Mwanza/Shinyanga (km 102)
Mwanangwa – Misasi – Salawe – Kahama (km 149)
Kibaoni – Majimoto – Kasansa – Muze – Kilyamatundu (km
200)
Magu – Bukwimba – Ngudu – Jojiro (km 64)
Tarime – Mugumu (km 87)
Njombe – Iyayi (km 74)
Amani – Muheza (km 34)
Nyahunge – Sengerema (km 68)
Mugakorongo – Rwambaizi – Murongo (km 125)
Morogoro (Bigwa) – Mvuha (km 78)
Morogoro Kibena -Lupembe -Mfuji (Morogoro/Njombe
Boarder) (km 125)
(Bigwa) – Kisaki (km 151)
Kamanga – Sengerema (km 35) (Mwanza)
Geita – Nzera – Nkome (km 54) (Geita)
Upanuzi wa (Tegeta) – Bagamoyo (km 57)
Kibada – Kimbiji (km 29.2)
Murugaram a – Rulenge – Nyakahura (km 85)
58
Karatu – Mbulu – Haydom – Singida (km 190)
Bariadi -Kisesa -Mwandoya -Ngoboko -Mwanhuzi -Sibiti-
Mkalama -Iguguno (km 289)
Mika – Utegi – Shirati (km 44)
Chimala – Matamba – Kitulo (km 51)
Upanuzi wa Kitonga Escarpment (km 10) (Ir inga)
Babati – Orkesumet – Kibaya (km 225)
Kongwa – Mbuyuni NARCO JCT – Kibaya – Orkemet (km
340)
Mbulu – Magugu (Mbuyu wa Mjerumani) (km 63)
Mafinga – Mgololo (km 77.6)
Nyololo – Igowole – Mtwango (km 40.4)
Igowole – Kasanga – Nyigo (km 54.5)
Madaba – Mundindi (Liganga) – Mkiu (km 46) (Ruvuma)
Kilwa – Liwale (km 258)
Liwale – Nachingwea – Ruangwa (185)
Kitai – Lituhi (km 93)
Babati (Dareda) – Dongobesh (km 60)
Mhutwe – Kamachumu – Muleba (km 53)
Uru – Mamboleo – Materuni (km 10.2)
Kongwa Ranch – Kiteto – Simanjiro – KIA (km 483)
Mto wa Mbu – Longido – Karatu – Ngoro ngoro (km 300 )
Sanya Juu – Longido (km 65)
Madaba – Mavanga – Ludewa (km 40)
Likuyufusi – Mkenda (km 124)
(f) Madaraja
(i) Kukamilisha ujenzi wa madaraja sita (6) yafuatayo :-
Kilombero na barabara za maingilio km 9
Kigamboni na barabara za maingilio km 10
Kavuu (Katavi)
Sibiti (Singida)
Lukuledi II (Lindi)
Ruvu Chini (Pwani)
59
(ii) Kuanza ujenzi / Ukarabati wa madaraja saba (7)
yafuatayo :-
Ruhuhu (Ruvuma)
Momba (Rukwa)
Kirumi (Mara)
Selander (daraja jipy a) (DSM)
Magara (Manyara)
Wami Chini (daraja jipya) (Pwani)
Pangani (Tanga)
(iii) Kuanza usanifu wa madaraja matatu (3) yafuatayo :-
Daraja la Simiyu (Mwanza)
Mzinga (DSM) na
Mlalakuwa (DSM )
60
Muonekano wa Daraja la Kigamboni litakapokuwa limekamilika kujengwa .
Ujenzi umekamilika zaidi ya asilimia 80.
(g) Kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar Es
Salaam kwa kufanya yafuatayo :-
Kuanza ujenzi wa barabara za juu (Flyovers) kwenye
makutano ya barabara maeneo yafuatayo: –
TAZARA
Ubungo
Chang’ombe
Uhasibu
KAMATA
61
Morocco
Mwenge
Magomeni
Tabata
Kuanza na k ukamilisha ujenzi wa barabara na reli ili
kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es
Salaam: –
(i) Kukamilisha Ujenzi (km 80.1)
Mbezi – Malamba Mawili – Kinyerezi – Banana ( km 14)
Tegeta Ki baoni – Wazo Hill – Goba – Mbezi/Morogoro R oad
(km 16.2 kati ya km 20)
Tangi Bovu – Goba (km 5.2 kati ya km 9)
Kimara Baruti – Msewe – Changanyikeni (km 2 kati ya 2.6)
Kimara Kilungule – External Mandela Road (km 8.8 kati ya
9)
Kigogo Round About – Bonde la Msimbazi –
Twiga/Msimbazi Jct.km(km 0.5 kati km 2.7)
Tabata Dampo – Kigogo (km 1.6 kati ya km 2.25)
Kibamba – Mlonganzila (km 8 kati ya km 12
Upanuzi wa Kimara – Kibaha na Madaraja ya Kibamba,
Kiluvya na Mpiji (km 23.8 kati ya km 25)
(ii) Kuanza Ujenzi (km 58.8)
Upanuzi wa Mwai Kibaki (Morocco – Kawe Round About)
na Garden Road ( km 9.1)
Banana – Kitunda – Kivule – Msongola (km 14.7)
Ardhi – Makongo – Goba (km 9)
Upanuzi wa barabara ya Uwanja wa N dege ( JNIA) – Pugu
(km 8)
Upanuzi wa barabara ya Mbagala – Kongowe – Mwandege
(km 4)
Upanuzi wa barabara ya DSM Port -TAZARA – Uwanja wa
Ndege ( JNIA) (km 14)
62
(iii) Kuanza ujenzi wa miundombinu ya mradi wa mabasi
yaendayo haraka (BRT) Awamu ya Pili (II) na ya T atu
(III): –
Awamu ya II: Barabara ya Kilwa na Kawawa (km 19 .3)
Awamu ya III: Barabara za Nyerere, Uhuru, Bibi Titi
Mohamed na
Azikiwe (Km 23.6)
(iv) Kuanza ujenzi wa reli ya usafirishaji wa abiria katika
jiji la Dar es Salaam.
(h) Miradi ya kupunguza msongamano katika majiji na miji
mingine yenye jumla ya km 102 ka ma ifuatavyo: –
Usagara – Kisesa (km 17) (Mwanza)
Shabiby – Arusha r oad Round about (km 1.6) (Dodoma),
Uyole – Songwe (km 40) (Mbeya)
Iringa Bypass (km 7)
Upanuzi wa barabara Mwanza – Mwanza Airport (km12),
Upanuzi wa Babara ya Arusha Mjini – Kisongo (km 8. 8),
Babati Bypass (km. 12)
Utofu – Majani Mapana – Duga Mwembeni (km 4) (Tanga)
(i) Vivuko
Kuimarisha usafiri wa majini katika mito, maziwa na bahari ili
kufanya barabara kuwa na kiunganishi cha uhakika kwa
kutekeleza miradi ifuatayo: –
(i) Ujenzi wa kivuko kipya c ha Kigongo – Busisi Mkoani
Mwanza ;
(ii) Kuanza ujenzi wa kivuko kipya cha Rugezi – Kisorya
mkoani Mwanza ;
(iii) Kuanza ujenzi wa kivuko kipya cha Pangani – Bweni
mkoani Tanga ;
(iv) Upanuzi wa jengo la abiria wa kivuko cha Magogoni –
Kigamboni upande wa Kigamboni ; na
(v) Kuanz a ujenzi wa Kivuko kipya cha Magogoni –
Kigamboni .
63
Uchukuzi
40. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali imeendelea kuchukua
hatua mbalimbali za kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji wa reli,
majini na usafiri wa anga na mafanikio yafuatayo y amepatikana: –
(a) Mashirika ya Reli
(i) Shirika la Reli nchini (TRL) limeendelea kuimarishwa
kwa kufanya yafuatayo: –
Kununua na kukarabati vifaa mbalimbali (vichwa
vya treni, mataruma, na mitambo ya kunyanyulia
mabehewa) ;
Kutandika reli z a ratili 80 kwa yadi kutoka Kitaraka
hadi Malongwe (kilometa 89) ;
Ujenzi wa Madaraja makubwa matatu ya stesheni
za Kilosa na Gulwe; na stesheni za Bahi na
Kintinku ; na
(ii) Kwa upande wa shirika la TAZARA, v ichwa vya treni
vya njia kuu vipya sita (6); mabehew a ya mizigo 90;
vipuri vya matengenezo ya vichwa vya treni vitatu
(3); na ukarabati wa mitambo ya kunyanyulia mizigo
vinne ( 4) vimenunuliwa na ukarabati umefanyika .
Aidha, mazungumzo kati ya Serikali ya Tanzania na
Zambia yanaendelea ili kuboresha shirika hilo.
(b) Ujenzi wa Reli Mpya
Upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa Reli mpya ya Dar es
Salaam -Kigali (Rwanda) na Msongati (Burundi) kwa kiwango
cha kimataifa (standard gauge) umekamilika. Aidha,
upembuzi yakinifu na usanifu kwa ajili ya ujenzi wa reli kwa
kiwango cha kimataifa kutok a Isaka hadi Mwanza
umekamilika.
(c) Bandari
(i) Huduma za uchukuzi kwenye maziwa zimeendelea
kuimarishwa kwa kuboresha bandari za Kigoma, Mbamba
Bay, Mwanza, Bukoba na Nansio; ikiwa ni pamoja na
kuondoa mchanga katika bandari ya Kig oma, kukarabati
64
chelezo, kufunga maboya ya kuongozea meli, kununua
Mobile Grove Crane tani 35, kununua mtambo wa
kuondoa mchanga majini (dreadger) na upembuzi
yakinifu wa Bandari Kavu ya Katosha. Aidha, uthamini wa
eneo la Kibirizi kwa ajili ya kujenga mae gesho ya vyombo
vidogo vidogo vya majini umekamilika ;
(ii) Bandari ya Dar es Salaam imeende lea kuboreshwa ikiwa
ni pamoja na ujenzi wa boy a la mafuta (SPM) na ununuzi
wa vifaa vya kuhudumia mizigo. Aidha, upembuzi yakinifu
wa kuboresha gati namba 1 -7 na utafiti wa ujenzi wa gati
(RoRo) kwa ajili ya kuhudumia meli za magari; ujenzi wa
mfumo wa kuhamisha mizigo ( conveyor system ) na
maghala (silo) kwa ajili ya kuhudumia shehena ya Kichele
umekamilika.
(iii) Eneo la Msanga Mkuu lenye hekta 2,623 kwa ajili ya
uendelezaji w a Bandari ya Mtwara na shughuli za EPZ
limetengwa na kazi ya upembuzi yakinifu kwa ajili ya
ujenzi wa Bandari hiyo umekamilika ; na
(iv) Ujenzi wa gati jipya la kisasa katika bandari ya Kilindoni –
Mafia umekamilika.
(d) Viwanja vya Ndege
(i) Upembuzi yakinifu na usani fu wa kina kwa ajili ya
kuboresha na kupanua jengo la pili la abiria katika
Kiwanja cha Kimataifa cha Julius Nyerere umekamilika ;
(ii) Ujenzi wa Kiwanja cha N dege cha Kimataifa cha
Songwe umekamilika na kuanza kutoa huduma za
usafiri wa anga. Aidha, ujenzi wa j engo kubwa la abiria
na uzio wa kiwanja unaendelea kukamilishwa ;
(iii) Upembuzi yakinifu wa ujenzi wa Kiwanja cha N dege
cha Mtwara umekamilika. Aidha, matengenezo katika
jengo la abiria na barabara ya kurukia na kutua ndege
umekamilika ;
(iv) Mradi wa kuboresha Kiwanj a cha N dege cha Kigoma
awamu ya kwanza umekamilika. Aidha, upanuzi na
65
ukarabati wa kiwanja hicho awamu ya pili chini ya
ufadhili wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya umekamilika ;
(v) Kazi za upanuzi na ukarabati wa Kiwanja cha N dege
cha Bukoba kwa kiwango cha lami k wenye barabara ya
kuruka na kutua ndege; barabara ya kiungo na
maegesho ya magari imekamilika. Aidha, ujenzi wa
jengo la abiria lipo katika hatua za mwisho za ujenzi ;
na
(vi) Ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Mafia
kwa kiwango cha lami umekamilika.
(e) Hali ya Hewa
Utambuzi wa hali ya hewa ni muhimu kwa shughuli za
kiuchumi zikiwemo za kilimo, uvuvi, usafiri hususan usafiri
wa anga na majini. Utambuzi wa hali ya hewa ni muhimu pia
kwa shughuli nyingine za kijamii ikiwa ni pamoja na kuweka
tahadhari za majanga. Ili kuimarisha huduma za utambuzi
wa hali ya hewa, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita,
yamefanyika mambo yafuatayo: –
(i) Rada mbili za utabiri wa hali ya hewa zenye ubora wa
kimataifa zimenunuliwa na kufungwa katika Mikoa ya
Dar es Salaam na Mwanza ;
(ii) Kituo cha kutoa taarifa za hali ya hewa kwa watumiaji
wa maeneo ya Ziwa Victoria kimeanzishwa mkoani
Mwanza. Ili kuhakikisha kwamba taarifa za hali ya
hewa zinawafikia wananchi na wadau wengine kwa
wakati, taarifa za hali ya hewa sasa zinatolewa
kwenye vyombo vya habari vikiwemo simu na
mitandao ya kijamii ; na
(iii) Vituo vitatu vya hali ya hewa (synoptic stations) vya
Kilwa Masoko, Mpandeni Songwe vimeanza kufanya
kazi. Aidha, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa
Kituo Kikuu cha H ali ya Hewa umekamil ika.
66
41. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Chama Cha Mapinduzi
kitaielekeza Serikali kufanya mambo yafuatayo: –
Miundombinu ya Huduma za Reli
(a) Kwa kushirikiana na sekta binafisi kuanza ujenzi wa reli
zifuatazo kwa kiwango cha kimataifa (standard gauge): –
(i) Dar es Salaam – Tabora – Kigoma/Mwanza
(ii) Uvinza – Msongati (Burundi) na Isaka – Kigali (Rwanda)
(iii) Mtwara – Songea – Mbamba Bay na matawi ya kwenda
Mchuchuma na Liganga
(iv) Tanga – Arusha – Musoma
(v) Kaliua – Mpanda – Karema
(b) Kuijengea uwezo Kampuni ya Reli Tanzania k wa kuongeza
idadi ya vichwa vya treni, mabehewa ya mizigo na abiria ili
kuimarisha utendaji wake ikiwa ni pamoja na kuimarisha
karakana za Morogoro, Tabora na Dar es Salaam ;
(c) Kukamilisha Sheria mpya ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na
Zambia (TAZARA) itakayos aidia kubadilisha mfumo wa
uendeshaji wa Shirika kwa lengo la kub oresha huduma za
abiria na mizigo ; na
(d) Kuendelea kuboresha usafiri wa reli jijini Dar es Salaam kwa
lengo la kupunguza msongamano.
Usafiri wa Majini
Kwa kushirikiana na sekta binafsi , kuendele a kuboresha huduma za uchukuzi
katika Bandari za mwambao kwa kufanya yatuatayo: –
(a) Kuanza ujenzi wa gati Na. 13 na 14 katika Bandari ya Dar es Salaam ;
(b) Kukamilisha uboreshaji wa gati Na. 1 – 7 ili kuimarisha utoaji wa
huduma katika Bandari ya Dar es Salaam ;
(c) Kuanza ujenzi wa gati la kushusha magari (RoRo) katika Bandari ya
Dar es Salaam ;
(d) Kuanza ujenzi wa bandari mpya z a Bagamoyo na Mwambani Tanga ;
(e) Kuanza na kukamilisha ujenzi wa magati manne ( 4) ya ziada katika
Bandari ya Mtwara ;
67
(f) Kukamilisha ujenzi wa Bandari ya Nyamisati ili kuboresha usafirishaji
wa kwenda na kutoka Mafia ;
(g) Kuendelea kuboresha Bandari ya Mwanza, upanuzi wa Bandari ya
Musoma na ujenzi wa magati ya Ntama, Lushamba na Kiyamkwiki ;
(h) Kuendelea na uboreshaji wa miundombinu ya bandari za Ziwa Nyasa
na Tanganyika ili kuimarisha huduma zitolewazo kwa kujenga magati
ya Kagunga, Kasanga, Kibirizi, Itungi na Kiwira ;
(i) Kuboresha mfumo wa uondoshaji mizigo katika Bandari ya Dar es
Salaam kwa lengo la kuongeza kiwango cha utendaji kwa kuweka
mfumo wa “electronic window System” na kufunga mita za kupima
mafuta ; na
(j) Kujenga na kukamilisha meli mbili za abiria na mizigo katika Ziwa
Tanganyika, meli moja ya abiria na mizigo katika Ziwa Victoria na meli
nyingine ya abiria na mizigo katika Ziwa Nyasa.
Usafiri wa Anga
Kwa kushirikiana na sekta binafsi , kuendelea kubor esha huduma za usafiri wa
anga kwa kufanya yatuatayo: –
(a) Kukamilisha mpango kabambe wa usafiri wa anga ;
(b) Kukamilish a ujenzi wa awamu ya kwanza ya Jengo la T atu la Abiria
(Terminal III) katika Kiwanja cha Ndege c ha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNIA) na kua nza ujenzi wa awamu ya pili ya Jengo la T atu la
JNIA;
(c) Kuanza na kukamilisha ujenzi vya Viwanja vya Ndege vya Shinyanga
na Sumbawanga kwa ku karabati barabara ya kutua na kuruka ndege
kwa kiwango cha lami ;
(d) Kujenga na kukamilisha awamu ya pili ya Viwanja vya N dege vya
Tabora na Kigoma ;
(e) Kuanza ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Msalato kwa kiwango cha
Kimataifa ;
(f) Kukamilisha upanuzi wa K iwanja cha Ndege cha Mwanza hususan
jengo la abiria na kufikia kiwango cha kimataifa ;
(g) Kuanza awamu ya pili ya mradi wa ujenzi , ukarabati na upanuzi wa
Viwanja vya N dege kumi na moja ( 11) vya mikoa vilivyofanyiwa
68
upembuzi yakinifu na usanifu wa kina vya Lindi, Kilwa Masoko,
Songea, Singida, Lake Manyara, Tanga, Iringa, Njombe, Simiyu,
Musoma na Moshi ; na
(h) Kuhamasisha uwekezaji wa Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) ili
kuimarisha huduma za Shirika la N dege la Taifa.
Huduma za Hali ya Hewa
Kuendelea kuboresha huduma za hali ya hewa kwa kufanya yatuatayo: –
(a) Kuanza ujenzi wa kituo kikuu cha utab iri wa hali ya hewa nchini ;
na
(b) Kuendelea ku boresha huduma za hali ya hewa nchini ili kufikia
kiwango cha kimataifa kwa kununua rada za hali ya hewa
zisizopungua tano.
Nishati
42. Kwa kutambua umuhimu wa nishati kwa maendeleo ya Taifa, katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali imechukua hatua za
kuhakikisha kuwa nishati ya kutosha inapatikana kwa lengo la kukidhi
mahitaji ya viwanda, taasisi zinazotoa huduma na wananchi kwa ujumla.
Nguvu kubwa imeelekezwa katika kuhakiki sha kwamba nishati ya
umeme ina sambazwa kwa gharama nafuu ili kuwaletea unafuu wa
maisha wananchi hasa wale wanaoishi maeneo ya vijij ini. Katika
kutimiza azma hiyo: –
(a) Mipango ya kuunganisha g ridi ya T aifa na nchi jirani imeendelea
kutekelezwa kwa lengo la ku imarisha biashara ya umeme. Miradi
muhimu ambayo utekelezaji wake unaendelea ni pamoja na: –
(i) Mradi wa Rusumo wa megawati 80 kwa ajili ya Rwanda –
Burundi -Tanzania ;
(ii) Mradi wa usafirishaji umeme wa gridi ya Kaskazini -Mashariki wa
usafirishaji umeme kati ya Ethiopia -Kenya –Tanzania ; na
(iii) Mradi wa Zambia – Tanzania -Kenya (ZTK Interconnector).
(b) Kiwango cha uunganishwaji umeme kwenye Mikoa na Wilaya ambako
gridi ya Taifa haijafika nchini kimeongezeka kutoka asilimia 5 mwaka
2010 hadi asilimia 36 mwaka 2015. Aidha, kiwango cha uunganishwaji
umeme v ijijini kimeongezeka kutoka asilimia 5 mwaka 2010 hadi
69
asilimia 7 mwaka 2014 kupitia utekelezaji wa awamu ya kwanza ya
Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini wenye miradi midogo 41
katika mikoa 16 ya Tanzania Bara (Arusha, Dodoma, Kagera, Kigoma,
Kilima njaro, Manyara, Mara, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Pw ani,
Rukwa, Shinyanga, Singida, Tabora na Tanga) ambapo jumla ya
wateja wapya 209,237 wameunganishiwa umeme hadi kufikia
Disemba, 2014;
(c) Ukiritimba wa TANESCO wa kuwa mzalishaji na msambazaji pekee wa
umeme umeondolewa na sasa sekta binafsi imeruhusiwa kushiriki
katika kuzalisha, kusambaza na kuuza umeme ;
(d) Ujenzi wa bomba la gesi lenye urefu wa km 542 kutoka Mnazi Bay
(Mtwara) hadi Dar es Salaam umekamilika. Aidha, ujenzi wa vituo vya
kupokelea gesi katika eneo la Somanga Fungu, Kinyerezi Dar es
Salaam na Tegeta umefikia wastani wa asilimia 96 ;
(e) Jumla ya futi za ujazo trilioni 55.08 za gesi imegunduliwa nchini hadi
kufikia mwaka 2015 ;
(f) Jumla ya nyumba za makazi 812, nyumba za ibada 27, shule 6 na
zahanati 8 zimepatiwa umeme wa jua pamoja na jumla ya taa za
mitaani 200 katika vijiji 10 kutoka Wilaya za Mlele, Kongwa na Uyui
kupitia M radi wa Maendeleo ya Nishati (Tanzania Energy Development
and Access Expansion – TEDAP ); na
(g) Mradi wa usambazaji gesi asilia kati ka Jiji la Dar es Salaam ili kukidhi
mahitaji ya sekta mbalimbali umeshaanza ambapo maandalizi ya ujenzi
wa miundombinu ya kusambaza gesi yamekamilika na kwa sasa
shughuli za upanuzi zinaendelea.
43. Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani ya 2015 –2020, Chama
Cha Mapinduzi kitaielekeza Serikali kuongeza kwa kiwango
kikubwa uzalishaji wa nishati ili kuendelea kukuza Sekta hiyo
na kuongeza mchango wake kwenye Pato la Taifa kwa
kutekeleza yafuatayo: –
Umeme
(a) Kuongeza uzalishaji wa umeme ili kuhakikisha wananchi
wanafikiwa na huduma hi i kuling ana na Sera ya Nishati ya Taifa .
70
Kwa kutekeleza miradi iliyoa inishwa kwenye Mpango Kabambe wa
Kuendeleza Sekta ya Umeme (Power System Master Plan – 2009-
2033) ili kukidhi mahitaji ya umeme nchini , kipaumbele kitatolewa
katika r asilimali za makaa ya mawe, maji (hydro), gesi asilia na
nishati jadidifu (renewable energy) ambapo lengo ni kufikia MW
4,915 mwaka 2020 kutoka MW 1,308 mwaka 2015 ; na
(b) Kukamilisha na kuimarisha mtandao wa usafirishaji na usambazaji
umeme ( National Grid ) unaounganisha nchi nzima kwa kutekeleza
miradi mikubwa ya ujenzi wa njia za kusafirisha umeme kwa ajili
ya kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika maeneo
mengi ya nchi yetu. Miradi hiyo ni pamoja na: –
(i) Mradi wa Backbone wa kV 400 unaounganisha mik oa ya
Iringa, Dodoma, Singida na Shinyanga wenye urefu wa km
670;
(ii) Mradi wa Makambako -Songea wa kV 220, ambao
unaunganisha mikoa ya Iringa, Njombe na Ruvuma km 250 ;
na
(iii) Mradi wa Kaskazini -Mashariki (North -East) unaounganisha
mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, K ilimanjaro na Arusha.
Aidha, mradi mwingine muhimu ni ule wa Kaskazini -Magharibi
(North -West), ambao unaunganisha mikoa ya Mbeya, Katavi,
Rukwa na Kigoma.
(c) Kuendelea kusambaza umeme wenye uhakika mijini na vijijini kwa
kufanya yafuatayo: –
(i) Kuendelea kuong eza bajeti ya Wakala wa Kusambaza
Umeme Vijijini ( REA) ili kuhakikisha upatikanaji wa umeme
wenye uhakika ;
(ii) Kukamilisha utekelezaji wa awamu ya pili ya mpango
kabambe wa kupeleka umeme vijijini (REA Turn -Key
Projects Phase II) yenye lengo la kuunganisha wat eja
250,000 utakapokamilika ; na
(iii) Kuanzisha REA (III) ambayo ina malengo yaafuatayo: –
71
Kuongeza wigo wa usambazaji umeme kutoka REA I
na II zilipoishia ;
Kufikisha umeme kwenye shule zote za sekondari,
hospitali na vyanzo vya maji ;
Kuongeza idadi ya vijiji ambavyo vinafikiwa na umeme ;
na
Kupeleka umeme maeneo yote ambayo si tija kwa
TANESCO kuwekeza.
(iv) Kuongeza k iwango cha uunganishaji umeme (connection
level) kutoka asilimia 36 mwaka 2015 hadi asilimia 60
ifikapo mwaka 2020 ; na
(v) Kutekeleza miradi ya kuungani sha gridi ya Taifa na gridi
za nchi jirani ambapo m iradi ya Zambia -Tanzania -Kenya ,
Burundi -Rwanda -Tanzania na Tanzania -Kenya -Ethiopia
itahusika .
Mafuta na Gesi Asilia
44. Kwa kuzingatia ugunduzi wa kiwango kikubwa cha gesi asilia
na matarajio ya upatikanaji w a mafuta, Chama Cha Mapinduzi
kitaendelea kuielekeza Serikali kusimamia sekta hii kwa
kuzingatia Sera na Sheria mbalimbali zilizopo zitakazowezesha
nchi kunufaika na rasilimali hii muhimu kwa uchumi wa nchi
yetu. Pamoja na kutekeleza Sera na Sheria hizo, m alengo
muhimu katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2020 ni pamoja
na:-
(a) Kuwezesha na kusimamia ujenzi wa miundombinu muhimu ya
gesi asilia na mafuta nchini pamoja na kukamilisha Mpango
Kabambe wa Matumizi ya Gesi Asilia (Natural Gas Utilisation
Master Plan );
(b) Kuhakikisha wananchi wanaopakana na miundombinu ya gesi
na ambako bomba la gesi linapita wanashiriki na kunufaika na
gesi;
(c) Kuwawezesha wananchi kwa ujumla washiriki na wanufaike
na fursa zinazotokana na uchumi wa gesi ;
72
(d) Kuendeleza mradi wa kugeuza gesi kuwa katika hali ya
vimiminika (Lique fied Natural Gas – LNG) ili kuwezesha mauzo
ya gesi asilia ndani na nje ya nchi ;
(e) Kuhamasisha na kuwawezesha wananchi kushiriki katika sekta
ndogo ya mafuta na gesi kwa kuzingatia Sera na Sheria
zilizopo ;
(f) Kuendelea kuhamasis ha utafutaji wa mafuta na gesi asilia ;
(g) Kuendelea kusomesha vijana wa Kitanzania katika ngazi
mbalimbali za vyuo vikuu, VETA , kulingana na mahi taji ya
rasilimali watu katika Sekta ya Mafuta na Gesi; na
(h) Kuendelea kusimamia ujenzi wa miundombinu muhimu ya
mafuta na gesi nchini ili kuleta ufanisi na tija katika kuvuna na
kutumia mafuta na gesi asilia.
(i) Kwa kutambua umuhimu wa nishati ya mafuta, Serikali: –
(i) Itahakikisha hifadhi za kimkakati zenye uwezo wa
kukidhi mahitaji ya mafuta kwa nchi yetu na nchi
jirani zinajengwa Dar es Salaam , Tanga na
Zanzibar ;
(ii) Itahamasisha sekta binafsi kutumia fursa ya
kijiografia kuigeuza Dar es Salaam kuwa soko
kubwa la mafuta ya jamii ya petroli kwa ukanda wa
Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara ;
(iii) Itahakikisha wakati wote sehemu zote z a nchi
zinapata mafuta yenye ubora unaokidhi viwango na
kwa bei inayoakisi gharama halisi kupitia Taasisi
zake (TPDC, EWURA na Wizara ya Nishati na
Madini ); na
(iv) Itahimiza matumizi ya gesi ya Petroli (Liquefied
Pretroleum Gas -LPG) na gesi asilia katika matu mizi
ya nyumbani na viwandani ili kupunguza matumizi
ya kuni na mkaa na hivyo kuhifadhi mazingira.
Nishati Jadidifu na Matumizi Bora ya Nishati
73
45. Kwa kuzingatia kwamba gesi asilia na makaa ya mawe ni
rasilimali zinazoisha (depletable), na kwa kuzingatia mad hara
ya mabadiliko ya tabianchi, Chama Chama Mapinduzi
kitaielekeza Serikali kuwekeza nguvu kubwa katika kuzalisha
nishati jadidifu kwa kufanya yafuatayo: –
(a) Kuzalisha umeme wa jua usiopungua MW 180; Joto ardhi MW
200 kwa kuzigatia uwezo uliopo wa kuzalisha hadi MW 5000 ;
(b) Kuzalisha umeme MW 100 kwa kutumia nguvu za upepo kufikia
mwaka 2020 ; na
(c) Kufanya tafiti ili kubaini na kupanga vyanzo mbadala kwa miaka
ijayo ili kuepusha Taifa kukosa nishati ya umeme.
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
46. Katika kipindi cha m iaka mitano iliyopita, Serikali imekuwa katika
jitihada za kuendeleza utekelezaji wa mipango na mikakati mbalimbali
kwa lengo la kuinua Sekta ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ili
kufikia maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Katika kipindi hicho,
mafaniki o yafuatayo yamepatikana: –
(a) Kuimarisha Utendaji wa Tume ya Sayansi na Teknolojia
(COSTECH ) kwa kuhakikisha :-
(i) Sheria ya Tume imepitiwa upya ili kuipa COSTECH
mamlaka ya kiudhibiti pamoja na kutambua mchango wa
ubunifu ; na
(ii) COSTECH imeanzisha taasisi za kuwa kuza wajasiriamali wa
TEHAMA ikiwemo ya Dar Teknohama Incubator (DTBi)
ambapo matokeo yake yamechangia kuanzishwa kwa
mfumo wa MAXMALIPO.
(b) Jumla ya watafiti 517 wamesomeshwa katika ngazi ya shahada
ya Uzamili na Uzamivu katika vyuo vikuu vya hapa nchini kat ika
kipindi cha mwaka 2010 hadi 2014 ;
(c) Katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2015 wagunduzi 11
walipewa Tuzo ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (TASTA).
Aidha, Taasisi nane ( 8) zilipewa Tuzo za Utafiti wa Sayansi na
74
Teknolojia (NARST) na Taasisi mbili ( 2) zimep atiwa Tuzo za
Mazingira (NAEM) ;
(d) Ujenzi wa awamu ya I na II ya Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano wenye urefu kilometa 7,560 umekamilika na
umesaidia watoa huduma kufikisha huduma za mawasilianao
kwa wananchi kwa uharaka zaidi, uhakika na kwa gharama
nafuu. Kuw epo kwa mkongo mmoja unaomilikiwa na Serikali
umepunguza gharama za huduma ya mawasiliano ambapo: –
(i) Gharama kwa mtumiaji wa mwisho zimeshuka kutoka
Shilingi 147 kwa dakika mwaka 2009 hadi Shilingi 67
kwa dakika mwaka 2014 ; na
(ii) Ada ya kuunganisha simu za miko noni imeshuka
kutoka Shilingi 115 kwa dakika mwaka 2009 hadi
Shilingi 34.92 kwa dakika mwaka 2014.
(e) Mfumo wa kusimamia mawasiliano umewekwa ili kubaini
takwimu zinazopita katika mitandao ya mawasiliano kwa
kutambua mapato na miamala ya fedha, kufuatilia na kugundua
mawasiliano ya ulaghai na kutambua taarifa za laini za simu na
za kifaa cha mawasiliano ;
(f) Zoezi la kuhamisha matangazo kutoka mfumo wa analojia
kwenda katika utangazaji wa Digiti awamu ya kwanza
limekamilika ; na
(g) Idadi ya wananchi wanaomiliki simu za kiganjani imeongezeka
kutoka milioni 2.9 mwaka 20 05 hadi milioni 32.01 mwaka 2015.
47. Mapinduzi ya kilimo, ufugaji, uvuvi na viwanda ambavyo Taifa
linataka yafanyike ili kuleta mageuzi ya uchumi, yatawezekana
kwa kuwekeza vema katika ujenzi wa msingi ima ra wa
maendeleo ya sayansi na teknolojia. Matumizi ya sayansi na
teknolojia katika shughuli za uzalishaji mali na utoaji huduma
katika sekta mbalimbali yatasaidia uchumi wetu kukua kwa
kasi na kuwapunguzia wananchi umas ikini pamoja na
kuongeza ajira.
75
Sekt a ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia katika kipindi cha
miaka mitano ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama
Cha Mapinduzi 2015 -2020, itaweka msisitizo mkubwa wa
vipaumbele kama ifuatavyo: –
(a) Kuanzisha vituo vya ubunifu ili kukuza makampuni ya TEHAMA
yanayoibukia kwa lengo la kuongeza ajira kwa vijana ;
(b) Kuandaa mazingira bora ya kusambaza matokeo ya utafiti na
teknolojia kwa watumiaji katika sekta za uzalishaji hususan
kilimo, mifugo, uvuvi na afya ;
(c) Kuendeleza matumizi ya teknolojia ya nyuklia katika tiba ya
saratani na kuongeza vituo kutoka vituo viwili (2) vya sasa hadi
sita (6) vitakavyohudumia kanda mbalimbali nchini, vituo vinne
vitakavyoongezwa ni: Hospitali ya Rufaa Mbeya, Mnazi Mmoja
(Zanzibar), KCMC pamoja na Dodoma ;
(d) Kuunganisha katika Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano baadhi ya
shule za msingi, shule zote za sekondari, ofisi zote za wakuu wa
wilaya/polisi (OCD), hospitali zote za wilaya, vyuo vikuu vyote
na vituo vya posta 65 ili kuweza kutumia fursa za TEHAMA
hususan Elimu M tandao, Maktaba Mtan dao na Afya Mtandao ;
(e) Kuanzisha kituo mahiri cha huduma za TEHAMA kwa
kushirikiana na sekta binafsi kwa lengo la kuhawilisha teknolojia
na kutoa ajira kwa Watanzania ;
(f) Kufikisha huduma za mawasiliano ya simu za viganjani kwa
wananchi wote kupitia Mfuko wa M awasiliano kwa Wote
(UCSAF) katika vijiji vyote vya Tanzania Bara na Zanzibar ;
(g) Kuendelea kuweka mazingira bora ya ushindani kwenye Sekta
ya Mawasiliano ili wananchi wengi waweze kumudu gharama za
mawasiliano ya simu ;
(h) Kutenga kila mwaka kiasi kisichopungua asilimia 1.0 ya Pato
Ghafi la Taifa (GDP) kwa ajili ya utafiti, maendeleo na
maonyesho ya matokeo ya utafiti ;
(i) Kuwalinda watumiaji wa simu za mikononi dhidi ya dhuluma,
wizi na uhalifu wa mitandao ; na
76
(j) Kuongeza idadi ya watumiaji mitandao (internet) kutoka milioni
9.0 mwaka 2015 hadi kufikia milioni 20.0 mwaka 2020.
77
SURA YA NNE
SEKTA YA HUDUMA ZA JAMII
48. Huduma bora za jamii kama afya, elimu, maji na nyinginezo ni nyenzo
muhimu katika kuondoa umasikini na kuharakisha maendeleo ya
wananchi. Katika kipindi ch a miaka mitano iliyopita, Serikali chini ya
uongozi wa Chama Cha Mapinduzi imeendeleza jitihada za kuhakikisha
kwamba wananchi wanaendelea kunufaika na huduma hizo. Kwa hivyo,
katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii 2015 -2020, Chama Cha
Mapinduzi kitai elekeza Serikali kuendeleza mafanikio yaliyopatikana
katika kipindi kilichopita ili wananchi waendelee kunufaika na huduma
za jamii ambazo ni za msingi katika jitihada za kuboresha maisha yao.
Afya
49. Ili kujenga Taifa lenye watu wenye afya bora inayowaweze sha kuzalisha
mali na kutoa huduma mbalimbali, katika kipindi cha mwaka 2010 -2015,
Serikali iliendelea kuyapa kipaumbele maeneo yaliyoainishwa katika
MKUKUTA na Malengo ya Milenia ambapo mafanikio yafuatayo
yamepatikana: –
(a) Vituo vya kutolea huduma ya Afya v imeongezeka kutoka 6,260
mwaka 2010 hadi vituo 7,014 mwaka 2015. Pia kuna kliniki 89
zinazohamishika (huduma za mkoba) katika mfumo wa utoaji wa
huduma za wazazi, meno, macho, moyo na sukari ambazo
huendeshwa na madaktari bingwa ;
(b) Udahili wa wanafunzi watar ajali umeongezeka kutoka 7,013
mwaka 2010 hadi wanafunzi 11,192 mwaka 2015 katika Vyuo
vya Afya na Ustawi wa Jamii ;
(c) Waajiriwa wapya wa kada za afya wameongezeka kutoka 7,471
mwaka 2010 hadi waajiriwa 9,345 mwaka 2014 ;
(d) Kupitia mpango wa hati punguzo, vyanda rua 8,753,438 vyenye
viuatilifu kwa ajili ya kaya zenye watoto chini ya miaka mitano,
vyandarua 7,785,787 kwa ajili ya wajawazito na vyandarua
4,960,111 kwa ajili ya watoto chini ya umri wa mwaka mmoja
78
vimesambazwa bure kwa lengo la kuboresha tiba ya malar ia,
kudhibiti mbu na kutoa kinga. Aidha, vyandarua 26,371,329
viligawiwa kwa wananchi bila malipo kupitia kampeni zilizolenga
watoto chini ya miaka mitano na ngazi ya Kaya. Matokeo yake
ni:-
(i) Vifo vitokanavyo na malaria vimepungua kutoka 33
mwaka 2010 hadi 12 kwa kila watu 1,000 mwaka 2014 ;
na
(ii) Idadi ya watu waliopatikana na malaria imepungua
kutoka watu 310 mwaka 2010 hadi 161 kwa kila watu
1,000 mwaka 2014.
(e) Mpango wa Upuliziaji wa viuatilifu ukoko katika kuta ndani ya
nyumba ili kuua mbu wanaoeneza malaria umetekelezwa kwa
mikoa ya Kagera, Mwanza, Mara na Geita ambapo zaidi ya kaya
1,440,000 zenye watu 6,500,000 zilinufaika ;
(f) Ujenzi wa kiwanda cha viuadudu (bio -larvicides) katika
Halmashauri ya Mji wa Kibaha kwa lengo la kuzalisha viuadudu
kwa ajili ya kudhib iti viluwiluwi vya mbu nchini umekamilika
ambapo Kata za Jiji la Dar es Salaam zimeanza kunufaika ;
(g) Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI) ilitoa huduma za kibingwa
za mkoba kwa wagonjwa 513 ambapo wagonjwa 1 16
walifanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ;
(h) Hospitali za Rufaa za Mikoa 24 zimeunganishwa kwenye
mtandao wa mkongo wa Taifa wa mawasiliano ili kutoa huduma
za afya kwa njia ya mtandao ;
(i) Vifaa vya kujimudu kwa watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na
shime sikio, viti mwendo, mashine za nukta nundu na fimbo
nyeupe kwa ajili ya makazi 17 ya wazee, wasiojiweza na vyuo
viwili vya ufundi vimenunuliwa. Jumla ya wazee 1,750 walipatiwa
huduma katika makazi 17 yanayomilikiwa na Serikali na 24
yanayomilikiwa na w akala wa hiari ;
(j) Bohari ya Dawa (MSD) imeendelea kushirikiana na Sekta Binafsi
katika kuhakikisha kuwa dawa na vifaa tiba vinapokosekana
79
katika bohari zake, Mshitiri/Mnunuzi wa Sekta Binafsi anakuwa
tayari kuwezesha upatikanaji wa dawa hizo kwa ajili ya vit uo vya
kutolea huduma za afya nchini ;
(k) MSD imeanza kupeleka shehena za dawa moja kwa moja hadi
vituo vya kutolea huduma za afya nchini ili kuboresha usambazaji
dawa na kupunguza gharama ;
(l) Jumla ya Wataalamu 1,553 wa Sekta ya Afya katika ngazi ya
Halmashaur i wamepata mafunzo ya uingizaji na utumiaji wa
taarifa kupitia mfumo wa ele ktroniki ili kufanikisha upatikanaji wa
takwimu za afya ambapo jumla ya kompyuta 133 kwa ajili ya
Halmashauri na Mikoa; na kompyuta 189 kwa ajili ya matumizi
ya mfumo wa hospitali z a Mikoa na Wilaya zilitolewa ;
(m) Watanzania 4,010,844 sawa na asilimia 9.2 wamejiunga na
Mfuko wa A fya ya Jamii (CHF) kufikia mwaka 2015 . Aidha,
asilimia 19.2 ya Watanzania wamefikiwa na huduma za bima kwa
kujumuisha mifuko yote ya Bima za Afya ;
(n) Huduma za mat ibabu ya kibingwa na uchunguzi zimeimarishwa.
Huduma hizo ni pamoja na upasuaji mkubwa wa moyo; upasuaji
wa mgongo na ubongo; kusafisha damu kwa wagonjwa wenye
matatizo ya figo; kuanzishwa kwa huduma ya matibabu ya
dharura katika Hospitali ya Taifa Muhimbi li (Emergency
Medicine); na kununua mashine za mionzi. Aidha, hadi sasa
jumla ya wagonjwa 671 walipata huduma ya upasuaji mkubwa
wa moyo; wagonjwa 211 walifanyiwa upasuaji maalum u: ubongo
29, mgongo 107, 56 waliwekewa viungo bandia vya nyonga na
19 viungo bandia vya goti ; na
(o) Mpango wa kutokomeza maambukizi mapya ya Virusi vya
Ukimwi ( VVU) kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto
umeanzishwa. Hadi sasa akina Mama walioanzishiwa tiba ya
maisha ni 72,207 kati ya mama wajawazito wa VVU watarajiwa
97,908. Mpango huu ume wezesha kiwango cha maambukizi
kupungua kutoka asilimia 8 mwaka 2010 hadi asilimia 5 mwaka
2015.
80
Moja ya ghala la Bohari Kuu ya Dawa kwa ajili ya kuhifadhi Dawa
katika Kanda
50. Kwa kuzingatia dhamira ya kuwa na wananchi wenye afya bora
watakaoweza kushiri ki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi
na kutoa huduma katika miaka mitano ijayo, Chama Cha
Mapinduzi kitaielekeza Serikali kuendelea kuhakikisha kwamba
wananchi wanapata huduma bora za afya kwa kufanya
yafuatayo: –
(a) Kuendeleza utekelezaji wa Mpango wa Ma endeleo wa Afya ya
Msingi (MMAM) wenye lengo la kuimarisha na kusogeza huduma
za afya karibu na wananchi kwa kuhakikisha kwamba: –
(i) Lengo la kila kijiji kuwa na Zahanati, Kata kuwa na Kituo
cha Afya na Wilaya kuwa na Hospitali linaendelea
kutekelezwa katika maeneo ambayo huduma hizi
hazijakamilika pamoja na kujenga hospitali za wilaya
katika wilaya zote mpya ;
81
(ii) Hospitali za Rufaa za Mikoa zinaendelea kuimarishwa na
kukamilisha ujenzi kwa mikoa mipya na ile ambayo haina
hospitali hizi ;
(iii) Kujenga hospitali katika wilaya mpya ;
(iv) Kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika Sekta ya Afya
kwa kupitia sera ya ubia baina ya Sekta ya Umma na
Binafsi ( PPP);
(v) Hospitali za Rufaa za Kanda zitaendelea kuimarishwa na
kujenga hospit ali nyingine tatu kwa ajili ya Kanda ya
Kusini, Ka ti na Magharibi ;
(vi) Kudahili wanafunzi 15,000 katika Vyuo vya Afya na Ustawi
wa Jamii ifikapo mwaka 2020 ikiwa ni jitihada za
kutosheleza mahitaji ya rasilimali watu katika sekta hii ;
(vii) Kukarabati, kujenga na kupanua miundombinu katika
vyuo vya mafunzo ya afya na kushirikisha Sekta Binafsi
katika uendeshaji wa vyuo ;
(viii) Kuajiri wataalam u zaidi wa afya kutoka ndani na nje ya
nchi pamoja na kuboresha mazingira ya kazi kwa lengo la
kuongeza ubora wa huduma za afya. Aidha, hospitali za
wilaya zitaendelea kuimarishwa k wa kuzipatia madaktari,
wauguzi, dawa na vifaa tiba vya kutosha ;
(ix) Kutoa motisha kwa watumishi ambao wanafanya kazi
katika maeneo yenye mazingira magumu ili kuwajengea
ushawishi wa kuendelea kutoa huduma za afya katika
maeneo hayo ; na
(x) Kujenga nyumba za watu mishi karibu na vituo vya kutolea
huduma.
(b) Kuimarisha mapambano dhidi ya malaria kwa kufanya
yafuatayo: –
(i) Kuwagawia wananchi vyandarua vyenye viuatilifu
22,360,386 bila malipo ;
(ii) Kutekeleza mpango wa upuliziaji wa viuatilifu ukoko katika
kuta za nyumba ili kuua mbu wanaoeneza malaria katika
mikoa ya Kigoma na Lindi ;
82
(xi) Kuendelea kutekeleza mpango wa kuangamiza viluwiluwi
vya mbu kwa kutumia viuadudu vya kibailojia katika Kata
za Jiji la Dar es Salaam ; na
(xii) Kununua na kusambaza dawa za malaria katika vituo
vyote vya kutolea huduma nchini.
(c) Kuimarisha upatikanaji wa huduma za dharura na za kawaida
kwa wagonjwa kupitia vituo vya huduma za afya hapa nchini.
Huduma hizi ni pamoja na magonjwa ya saratani, mishipa ya
fahamu, mapafu, figo, huduma za magonjwa ya moyo,
upasuaji mbalilmbali ikiwamo upasuaji wa mifupa ;
(d) Hospitali ya Taifa Muhimbili itaendelea kutoa huduma za
kibingwa za mkoba katika Hospitali za Rufaa za Kanda ;
(e) Kuunganisha hospitali za rufaa za Mikoa na Wila ya na hospitali
nyinginezo kwenye mfumo wa matibabu mtandao
(telemedicine) ;
(f) Halmashauri za Wilaya zitaelekezwa kutenga bajeti kwa ajili ya
kununulia vifaa vya kujimudu kwa lengo la kuwawezesha watu
wenye ulemavu ;
(g) Bohari ya Dawa itakamilisha ujenzi wa magha la ya kisasa ya
kuhifadhia dawa katika mikoa ya Tanga, Tabora, Mtwara na
Dar es Salaam. Aidha, Serikali itaendelea kushirikisha Sekta
Binafsi kuwezesha upatikanaji wa dawa pale zinapokosekana
katika Bohari ya Dawa ;
(h) Kuongeza Washitiri Binafsi 17 katika miko a tisa kwa ajili ya
ununuzi wa dawa pale ambapo hazipo Bohari ya Dawa ;
(i) Kuunganisha mifumo ya ukusanyaji na utoaji taarifa za afya ili
kufikia lengo la kuwa na mfumo mmoja unaokusanya na kutoa
taarifa za afya nchini. Aidha, mfumo wa ukusanyaji taarifa kwa
njia ya simu za mkononi utasambazwa nchi nzima ;
(j) Kuweka utaratibu utakaowezesha wananchi kuwa na Bima ya
Afya ili kumudu gharama za matibabu ;
(k) Kuimarisha huduma za matibabu ili kupunguza gharama za
kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa kufanya yafuatayo: –
83
(i) Kununua mashine za mionzi (LINAC machine) kwa
ajili ya tiba ya saratani ;
(ii) Kununua vifaa vya kisasa na kuwajengea uwezo
wataalam ili kuhudumia wagonjwa wengi wa moyo
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na hospitali za
rufaa za Kanda ;
(iii) Kununua mashine za mionzi (CT -Scan, MRI) kwa ajili
ya kutoa huduma za upasuaji wa mgongo na ubongo ;
na
(iv) Kuimarisha mtandao wa Hospital i za Taifa pamoja na
Huduma za Ubingwa wa J uu zikiwemo zile za upasuaji
wa moyo; huduma kwa wagonjwa wa saratani;
upasuaji wa ubongo na mishipa ya faham u na
upasuaji kupitia tundu dogo kwa kutumia kifaa
maalum u ikiwa ni pamoja na kuchuja damu na
kupandikiza figo kwa wagonjwa wenye matatizo ya
figo.
(l) Kupanua huduma za matibabu mtandao (telemedicine) pamoja
na zile za kutumia mtandao wa simu pamoja na kutoa mafunzo
kwa watumishi yatakayowawezesha kutoa huduma za
kibingwa. Aidha, vituo vingine v ya saratani vitaongezwa katika
hospitali ya KCMC na hospitali ya rufaa ya Mbeya ili kurahisisha
upatikanaji wa huduma kwa wananchi ;
(m) Kukamilisha ujenzi wa hospitali za M loganzila, Mtwara na Chuo
Kikuu cha Dodoma ;
(n) Kukarabati na kuimarisha huduma za kibin adamu katika vituo
vya kutolea huduma za ustawi wa jamii vikiwemo makazi 17 ya
wazee, mahabusi saba za watoto walio katika mkinzano na
sheria pamoja na shule moja ya maadil isho;
(o) Kuimarisha upatikanaji wa haki na huduma za makundi
maalum u wakiwemo watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism)
na watoto wanaoishi mitaani ikiwa ni pamoja na kuanzisha
Kamati za Ulinzi wa Mtoto katika Halmashauri zote ;
84
(p) Kukamilisha Sera ya Huduma za Usta wi wa Jamii pamoja na
Mkakati wake wa Utekelezaji. Aidha, Halmashauri zitahakikisha
wazee wanatambuliwa na kupewa matibabu bure katika
hospitali za Serikali ;
(q) Kuimarisha Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto kwa kuzingatia
vipaumbele vya Tekeleza kwa Matokeo Maku bwa Sasa (BRN)
kwa kufanya yafuatayo: –
(i) Kuzijengea uwezo H ospitali na Vituo vya Afya ili kutoa
huduma kamili ya Afya ya U zazi na Mtoto pamoja na
upasuaji kwa mama wajawazito ;
(ii) Kuanzisha Benki za Damu katika Mikoa itakayoanza
kutekeleza mpango wa kutoa hudum a kamili ya afya ya
uzazi na mtoto. Vilevile, huduma za uzazi wa mpango
zitapewa kipaumbele ;
(iii) Kuzijengea uwezo Z ahanati na Vituo vya Afya katika
mikoa ya Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Kigoma kutoa
huduma ya msingi ya dharura ya Afya ya Uzazi na
Mtoto;
(iv) Kutoa huduma za mkoba (mobile clinic) hasa maeneo
ya vijijini ; na
(v) Kuendelea kutekeleza mpango wa kutokomeza
maambukizi mapya ya VVU kutoka kwa Mama kwenda
kwa Mtoto.
Elimu
51. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali imeendelea kuchukua
hatua mbalimbal i katika kuboresha, kuimarisha na hata kupanua Elimu
ya Awali hadi ya Chuo Kikuu kwa lengo la kuhakikisha kwamba elimu
katika ngazi zote inakuwa na ubora unaostahili ili kuwawezesha vijana
na makundi mengine kumudu ushindani wa soko la ajira ambalo wigo
wake umepanuka ndani na nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Katika
kipindi hicho, yamepatikana mafanikio yafuatayo: –
(a) Elimu ya Awali
(i) Idadi ya shu le za msingi zenye madarasa ya E limu ya
Awali imeongezeka kutoka shule 10,612 mwaka 2010
85
hadi shule 14,783 ambayo yana walimu 13,600 mwaka
2015;
(ii) Stashahada ya E limu ya Awali ya miaka miwili katika
vyuo 19 vya serikali imeanzishwa kwa lengo la kupata
walimu wenye weledi wa juu katika ngazi ya Elimu ya
Awali; na
(iii) Idadi ya matundu ya vyoo imeongezeka kutoka 128,847
mwaka 2006 hadi 157,162 mwaka 2013.
(b) Elimu ya Msingi
(i) Katika kuimarisha utoaji wa m afunzo kwa walimu wa
masomo ya H isabati, Kiingereza na S ayansi, vigezo
vya kujiunga na mafunzo ya ualimu vimepandishwa
hadhi kutoka ufaulu wa daraja la nne hadi kuanzia
ufaulu wa d araja la kwanza mpaka daraja la tatu kwa
waliofaulu masomo hayo ;
(ii) Kupitia mpango wa kuwajengea uwezo walimu na
mwanafunzi, jumla ya walimu 9,814 katika
Halmashauri 40 wakiwemo walimu 3,272 wa somo la
Hisabati na 3,272 wa somo la Kiingereza
wamejengewa uwez o wa kuyamudu masomo ya
Hisabati, Sayansi na Lugha. Aidha, Stashahada ya
Elimu ya Msingi imeanzishwa katika vyuo vinne (4)
UDOM, Morogoro, Bustani na Marangu vyenye uwezo
wa kudahili walimu tarajali 713 kwa mwaka ili
kuandaa walimu mahiri watakaofu ndisha E limu ya
Msingi;
(iii) Maslahi ya walimu yameendelea kuboreshwa
kulingana na ukuaji wa uchumi ;
(iv) Madai mbalimbali ya walimu yameendelea kulipwa
baada ya kuhakikiwa ;
(v) Ruzuku ya W anafunzi (Capitation Grants) imeendelea
kutolewa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya
kufund ishia na kujifunzia katika shule zote za Serikali
nchini ;
86
(vi) Stashahada ya Elimu ya Msingi katika vyuo vitatu ( 3),
Stashahada ya Juu ya Elimu masomo ya Sayansi
katika vyuo vitatu ( 3), Stashahada ya Juu ya Elimu
masomo la Lugha katika chuo kimoja ( 1) na
Stasha hada ya Elimu ya Michezo katika chuo kimoja
(1) zimeanzishwa ili kuweza kuandaa walimu mahiri
watakaofundisha E limu ya Msingi kwa kuwajengea
uwezo wa kumudu maarifa na stadi muhimu katika
kutekeleza mitaala kwa ufanisi ;
(vii) Uandikishaji wa watoto wa miaka 7 -13 umeongezeka
kutoka wanafunzi 6,499,581 mwaka 2005 hadi
wanafunzi 7,679,877 mwaka 2013 ;
(viii) Idadi ya uandikishaji wa wanafunzi wenye ulemavu
imeongezeka kutoka wanafunzi 27,422 mwaka 2009
hadi wanafunzi 31,488 mwaka 2013 ;
(ix) Jumla ya shule za msingi 7,165 sawa na asilimia 37.4
zilikaguliwa mwaka 2013 kwa lengo la kuboresha
kiwango cha elimu ;
(x) Idadi ya walimu walioajiriwa imeongezeka kutoka
135,013 mwaka 2005 hadi 189,487 mwaka 2013 ;
(xi) Uwiano wa mwalimu kwa mwanafunzi umeimarika
kutoka uwiano mwalimu mmoja wanafunzi 5 6 (1:56 )
mwaka 2005 hadi uwiano wa mwalimu mmoja
wanafunzi 43 (1:43) mwaka 2013 ;
(xii) Uwiano wa kitabu kwa wanafunzi umeboreshwa
kutoka kitabu kimoja wanafunzi saba (1:7) mwaka
2010 kufikia wastani wa kitabu kimoja wanafunzi
watatu (1:3) mwaka 2014 ;
(xiii) Idadi ya nyumba za walimu imeongezeka kutoka
38,448 mwaka 2006 hadi 161,007 mwaka 2013 ; na
(xiv) Idadi ya wanafunzi wanaoendelea na E limu ya
Sekondari (Kidato cha Kwanza) imeongezeka kutoka
wanafunzi 403,873 sawa na aslimia 84.3 mwaka
87
2010 hadi 451,392 mwaka 2015 sawa na asilimia
100.
(c) Elimu ya Sekondari
(i) Idadi ya walimu wa sekondari imeongezeka kutoka
40,517 mwaka 2010 hadi walimu 80,529 mwaka 2014
na hivyo kufikia uwiano Kitaifa wa mwalimu mmoja
kwa wanafunzi 22 (1:22);
(ii) Walimu wa masomo ya Sayansi za J amii
wameongezeka ha di kufikia 52,816 mwaka 2014 na
hivyo kuwa na ziada ya walimu 2,960 ikilinganishwa
na mahitaji ya walimu 49,856 wa fani hizo ;
(iii) Walimu wa Sayansi na H isabati wameendelea
kupatiwa mafunzo ili kuboresha fani hizo ambapo
vifaa vya maabara na kemikali vyenye tha mani ya
Shilingi milioni 327.7 vimenunuliwa na kusambazwa.
Aidha, jumla ya vitabu milioni 4,485,530 vya sayansi
vimenunuliwa na kusambazwa katika shule mbali
mbali nchini ;
(iv) Hadi kufikia mwaka 2014, kupitia Mpango wa
Maendeleo ya Elimu ya Sekondari awamu ya pili
(MMES II) , mafunzo ya Sayansi na Hisabati
yametolewa kwa walimu 9,004 katika mzunguko wa
mada za mwanzo na walimu 7,863 kwa mzunguko wa
mada za pili na walimu 182 wa meanza mzunguko wa
mada za tatu; na
(v) Idadi ya maabara imeongezeka kutoka 1,478 mwaka
2005 hadi 4,237 mwaka 2015 na maabara 5,974 zipo
katika hatua mbalimali za ujenzi.
88
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisikiliza maelezo kutoka
kwa mmoja wa wanafunzi wa shule za Sekondari wakati wa uzinduzi wa
moja ya Maabara zilizokamilika kujengwa.
(d) Elimu ya Ualimu
(i) Mafunzo tarajali ya walimu wa Shule za M singi
watakaofundisha masomo mawili yameanza kutolewa
ambapo wanachuo 1,964 wa Diploma ya Juu ya Elimu
ya S ekondari na wanachuo 178 wa Diploma ya
Sayansi wa Shule za Msingi wamedahiliwa kw a
mwaka 2014/15 katika Chuo Kikuu cha Dodoma ;
(ii) Kati ya mwaka 2010 na 2015, wakufunzi 331 wa V yuo
vya Ualimu walipatiwa mafunzo ya namna ya kutumia
89
TEHAMA katika kufundisha na kujifunza. Aidha, vyuo
vyote vya ualimu (34) vimepatiwa kompyuta na hivyo
kuwapati a fursa wakufunzi kuandaa mada zao na
maandiko mengine kwa kutumia teknolijia hiyo ;
(iii) Jumla ya Shilingi bilioni 4.3 zimetumika kukarabati
miundombinu ya vyuo vya Ualimu Patandi, Bustani na
Vikindu ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na
kufundishia ; na
(iv) Maab ara za Vyuo vya U alimu vyenye mchepuo wa
Sayansi zimeboreshwa kwa kuzinunulia vifaa vyenye
thamani ya Shilingi milioni 379.8 katika maabara na
kemikali za masomo ya Sayansi (Fizikia, Kemia na
Biolojia) katika vyuo saba vya U alimu vya Korogwe,
Kleruu, Butim ba, Songea, Tukuyu, Monduli na
Morogoro.
(e) Elimu ya Juu
(i) Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Juu wa mwaka
2010 umeandaliwa na utekelezaji wake umechangia
wanafunzi wa kidato cha sita wanaojiunga na V yuo
Vikuu kuongezeka kutoka wanafunzi 34,564 mwaka
2009/2010 h adi wanafunzi 40,452 mwaka 2014/2015
sawa na asilimia 14.6 ;
(ii) Utaratibu wa utoaji na urejeshwaji mikopo kwa
wanafunzi wa Elimu ya Juu umeboreshwa ambapo: –
Dawati la Mikopo limeanzishwa katika kila Chuo ;
Idadi ya wanafunzi ambao wamepata mikopo
imeongezeka kutoka wanafunzi 72,035 mwaka
2009/2010 hadi kufikia 99,928 Mwezi Machi,
2015 sawa na ongezeko la asilimia 27.9 ; na
Utaratibu wa urejeshaji wa makopo umeendelea
kuboresha ambapo hadi kufikia tarehe 31 Machi,
2015 jumla ya Shilingi bilioni 75.57
zemerejeshw a kati ya Shilingi bilioni 165.0 ya
mikupuo inayopaswa kuwa imerejeshwa.
90
Makusanyo haya ni asilimia 45.4 ya kiwango
kinachopaswa kuwa kimekusanywa.
(iii) Bajeti kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu imeendelea
kuongezeka kutoka Shilingi bilioni 186.48 mwaka
2010 h adi Shilingi bilioni 328.313,44 mwaka 2015
sawa na ongezeko la asimia 43.2 ;
(iv) Ujenzi na ukarabati wa majengo mapya 25 kwa ajili
ya kumbi za mihadhara, maabara na ofisi za
wafanyakazi katika vyuo vikuu vya UDSM, OUT,
DUCE, MUCE, SUA, DIT na ARU umekamilika n a
utaongeza nafasi za kusomea wanafunzi hadi kufikia
47,622 ;
(v) Idadi ya wanafunzi wanaosoma katika Vyuo Vikuu
imeongezeka kutoka wanafunzi 139,638 mwaka 2010
hadi kufikia wanafunzi 218,959 mwaka 2014 sawa
na asilimia 36.2 ;
(vi) Idadi ya wanafunzi wa kike wa naosoma Elimu ya Juu
imeongezeka kutoka wanafunzi 53,376 kati ya
wanafunzi 141,671 waliodahiliwa mwaka 2010/11
hadi kufikia wanafunzi 78,800 kati ya wanafunzi
218,959 waliodahiliwa mwaka 2014/2015 ;
(vii) Taasisi 23 za Elimu ya Juu ka ti ya 32 zimeunganishwa
katika Mkongo wa Taifa ili kuimarisha ufundishaji na
uendeshaji wa elimu kwa njia ya mtandao hadi
kufikia mwaka 2015 ;
(viii) Chuo Kikuu Huria na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
vimeanza kutoa mafunzo kwa njia ya masafa baada
ya kuunganishwa na Mkongo wa Taifa na kuwezesh a
wahadhiri kutoa elimu kwa njia ya masafa na kuweza
kuwafikia wanafunzi wengi mikoani ; na
(ix) Idadi ya Vyuo Vikuu na V yuo Vikuu Vishiriki
vimeongezeka kutoka 19 mwaka 2010 hadi 49
mwaka 2015.
(f) Elimu ya Mafunzo ya Ufundi
91
(i) Vyuo vya Ufundi S tadi vimeongezeka kuto ka vyuo 672
mwaka 2010 hadi kufikia vyuo 755 mwaka 2014 ikiwa
ni ongezeko la aslimia 12.35 ;
(ii) Vyuo vya Elimu ya U fundi vimeongezeka kutoka 240
mwaka 2010 hadi 473 mwaka 2014 ikiwa ni ongezeko
la asilimia 97.08 ;
(iii) Udahili wa wanachuo katika V yuo vya Ufundi S tadi
umeongezeka kutoka wanachuo 78,586 mwaka 2010
hadi kufikia wanachuo 145,511 mwaka 2014 ikiwa ni
ongezeko la asilimia 85.16 ;
(iv) Udahili katika vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo
umeongezeka kutoka wanachuo 85,040 mwaka 2010
hadi wanachuo 113,080 mwaka 2014 ikiwa ni ongezeko
la asilimia 33.81 ; na
(v) Udahili wa wasichana katika Vyuo vya Ufundi Stadi
umeongezeka kutoka 52,154 mwaka 2010 hadi 56,849
mwaka 2014. Aidha, udahili wa wasichana katika vyuo
vya Elimu ya Ufundi umeongezeka kutoka 38,698
mwaka 2010 kuf ikia 53,891 mwaka 2014.
(g) Elimu ya Watu Wazima yenye Manufaa
(i) Idadi ya wanafunzi wa Elimu Masafa na Ana kwa Ana
(ODL) imeongezeka kutoka wanafunzi 5,767 mwaka
2005 hadi kufikia wanafunzi 9,399 mwaka 2013 ; na
(ii) Jumla ya watu wazima 907,771 (wanaume 434,466 na
wanawake 473,305) wamejiunga na Elimu ya Watu
Wazima na kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu
(KKK), na kujifunza fani nyingine za kilimo, ufundi,
ufugaji na usindikaji wa bidhaa mbalimbali ambapo
wameweza kuongeza fursa za kujiajiri.
52. Elimu ya kisasa na hasa yenye mwelekeo wa Sayansi na
Teknolojia ina nafasi ya pekee katika kufanikisha ujenzi wa
msingi wa uchumi wa kisasa wa Taifa linalojitegemea. Kwa
kutambua ukw eli huu, CCM inaipa kipaumbele Sekta ya Elimu
92
umuhimu wa kipekee ili kuiendeleza sekta hii. K atika kipindi
cha miaka mitano ijayo (2015 -2020), CCM itahakikisha Serikali
inasimamia Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya
mwaka 2014 kwa ku tekeleza yafuatayo: –
(a) Kuandaa mfumo, muundo na taratibu nyumbufu za kutoa Elimu
ya Awali na Elimumsingi (1+6+ 4) bila malipo ili kuhakikisha
kwamba: –
(i) Uandikishwaji rika lengwa la watoto wa darasa la Elimu
ya Awali unaongezeka kutoka asilimia 45 mwaka 2015
hadi asilimia 100 mwaka 2020 ;
(ii) Uandikishwaji rika lengwa la watoto wa Darasa la
Kwanza unaongezeka kutoka asil imia 95 mwaka 2015
hadi asilimia 100 mwaka 2020 ; na
(iii) Uandikishwaji rika lengwa la Wanafunzi wa Kidato cha
Kwanza unaongezeka kutoka asilimia 60 mwaka 2015
hadi asilimia 80 mwaka 2020.
(b) Kuhuisha taratibu za kujiunga na taasisi zinazotoa elimu na
mafunzo kati ka ngazi mbalimbali kwa kutambua sifa
zinazopatikana katika mifumo na taasisi tofauti ili kuhakikisha
kwamba: –
(i) Asilimia 20 ya wahitimu wa Elimumsingi wanaendelea
na masomo katika ngazi za Sekondari ya J uu na
asilimia 80 kuendelea na elimu au mafunzo ya ufu ndi
katika ngazi ya cheti, stashahada au shahada
kulingana na sifa, vipaji au vipawa ;
(ii) Asilimia 80 ya wahitimu wa Elimu ya Sekondari ya Juu
kujiunga na Elimu ya Juu ya Taaluma na asilimia 20
kuendelea na Elimu ya U fundi, katika ngazi ya cheti,
stashahada au shahada kulingana na sifa ; na
(iii) Asilimia 70 ya wahitimu wa Elimu au M afunzo ya
Ufundi na T aaluma wanapata ajira kwa kujiajiri au
kuajiriwa.
(c) Kudurusu na kuhuisha muundo wa mitaala ili elimu katika ngazi
mbalimbali ikamilike kwa muda wenye tija na itilie maan ani
93
matokeo ya kusoma yenye kujenga ujuzi, maarifa ya
kujitegemea, weledi na kuwawezesha wahitimu kumudu na
kufanya kazi mbalimbali za kuajiriwa au kujiajiri ;
(d) Kuhuisha vigezo na utaratibu wa kuhakiki, kusimamia na kupima
utekelezaji wa mitaala katika shule na taasisi za elimu na
mafunzo katika ngazi zote ili kuhakikisha kwamba: –
(i) Ufaulu wa mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi
unaongezeka kutoka asilimia 57 mwaka 2015 hadi
asilimia 90 mwaka 2020 na asilimia ya wanafunzi
wanaoendelea na Kidato cha Kwanza kuong ezeka
kutoka asilimia 55.5 hadi asilimia 100 ;
(ii) Ufaulu wa mtihani wa Kidato cha Nne unaongezeka
kutoka wastani wa asilimia 69.8 mwaka 2015 hadi
asilimia 90.0 mwaka 2020 na ufaulu wa daraja la I –
III unaongezeka kutoka wastani wa asilimia 30.8 hadi
asilimia 50.0; na
(iii) Idadi ya wataalamu wenye ujuzi wa juu
wanaongezeka kutoka asilimia 3 hadi asimilia 10
mwaka 2020, ujuzi wa kati kutoka asilimia 13 hadi 30
na ujuzi wa chini kupungua kutoka asilimia 84 hadi
60.
(e) Kuimarisha ithibati na udhibiti wa ubora wa elimu na mafunzo ili
kuhakikisha kwamba: –
(i) Asilimia 60 ya wanafunzi wanahitimu shahada kwenye
sekta ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kukua
kwa uchumi ;
(ii) Programu tatu ( 3) au zaidi za mafunzo zinaanzishwa
zenye kukidhi mahitaji na kuleta maendeleo ya kijamii
na kiuchumi kulingana na mahitaji ya kitaifa, kikanda
na kimataifa ;
(iii) Asilimia 70 ya wahitimu katika ngazi zote wawe katika
mrengo wa sayansi, ufundi, hisabati na teknolojia ;
94
(f) Kuandaa na kutumia utaratibu wa upatikanaji na usambazaji
wa vitabu vya kiada na zi ada kwa ngazi zote za elimu na
mafunzo ili kuhakikisha kwamba: –
(i) Uwiano wa kitabu c ha kiada kwa mwanafunzi katika
Elimumsingi unaongezeka kutoka 1:3 mwaka 2015
hadi 1:1 mwaka 2020 ;
(ii) Asilimia 50 ya fedha za ruzuku ya uendeshaji wa
shule zinatumika kuchapisha na kusambaza vitabu
vya kiada ; na
(iii) Uwiano wa vitabu vya ziada kwa kila somo kwa
mwanafunzi katika Elimumsingi kuwa 1:10.
(g) Kuandaa utaratibu, kuimarisha mfumo wa udahili na kutumia
fursa za elimu na mafunzo ndani na nje ya nchi kwa makundi
yote ya jamii kwa usawa katika ngazi zote hususan katika
ufundi, hisabati, sayansi na teknolojia ili kuhakikisha
kwamba: –
(i) Asilimia 100 ya wahitaji wa mikopo kwa ajili ya
kusomea fani ya udaktari wanapata mikopo ;
(ii) Ufadhili wa nafasi 500 za masomo ya fani ya udaktari
zinapatik ana kila mwaka ili kupunguza pengo la
uhaba wa madaktari nchini ;
(iii) Asilimia 100 ya wale wenye mahitaji maalum u, vipaji
na vipawa wataotambulika watapata fursa za
kuendelea na masomo katika ngazi mbalimbali ; na
(iv) Shule moja maalum u ya Ufundi (Specialized Techni cal
Schools) au zaidi inaanzishwa kila mkoa ambayo
itadahili wanafunzi wenye vipaji mbalimbali na
kuwaendeleza kwenye fani mbalimbali zenye tija kwa
maendeleo ya Taifa.
(h) Kuandaa mpango wa kuwawezesha walimu na wanafunzi
kutumia TEHAMA katika kufundishia na kujifunzia ili
kuhakikisha kwamba: –
(i) Asilimia 80 ya walimu wanaandaliwa na kutumia
TEHAMA kufundishia katika ngazi zote ; na
95
(ii) Asilimia 70 ya taasisi zote zinazotoa elimu na mafunzo
zinaunganishwa katika M kongo wa Taifa.
(i) Kuhuisha miongozo ya Elimu na M afunzo i li kuondoa vikwazo
vinavyosababisha mwanafunzi kushindwa kukamilisha
mzunguko wa elimu au mafunzo ili kuhakikisha kwamba: –
(i) Mdondoko katika Elimumsingi unapungua kutoka
wastani wa asilimia 8.2 mwaka 2015 hadi asilimia 2
mwaka 2020 ;
(ii) Wasichana wote wa E limumsingi wanaoacha shule kwa
sababu ya kupata ujauzito wataendelea na masomo ; na
(iii) Wanafunzi wanaomaliza mzunguko wa elimu katika
ngazi ya Elimumsingi wanaongezeka kutoka asilimia 67
mwaka 2015 hadi asilimia 95 mwaka 2020.
(j) Kuandaa walimu, wakufunzi na wahadhir i mahiri hususan
katika masomo ya hisabati, lugha, sayansi, teknolojia na
ufundi ili kuhakikisha kwamba: –
(i) Uondokaji wa walimu, wakufunzi na wahadhiri
unapungua kutoka wastani wa asilimia 0.8 mwaka
2015 hadi asilimia 0.2 mwaka 2020 ;
(ii) Tatizo la uhaba wa wali mu wapato 24,000 wa masomo
ya sayansi na hisabati kwa shule za Sekondari
linapungua kwa kutoa mafunzo kwa walimu 5,000 wa
masomo hayo kila mwaka ; na
(iii) Idadi ya wahadhiri wanaongezeka kutoka wahadhiri
6,880 mwaka 2015 hadi wahadhiri 10,000 mwaka 2020.
(k) Kuandaa mpango kabambe wa kuongeza udahili katika taasisi
za elimu na mafunzo kwa kuzingatia mahitaji ya rasilimali
watu na ujuzi kwa maendeleo ya Taifa na soko la ajira
hususan ujuzi unaohitajika au kuhusiana na sekta zinazokua
haraka na zinazojitokeza mfano maf uta, gesi na madini ili
kuhakikisha kwamba: –
(i) Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo na Sayansi Shirikishi
cha Mwalimu J.K. Nyerere (Butiama) unakamilika na
96
kuanzisha na kukamilisha ujenzi wa Chuo Kikuu cha
Sayansi za Madini Shinyanga ;
(ii) Ujenzi wa Chuo cha Ufundi St adi (VETA) cha Mkoa wa
Kagera utafanyika ;
(iii) Udahili katika vyuo vya Ufundi Stadi unaongezeka
kutoka wastani wa wanafunzi 150,000 mwaka 2015
hadi wanafunzi 700,000 mwaka 2020 ;
(iv) Udahili katika vyuo vya Ufundi vya Kati unaongezeka
kutoka wastani wa wanafunzi 30, 000 mwaka 2015
hadi wanafunzi 285,600 mwaka 2020 ; na
(v) Udahili katika ngazi ya shahada unaongezeka katika
vyuo vya elimu ya Juu kutoka wastani wa wanafunzi
60,000 mwaka 2015 hadi wanafunzi 117,000 mwaka
2020.
(l) Kushirikiana na wadau katika kuimarisha mfumo wa
ugharimiaji wa elimu ya mafunzo ikiwemo mikopo na ruzuku
ili uwe endelelevu na wenye vyanzo anuai;
(m) Kuweka utaratibu wa ada na michango mbalimbali katika
shule na vyuo binafsi ili kusimamia kwa ufanisi masuala ya
ada na michango ;
(n) Kuandaa uta ratibu wa us hirikiano baina ya S ekta ya Umma,
Binafsi na Jamii katika ugharamiaji wa maendeleo ya elimu na
mafunzo katika ngazi zote ili kuhakikisha kwamba: –
(i) Mchango wa Sekta Binafsi katika kudahili wanafunzi
katika vyuo vya Ufundi ngazi ya kati unaongezeka
kutoka asi limia 21 mwaka 2015 hadi asilimia 25
mwaka 2020 ; na
(ii) Mchango wa Sekta Binafsi kudahili wanafunzi katika
ngazi ya shahada unaongezeka kutoka asilimia 35
mwaka 2015 hadi asilimia 40 mwaka 2020.
(iii) Bajeti ya Sekta ya Elimu na Mafunzo inaongezeka
kutoka asilimia 17.6 mwaka 2015 hadi asilimia 25 ya
bajeti ya Serikali mwaka 2020 ;
97
(iv) Bajeti ya Elimumsingi inaongezeka kutoka asilimia 71
mwaka 2015 hadi asilima 75 ya B ajeti ya Sekta ya
Elimu na Mafunzo mwaka 2020 ;
(v) Bajeti ya Elimu ya Ufundi na Elimu ya Juu inaongezeka
hadi kufikia asilimia 25 ya Bajeti ya Sekta ya Elimu na
Mafunzo ifikapo mwaka 2020 ; na
(vi) Kuendelea kusimamia Sera ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi ya mwaka 2015 ambayo inaifanya elimu ya
Msingi hadi S ekondari kuwa ya lazima na bila ya
malipo .
(o) Kuanzisha Tume ya Wal imu itakayosimamia Maendeleo na
Maslahi ya Walimu wote Nchini.
Maji
53. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali imeendelea kutekeleza
Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji kwa lengo la kuongeza
upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wa nanchi wote
hususan wale ambao wanaishi maeneo ya vijijini. Katika kipindi hicho
yafuatayo ni baadhi ya mafanikio yaliyopatikana: –
(a) Serikali imeend elea kuimarisha huduma za maji V ijijini kwa
kukarabati, kujenga na kupanua miundombinu ya maji, hali
iliyocha ngia upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama
Vijijini kuongezeka kutoka asilimia 53.5 mwaka 2005 hadi
kufikia asilimia 67.7 mwaka 2015;
(b) Serikali imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali yenye lengo la
kuboresha huduma y a maji safi na salama Mijini. Kut okana na
jitihada hizo, kiwango cha upatikanaji maji kwa wakazi wa Miji
Mikuu ya Mikoa kimeongezeka kutoka asilimia 74 mwaka 2005
hadi asilimia 86 mwaka 2014. Aidha, katika jiji la Dar es Salaam
pamoja na Miji ya Bagamoyo na Kibaha, kiwango cha
upatikanaji maji kimeongezeka kutoka asilimia 55 hadi asilimia
68 katika kipindi hicho.
(c) Maabara za maji 16 na Kituo cha Utafiti cha kuondoa madini ya
fluoride cha Ngurdoto kilichoko Arusha zimejengewa uwezo kwa
kuzipatia dawa za kufanyia uchunguzi, mashine pamoja na
98
usafiri. Aidha, maabara za maji katika mikoa ya Kigoma,
Singida, Shinyanga na Bukoba zimekarabatiwa ;
(d) Wananchi wameendelea kushirikishwa katika utekelezaji wa
miradi ya maji vijijini ambapo vyombo vya watumiaji maji
(COWSOs) 520 vimeundwa katika Halmasha uri mbalimbali
nchini ; na
(e) Usimamizi wa rasilimali za maji umeendelea kuimarishwa na
yamepatikana mafanikio yafuatayo: –
(i) Jumuiya 91 za Watumiaji Maji zimeundwa ; na
(ii) Maeneo 26 ya vyanzo vya maji yametathminiwa na
kuzungushiwa uzio pamoja na maeneo ya maji ch ini ya
ardhi ya Maisaka na Makutupora.
(f) Ujenzi wa mabwawa manne ya Nyambele (Bunda),
Kinyambwiga (Bunda) Nyashitanda (Misungwi) na New Sola
(Maswa) umekamilika na yamekabidhiwa kwa wananchi ;
(g) Mradi wa maji wa Kahama/Shinyanga umekamilika ambapo
upanuzi wa mradi unaendelea katika maeneo ya V ijiji
vilivyoainishwa pamoja na Miji iliyopo katika W ilaya hiyo.
Aidha, M ji wa Ngudu , wilayani Kwimba tayari umeunganishwa
kwenye mradi huo na wananchi wanapata maji ; na
(h) Upanuzi na ukarabati wa miundombinu ya majitak a
umefanyika katika M iji ya Moshi, Tanga, Arusha, Mbeya,
Iringa, Songea, Tabora, Mwanza, Morogoro, Dar es Salaam na
Dodoma.
99
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa
Nachingwea ma ra baada ya kuzindua mradi wa maji wenye thamani
ya Shilingi Bilioni 34.6 unaojumuisha Wilaya za Nachingwea na Masasi
Mkoani Mtwara.
54. Pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi kilichopita,
bado zipo changamoto mbalimbali katika kutekeleza miradi ya
maji nchini. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Chama Cha
Mapinduzi kitaielekeza Serikali kukabiliana na changamoto
hizo kwa kutekeleza yafuatayo: –
(a) Kuboresha huduma ya maji vijijini kutoka asilimia 67.7 mwaka
2015 hadi asilimia 85 mwaka 2020 kwa kuf anya yafuatayo: –
100
(i) Kuendelea kutekeleza lengo la kuwapatia wananchi
waishio vijijini huduma ya maji safi, salama na ya
kutosha kama yalivyo Malengo ya Milenia ;
(ii) Kujenga vituo vya kuchotea maji 93,051
vitakavyohudumia watu 23,262,876 ambavyo
vitaongeza idadi ya watu wanaopata huduma ya maji
safi na salama kutoka 20,022,283 mwaka 2015 hadi
kufikia 43,285,159 mwaka 2020 sawa na asilimia
53.7; na
(iii) Kuhamasisha ujenzi wa miundombinu ya kuvuna maji
ya mvua katika majengo ya Serikali, asasi za umma na
binafsi na nyu mba za watu binafsi.
(b) Kuboresha huduma ya Maji Mijini kwa kufanya yafuatayo: –
(i) Kuongeza upatikanaji wa huduma za maji katika Jiji la
Dar es Salaam kutoka asilimia 68 mwaka 2015 hadi
kufikia asilimia 95 mwaka 2020 ;
(ii) Kuongeza upatikanaji wa huduma za maji ka tika miji
mikuu ya mikoa kutoka asilimia 86 mwaka 2015 hadi
kufikia asilimia 95 mwaka 2020 ;
(iii) Kuongeza upatikanaji wa huduma za maji katika miji
mikuu ya wilaya, miji midogo na maeneo ya miradi ya
Kitaifa kutoka asilimia 57 mwaka 2015 hadi kufikia
asilimia 9 0 mwaka 2020 ; na
(iv) Kujenga Bwawa la Kidunda ili kuboresha huduma ya
maji katika Jiji la Dar es Salaam.
(c) Kukamilisha miradi mikubwa ya maji na kuhakikisha vijiji vyote
vilivyopo kando kando ya miradi hiyo mikubwa vinanufaika.
Miradi hiyo ni: –
(i) Mradi wa kut oa maji Ziwa Victoria kwenda Nzega,
Tabora na Igunga ;
(ii) Mradi wa Maji wa Chalinze awamu ya tatu ;
(iii) Mradi wa Maji wa Same – Mwanga – Korogwe ; na
101
(iv) Miradi ya Maji katika miji mikuu ya mikoa mipya ya
Geita, Simiyu, Njombe na Katavi.
(d) Kupanua na kuboresha miradi ya maji ya kitaifa ifuatayo: –
(i) Mradi wa Wanging’ombe, Maswa, Mugango -Kiabakari,
Handeni Trunk Main (HTM), Chalinze, Makonde na
Kahama -Shinyanga ; na
(ii) Mradi wa kutoa maji kutoka Mto Ruvuma kwenda Mji
wa Mtwara ili kukidhi mahitaji ya maji katika uka nda
huo kutokana na ongezeko la watu na shughuli za
uwekezaji baada ya kugundulika kwa gesi asilia.
(e) Kuanzisha miradi ya ujenzi wa mabwawa katika mikoa yenye
ukame kama ifuatavyo: –
(i) Ujenzi wa mabwawa ya kuvuna maji ya mvua kwa
ajili ya matumizi ya binad amu, mifugo na kilimo
katika mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, Mara,
Simiyu, Arusha, Shinyanga, Manyara na maeneo
mengine yenye ukame ;
(ii) Ujenzi wa mabwawa manane ya kimkakati kwa ajili ya
kuhifadhi mazingira, kuzuia mafuriko na matumizi
mengine ; na
(iii) Kukamilisha ukarabati wa mabwawa ambayo tayari
yamekwisha jengwa.
55. Shughuli nyingine zitakazofanyika ili kuboresha huduma ya
upatikanaji wa maji mijini na vijijini ni kama ifuatavyo: –
(a) Kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwenye vijiji
vinavyozunguka ma ziwa ya Tanganyika, Nyasa na Victoria ;
(b) Kuendelea na uchimbaji wa visima vya maji na kutumia
pampu za maji zinazotumia nishati ya jua ;
(c) Kuiwezesha S ekta Binafsi kutoa huduma ya maji safi kwa
mfumo wa ubia na Sekta ya Umma;
(d) Kuendelea kuhamasisha wananchi kuu nda Jumuiya za
Watumia Maji Vijijini katika Mabonde yote ya maji nchini
102
ifikapo mwaka 2020 ili kuwashirikisha wananchi kikamilifu
katika kupanga, kujenga, kuendesha na kumiliki miradi ya
maji;
(e) Kujenga na kukarabati Maabara za Maji kwa ajili ya
kusimamia ub ora wa maji nchini na kutoa taarifa za hali ya
ubora wa maji kila mwaka ;
(f) Kuziongezea uwezo wa kiutendaji taasisi zinazoshughulika na
Sekta ya Maji ambazo ni Chuo cha Maji, Wakala wa Uchimbaji
Visima na Ujenzi wa Mabwawa na Bohari Kuu ya Maji ili
kuongeza u fanisi wa taasisi hizo ;
(g) Kuendelea kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika matumizi
endelevu na usimamizi bora wa rasilimali za maji shirikishi ;
(h) Kuweka mfumo madhubuti na endelevu wa utunzaji wa
vyanzo vya maji na udhibiti wa uchafuzi wa vyanzo hivyo ;
(i) Kufany a tafiti za upatikanaji maji chini ya ardhi katika maeneo
mbalimbali nchini ili kuendeleza rasilimali hiyo kwa matumizi
mbalimbali ;
(j) Kuimarisha mtandao wa ukusanyaji takwimu za rasilimali za
maji kwa ajili ya kupata taarifa sahihi za hali ya rasilimali za
maji nchini ili kuwezesha mgawanyo mzuri wa maji na
kupunguza migogoro baina ya watumia maji ; na
(k) Kuanzisha Mfuko wa Maji wa Taifa (National Water
Investment Fund) kwa ajili ya kuharakisha ujenzi wa miradi
nchini.
Majitaka
(a) Kuongeza kasi ya ujenzi wa miundomb inu ya uondoshaji majitaka
nchini.
(b) Kuiwezesha Sekta B inafsi kutoa huduma ya majitaka kwa mfumo
wa ubia na Sekta ya U mma.
SURA YA TANO
UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI
103
56. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali imeendelea kutekeleza
Sera ya Taifa y a Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa kuanzisha na
kuendesha program u za kukabiliana na changamoto za umasikini kwa
wananchi na ukosefu wa ajira hususan kwa vijana ambapo mafanikio
yafuatayo yamepatikana: –
(a) Dhamana ya mikopo yenye jumla ya shilingi bilioni 10. 5
imetolewa na kuwanufaisha wana nchi 10,646 katika vikundi 300
kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Mtwara, Mbeya,
Rukwa, Singida, Dodoma, Manyara, Ruvuma, Tanga, Kagera na
Lindi;
(b) Kuanzishwa kwa mafunzo ya ujasirimali kwa vijana wahitimu wa
Vyuo Vikuu y enye lengo la kuwawezesha kujiajiri kwa kutumia
fursa zilizopo badala ya kutegemea ajira za sekta rasmi ;
(c) Kampuni 1,728 zimesajiliwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Sekta
Binafsi Tanzania (TPSF) ambapo Kampuni 786 zilipata kiasi cha
shilingi bilioni 7.8 kama mitaji kwa ajili ya kuanzisha na
kuendeleza miradi ya kiuchumi ;
(d) Mfuko wa Ufundi na Utafiti umeanzishwa kwa ushirikiano na
Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), ambapo kiasi cha Shilingi bilioni
16.5 zilitolewa kwa vyuo tisa vya Elimu ya Juu kati ya vyuo 49
vilivyotuma maombi kwa ajili ya vifaa vya kufundishia ;
(e) Uhamasishaji wa kuanzisha Ushirika wa Kuweka na Kukopa
(SACCOS na VICOBA) umewezesha SACCOS kuongezeka kutoka
1,875 mwaka 2005 hadi 9,468 mwaka 2013 . Idadi ya VICOBA
imeongezeka hadi kufikia 23,000 mwaka 2 015 vyenye
wanachama 700,000 na mtaji wa Shilingi bilioni 86 . Aidha,
wanachama wa SACCOS na vikun di vingine vya kijamii m ilioni
1.6 wamepatiwa mafunzo ya ujasiriamali. Kati ya hao, wanawake
ni asilimia 53 na w anaume ni asilimia 47.
(f) Shirikisho la Mafundi Se remala limeanzishwa kwa lengo la
kuboresha uzalishaji wa samani ili kukidhi mahitaji ya soko la
ndani na nje ;
104
(g) Mfuko wa Uwezeshaji Wajasiriamali Wadogo umeboreshwa na
mafanikio yafuatayo yamepatikana: –
(i) Mikopo imeongezeka kutoka shilingi bilioni 25.1 mwaka
2010 hadi kufikia bilioni 57.7 mwaka 2014 na kunufaisha
wajasiriamali 95,336. Aidha, urejeshaji wa mikopo
umefikia asilimia 93.8 ; na
(ii) Mfuko umeongeza ajira 650,000 na kuzijengea uwezo
asasi ndogo ndogo za kifedha 590. Aidha, wajasiriamali
8,665 wamepati wa ujuzi wa kuendesha biashara zao.
(h) Mfuko wa Udhamini wa Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati
kupitia Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa Mauzo ya Bidhaa
Nje, umeongezewa mtaji kutoka Shilingi bilioni 6 mwaka 2010
hadi shilingi bilioni 30.81 mwaka 2014. Aidha, mf uko umetoa
dhamana ya Shilingi milioni 448.59 ambapo asilimia 80 ya
dhamana imetumika kuwezesha shughuli za kilimo,
kuhamasisha uundaji wa mfumo wa Stakabadhi za Mazao
Ghalani na kuchochea watu wengi kufanya biashara ya mauzo
ya nje ; na
(i) Mikopo yenye thaman i ya shilingi bilioni 50.03 imetolewa kwa
wajasiriliamali chini ya mpango wa uwezeshaji wananchi
kiuchumi na kuongeza ajira. Mikopo hiyo imetolewa kupitia
Benki za CRDB na NMB na kuwanufaisha wajasiriamali
74,701.
57. Kwa kutambua kwamba kuwawezesha wananchi kiuchumi ni
hatua ya msingi katika kujenga Taifa lililoimarika kiuchumi na
lenye lengo la kujitegemea, katika kipindi cha miaka mitano
ijayo, Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza Serikali kutekeleza
yafuatayo: –
(a) Kuhakikisha kuwa shughuli zote zenye mwelekeo wa ushirika
zinapewa msukumo stahiki kwa kuhamasisha na kusimamia
kwa nguvu uanzishaji wa vikundi vya ushiri ka kama vile
SACCOS na VICOBA; Vyama vya Mazao, Ufugaji na Uvuvi
105
hasa ikizingatiwa kuwa ushirika ndiyo silaha kuu ya wanyonge
na nguzo kuu ya ujenzi w a Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ;
(b) Kuweka mfumo wa kuvitambua, kuvisajili na kuviwezesha
vikundi vyote vyenye mwelekeo wa ushirika na ujasiriamali ;
(c) Kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kuhakikisha kwamba
fursa ya mikopo kwa ajili ya mitaji inapatikana bila ya urasimu
na kwa masharti nafuu na kuwafikia wananchi wengi mijini na
vijijini ;
(d) Kutenga kiasi cha shilingi milioni 50 kwa kila Kijiji kama Mfuko
wa Mzunguko (Revolving Fund) kwa ajili ya kukopesha
vikundi vya wajasiriamali kupitia Ushirika wa Kuweka na
Kukopa (SACCOS) katika vijiji husika ;
(e) Kusaidia wafanyabiashara wadogo kwa kufanya yafuatayo: –
(i) Kutenga maeneo mahsusi katika kila Halmashauri
kwa ajili ya biashara ndogo ndogo ;
(ii) Kuondoa kero na malalamiko kuhusu ushuru na kodi
zinazoto zwa na Halmashauri ambaz o zina kwamisha
jitihada za wafanyabiashara wadogo kujikwamua
kimaisha ;
(iii) Kuwarasimisha wafanyabiashara wadogo ili biashara
zao zitambuliwe kisheria kwa kuwapatia leseni,
mafunzo ya ujasiriamali na kuwaunganisha na asasi
za fedha ili wapate mikopo yenye masha rti nafuu ;
(iv) Kuanzisha Ma mlaka ya Usimamizi wa Biashara Ndogo
na za K ati;
(v) Kuanzisha mfuko mkubwa wa kitaifa wa wajasiriamali
wadogo na wa kati kwa kushirikiana na Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii na asasi nyingine za fedha ;
(vi) Kuweka utaratibu uta kaozitaka Halmasha uri kutenga
asilimia 30 ya thamani ya manunuzi yake kwa ajili ya
biashara, kampuni au vikundi vinavyomilikiwa na
vijana/wanawake ; na
106
(vii) Kuhakikisha kazi za ujenzi unaogharamiwa na Serikali
katika maeneo ya vijijini kwa mfano ujenzi wa
barabara, shule na zahan ati zinatolewa kwa vikundi
vya vijana na wanawake katika maeneo husika.
(f) Kuhamasisha ushiriki wa Sekta Binafsi katika uwekezaji kwa
kufanya yafuatayo: –
(i) Kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Ubia baina ya
Sekta ya Umma na Sekta Binafsi na kukamilisha
marekebis ho ya Sera na Sheria ya Uwekezaji na
pia kuandaa Sera ya Maendeleo ya Sekta Binafsi ;
(ii) Kuondoa vikwazo vya kuanzisha na kuendesha
biashara kwa kupitia upya Sheria, Kanuni na
Taratibu za biashara ili kuvutia uwekez aji kutoka
ndani na nje ya nchi; na
(iii) Kuhamasi sha Sekta Binafsi kushiriki katika miradi
ya ubia na sekta ya umma pamoja na kuandaa
mazingira rafiki ya biashara kwa lengo la kuvutia
uwekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Urasimishaji Mali za Wanyonge :
58. Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyon ge
Tanzania (MKURABITA) ulianzishwa kwa lengo la
kuwawezesha wananchi na kuwapa nguvu ya kiuchumi hasa
wanyonge mijini na vijijini kwa kuwawezesha kumiliki ardhi na
kufanya biashara katika mfumo rasmi wa kisasa
unaoendeshwa kwa mujibu wa Sheria. Hivyo, kup itia
urasimishaji rasilimali na biashara, MKURABITA ni nyenzo
muhimu ya uwezeshaji wananchi kiuchumi, kupunguza
umas ikini na kuongeza ajira nchini. Katika kipindi cha miaka
mitano ya Ilani hii ya 2015 -2020, Chama Cha Mapinduzi
kitaielekeza Serikali kutekel eza yafuatayo: –
(a) Kuongeza kasi ya utambuzi, usajili na umiliki wa ardhi pamoja
na kuendeleza urasimisha ji wa rasilimali za wananchi,
107
kuwashirikisha na kuwawezesha kutumia rasilimali zao kama
dhamana ya kupata mitaji;
(b) Kutekeleza mipango ya matumizi bora ya a rdhi kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali wa ardhi wakiwemo Tume
ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi na
Halmashauri za Miji, Majiji na Wilaya ili kukamilisha kazi ya
upimaji wa mipaka ya vijiji vyote na kuwahamasisha wananchi
kuchangia upimaji wa mashamba yao na kuwapatia hati miliki
za kimila;
(c) Kuanzisha chombo cheye nguvu ya kisheria kitakachoratibu
shughuli za urasimishaji rasilimali za wananchi; na
(d) Kuanzisha Mfuko Maalumu wa kugharamia shughuli za
urasimishaji amb ao utaziwezesha Halmashauri za Wilaya, Miji
na Majiji kukopeshwa kwa masharti nafuu. Mfuko huu
utaendeshwa kwa utaratibu wa Dhamana ya Benki ( Bank
Guarantee Scheme) .
Kuwawezesha Vijana Kujiajiri
59. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali imeendelea kutekeleza
mipango mbalimba li ya kuongeza ajira kwa vijana kwa kuanzisha na
kuendesha programu za kukabiliana na ongezeko kubwa la vijana
wanaofuzu Elimu ya Msingi, Sekondari, Vyuo na Vyuo Vikuu kila mwaka
wanaohitaji ajira ambapo mafanikio yafuatayo yamepatikana: –
(i) Takriban vijana m ilioni 16 wameajiriwa katika sekta
mbalimbali nchini katika k ipindi cha mwaka 2011 hadi 2015;
(ii) Mikopo ya masharti nafuu yenye thamani ya Shilingi bilioni
5.8 imetolewa kwa SACCOS 244 na vikundi vya vijana 667
katika kipindi cha 2014/15 ;
(iii) Jumla ya vijan a 35,000 wamepewa mafunzo ya ujasiriamali
ambapo kati yao , vijana 11,500 wa likuwa wahitimu wa elimu
ya juu; na
(iv) Wahitimu 325 wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine ,
wamepatiwa mafunzo ya ujasiriamali pamoja na kuwezeshwa
108
kupata mitaji kupitia ushirikiano wa Seri kali na Umoja wa
Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUGECO).
60. Chama Cha Mapinduzi kinatambua umuhimu wa vijana ambao
ni kundi kubwa la nguvukazi. Changamoto zinazowakabili ni
pamoja na ukosefu wa ajira, elimu na maarifa ya kisasa katika
uzalishaji mali, mitaji, biashara na ujasiriamali. Katika kipindi
cha utekelezaji wa Ilani hii, Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza
Serikali kufanya yafuatayo: –
(a) Kuhakikisha kwamba Halmashauri zote nchini zinaendelea
kutenga, kurasimisha, kupima na kuyawekea miundombinu
maeneo maalum u ya vijana kwa ajili ya shughuli za uzalishaji
mali katika sekta mbalimbali hususan kilimo, ufugaji, madini,
viwanda vidogo, uvuvi, mawasiliano na biashara;
(b) Kuziwezesha SACCOS za vijana katika Halmashauri zote nchini
kupata mikopo kutoka kwe nye ben ki na taasisi nyingine za
fedha;
(c) Kuwajengea uwezo vijana kutumia TEHAMA katika kuboresha
uzalishaji mali, ufanisi, viwango na kutafuta masok o katika
shughuli zao za uchumi;
(d) Kuwawezesha vijana wanaohitimu Elimu ya Juu na Vyuo vya
Ufundi kuunda makamp uni kulingana na fani zao kwa lengo la
kuwapatia mitaji na nyenzo kupitia taasisi za fedha na mifuko
mingine ya uwezesha ji;
(e) Kuhamasisha na kuweka mazingira yatakayowezesha vijana
wajasiriamali wadogo kujiunga na M ifuko ya Hifadhi ya J amii
ili kuweza kupata mikopo na kunufaika na mafao meng ineyo
yatolewayo na mifuko hiyo;
(f) Kuviwezesha Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs) ili
viweze kutoa mafunzo ya ujasiriamali, stadi za maisha, ujasir i,
uongozi na TEHAMA kwa vijana;
(g) Kuhakikisha Halmashauri zote nchini zinaa nzisha vituo
maalum u ili kuwawezesha vijana kupata sehemu ya kujifunza
109
kwa vitendo shughuli mbalimbali za ujasiriamali na kupata
taarifa mbalimbali za maendeleo;
(h) Kuwawezesha vijana wanaohitimu Vyuo V ikuu na Vyuo vya
Kati kufanya kazi kwa kujitolea katika asasi mbalimbali kwa
lengo la kuwapatia uzoefu na maadili ya kazi ili waweze
kuajirika au kujiajiri wenyewe ; na
(i) Kuhakikisha kwamba Halmashauri zote nchini zinaendelea
kutenga fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Vijana
kwa mujibu wa Sheria ili kuwezes ha upatikanaji wa mikopo
yenye masharti nafuu.
Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi
61. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, jitihada za kuwaendeleza
wanawake zimeendelea kuchukuliwa kwa kutunga Sera, Sheria na
Programu mbalimbali zenye lengo la kuongeza furs a za kiuchumi na
kuwajengea uwezo wa kitaaluma, kibiashara, mbinu za kupata mitaji,
masoko pamoja na mikopo.
62. Fursa hizo zimewawezesha wanawake kujiajiri katika shughuli
mbalimbali za kiuchumi na hivyo kuinua vipato vyao na vya familia.
63. Kwa kutambua kuw a uwezeshwaji wa wanawake kiuchumi
umeleta maendeleo na mabadiliko makubwa kwa wanawake,
familia na Taifa kwa ujumla na kwa kutambua kuwa wanawake
ndio wazalishaji wakuu wa chakula na walezi wa familia,
Chama Cha Mapinduzi, katika miaka mitano ijayo, kitai elekeza
Serikali kuendelea kuwaendeleza wanawake kiuchumi kwa
kufanya yafuatayo: –
(a) Kuendelea kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu, elimu ya
ujasiriamali na biashara ili kuwawezesha kuongeza ajira, ujuzi
wa kujiajiri, fursa za kipato na kujikimu ;
(b) Kuwahamas isha kuanzisha na kujiunga katika vikundi vya
uzalishaji mali, vikundi vya kuweka na kukopa (SACCOS na
110
VICOBA) na kuwawezesha kimtaji ili kupanua shughuli zao za
uzalishaji mali ;
(c) Kuwahamasisha kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ili
kuweza kupata mikop o na kunufaika na mafao mengineyo
yatolewayo na mifuko hiyo hasa mafao ya uzazi na elimu ;
(d) Kuhakikisha kwamba Halmashauri zote nchini zinaendelea
kutenga fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya
Wanawake kwa mujibu wa Sheria ili kuwezesha upatikanaji
wa mi kopo yenye masharti nafuu ; na
(e) Kuondoa kero na malalamiko ya wanawake wajasiriamali hasa
mama lishe, wauza mbogamboga, wauza maandazi/vitumbua
kuhusu maeneo ya kufanyia biashara, ushuru na kodi
zinazotozwa na Halmashauri ambazo zinakwamisha jitihada
zao za kujikwamua kimaisha.
111
SURA YA SITA
MAZINGATIO MAALUMU YA ILANI KUHUSU ZANZIBAR
Mwenyekiti wa CCM Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiwatambulisha
Mgombea wa CCM wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu
John Pombe Magufuli (kulia) na Mgom bea wa CCM wa Urais wa Zanzibar
Ndugu Mohamed Shein
112
Utangulizi
64. Katika Sura hii, Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 – 2020,
inaelezea na kuainisha maeneo muhimu ya Sera za CCM, kwa kuzingatia
mazingira maalumu ya Zanzibar (SMZ) . Kwa kutambua na kur idhika na
Sera hizo ambazo zinazingatia maslahi mapana ya Taifa letu yaani haki,
umoja, mshikamano, uwazi na uwajibikaji , Wazanzibari wameendelea
kuiunga mkono CCM na kuipa ridhaa ya kuongoza Serikali ya Mapinduzi
kwa kuichagua katika chaguzi zote zilizopi ta.
65. Katika kipindi cha mwaka 2010 – 2015 cha Awamu ya Saba ya Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar, chini ya uongozi wa Dkt. Ali Mohamed Shein,
Zanzibar imeendelea kupiga hatua kubwa ya maendeleo kisiasa,
kiuchumi na kijamii.
MAFANIKIO NA MALENGO YA KIUCHU MI
66. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi mahiri wa Dkt. Ali
Mohamed Shein imeweza kutekeleza kwa mafanikio makubwa, Ilani ya
CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 – 2015 na kuendelea
kuimarisha umoja wa kitaifa na utoaji wa huduma mbalimbali za
kiuchumi na kijamii. Baadhi ya mafanikio hayo ya kujivunia ni kama
yafuatayo: –
Hali ya Uchumi
67. Katika miaka mitano iliyopita Sekta ya Uchumi imepata mafanikio
yafuatayo: –
(a) Kukuza Uchumi:
(i) Pato la Taifa limeongezeka kutoka thamani ya Shiling i
bilioni 1,050.8 mwaka 2010 hadi kufikia thamani ya
Shilingi bilioni 2,138.5 mwaka 20 14. Kiwango cha
ukuaji wa uchum i kiliongezeka kutoka asilimia 4.3
mwaka 2010 hadi asilimia 7.0 mwaka 2014;
(ii) Mfum uko wa bei umeshuka kutoka asilimia 6.1
mwaka 2010 hadi asilimia 5.6 mwaka 2014 ;
113
(iii) Pato la kila mwananchi limeongezeka kutoka shilingi
856,000 sawa na dola za Kimarekani 613 mwaka
2010 na kufikia shilingi milioni 1.56 sawa na Dola 939
mwaka 2014 ;
(iv) Kiwango cha thamani ya bidhaa zilizosafirishwa nje,
kiliongezeka kutoka shilingi bilioni 18 mwaka 2010
hadi kufikia shilingi bilioni 133.6 mwaka 2014 ; na
(v) Kiwango cha ukusanyaji wa mapato ya ndani
kimeongezeka kutoka shilingi bilioni 181.379 mwaka
2010/2011 had i shilingi bilioni 330.7 mwaka
2013/2014.
(b) Maeneo Huru ya Kiuchumi
(i) Mpango Mkuu wa Matumizi ya Ardhi (Land Use Plan)
wa eneo Huru la Kiuchumi la Fumba, umekamilika.
Jumla ya hekta 3,000 zimewekewa mipaka na
kugawanywa katika eneo la vijiji vya asili (hekta
1,310), eneo la uwekezaji (hekta 743) na eneo la
akiba (hekta 947 ). Aidha, maandalizi ya kulifungua
kiuchumi Eneo Huru la Kiuchumi la Micheweni,
yanaendelea.
(ii) Hadi kufikia mwaka 2014, jumla ya miradi 165, yenye
mtaji wa thamani ya Dola za Kimarekani milioni 526.7
imeidhinishwa kuwekezwa na Maml aka ya Uwekezaji
Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) ikilinganishwa na
miradi 33 mwaka 2010 yenye mtaji wa thamani ya
Dola za Kimarekani milioni 115.2. Miradi 63 kati ya
hiyo, ni ya wawekezaji Wazalendo, na 90 ni ya
wageni. Miradi hiyo yote inazalisha ajira zi patazo
6,658 kwa wananchi.
(c) Uwakilishi wa Sekta Binafsi:
Baraza la Biashara la Zanzibar limeanzishwa na kushiriki
katika majadiliano ya ubia wa uwekezaji kwa maendeleo ya
viwanda na mashirikiano kwa ajili ya wote( Smart Partneship
Dialogue ). Miongoni mwa yaliyojadiliwa katika vikao hivyo ni
114
pamoja na kuimarisha mapato, kukuza Pato la Taifa na
Faharisi ya Bei ya mtumiaji.
(d) Mazingira Bora ya Kiuchumi:
Sheria ya Fedha na Uwekezaji imefanyiwa mapitio ili iendane
na mazingira halisi ya kiuchumi na kutoa n afasi zaidi ya
kuzitangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini. Kutokana na
hatua hizo, wawekezaji kutoka nje wameweza kujitokeza na
kuwekeza katika miradi ya maendeleo .
(e) Kupambana na Umasikini:
(i) Mifuko ya mikopo kwa wananchi na wafanyabiashara
wadogo wadogo, yaani Mfuko wa Kujitegemea na
Mfuko wa JK & AK imeunganishwa pamoja na
kuanzishwa mfuko mmoja tu (Mfuko wa
Kuwawezesha Wananchi Kiuchumi). Mfuko huo
umezinduliwa ukiwa na mtaji wa shilingi bilioni 2.31 .
Aidha, mikopo 1,603 yenye thamani ya shiling i bilioni
1.45, imetolewa katika shehia 305 Unguja na Pemba
na kutoa ajira za moja kwa moja 20,614,
zilizowahusisha w anawake 11,873 na wanaume
8,741;
(ii) Utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mfuko wa Maendeleo
ya Jamii (TASAF II) umekamilika ambapo miradi 656
yenye thamani ya S hilingi bilioni 9.4 imetekelezwa.
Kati yake miradi 324 ni ya Unguja na 332 ni ya
Pemba. Miradi hiyo inahusu shughuli za kijamii, uvuvi
(ununuzi wa boti na zana za kuvulia) pamoja na
mapambano dhidi ya UKIMWI.
(iii) Utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya M fuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF III) umeanza katika
Shehia 40 za Unguja na Pemba (Unguja 20 na Pemba
20) ambapo miradi 103 (Unguja 68 na Pemba 35)
yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.1 imeanzishwa.
Miradi hiyo inahusu ujenzi wa skuli za maandalizi,
ujenz i wa matuta ya kuzuia maji ya bahari, hifadhi ya
115
mazingira na ukarabati wa njia za ndani. Jumla ya
kaya masikini 6,598 zimenufaika na miradi hiyo.
(iv) Vikundi vya kiuchumi 250 na wajasiriamali 6,000
wamepatiwa mafunzo ya ujasiriamali,
wakiwemo wahitimu wa vy uo vikuu 250, ili kubadili
mitazamo yao na kuwajengea uwezo wa kujiajiri wao
wenyewe ; na
(v) Kituo cha kulelea wajasiriamali kimeanzishwa. Kituo
hicho ni cha kwanza na cha aina yake katika ukanda
wa Afrika Mashariki, na kinatoa mafunzo katika fani
za Uchumi, TEHAMA, Utalii na U sindikaji wa Mazao ya
Biashara.
Kukuza Uchumi
68. Katika kipindi kilichopita (2010 -2015), Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar chini ya uongozi wa CCM, imefanikiwa kwa
kiwango kikubwa kukuza uchumi na kuimarisha huduma za
kiuchumi na kijamii . Katika kipindi cha miaka mitano ijayo
(2015 -2020), CCM itaendeleza mafanikio hayo na kuandaa
Mipango ya kipaumbele ili kufanikisha huduma za kilimo, utalii
endelevu pamoja na kujenga mazingira bora ya biashara na
kuimarisha huduma za jamii kwa kutekeleza yafuatayo: –
(a) Kufanya mapitio ya Mpango wa Kukuza Uchumi na
Kupunguza Umasikini (MKUZA) na kuandaa mkakati mpya wa
utekelezaji wa Mpango huo (MKUZA III) na Dira ya
Maendeleo ya Zanzibar (Vision 2020) ;
(b) Kujenga mazingira yatakayowezesha uchumi wa Zanz ibar
kufikia kiwango cha uchumi wa nchi zenye kipato cha kati,
kiwango cha ukuaji wa uchumi kufikia wastani wa asilimia 10,
mfumuko wa bei kubaki katika tarakimu moja na wastani wa
pato la kila mwananchi kuongezeka kutoka kiwango cha sasa
cha wastani wa do la za Kimarekani 939 (shilingi 1,340,000)
hadi dola 1950 (shilingi 3,500,000) ifikapo mwaka 2020 ;
116
(c) Kuendeleza udhibiti wa mapato na nidhamu katika matumizi
ya Serikali, kuziba mianya ya uvujaji wa mapato ya Serikali na
kuanzisha Msimamizi wa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu ;
na
(d) Kupunguza utegemezi kwa Wahisani wa Maendeleo,
misamaha ya kodi isiyo na tija kwa Taifa na kuongeza
kiwango cha ukusanyaji wa mapato ya ndani kutoka Shilingi
bilioni 330.7 mwaka 2013/2014 hadi kufikia Shilingi bilioni 800
ifikap o mwaka 2020/21 na kushusha kiwango cha nakisi ya
Bajeti ya Serikali kutoka uwiano wa asilimia 8 ya Pato la Taifa
mwaka 2014/2015 hadi kufikia asilimia 7 ifikapo mwaka
2019/2020.
Mchango wa Sekta Binafsi
69. Sekta Binafsi hutoa mchango mkubwa katika kukuza u chumi na
maendeleo ya Taifa. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010 –
2015), Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA),
iliidhinisha jumla ya miradi 35 yenye thamani ya dola za Kimarekani
bilioni 1.06 na kutengeneza ajira 1,365. Ili kuongez a mchango wa Sekta
Binafsi katika kukuza Uchumi wa Zanzibar, Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar chini ya uongozi wa CCM, itatekeleza yafuatayo: –
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sera, Mw ongozo na Sheria ya
Ushirikiano b aina ya Sekta ya Umma na Sekta B inafsi na
kuharakisha utekelezaji wa miradi yenye tija inayopendekezwa
kufanyika ;
(b) Kukamilisha utekelezaji wa Mpango wa uendelezaji wa mji mpya
wa kisasa katika Maeneo Huru ya Uchumi ya Fumba na
Micheweni, na kuweka vivutio kwa wawekezaji wa Sekta ya
Viwanda ; na
(c) Kujen ga mazingira endelevu ya kuwawezesha kimtaji
wawekezaji wa ndani na kuwaunganisha na wawekezaji wa nje
pamoja na kuv ishawishi Vyombo na Taasisi za F edha nchini,
kuwapatia mikopo yenye riba na masharti nafuu na kupunguza
117
urasimu na vikwazo katika biashara, ukiwemo mlolongo wa
leseni na kodi.
Kupambana na Umasikini
70. Ili kuongeza nguvu na kasi ya kupambana na umasikini katika kipindi
kilichopita (2010 -2015), Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
umeanzishwa. Kwa kupitia mfuko huo wananchi wengi hususan vijana,
wanawake na wafanyabishara wadogo wadogo wameweza kupatiwa
mitaji (mikopo) na kujikwamua kiuchumi. Katika kipindi cha miaka
mitano ijayo (2015 -2020), CCM itaendeleza jitihada hizo na kuielekeza
Serikali kutekeleza yafuatayo: –
(a) Kuendelea kuimarisha Mfuko wa Uwezeshaji wa Wananchi
Kiuchumi ili kuongeza uwezo wake wa kutoa mikopo kwa
wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo , kuimarisha Kituo cha
Kulelea Wajasiriamali na kuendelea kutoa mafunzo mbalimbali ili
kuwajengea uwezo wa kujiajiri na kuondokana na umasik ini;
(b) Kuendelea kuwahamasisha wananchi kuunda vikundi vya ushirika
na hasa ushirika wa uzalishaji mali, vikundi vya kuweka na kukopa
(SACCOS), VICOBA pamoja na BENKI NDOGO vyenye wanachama
wengi na kuleta tija kwa jamii ;
(c) Kuimarisha Mfuko wa Maendeleo ya Jam ii (TASAF) ili kukamilisha
Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF III) na
kubuni programu nyingine za kusaidia jamii kupambana na
umasikini ; na
(d) Kuendelea kuimarisha na kusimamia Mfuko wa Maendeleo ya
Jimbo na kuhakikisha kwamba, fedha za mf uko huo zinatumika
kwa lengo lililokusudiwa na hususan kuimarisha huduma za jamii.
(e) Kuzihamasisha asasi za kifedha nchini kuanzisha dirisha maalumu
kwa ajili ya kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu wanawake
na vijana. Aidha, idara maalumu ya mikopo itaanzi shwa ili
kusimamia majukumu yafuatayo: –
(i) Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Asasi za Mikopo Nafuu
(Micro -Finance Policy) ili kuwawezesha wananchi wengi
zaidi kunufaika na huduma za kifedha kwa masharti nafuu ;
118
(ii) Kutoa mikopo 5,000 yenye thamani ya shilingi bilio ni 2.5
itakayowanufaisha jumla ya wananchi 50,000 kutoka
makundi mbalimbali ya jamii hususan wanawake, vijana na
walemavu Unguja na Pemba ;
(iii) Kuimarisha huduma za mikopo kwa kutumia njia mbalimbali
ikiwemo teknolojia ya mitandao ya simu ili kupunguza
gharama na muda wa upatikanaji na urejeshaji wa fedha za
mikopo ; na
(iv) Kuongeza kiwango cha dhamana ya Serikali katika benki
kutoka shilingi milioni 100 hadi shilingi milioni 500 ili ziweze
kuwahudumia wajasiriamali 50,000.
(f) Kuanzisha jumla ya vituo kumi vya huduma za biashara, kimoja
kwa kila Wilaya ili kuongeza tija katika shughuli za wajasiriamali
na wafanyabiashara wadogo.
Sekta za Uzalishaji Mali
Kilimo
71. Sekta ya Kilimo inachangia asilimia 31 katika Pato la Taifa (GDP) na
kuwawezesha wananchi walio wengi kujikim u kimaisha na kuwapatia
uhakika wa chakula na lishe bora. Katika kipindi cha miaka mitano
iliyopita, Sekta ya Kilimo imepata mafaniko yafuatayo: –
(a) Sera ya Masoko na Bidhaa za Kilimo imepitishwa na kuanza
kutumika. Sheria ya kuanzishwa kwa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo
Zanzibar, Sheria ya Haki Miliki za Wagunduzi wa aina mpya za
mbegu za mimea, Sheria ya Uhifadhi na Utibabu wa Mimea na
Sheria ya Uhakika wa Chakula na Lishe zimepitishwa ;
(b) Mashamba darasa 1,200 ya wakulima yameanzishwa. Wakulima
2,800 wa zao la m punga na 1,500 wa zao la muhogo na mboga
mboga wamepatiwa mafunzo. Jumla ya tani 674,334 za mazao
ya chakula zimezalishwa mwaka 2014 ikilinganishwa na tani
346,535 zilizovunwa mwaka 2013. Ongezeko hilo ni sawa na
asilimia 95 ;
(c) Jumla ya matrekta mapya 45 yam enunuliwa, matrekta
makongwe 37 yamefanyiwa matengenezo na mashine za
kuvunia mpunga 14 zimenunuliwa. Eneo la uzalishaji wa zao la
119
mpunga limeongezeka kutoka hekta 10,000 mwaka 2010 hadi
hekta 34,000 mwaka 2015. Kiwango cha uzalishaji wa zao hilo
kimeongez eka kutoka tani 20,000 hadi tani 33,655. Idadi ya
kaya zinazojishughulisha na kilimo imeongezeka kuto ka 10,000
mwaka 2010 hadi 70,000 mwaka 2014 ;
(d) Mafunzo ya nadharia na vitendo yametolewa kwa wakulima 400
juu ya mbinu za kilimo bora cha mpunga wa umwagilia ji.
Wakulima 2,000 (700 Pemba na 1,300 Unguja) walipatiwa
mafunzo juu ya mbinu bora za uzalishaji mpunga ;
(e) Eneo la kilimo cha umwagiliaji limeongezeka kutoka hekta 600
mwaka 2010, hadi hekta 800 mwaka 2014. Jumla ya hekta 200
za miundombinu ya umwagiliaji m aji zimeimarishwa. Kiwango
cha uzalishaji wa mpunga wa kumwagilia maji kimeongezeka
kutoka tani 2 mwaka 2010 hadi tani 4 kwa hekta mwaka 2014 ;
(f) Matumizi ya pembejeo kati ya mwaka 2010 hadi 2015
yameongezeka kutoka tani 13 hadi 750 za mbegu tani 203 hadi
1,500 za mbolea na lita 10,000 hadi 30,000 za dawa ya kuulia
magugu. Wakulima 61,500 wa mpunga wa kumwagilia maji na
wa kutegemea mvua wamepatiwa ruzuku ya bei za pembejeo
(asilimia 75) ;
(g) Vikundi 33 vya wakulima 65 2 (wanawake 345 na wanaume
307) vimeanzishwa na kupatiwa mafunzo ya kilimo cha
mbogamboga na matunda ;
(h) Chuo cha Kilimo cha Kizimbani kimeimarishwa. Idadi ya
wanafunzi wa ngazi ya cheti imeongezeka kutoka 300 mwaka
2010 hadi 741 mwaka 2014. Mafunzo ya Stashahada katika fani
ya uzalishaji mifugo na uza lishaji wa mazao na kilimo
mjumuisho yameanza kufundishwa ;
(i) Kituo cha Utafiti cha Kizimbani kimepandishwa hadhi kuwa
Taasisi kamili ya Utafiti wa Kilimo. Ujenzi wa maabara mpya ya
utafiti wa zao la mpunga na ukarabati wa maabara ya udongo
na maabara ya usa rifu wa mazao umekamilika. Mbegu nne
mpya za muhogo na mbili za viazi vitamu vyenye viini lishe na
kustahamili ukame zimegunduliwa ;
120
(j) Jumla ya miche 3,500,000 ya mikarafuu imeoteshwa katika
vitalu mbalimbali vya Serikali. Kati ya hiyo miche 2,216,328
yenye t hamani ya shilingi bilioni 4.4 imetolewa kwa wakulima
bila ya malipo. Kiwango cha uzalishaji wa karafuu
kimeongezeka kutoka tani 2,673 mwaka 2010 hadi kufikia tani
5,340 mwaka 2014. Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 50 ;
(k) Jumla ya tani 11,477 za karafuu zen ye thamani ya dola za
Kimarekani milioni 130.82 zimesafirishwa na kuuzwa nje ya
nchi. Bei ya kuuzia karafuu kwa wakulima imeongezeka kutoka
shilingi 5,000 hadi shilingi 14,000 kwa kilo moja. Bei hiyo ni
sawa na asilimia 80 ya bei ya karafuu katika soko la dunia ; na
(l) Jumla ya miche ya minazi mirefu 89,200 (Unguja 52,900 na
Pemba 36,300) imeoteshwa na kupandwa katika kipindi cha
2010 hadi 2014.
121
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali
Mohamed Shein akiangalia zao la karafuu alipotembele a katika
shamba la Bw.Said Sinani (hayupo pichani) Chumbageni – Kusini
Pemba akiwa katika ziara maalum
72. Kwa kutambua kwamba bado zipo changamoto zinazowakabili
wakulima walio wengi, katika kipindi cha miaka mitano ijayo
(2015 – 2020), Serikali ya Mapindu zi ya Zanzibar, chini ya
uongozi wa CCM itaendelea kuzipatia ufumbuzi changamoto
hizo kwa kutekeleza yafuatayo: –
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria na Kanuni za kilimo
bora kwa kuzingatia Mpango Mkuu wa Umwagiliaji Maji
pamoja na programu ya mapinduzi y a kilimo na usimamizi wa
raslimali za misitu ;
(b) Kuongeza idadi ya Mabwana/Mabibi shamba kutoka 172
mwaka 2014 hadi kufikia mmoja kwa kila Shehia ifikapo
mwaka 2020 na kuendeleza mafunzo kwa wakulima na kutilia
mkazo matumizi ya Kanuni za Kilimo Bora katika uzalishaji wa
mazao ya chakula na biashara pamoja na matumizi ya zana
za kisasa ;
(c) Kuendeleza kilimo cha umwagiliaji maji kwa kuzingatia
Mpango Mkuu wa Kilimo cha Umwagiliaji maji na kuimarisha
eneo la hekta 2,105 za miundombinu ya umwagiliaji maji
katika b onde la Cheju, Kilombero, Chaani, Mlemele na
Makwararani ;
(d) Kuongeza uzalishaji na ubora wa zao la karafuu pamoja na
uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara hususan
manjano, hiliki, tangawizi, pilipilimanga, kungumanga, kilimo
cha alizeti na kuanzisha maz ao mapya ya biashara ;
(e) Kuimarisha vituo vya huduma na udhibiti wa maradhi ya
mazao, wadudu waharibifu pamoja na ukaguzi na karantini
dhidi ya maradhi na wadudu waharibifu wa mimea na mifugo
ili kudhibiti maradhi ya mimea na mifugo nchini ;
122
(f) Kuendeleza utafiti wa mbegu bora za mazao ya chakula,
biashara, mboga mboga na matunda na kuhakikisha kwamba,
matumizi ya takwimu na matokeo ya utafiti huo yanawafikia
wakulima na kutumika kufanya maamuzi ;
(g) Kukiimarisha Chuo cha Kilimo Kizimbani ili kuongeza idadi ya
wataala mu wa kilimo na mifugo nchini kwa kukifanya kuwa
Chuo Kikuu Kishiriki cha Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) ;
(h) Kuhamasisha Sekta Binafsi kujenga viwanda vya usarifu wa
mazao ili kuongeza thamani na ubora wa mazao ya mboga na
matunda, nazi na karafuu ili kukuza ki pato cha wakulima na
kurahisisha upatikanaji wa soko ;
(i) Kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Hifadhi ya Taifa ya
Chakula ili kujikinga na balaa la njaa na ukosefu wa chakula
na lishe ; na
(j) Kuwawezesha wakulima kumudu gharama za matumizi ya
teknolojia katika kuon geza ufanisi wa matumizi ya ardhi na
uzalishaji wenye tija kupitia utekelezaji wa programu ya
kuwawezesha wakulima wa vijijini.
Ufugaji
73. Umuhimu wa ufugaji bora na wa kisasa unazingatia haja ya kuongeza
tija na ubora wa mazao ya mifugo kutokana na uhaba wa ardhi,
ongezeko la idadi ya watu na kupanuka kwa shughuli za maendeleo ya
kiuchumi na kijamii. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Sekta ya
Mifugo imepata mafanikio yafuatayo: –
(a) Wafugaji 23,393 wa ng'ombe, mbuzi na kuku wametembelewa na
kupatiwa usha uri wa kitaalamu pamoja na mbinu za ufugaji wa
kisasa. Pia vituo vya wafugaji 570 vimeanzishwa ili kutoa mafunzo
kwa wafugaji ;
(b) Uzalishaji wa maziwa umeongezeka kutoka lita 4,343,351 mwaka
2010 hadi 27,243,351 mwaka 2014. Aidha, jumla ya wafugaji 40
wamepat iwa mafunzo ya usindikaji wa mazao ya maziwa.
Uzalishaji wa mayai umeongezeka kwa asilimia 14 kutoka
164,270,132 mwaka 2010 hadi 186,870,292 mwaka 2014 ;
123
(c) Huduma za upandishaji wa ng'ombe kwa sindano zimeimarishwa.
Jumla ya ng'ombe 6,400 wamepandishwa kwa k utumia mbegu za
kisasa ;
(d) Vituo vya huduma za utibabu wa mifugo vimefanyiwa ukarabati
na kupatiwa madawa. Watoa huduma za msingi 42 na madaktari
wasaidizi 90, wamepatiwa mafunzo Unguja na Pemba ;
(e) Kiwanda kikubwa cha usarifu maziwa cha Azam Dairy
kimeanzishwa huko Fumba na tayari kimeanza uzalishaji. Kiwanda
hicho kitatoa ajira 200. Aidha, k iwanda kingine cha kusarifu kuku
kimeanzishwa huko Maruhubi ; na
(f) Wafugaji wameshajiishwa na kupatiwa mafunzo juu ya matumizi
ya samadi kama chanzo cha nishati mbadala na kup atiwa
utaalamu wa kutumia na kutunza mitambo ya Biogesi. Jumla ya
mitambo 32 imejengwa Unguja na Pemba.
74. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015 -2020), SMZ chini
ya uongozi wa CCM itaendelea ku himiza ufugaji wa kisasa wa
ng’ombe wa maziwa na nyama, mb uzi pamoja na kuku wa
nyama na mayai ili kuongeza tija na kipato cha wafugaji kwa
kutekeleza yafuatayo: –
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria na Programu mbalimbali
za elimu kwa wafugaji ili kuwawezesha wafugaji wadogo
kutekeleza kanuni za ufugaji wa kis asa na kuongeza uzalishaji
wa mazao ya mifugo na kukidhi mahitaji na viwango vya soko
la ndani na nje ;
(b) Kuimarisha vituo vya utafiti na huduma za kinga na tiba za
mifugo na kuwapatia wafugaji huduma ya upandishaji wa
ng'ombe kwa sindano ili kupata mbegu bo ra pamoja na
kuhamasisha sekta binafsi kutoa huduma za afya na pembejeo
za mifugo ;
(c) Kuhamasisha wawekezaji wa ndani na nje ili kuwekeza katika
sekta ya mifugo na viwanda vya usindikaji wa mazao ya mifugo ;
na
124
(d) Kuongeza uwezo wa kitaaluma kwa wafanyakazi wa se kta ya
mifugo.
Uvuvi na Mazao ya Baharini
75. Uvuvi na uzalishaji wa mazao ya bahari ni moja ya shughuli muhimu za
kiuchumi zinazofanywa na wananchi wengi wanaoishi pembezoni mwa
mwambao wa bahari. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010 –
2015) , Sekta ya Uvuvi imepata mafanikio yafuatayo: –
(a) Vikundi 167 vya wavuvi wadogo wadogo na vikundi 48 vya
Uhifadhi wa Mazingira ya B ahari vimeanzishwa na kupatiwa
mafunzo pamoja na msaada wa vifaa mbalimbali vya uvuvi.
Leseni za uvuvi 32,500 zimetolewa na vyombo 10,2 10
vimesajiliwa ambapo tani 148,535 za samaki zenye thamani
ya shilingi bilioni 572.5 zimevuliwa ;
(b) Vikundi 144 vya Uvuvi na U fugaji wa Viumbe vya Baharini
(samaki, kaa na majongoo) vikiwemo vile vya ufugaji wa
chaza na lulu vimeanzishwa na kupatiwa mafunz o, vitendea
kazi pamoja na vifaranga vya samaki 33,081. Mabwawa sita
(6) ya mfano (mashamba darasa) ya kufugia samaki
yamejengwa Unguja na Pemba na wajasiriamali 59 wa mazao
ya baharini walipelekwa China ili kupata mafunzo ya ufugaji
wa mazao ya baharini ;
(c) Kanuni za Usimamizi wa Maeneo ya Hifadhi zimeandaliwa na
kuchapishwa katika Gazeti Rasmi la Serikali. Kanuni hizo
zinahusu maeneo ya zamani ya MENAI, MIMCA na PECCA
pamoja na maeneo mapya ya Tumbatu na Changuu – Bawe.
Pia ulinzi shirikishi umeimarishwa kw a kuanzisha kitengo cha
kusimamia maeneo yote ya hi fadhi za baharini na kuanzisha
Kamati za D oria Vijijini;
(d) Kwa kushirikiana na Taasisi ya Sayansi ya Bahari (IMS) na
Kampuni ya ununuzi wa mwani ya Birr , utafiti umefanywa juu
ya uwezekano wa kulima mwani a ina ya "cottonii" kwenye
kina kirefu cha maji huko Fundo, Shumba Mjini, Mkia wa
Ng'ombe, Tumbe na Makangale Pemba na kubaini mafanikio
125
mazuri. Jumla ya tani 51,687 zenye thamani ya shilingi bilioni
18.7 zimezalishwa na kusafirishwa nje ya nchi ;
(e) Ili kuwaen deleza wakulima wa mwani, jumla ya vihori 100
vimetolewa kwa njia ya mkopo. Vihori hivyo vimetolewa kwa
vikundi 50 vya Wanawake wanaolima mwani kwa wingi katika
vijiji 10 vya Unguja ili ku rahisisha usafirishaji wa mwani
kutoka baharini. Vile vile , mashine za kukaushia mwani na
matunda kwa nguvu za jua baada zimeanza kutumika ; na
(f) Idadi ya leseni za uvuvi wa Bahari Kuu imeongezeka kutoka
23 mwaka 2009/2010 hadi 77 mwaka 2013/2014. Mapato
yatokanayo na leseni hizo, nayo yameongezeka kutoka
shilingi billion 1.1 2 mwaka 2009/2010 hadi kufikia shilingi
bilioni 3.30 mwaka 2013/2014.
Kilimo cha Mwani ni moja ya kilimo kinacholimwa na Wananchi walio
kando ya bahari kutokana na kipato chake husaidia wakulima wa Zao
hilo, Kama wanavyoonekana Wakinamama wa Kijiji cha Kojani wakiwa
katika eneo lao la kilimo hicho kattiba bahari ya kujani wa kipanda
mwani. kilimo hicho kat ika bahari ya kujani wakipanda mwani.
126
76. Kwa kutambua mchango mkubwa wa uvuvi na mazao ya
baharini katika kuimarisha uchumi wa Zanzibar na kipato cha
mwananchi , Chama Cha Mapinduzi katika kipin di cha miaka
mitano ijayo (2015 -2020) kitaielekeza SMZ kuendeleza uvuvi
na mazao ya baharini kwa kasi zaidi kwa kutekeleza
yafuatayo: –
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sera na Sheria za Uvuvi ili
kuimarisha usimamizi wa ras ilimali za bahari na uhifadhi wa
mazingira na kuendeleza jitihada za kuwahamasisha wavuvi
wadogo kuanzisha vikundi vya ushirika na kuwapatia mafunzo
na mikopo nafuu ya zana za kisasa ili kuongeza mapato yao ;
(b) Kuandaa Mpango na mazingira ya kuvutia Sekta Binafsi
kuwekeza katika uvuvi wa bahari kuu, utengenezaji wa boti za
uvuvi, ujenzi wa vyumba vya baridi (cold rooms) pamoja na
viwanda vya kusindika samaki. Aidha, wavuvi hasa vijana
watahamasishwa na kupatiwa mafunzo na zana za kisasa
zitakazowawezesha kuvua katika kina kirefu cha maji ;
(c) Kuendelea kununua vihori 500 vya kubebea mwani na
kuvisambaza kwa wakulima wa mwani 3,000 Unguja na
Pemba ili kuongeza uzalishaji wa mwani na kuhamasisha
wafugaji wa samaki, chaza, kaa, kamba na majongoo ili
kuendeleza uzali shaji wa maz ao hayo na kusimamia utafutaji
wa masoko ;
(d) Kuendelea kusimamia mpango shirikishi wa maeneo ya
hifadhi ya bahari yakiwemo maeneo ya Tumbatu, Chumbe –
Bawe, Menai na MIMCA kwa Unguja na Kisiwa Panza, Kokota
na Mwambe kwa PECCA -Pemba; na kuhakikisha kwamba,
jamii inayozunguka maeneo hayo inanufaika na uhifadhi huo ;
na
(e) Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kwa pamoja zitaandaa Sera ya Uvuvi
wa Bahari Kuu ili kuvutia wawekezaji wa n dani na wa nje
kuwekeza kati ka Sekta ya Uvuvi wa bahari kuu, kujenga
127
viwanda vya kusindika samaki, kuanzisha Chuo c ha Mafunzo
ya Uvuvi na kujenga B andari ya Uvuvi.
Maliasili
77. Visiwa vya Unguja na Pemba vimesheheni utajiri wa maliasili ambazo ni
kivutio kikubwa cha watalii. Katika kipi ndi cha miaka mitano iliyopita,
Sekta ya Maliasili imepata mafanikio yafuatayo: –
(a) Mpango wa Matumizi ya Misitu, Sera ya Misitu na Sheria ya
Uhifadhi na Usimamizi wa Rasilimali za Misitu umeandaliwa ili
kuimarisha udhibiti na uhifadhi wa maliasili zikiwemo r asilimali za
misitu, maliasili zisizorejesheka, wanyama pori pamoja na
bayoanuai. Aidha, wananchi wameshirikishwa kikamilifu katika
usimamizi na uhifadhi wa maeneo tengefu ya Jozani na Ngezi
pamoja na misitu ya asili ya Masingini, Msitu Mkuu na Kiwengwa .
(b) Ushirikishwaji wa wananchi umefanyika katika utunzaji na
uhifadhi wa wanyama adimu walio kat ika hatari ya kutoweka
hususan Kima Punju, Popo wa Pemba na Paa N unga. Maeneo
mapya ya hifadhi ya Kima P unju huko Muyuni na Jambiani
yameanzishwa. Jumla ya mikataba 50 ya usimamizi wa misitu ya
jamii na matumizi endelevu ya maliasili imefikiwa kati ya Serikali
na wananchi. Chini ya mikataba hiyo, kaya 4,500 zimepatiwa
majiko ya gesi bila ya malipo ; na
(c) Wananchi wamehamasishwa kuanzisha miradi ya ufugaji wa
nyuki ambapo jumla ya mizinga ya kisasa 3,000 imesambazwa
kwa wafugaji na kupatiwa fursa ya soko la ndani na nje ya nchi.
78. Ili kuendeleza zaidi sekta ya maliasili, katika kipindi cha miaka
mitano ijayo (2015 -2020) , CCM itaielekeza SMZ kutekeleza
yafuatayo: –
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sera na Sheria ya Misitu na
Uhifadhi wa Raslimali zisizorejesheka na kutoa taaluma ya
udhibiti wa raslimali hizo kwa jamii ;
(b) Kuimarisha maeneo ya hifadhi na usimamizi wa wanyama pori
walio katik a hatari ya kutoweka wakiwemo Paa Nunga, Kima
128
Punju na Popo wa Pemba ili kuongeza idadi ya wanyama
hao na kuimarisha utalii wa kimaumbile (eco-tourism) ;
(c) Kusimamia matumizi endelevu ya rasimali za misitu ya jamii
na kuongeza kiwango cha uzalishaji wa asali kutoka tani 5
mwaka 2014, hadi kufikia tani 1 0 mwaka 2020 ; na
(d) Kuendeleza kazi ya uatikaji na usambazaji wa miche ya misitu
na kuhamasisha upandaji na utunzaji wa miti.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abrahaman Kinana akijumuika na
wananchi wa kikundi cha kuhifadhi Mazingira Fuoni Kibondeni
katika upandaji wa miti ya mikoko ili kutunza mazingira ya
eneo hilo, akiwa katika ziara yake kukagua miradi ya
maendeleo na utekeleza ji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM
129
Mazingira na Mabadiliko Tabianchi
79. Mazingira ni suala mtambuka ambalo linagusa sekta mbalimbali za
kiuchumi na kijamii. Aidha, upo uhusiano tegemezi kati ya mazingira na
maendeleo na kwamba uharibifu wa mazingira si tu husababisha
umasikini , bali umasikini nao husababisha uharibifu wa mazingira. Katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita, yamepatikana mafanik io kutokana na
utunzaji na uhifadhi wa mazingira kama ifuatavyo: –
(a) Sera ya Mazingira ya mwaka 1992 imefanyiwa mapitio na
Sera Mpya ya Mwaka 2013 imezinduliwa. Ili kuimarisha
uhifadhi na usimamizi wa mazingira , Sheria ya Mazingira ya
Mwaka 1996 imefanyiwa ma rekebisho na Sheria Mpya ya
Mazingira ya Mwaka 2015 pamoja na Kanuni ya Usimamizi wa
Maliasili zisiorejesheka na Kanuni ya Marufuku ya Mifuko ya
Plastiki zimepitishwa ;
(b) Jumla ya miradi 221 imefanyiwa ukaguzi wa kimazingira na
kupatiwa ushauri wa kitaalamu. Miradi mingine 32 ya
uwekezaji imefanyiwa tathmini ya kimazingira na kupatiwa
vyeti vya mazingira ;
(c) Jumla ya miche 6,020,861 ya misitu na miti ya matunda
imesambazwa na kupandwa katika maeneo mbalimbali
yakiwemo maeneo yaliyoathirika kwa uchimbaji wa mchang a,
uchimbaji wa kifusi na matofali ya mawe ; na
(d) Utafiti wa athari za mabadiliko ya tabianchi umefanyika.
Maeneo 148 (Unguja 25 na Pemba 123) yamebainika
kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi kwa kuingiwa na maji
ya chumvi kutoka na na kupanda kwa kina cha ba hari.
80. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015 -2020), CCM
itaielekeza SMZ kuendeleza udhibiti wa hifadhi ya mazingira
kwa kutekeleza yafuatayo: –
(a) Kuendelea kusimamia Sera na Sheria ya Mazingira na
ushirikishwaji wa jamii katika utunzaji na uhifadhi wa
mazingira kwenye maeneo yao ;
130
(b) Kufanya tathmini za athari za Kimazingira, ukaguzi wa
Kimazingira na ufuatiliaji wa Kimazingira katika maeneo
mbalimbali ya nchi ;
(c) Kusimamia mabadiliko ya tabianchi na elimu kwa wananchi juu
ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira ;
(d) Kuanzisha vituo viwili vya usarifu wa taka ngumu (Unguja 1 na
Pemba 1) kwa lengo la kuhifadhi mazingira na kuzalisha ajira
kwa vijana ; na
(e) Kukamilisha ujenzi wa ukuta katika kingo za barabara ya
Mizingani ili kuzuia athari za mmomonyoko wa ardhi
unaosababish wa na bahari.
Utalii
81. Zanzibar ni miongoni mwa visiwa vyenye historia na vivutio mbalimbali
vya utalii zikiwemo fukwe za kuvutia, misitu ya asili, wanyama adimu,
magofu na urithi wa kimataifa wa Mji Mkongwe. Katika kipin di cha
miaka mitano iliyopita, Sekta ya Utalii imepata mafanikio yafuatayo: –
(a) Sheria ya Kamisheni ya Utalii imefanyiwa marekebisho na Kanuni
za Sheria ya Kamisheni ya Utalii na ile ya Chuo cha Utalii
zimepitishwa na kuanza kutumika. Chini ya sheria hio mpya
(Sheria Na. 7/2012) Kamati za Utalii za wilaya zimeanzishwa ;
(b) Ofisi ya Uwakala wa Utangazaji Utalii nchini India imeanzishwa na
masoko mapya ya utalii ya India, China, Uturuki na Urusi
yameibuliwa. Kutokana na hatua hizo, watalii 1,863 kutoka India,
2001 kutoka China na 840 kutoka Uturuki wa lipokelewa ;
(c) Idadi ya watalii walioingia Zanzibar imeongezeka kutoka 132,836
mwaka 2010 hadi 310,500 mwaka 2014. Kukamilika kwa ujenzi
wa chumba cha chini ya bahari katika hoteli ya Manta Reef huko
Makangale Pemba ni moja ya kivutio kikubwa cha watalii ;
(d) Utafiti wa kiikolojia kwenye N gome ya Mazrui – Chwaka na Tumbe
(Pemba ) na Ngome Kongwe na Forodhani (Unguja ) umefanyika.
Maeneo mapya manane ( 8) ya kihistoria yakiwemo Kiumbi,
Kiwengwa, Muyuni, Dimani, Mwanampambe, Mwana wa Mwana,
Tazari na kijiji kilichozama Mkumbuu yameibuliwa. Jengo la
131
Makumbusho ya Hamamni Baths yamefanyiwa ukarabati ili
kulirudisha katika hali yake ya awali ;
(e) Uhakiki wa hoteli na kuzipangia madaraja umefanyika. Hoteli 71
zilifikia vigezo vilivyowekwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki
zikiwemo hoteli za nyota tano 16 , nyota nne tisa, nyota tatu 43
na nyota mbili sita; na
(f) Chuo cha Maendeleo ya Utalii kimeimarishwa. Jumla ya wahitimu
983 (wanawake 386 na wanaume 597) wa mehitimu masomo yao
katika ngazi ya Shahada na Stashahada. Walimu sita wamepa tiwa
mafunzo ya juu.
Watalii wanaotembelea katika Visiwa vya Zanzibar hupata fursa za
kutembelea maeneo ya Historia na vivutio vya Utalii ndani ya
Zanzibar na vitongoji vyake. Kama wanavyoonekana Watalii hawa
waliofika Zanzibar wakipata historia ya Nyum ba ya Marcury ilioko
132
katika mtaa wa shangani ndani ya mji mkongwe wa Unguja.Wageni
wengi wanaotembelea Zanzibar hufika katika nyumba hii ikiwa katika
medali ya historia ya Zanzibar
82. Ili kuendeleza Sekta ya Utalii na kuifanya iwe endelevu na
kutoa mchango mkubwa zaidi katika uchumi wa Zanzibar,
katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015 -2020), CCM
itaielekeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutekeleza
yafuatayo: –
(a) Kufanya mapitio ya Sera ya Utalii na kusimamia utekelezaji wa
Sheria na Kanuni zinazohusiana na sekta hii pamoja na kuandaa
mpango wa kukusanya taarifa na takwimu za idadi ya hoteli na
taarifa nyingine ili kufahamu thamani halisi ya mchango wa
sekta kwenye Pato la Taifa ;
(b) Kuendelea kuhamasisha Sekta Binafsi kuanzisha miradi ya
ujenzi wa hoteli za kitalii hususan hoteli za daraja la kwanza na
kuongeza idadi ya watalii wanaoingia Zanziabr kutoka 310,500
mwaka 2014 hadi 500,000 mwaka 2020 ;
(c) Kuimarisha kikosi maalum u cha ulinzi na ushirikishwaji wa
wananchi kwa kuanzisha vituo vitatu vya utoaji taarifa zikiwemo
za uhalifu ili kuimarisha usalama wa watalii wanaotembelea
Zanzibar ;
(d) Kuendeleza utalii wa kumbukumbu za kihistoria, kiutamaduni na
kimaumbile wenye kutunza mazingira na kuibua maeneo mapya
likiwemo jengo la "Living Stone House"(Kinazini), jengo l a Tip
Tip (Forodhani), jengo la Baraza la Kutunga Sheria "Legislative
Council" (Mnazi Mmoja) na jengo la Mwinyimkuu (Dunga) ili
kuongeza idadi ya watalii na muda wa kukaa nchini ;
(e) Kuendeleza jitihada ya kuvitangaza vivutio vya utalii kwa
kuanzisha Kitengo c ha Masoko, O fisi tatu za kutangaza utalii,
kuanzisha masoko kwa njia shirikishi na mtandao na kufanya
utafiti ili kuibua masoko mapya hasa katika Bara la Asia na
Mashariki ya Kati ;
133
(f) Kuimarisha bidhaa na huduma za utalii kwa kuanzisha vituo 10
vya huduma na bidhaa za utalii zina zotokana na asili ya
Mzanzibari sambamba na utoaji wa huduma kwa watalii katika
bustani nane za kimaumbile zitakazozalisha ajira 1,000 ;
(g) Kuihamasisha jamii kushiriki katika utalii wa ndani na kutoa
mafunzo kwa vijana 680 ili kuwawezesh a kujiajiri wenyewe
kupitia Sekta ya Utalii na kutengeneza ajira 100,000 za moja
kwa moja na zisizo za moja kwa moja; na
(h) Kukiunganisha Chuo cha Utalii na SUZA ili kutoa mafunzo ya
Shahada ya Utalii .
Viwanda na Biashara
83. Uchumi wa viwanda una nguvu kubwa ya kuziwezesha sekta ny ingine
za uchumi kuingia katika mkondo wa uchumi wa kisasa. Aidha, Sekta ya
Biashara ina umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya uchumi na ustawi wa
wananchi. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010 -2015) , Sekta
ya Viwanda na Biashar a imepata mafanikio yafuatayo: –
(a) Sera ya Biashara imefanyiwa mapitio na Sheria Mpya ya Utoaji Leseni
za Biashara na Usajili imepitishwa. Aidha, sheria ya kusimamia
mwenendo wa biashara na kumlinda mtumiaji, sheria ya m izani
na vipimo na sheria ya b iashara z imefanyiwa mapitio ;
(b) Miradi 817 ya viwanda na ya wajasiriamali imekaguliwa na kupatiwa
ushauri wa kitaalamu. Wazalishaji wadogo wadogo 189 (Unguja
119 na Pemba 70) wamepatiwa mafunzo juu usindikaji mazao,
ujasiriamali, kuongeza thamani ya mazao na mbinu za kuendeleza
biashara zao . Vikundi 500 vya wajasiriamali vimeweza kushiriki
katika maonesho ya Kikanda na Kimataifa ;
(c) Sheria mpya ya Biashara imepitishwa. Chini ya Sheria hi yo, Taasisi ya
Viwango ya Zanzibar (ZBS) na Alama ya Utambulisho (logo) na
Alama ya Ubora wa Bidhaa (Standard Mark) ambayo itaonesha
ubora wa bidhaa hizo pia imeanzishwa ili kusimamia ubora wa
bidhaa zinazozalishwa na kuingizwa nchini na kukuza maso ko ya
ndani na nje ;
134
(d) Kiwanda cha Sukari cha Mahonda kimepatiwa mwekezaji na
kimefanyiwa ukara bati mkubwa pamoja na kupatiwa mashine
mpya na kuimarisha mashamba ya miwa. Jumla ya wafanyakazi
350 wameajiriwa na usindikaji wa sukari tayari umeanza ;
(e) Kiwanda cha Makonyo huko Pemba kimeimarishwa kwa kupatiwa
mashine mpya ya kupimia ubora wa mafuta ya mi mea (Gas
Chromolography) na mashine ya kuwekea mafuta kwenye ujazo
mdogo. Kiwanda pia kimeingia makubaliano ya kibiashara na
Kampuni ya Land ya Japan ili kuuza mafuta ya mimea katika soko
la Japan ;
(f) Mradi wa Tasnia Chapa (Branding) umeanzishwa ili kuil inda na
kuipa hadhi zaidi karafuu ya Zanzibar na kuitangaza Zanzibar
kupitia bidhaa nyingine za viungo zikiwemo mdalasini, pilipili hoho
na pilipili manga; na
(g) Shirika la Biashara Zanzibar ( ZSTC) limefanyiwa mabadiliko
makumbwa ambapo: –
(i) Zao la karafuu hal ikubinafishwa na mpango wa
kuliendeleza umetayarishwa;
(ii) Magendo ya karafuu yamepungua sana kutokana na
ushirikishwaji wa wananchi; na
(iii) Sheria ya maendeleo ya karafuu na Mfuko wa
Maendeleo ya Karafuu umeanzishwa.
84. Ili kuendeleza shughuli za viwanda na biashar a na kuinua
Uchumi wa Zanzibar, katika kipindi cha miaka mitano ijayo
(2015 -2020), CCM itaielekeza SMZ kuchukua hatua zifuatazo: –
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Uendelezaji wa Viwanda
Vidogo na vya Kati na kuandaa vivutio kwa ajili ya uwekezaji
wa viwand a vikubwa ;
(b) Kuandaa mkakati wa kuendeleza Sekta B inafsi pamoja na
programu ya kuwakuza wawekezaji wa ndani na wajasiriamali
wadogo wadogo na wa kati (SME’s) kwa kuwapatia mafunz o,
135
mitaji na huduma za kiufundi ili kuzalisha bidhaa bora zenye
kukabili ushinda ni wa soko la ndani na nje ya nchi ;
(c) Kuendeleza viwanda chini ya Maeneo Maalumu ya Kiuchumi
(SEZ) na kuwavutia wawekezaji wenye mitaji mikubwa
kuwekeza katika miundombinu ya viwanda vinavyozalisha
ajira kwa wingi, vikiwemo viwanda vya kushona nguo,
usindika ji mazao, usindikaji samaki na viwanda vya kusarifu
(kuchakata) mazao ya kilimo na mifugo ;
(d) Kufanya mapitio ya Sera ya Biashara ya Mwaka 2006 ,
kuandaa Sera Mpya ya Biashara na kuanzisha chombo
maalumu cha kuwaendeleza wajasiriamali wadogo na kufanya
utafiti juu ya gharama za biashara kwa lengo la kuchochea
ukuaji wa biashara na kuondosha urasimu katika utoaji wa
leseni ;
(e) Kuimari sha utengamano wa kikanda (EAC, SADC, IOR, ACP)
na kuhamasisha matumizi ya fursa za masoko ya EAC, SAD C
na AGOA na kuandaa Mkakati wa Kukuza Mauzo ya Nje
(Zanzibar National Export Strategy) ;
(f) Kuanzisha na kuendeleza ujenzi wa Kiwanja cha Maon yesho
ya Biashara cha Kimataifa na kuhamasisha ushiriki wa
wajasiriamali wa Zanzibar katika Maonyesho ya Biashara ya
Kimataifa ndani na nje ya nchi ;
(g) Kuimarisha mfumo wa ukusanyaji, uhifadhi, uchambuzi na
usambazaji wa taarifa za masoko na kufanya utafiti wa
masoko na bei ili kupanua wigo wa mahitaji ya masoko
mbalimbali. Aidha, wajasiriamali watapatiwa mafunzo ya
kuwajengea uwezo na mbinu za kuweza ku yafikia masoko
hayo; na
(h) Kusimamia utekelezaji wa Taasisi ya Viwango ya Zanzibar
(ZBS) na kukamilisha mkakati wa utambulisho wa karafuu ya
Zanzibar na uhamasisha ji matumizi ya tasnia malibunifu
(Intellectual Property Right) ili kuendeleza tija.
Vyama v ya Ushirika
136
85. Vyama vya U shirika bado vina nafasi muhimu katika kuwaunganisha na
kuwawezesha wananchi kubadili maisha yao na kujiendeleza kiuchumi.
Aidha, Vyama vya Ushirika wa Kuweka na Kukopa (SACCOS) ni nyenzo
ya kuwapatia wananchi mitaji kutokana na mic hango yao na mikopo
kutoka katika vyombo na taasisi za fedha. Katika kipindi cha miaka
mitano iliyopita (2010 -2015) , utekelezaji wa Sera na Sheria ya Vyama
vya Ushirika imefanyika na kupata mafanikio yafuatayo: –
(a) Vyama vipya vya U shirika 749 vimesajiliwa zi kiwemo SACCOS
16, na vyama vya uzalishaji mali na huduma 826. Idadi ya
vyama vya ushirika imefikia 2,493 vikiwa na jumla ya
wanachama 39,664 Unguja na Pemba ;
(b) Vyama vya ushirika 485 vimefanyiwa ukaguzi wa hesabu na
ripoti za ukaguzi huo kuwasilishwa kwenye Mikutan o Mikuu ya
vyama hivyo. Aidha, Vyama vya U shirika 2,243 vimefanyiwa
ukaguzi wa kawaida ili kutathmini hali ya uendeshaji,
utekelezaji wa sheria na uandishi wa vitabu vya hesabu ;
(c) SACCOS 203 zimefanyiwa uthamini na kupangiwa madaraja
ya ubora. Mtaji w a SACCOS hizo umefikia shilingi bilioni 3.5.
Jumla ya SACCOS 17 zimeunganishwa na taasisi mbalimbali
za fedha na kuweza kupatiwa mikopo yenye thamani ya
shilingi bilioni 3 ili kuimarisha mitaji katika biashara zao ; na
(d) Jumla ya wanachama 13,953 wakiwemo wan awake 8,923 na
wanaume 5,030 wamepatiwa mafunzo ya aina mbalimbali juu
ya uendeshaji wa Vyama vya Ushirika. Aidha, Sekta ya
Ushirika imeweza kutoa ajira binafsi 6,835 (wanawake 2,948
na wanaum e 3,887) kutokana na Vyama vya U shirika 88.
86. Ili kuendeleza Sekta ya Ushirika, katika kipindi cha miaka
mitano ijayo (2015 -2020) , CCM itaielekeza SMZ kutekeleza
yafuatayo: –
(a) Kuifanyia mapitio Sera ya Vyama vya Ushirika na kusimamia
utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Ushirika na upatikanaji
wa takwimu zitakazosaidia kua ndaa mipango na kuleta
137
mageuzi katika Sekta ya Ushirika na kuimarisha uchumi wa
Taifa;
(b) Kufanya usajili wa vyama vipya vya ushirika 600 vya uzalishaji
(kilimo, mifugo, viwanda vidogo vidogo, uvuvi na huduma)
pamoja na SACCOS 50 kubwa ;
(c) Kuziima risha SACCOS na Asasi Ndogo za F edha kwa kuzipatia
mafunzo ya kitaaluma , uongozi na kuwaongez ea mitaji ili
ziweze kutekeleza shughuli zake kwa ufanisi kwa lengo la
kuongeza ajira ;
(d) Kuwapatia mafunzo ya uongozi na uendeshaji wanachama
15,000 wakiwemo viongozi 3,000 na wan achama 12,000 wa
vyama vya ushirika na kuvifanyia ukaguzi vyama 3,000 vya
ushirika ; na
(e) Kusimamia uanzishaji na kuviimarisha vyama vikuu vitatu vya
kisekta (kilimo na masoko, kazi za mikono na huduma) ili
kujenga sauti ya pamoja na utoaji wa huduma muhimu z a
kisekta katika kuendeleza Vyama vya Ushirika vya Msingi.
Sekta za Miundombinu ya Kiuchumi
87. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010 -2015) , Sekta ya
Miundombinu imepata mafanikio yafuatayo: –
Barabara
(a) Jumla ya Kilomita 656 (Unguja Km. 430 na Pemba 226) za
barabara za lami zilizokwishajengwa zimefanyiwa
matengenezo ;
(b) Ujenzi wa barabara ya Mfenesini hadi Bumbwini (Km.13) na
barabara ya Welezo hadi Dunga (Km. 12.75) kwa kiwango
cha lami umekamilika. Vile vile, Kilomita 108.9 za barabara za
Pemba zimej engwa kwa kiwango cha lami ;
(c) Jumla ya Kilomita 124.7 za barabara za Unguja zimejengwa
kwa viwango mbalimbali. Kilomita 18 zimeje ngwa kwa
kiwango cha lami Km. 14 kwa kiwango cha
changarawe , Km. 12 ujenzi bado unaendelea na km 80.7
zimefanyiwa upembuzi yakini fu na ubunifu wa michoro ; na
138
(d) Kwa upande wa Pemba, jumla ya Km. 203.4 za barabara
zimejengwa kwa viwango mbalimbali. Kilomita 103.0
zimejengwa kwa kiwango cha lami, Km. 60.3. kwa kiwango
cha changarawe na Km. 40.1 zimefanyiwa upembuzi yakinifu
pamoja na mic horo.
Barabara mpya ya Amani – Mtoni ambayo ilifunguliwa rasmi na Makamu wa
Pili wa Rais Mhe. Balozi Seif Ali Iddi wakati wa maadhimisho ya kutimiza
miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
88. Ili kuendeleza kazi ya kuimarisha miundombinu ya barabara,
katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015 -2020) , CCM
itahakikisha kuwa SMZ inatekeleza kazi zifuatazo: –
(a) Kuendeleza kazi ya utunzaji na matengenezo ya barabara
zilizokwisha kujengwa na kufanya marekebisho katika maeneo
yanayotuama maji ya mvua na kuathiri ubora wa barabara
hizo;
(b) Kukamilisha ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya
Jendele –Cheju –Kaebona (km 11.7) na Koani –Jumbi (km 6.3)
139
kwa Unguja na barabara ya Ole – Kengeja (Km 35),
Mkanyageni – Kangani (Km 6.5), Finya – Kicha (Km 8.8) na
Mgagadu – Kiwani (Km 7.6) kwa Pemba ;
(c) Kujenga jumla ya ki lomita 160.8 za barabara kwa kiwango
cha lami Unguja na kilomita 51.1 za barabara kwa kiwango
cha lami huko Pemba kwa mpango ufuatao: –
(i) Unguja
Matemwe – Muyuni (Km 7.6)
Kichwele – Pangeni (Km 4.8)
Kinduni – Kichungwa ni – Kitope (Km 3.5)
Umbuji – Uroa (Km 6.9)
Fuoni – Kombeni (Km 8.6)
Jozani – Charawe – Ukongoroni – Bwejuu (Km 23.3)
Mkwajuni – Kijini (Km 9.4)
Pale – Kiongole (Km 4.6)
Malindi Port – Kinazini – Mtoni – Bububu (Km 11.2)
Creek road – Mkunazini – Mnazi moja (Km 1.3)
Tunguu – Fuoni – Magomeni – Kariakoo – Mkunazini (Km
16.3)
Welezo – Amani – Ng’ambo (Km 2.9)
Mtoni – Amani – Kiembesamaki (Km 8.5)
Airport – Kiembesamaki – Kilimani – Mnazimmoja (Km
6.6)
Bububu – Mahonda – Mkokotoni (Km 31)
Kizimbani – Kiboje (Km 7.2)
Melitano – Kwarara (Km 1)
Kijitoupele – Fuoni – Mambosasa (Km 2.5)
Sharifumsa – Mwanyanya – Bububu Skuli (Km 3.6)
(ii) Pemba
Chake – Wete (Km 22.1)
Mkoani – Chake (Km 27)
Mji wa Wete (Km 2)
(d) Kuendeleza kazi ya uwekaji wa taa za kuongoza magari kwa kuweka
taa sita (Unguja nne ( 4) na Pemba mbili ( 2) ili kupunguza
140
msongamano wa magari katika baadhi ya maeneo ya miji
hususan Zanzibar, Wete na Chake Chake Pemba ; na
(e) Kuimarisha K arakana Kuu ya Serikali kwa mashirikiano na Sekta
Binafsi ili kuon geza ufanisi na utoaji wa huduma bora za kiufundi
kwa Taasisi mbalimbali za Serikali na watu binafsi.
Bandari
89. Bandari ni mlango mkuu wa biashara na chachu ya ukuaji wa uchumi
wa Taifa na wananchi kwa jumla. Katika kipindi cha miaka mitano
iliyopita (2010 -2015) , mafanikio yaliyofikiwa kwenye eneo la bandari ni
kama ifuatavyo: –
(a) Shirika la Bandari kwa kushirikiana na Kampuni ya AZAM
MARINE limejenga majengo ya kuhudumia abiria likiwemo
jengo la Watu Mashuhuri (VIP) katika Bandari ya Malindi,
pamoja na kuimar isha huduma nyi ngine za abiria ;
(b) Eneo la kuhifadhia makontena lenye ukubwa wa kilomita za
mraba 6,000 katika Bandari ya Malindi limefanyiwa
matengenezo ili kuongeza ufanisi. Aidha, vifaa na mitambo
mipya ya kisasa imenunuliwa ;
(c) Matengenezo makubwa yamefanyik a katika gati ya Mkoani
Pemba. Kiungo cha gati hiyo ambacho kiliathirika kutokana na
nguvu za mawimbi ya meli pia kimefanyiwa matengenezo ;
(d) Ili kuimarisha gati ndogo ya Mkokotoni, kazi ya uchunguzi wa
athari za kimazingira imekamilika. Aidha, mpango wa ujen zi
wa gati hiyo tayari umeandaliwa ; na
(e) Kazi ya upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa Bandari mpya
ya Mpigaduri imekamilika. Mjenzi wa Bandari hiyo, Kampuni
ya China (Harbour Engineering Company) ameteuliwa na
fedha kwa ajili ya ujenzi huo tayari zimepa tikana.
90. Ili kuendeleza na kuimarisha bandari katika kipindi cha miaka
mitano ijayo (2015 -2020) , CCM itahakikisha kwamba, SMZ
inatekeleza kazi zifuatazo: –
141
(a) Kukamilisha ujenzi wa bandari mpya ya kuhudumia mizigo
katika eneo la Mpigaduri na kuiendeleza Bandar i ya Malindi
kwa kuongeza vifaa vya huduma kwa abiria pamoja na
mizigo ;
(b) Kuimarisha na kuendeleza Bandari ya Mkoani -Pemba kwa
kuipatia vifaa vya kisasa vya kuhudumia abiria na mizi go.
Aidha, kwa kushirikiana na Sekta B inafsi, gati ya Wete
itaimarishwa ;
(c) Kuimarisha gati ya Mkokotoni kwa kukamilisha kazi ya ujenzi
wa jeti kwa ajili ya huduma za usafiri wa wananchi wa
Tumbatu na usafirishaji wa mizigo kwa majahazi ; na
(d) Kuliimarisha Shirika la Meli ili lijiendeshe kibiashara na
kununua meli nyingine mpya ya abiri a na moja ya mafuta.
Usafiri wa Baharini
91. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010 -2015) , yamepatikana
mafanikio yafuatayo: –
(a) Sheria ya kuanzisha Shirika la Meli la Zanzibar imefanyiwa
mapitio na sheria mpya imepitishwa. Mpango wa mageuzi ya
kimuun do na uendeshaji umeanza kutekelezwa. Jumla ya meli
mbili za Shirika hilo; M V. Maendeleo na M V.Ukombozi
zimefanyiwa matengenezo makubwa ;
(b) Serikali imenunua meli mpya ya abiria na mizigo yenye uwezo
wa kubeba abiria 1,200 na tani 200 za mizigo ili kuimaris ha
huduma za usafiri kwa wananchi hususan kati ya Kisiwa cha
Unguja na Pemba ;
(c) Ofisi ya Mrajisi wa Meli na Mamlaka ya Usafiri wa Baharini
"Zanzibar Maritime Authority” (ZMA) imeimarishwa. Kwa
kushirikiana na SUMATRA na mamlaka hiyo imeweza kufanya
ukaguzi w a mara kwa mara wa vyombo vya baharini na
kupunguza kwa kiasi kikubwa ajali za mara kwa mara za
vyombo vya baharini ; na
(d) Wawekezaji wa ndani na nje wameendelea kushajiishwa ili
kuwekeza katika sekta ya usaf iri wa baharini. Jumla ya
142
kampuni 23 tayari zimewek eza katika sekta ya usafiri wa
baharini.
92. Ili kuendeleza na kuimarisha usafiri wa baharini, katika kipindi
cha miaka mitano ijayo, CCM itahakikisha kwamba, SMZ
inaendelea kusimamia Utekelezaji wa Sheria na Kanuni za
usafiri wa baharini ili kupunguza ajali za vyombo vya bahar ini
kwa kuimarisha utendaji wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini
(ZMA) .
Usafiri wa Anga
93. Uimara wa Sekta ya Usafiri wa Anga huchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji
wa Sekta ya Utalii, biashara na kukuza uchumi wa nchi. Katika kipindi
cha miak a mitano iliyopita (2010 -2015) , yamepatikana mafanikio
yafuatayo: –
(a) Ujenzi wa jengo jipya na eneo la maegesho ya ndege
umeanzishwa i li kukiimarisha Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Abeid Amani Karume . Kazi ya ujenzi wa
maegesho na njia za kurukia ndege umekamilika ;
(b) Ujenzi wa uzio wenye urefu wa kilomita 8.59 unaozunguka
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume
umekamilika ; na
(c) Hali ya usalama katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha
Abeid Amani Karume imeimarishwa. Vifaa vya ukaguzi
vikiwemo“walk through doors, x – ray machine, hand held
metal na under search mirrors" vimenunuliwa. Pia
wafanyakazi wa kada mbalimbali wamepatiwa mafunzo
yanayohusiana na kazi zao.
94. Ili kuiendeleza Sekta ya U safiri wa Anga katika kipindi cha
miaka mitano ija yo (2015 -2020) CCM itahakikisha kwamba,
SMZ inatekeleza kazi zifuatazo: –
(a) Kukamilisha ujenzi wa jengo jipya la abiria katika Kiwanja cha
Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume (AAKIA) ili
143
kuongeza idadi ya abiria wanaotumia kiwanja hicho, kiwango
cha m izigo na kuongeza mapato ya Serikali ;
(b) Kuendelea kuimarisha miundombinu na huduma za abiria,
ndege na mizigo katika Kiwanja cha Ndege cha Karu me-
Pemba ikiwemo kuongeza urefu na uwekaji wa taa katika
barabara ya kurukia na kutulia ndege, huduma za umeme na
kukamilisha ujenzi wa uzio ; na
(c) Kuendelea kuwapatia mafunzo na vifaa vya kisasa
wafanyakazi wa viwanja vya ndege vya Unguja na Pemba
pamoja na kuimarisha huduma za zimamoto na usalama wa
viwanja vya ndege.
Nishati
95. Sekta ya Nishati hususan umeme , ni nyenzo mu himu katika kukuza
uchumi na maendeleo ya jamii. Aidha, matumizi ya nishati ya umeme
hurahisisha shughuli nyingi za kiuchumi, kuongeza kasi ya uzalishajimali
na kuwawezesha wananchi kujiajiri wao wenyewe. Katika kipindi cha
miaka mitano iliyopita, yamepati kana mafanikio yafuatayo: –
(a) Sera ya Nishati imeanzishwa na Mpango Mkakati wa
utekelezaji wa Sera hiyo umeandaliwa. Aidha, Sheria ya
Udhib siti wa huduma za Maji na Nishati (ZURA) imepitishwa ;
(b) Mradi wa ujenzi wa njia ya pili ya umeme inayopita chini ya
bahar i kutoka Ras Kiromoni -Tanzania Bara hadi Fumba –
Unguja (Mradi wa MCC) umekamilika na kuongeza kiwango
cha upatikanaji wa umeme kutoka Megawati 45 hadi kufikia
Megawati 145 kwa Unguja ;
(c) Kazi ya ujenzi wa njia ya umeme ya megawati 20 inayopita
chini ya bahari kutoka Tanga hadi Pemba (Mradi wa NORAD)
imetekelezwa na kumaliza kabisa tatizo la umeme katika
kisiwa hicho ;
(d) Njia kubwa ya Umeme yenye u refu wa kilomita 5.2
imejengwa katika vijiji vya Kibonde Maji na Pongwe kwa
Unguja na Kivugo na Kichuwani kwa Pemba. A idha, vijiji 129
vimefikishiwa huduma ya umeme Unguja na Pemba sawa na
asilimia 105 ya lengo lililowekwa (vijiji 123) ;
144
(e) Vyanzo vya nishati mbadala ya umeme ukiwemo umeme wa
jua, mawimbi ya bahari, upepo na gesi asilia vimefanyiwa
uhakiki. Kampuni kutoka Ita lia imeteuliwa kuanza utafiti
katika maeneo hayo ; na
(f) Vijana 32 wanaendelea kupatiwa mafunzo katika vyuo
mbalimbali ndani na nje ya nchi ili kuwatayarisha kwa ajili ya
kuendeleza sekta ya mafuta na gesi asilia.
96. Ili kuimarisha Sekta ya Nishati ambayo inajum uisha umeme,
nishati mbadala, mafuta na gesi asilia katika kipindi cha miaka
mitano ijayo (2015 -2020) , SMZ chini ya uongozi wa CCM
itatekeleza kazi zifuatazo: –
(a) Umeme na nishati mbadala:
(i) Kusimamia utekelezaji wa Sera na Sheria ya Nishati
ya Mwaka 2009 na ku endeleza juhudi za upatikanaji
wa umeme na nishati mbadala ;
(ii) Kuimarisha shughuli za usimamizi wa huduma za
umeme na usambazaji wa nishati hiyo mijini na vijijini
vikiwemo visiwa vidogo vidogo vinavyoishi watu; na
(iii) Kuimarisha Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) kwa
lengo la kuliwezesha kujiendesha kibiashara.
(b) Mafuta na Gesi Asilia:
(i) Kuandaa Sera na Sheria ya Mafuta na Gesi Asilia ;
(ii) Kuendeleza jitihada za kuwajengea uwezo watendaji
pamoja na kuhamasisha vijana kujiunga na masomo
ya fani ya Mafuta na Gesi Asilia; na
(iii) Kuandaa mpango shirikishi utakaohakikisha kwamba
wananchi wananufaika na kupata fursa za kiuchumi
na kijamii kutokana na shughuli za utafutaji na
uchimbaji wa mafuta na gesi asilia.
Ardhi
97. Ardhi ni raslimali muhimu katika ujenzi wa uchumi wa Taifa. Aidha,
moja ya malengo ya Mapinduzi ya Zanzibar ya tarehe 12 Januari 1964 ,
ni kuondoa umiliki wa ardhi mikononi mwa wachache na kuhakikisha
145
kwamba ardhi yote ya Zanzibar inamilikiwa na wananchi wenyewe na
kuwawezesha kuondokana na umasikini, dhuluma na ubaguzi w a
kitabaka. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010 -2015) ,
mafanikio yafuatayo yamepatikana: –
(a) Sera Mpya ya Ardhi imeandaliwa na utoaji wa Hati Mpya za
Matumizi ya Ardhi na kuzibadilisha zile za zamani
imetekelezwa katika Shehia 20 Unguja na Pemba ;
(b) Jumla ya maeneo 3,541 katika Shehia 22 za Unguja na Pemba
yamesajiliwa na Mrajis wa Ardhi. Vile vile, nyumba, viwanja
na mashamba 22,746 yametambuliwa Unguja na Pemba. Hati
Mpya za Ardhi 1,310 na viwanja 1,691 zimetolewa kwa ajili ya
matumizi mbalimbali n a mikataba 223 ya ardhi imetolewa
kwa wawekezaji ;
(c) Mapitio na utayarishaji wa Mpango Mkuu wa Kitaifa wa
Matumizi Bora ya Ardhi (National Land Use Plan) na
utayarishaji wa Mpango Kabambe (Master Plan) ya Mji wa
Zanzibar imetekelezwa ;
(d) Kazi ya kufanya mapitio na marekebisho ya ramani ya
Zanzibar pamoja na miji ya Zanzibar, Chake Chake, Wete na
Mkoani pamoja na visiwa vidogo vidogo imetekelezwa.
Ramani mpya ya Kisiwa cha Unguja na Pemba tayari
zimechapishwa na kuanza kutumika ;
(e) Kazi ya utambuzi wa umiliki wa ard hi katika maeneo ya
ukanda wa pwani na fukwe imetekelezwa. Jumla ya wamil iki
1,600 wametambuliwa katika K ijiji cha Nungwi na 1,000
katika Kijiji cha Paje. Maeneo ya Chwaka kwa Unguja na
Michenzani kwa Pemba pia yamepimwa. Kazi ya utambuzi wa
umiliki wa ard hi katika maeneo ya miji kwa majaribio (Pilot)
pia imefanyika. Jumla ya wamiliki 6,000 wametambuliwa na
kusajiliwa ; na
(f) Idadi ya Mahakimu katika Mahakama za Ardhi imeongezeka
kutoka watatu ( 3) hadi sita ( 6) na Washauri (Assessors )
kutoka 19 hadi 27. Hatua hiyo imeongeza ufanisi na kasi ya
kusikiliza mashauri yanayohusiana na migogoro ya ardhi na
146
kuyatolea uamuzi. Mah akama ya Ardhi ya Mkoa wa Kaskazini
Unguja na Kusini Pemba pia zimeanzishwa.
98. Ili kuendeleza Sekta ya Ardhi, katika kipindi cha miaka
mitano i jayo (2015 -2020) , CCM itahakikisha kuwa, SMZ
inatekeleza malengo yafuatayo:
(a) Kuendeleza kazi ya Usajili wa Ardhi katika maeneo yote ya
Unguja na Pemba kwa mujibu wa Sera na Sheria ya Ardhi.
Aidha, ramani zote za visiwa vya Unguja na Pemba
zitaendelea kufany iwa mapitio na marekebisho kwa mujibu
wa mahitaji na mabadiliko yatakayojitokeza ;
(b) Kuendeleza kazi ya upimaji wa viwanja na utoaji wa Hati kwa
ajili ya matumizi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii kwa
kuzingatia Mpango wa Kitaifa wa Matumizi Bora ya Ardhi
(National Land Use Plan) pamoja na ramani ya mji na za miji ;
na
(c) Kuendeleza jitihada za kupunguza migogoro ya ardhi kwa
kuimarisha huduma za Mahakama za Ardhi katika Mikoa yote
ya Unguja na Pemba. Aidha, jamii itaelimishwa juu ya
umuhimu wa kutambua na kufuat a Sheria mbalimbali za ardhi
ikiwemo utambuzi, upimaji na usajili .
Sekta za Huduma za Jamii
Elimu
99. Elimu ni moja ya haki ya msingi kwa kila mwananchi na nyenzo muhimu
ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Katika kipindi cha miaka mitano
iliyopita (2010 -2015), Sekta ya elimu imepata mafanikio yafuatayo: –
(a) Elimu ya Maandalizi:
(i) Idadi ya Skuli za Maandalizi zimeongezeka kutoka 238
mwaka 2010 hadi 279 mwaka 2015. Ujenzi wa Skuli za
Maandalizi za Tunduni, Kama, Potoa, Jongowe na
Konde umekamilika na skuli ya maan dalizi ya
Machomane -Pemba imefanyiwa ukarabati mkubwa ; na
147
(ii) Idadi ya wanafunzi imeongezeka kutoka 29,732 (15,216
wasichana na 14,516 wa vulana ) mwaka 2010 hadi
38,808 (19,654 wa sichana na 19,154 wa vulana ) mwaka
2015. Idadi ya walimu 382 wamepatiwa mafunzo ya
kusomesha ngazi ya Elimu ya Maandalizi.
(b) Elimu ya Msingi:
(i) Ujenzi wa Skuli ya Msingi ya Mwanakwerekwe
umekamilika. Idadi ya skuli imeongezeka kutoka 299
mwaka 2010 hadi 359 mwaka 2015. Madarasa mapya
563 yamejengwa, madawati 7,955, viti 2,371 na
meza 2,329 zimechongwa na kusambazwa katika
madarasa hayo Unguja na Pemba ;
(ii) Idadi ya wanafunzi walioandikishwa darasa la kwanza
imeongezeka kutoka 38,743 (19,163 wa sichana na
19,580 wa vulana ) mwaka 2010 na kufikia 43,062
(21,129 wa sichana na 21,933 wa vulana ) mwaka
2015. Walimu wa ngazi ya cheti 949 wameajiriwa na
kupelekwa katika skuli za msingi Unguja na Pemba ;
(iii) Mazingira ya skuli za msingi yameimarishwa kwa
kukarabatiwa na kujengwa njia rafiki ili kuwezesha
wanafunzi wenye ulemavu kuingia madarasani kwa
urahisi. Jumla ya wanafunzi 203 wenye mahitaji
maalumu wameandikishwa na kuanza Elimu ya
Msingi; na
(iv) Jumla ya skuli 248 za msingi zimepatiwa komp yuta
mbili kila moja kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu na
skuli 20 zimepatiwa maabara za kuhamishika (mobile
lab) na pia skuli 25 zimepat iwa vifaa vya kuunganisha
mawasiliano (bridge IT) Unguja na Pemba.
(c) Elimu ya Sekondari:
(i) Idadi ya wanafunzi wa Sekondari (kidato cha 1 -4)
imeongezeka kutoka 78,165 (41,804 wa sichana na
148
36,361 wa vulana ) mwaka 2012 hadi 79 ,662 (43,544
wasichana 36,118 wa vulana ) mwaka 2014 ;
(ii) Idadi ya Skuli za Sekondari imeongezeka kutoka 194
mwaka 2010 hadi 213 mwaka 2014. Skuli mpya 19
zimejengwa na madarasa mapya 263 yamejengwa
katika skuli mbalimbali za Sekondari Unguja na
Pemba ;
(iii) Skuli kon gwe 6 za S ekondari zimefanyiwa ukarabati
mkubwa. Skuli hizo ni Hamamni, Forodhani na
Tumekuja kwa Unguja na Utaani, Fidel -Casro na
Uweleni kwa Pemba. Ujenzi wa ghorofa ya pili ya
Skuli ya Sekondari ya Donge unaendel ea. Aidha,
nyumba za walimu 27 zimejengwa katika skuli
mbalimbali Unguja na Pemba ; na
(iv) Jumla ya walimu 10 wamepatiwa mafunzo nje ya
nchi, 450 wamepatiwa mafunzo ya kuinua uwe zo wao
wa kufundisha masomo ya Hisabati na S ayansi na
wafanyakazi wa kad a nyingine za elimu 2,867
wameendelezwa kwa kupatiw a mafunzo katika vyuo
mbalimbali katika ngazi ya cheti, stashahada,
shahada ya uzamili na uzamivu.
149
Jengo la Skuli ya Secondary ya Faraja lililofunguliwa na Makamo wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi Kwamtipura Mjini Zanzibar
ikiwa ni miongo ni mwa shamra shamra za Maadhimisho ya miaka 51ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
(d) Elimu Mbadala na Elimu ya Watu Wazima:
(i) Kituo cha Elimu Mbadala cha Rahaleo kimeendelea
kutoa mafunzo katika fani tofauti. Idadi ya wanafunzi
katika k ituo hicho imeongezeka kuto ka 24 6
(wanawake 67 na wanaume 179) mwaka 2011 hadi
305 (wanawake 73 na wanaume 232) mwaka 2015 ;
na
(ii) Jumla ya vikundi vya kiuchumi 250 na wajasiriamali
6,000 wamepatiwa mafunzo ya ujasiriamali kupitia
madarasa ya Elimu ya Watu Wazima, Unguja na
Pemba.
(e) Kuimarisha Huduma za M aktaba:
150
(i) Ujenzi wa Maktaba Kuu ya Zanzibar umekamilika.
Zabuni ya ujenzi wa Maktaba Kuu , Tawi la Pemba, pia
imetangazwa na Shirika la Huduma za Maktaba
limeanzishwa ; na
(ii) Jumla ya maktaba nane (8) za jamii zimeanzishwa
katika maeneo ya C humbuni, Welezo, Kiembesamaki,
Mpapa, Uzini, Fumba, Bweleo na Tumbatu kwa
upande wa Unguja kwa mashirikiano na jumuiy a isiyo
ya kiserikali (MJUKIZA). Aidha, wananchi
wamehamasishwa kuanzisha Maktaba za J amii katika
maeneo wanayoishi.
(f) Vyuo vya Elimu ya Juu:
(i) Idadi ya wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Taifa
(SUZA), Zanzibar University (ZU) na Univesity
Collage of Education Zanzibar (UCEZ) imeongezeka
kutoka 3,624 mwaka 2010 hadi 6,038 mwaka 2014.
Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 67 ;
(ii) Ujenzi wa Chuo Kikuu c ha SUZA huko Tunguu
umekamilika. Majengo mapya manne ( 4) yamejengwa
na kuwekewa samani, kompyuta na vifaa vya
maabara. Idadi ya wanafunzi waliodahiliwa
imeongezeka kutoka 1,972 (wanawake 853 na
wanaume 1119) mwaka 2010 hadi 2,078 (wanawake
1,244 na wanaume 834) mwaka 2015. Wahitimu wa
fani mbalimbali nao wameongezeka kutoka 524
(wanawake 347 na wanaume 177) mwaka 2010 hadi
749 (418 wanawake na wanaume 331) mwaka 2015 ;
na
(iii) Idadi ya wanafunzi wanaodhaminiwa na Bodi ya
Mikopo ya Elimu ya Juu imeongezeka kutoka 1,022
(wanawake 534 na wanaume 488) mwaka 2010 hadi
2,658 (wanawake 1,372 na wanaume 1,286) mwaka
2015.
(g) Kuimarisha Mafunzo ya Ualimu:
151
(i) Ujenzi wa Chuo cha Ualimu cha Benjamin William
Mkapa, kilichopo Mchangamdogo , Wete Pemba
umekamilika. Mafunzo ya u alimu yametolewa katika
Chuo cha Kiislamu Mazizini Unguja, Chuo cha Kiislamu
Kiuyu na Chuo cha Benjamin William Mkapa huko
Pemba ;
(ii) Jumla ya walimu 4,031 wamemaliza mafunzo kati yao
238 wamemaliza mafunzo ya ngazi ya Cheti cha Elimu
Jumuisho, 951 wamemaliza ngazi ya Stashahada ya
Elimu ya S ekondari, 1,823 wamemaliza ngazi ya
stashahada ya Elimu ya Msingi na walimu 1,019
wamemaliza Mafunzo ya Ualimu wa Dini na Kiarabu ;
(iii) Chuo Kikuu cha SUZA kimeanzisha Diploma ya
Sayansi ya Ualimu yenye wanafunzi 102 na Diploma
ya Uongozi yenye wanafunzi 100. Aidha, hatua za
awali za kutayarisha m taala wa ualimu Cheti ngazi ya
Maandalizi zimeanza ;
(iv) Kitivo cha Tiba (Faculty of Medicine) kimeanzishwa na
sasa wanafunzi 66 wa mwaka wa kwanza na wa pili
wanendelea na masomo;
(v) Jumla ya walimu 2,481 wamepatiwa mafunzo ya
ualimu kwa njia ya Elimu Masafa kwa kupitia Vituo
vya Walimu (TCs) na kuweza kupandishwa daraja na
kukidhi vigezo vya kufundisha ngazi ya Elimu ya
Msingi; na
(vi) Mradi maalumu umeanzishwa ili kuendeleza mafunzo
ya walimu wa s ayansi na hisabati. Programu ya
Maendeleo ya Walimu (Teachers Advancement
Programme – TAP) imeanzishwa na kufanikiwa kutoa
mafunzo kwa walimu Unguja na Pemba. Pia vituo vya
ualimu vya Dunga na Kiembesamaki vimepatiwa
kompyuta kwa ajili ya kurahisisha uweka ji wa
kumbukumbu kupitia mradi huu.
(h) Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Amali:
152
(i) Ujenzi wa Vituo vya Elimu ya Amali vya Mkokotoni –
Unguja na Vitongoji -Pemba umekamilika. Mafu nzo ya
Amali yametolewa katika K ituo cha Mkokotoni na
Mwanakwerekwe -Unguja na Vitongo ji-Pemba. Jumla
ya wanafunzi 3,130 (936 wanawake na 2,194
wanaume) wamepatiwa mafunzo ya Elimu ya Amali
katika vyuo hivyo ;
(ii) Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume, ambayo
hutoa mafunzo ya fani mbalimbali za ufundi
imeimarishwa. Ukarabati wa miundombinu ya maji na
umeme pamoja na karakana ya uhunzi umefanyika.
Idadi ya wanafunzi katika Taasisi hiyo imeongezeka
kutoka 237 (wanawake 55 na wanaume 182) mwaka
2010 hadi 1,308 (wanawake 250 na wanaume
1,058) mwaka 2015 ; na
(iii) Ujenzi wa madarasa manne ( 4) katika Skuli ya Ufundi
ya Kengeja -Pemba umekamilika na kupatiwa huduma
ya umeme na vifaa vya kisasa vya kufundishia
pamoja na karakana.
100. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015 -2020), SMZ chini
ya uongozi wa CCM itaendeleza jitihada za kusimamia ukaguzi
ili kuendeleza ubora wa elimu katika ngazi zote pamoja na
kutekeleza yafuatayo: –
(a) Elimu ya Maandalizi
(i) Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Makuzi na Malezi ya
Mtoto na kuongeza kiwango cha uandikishaji kutoka
asilimia 31 Mwaka 2014 hadi kufikia asilimia 50 mwaka
2020;
(ii) Kuwahamasisha wananchi na Sekta Binafsi kuongeza
idadi ya madar asa pamoja na kujenga skuli za
Maandalizi hususan katika maeneo ya vijijini ; na
153
(iii) Kuimarisha mazingira rafiki ya skuli kwa mtoto kujifunza
kwa kutekeleza Programu ya Lishe katika skuli 40 za
Maandalizi na kuanzisha vituo 150 vya Tucheze
Tujifunze katika Wilaya ya Kaskazini "A" na Kaskazini
"B" Unguja na Micheweni na Mkoani -Pemba.
(b) Elimu ya Msingi
(i) Kuongeza kiwango halisi cha uandikishaji wanafunzi
kutoka asilimia 83.7 mwaka 2013 hadi kufikia as ilimia 100
mwaka 2020 ;
(ii) Kujenga Skuli za M singi 10 za ghorofa (Unguja 6 na
Pemba 4) katika maeneo yenye upungufu na
msongamano mkubwa wa wanafunzi ;
(iii) Kuimarisha Programu ya L ishe katika Skuli za Msingi zilizo
katika mazingira magumu; na
(iv) Kutekeleza lengo la k utoa elimu bila malipo katika elimu
ya msingi kwa kutowachangisha wazee micha ngo yoyote .
(c) Elimu ya Sekondari
(i) Kuongeza kiwango cha uandikishaji kutoka asilimia 60
mwaka 2014 hadi asilimia 80 mwaka 2020 ;
(ii) Kukamilisha ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Kibuteni n a
Donge Unguja; na Mkanyageni , Pemba. Aidha, mabweni
(dakhalia) ya kulala wanafunzi katika skuli zilizo mbali na
makaazi ya wananchi hususan Skuli ya Sekonda ri ya
Mtule, Matemwe na Chwaka -Tumbe yatajengwa ;
(iii) Kukamilisha ujenzi wa skuli 20 na ujenzi wa madara sa
500 na kuimarisha Elimu ya Sayansi na Hisabati kwa
wanafunzi wa Sekondari ; na
(iv) Kuimarisha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(TEHAMA) na ufundishaji wa somo la kompyuta katika
Skuli zot e za Sekondari sambamba na kuzipatia idadi ya
kompyuta za kutosha.
(d) Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Amali
154
(i) Kukamilisha ujenzi wa Makao Makuu ya Mamlaka ya
Mafunzo ya Amali na kujenga Kituo cha Mafunzo ya Amali
huko Makunduchi Unguja na Daya Mtambwe -Pemba ;
(ii) Kuviimarisha vituo vya Mafunzo ya Amali kwa kuvipatia
vifaa vya kisasa ili viweze kutoa mafunzo kwa njia ya
vitendo na nadharia ikiwa pamoja na kuimarisha mitaala
ya mafunzo kwa kuanzisha fani zinazoendana na mahitaji
ya soko la ajira ili kuwawezesha vijana wengi zaidi kujiajiri
hususan Sekta ya Utalii, Uvuvi na Kilimo ; na
(iii) Kukamilisha ujenzi wa jengo jipya la madarasa katika
Taasisi ya Sayansi ya Karume ili kuongeza idadi ya vijana
wanaojiunga na Taasisi hiyo na kupatiwa stadi mbalimbali
za maisha.
(e) Mafunzo ya Ualimu
(i) Kuimarisha utoaji wa mafunzo ya u alimu kazini na vyuoni
kwa ngazi ya Cheti na Diploma kwa walimu 5 ,000 ifikapo
mwaka 2020 ;
(ii) Kuviimarisha Vituo vya Walimu (TCs) vilivyopo sasa kwa
kuvipatia vifaa vya kujifunzia, kufundishia na TEHAMA ; na
kuendeleza mashirikiano kati ya vituo hivyo na taasisi
mbalimbali zinazotoa mafu nzo ya ualimu ; na
(iii) Kutoa mot isha kwa walimu wanaofanya kazi, kuhamasisha
walimu kujiendeleza kielimu kwa kuwapatia ruzuku za
masomo na kuwapandisha daraja kazini.
(f) Elimu ya Juu
(i) Kuanzisha Awamu ya Pili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha
Taifa (SUZA) ; kujenga Chuo K ikuu kipya katika eneo la
Dole; na kuimarisha mashirikiano na Vyuo Vikuu mbali
mbali vya ndani na nje ya nchi na kutoa fursa za
masomo ya Elimu ya Juu nje ya Zanzibar ;
(ii) Kuongeza nafasi za masomo katika Elimu ya Juu na
kuimarisha Mfuko wa Bodi ya Mikopo ili kuongeza idadi
ya wanafunzi watakao nufaika kutoka 2,658 mwaka
2015 hadi kufikia 22,404 mwaka 2020 ; na
155
(iii) Kuongeza idadi ya wanafunzi wa kike wanaojiunga na
Elimu ya Juu hususan katika fani za sayansi, ufundi,
udaktari na teknolojia.
(g) Elimu Mbadala na Elimu ya Watu Wazima
(i) Kuendeleza jitihada za kuhamasisha vijana kujiunga na
madarasa ya Elimu Mbadala ili kuwawezesha kujiajiri ; na
(ii) Kuimarisha utoaji wa Elimu Endelevu kwa watu wazima
na kuongeza idadi ya watu wanaojua kusoma, kuandika
na kuhesabu kutoka asilimia 85 .7 na kufikia asilimia 90
mwaka 2020.
(h) Elimu Mjumuisho
(i) Kukamilisha Sera ya Elimu Mjumuisho na kuimarisha
miundombinu na mazingira ya skuli ili kukidhi mahitaji ya
utoaji wa Elimu Mjumuisho na stadi za maisha ; na
(ii) Kuimarisha uwezo wa walimu wa Elimu Mjumuisho kwa
kuwapatia mafunzo jumla ya walimu 500 na kuandaa
Kamusi ya Lugha ya Alama.
(i) Michezo na Utamaduni katika Skuli
Kufufua na kuendeleza Michezo na U tamaduni kwa wanafunzi
wa skuli za Msingi na Sekondari na kuanzisha somo la michezo
katika Skuli teule sita za Sekondari nne (4) Unguja na Pemba
mbili (2).
(j) Uhifadhi wa Kumbukumbu za Kihistoria na Mambo ya
Kale
(i) Kuendeleza utekelezaji wa Mpango wa Uhifadhi wa
Mambo ya Kale na kuanzisha Taasisi ya Nyaraka na
Kumbukumbu za Kale pamoja na vituo vya kuhifadhia
kumbuku mbu katika kila Mkoa ; na
(ii) Kusimamia uendeshaji, utunzaji na matengenezo ya
Makumbusho ya Mnazi Mmoja, Beit-Ajab, Kasri ya
Forodhani, J engo la Kale la Mtoni pamoja na kuendeleza
ukusanyaji wa kumbukumbu na nyaraka za Serikali
kutoka katika taasisi mbalimbali za Serikali na kuzihifadhi
katika mfumo wa komputa.
156
(k) Nyumba za Walimu
Kujenga jumla ya nyumba 40 za Walimu, Unguja (24) na Pemba
(16) na kukamilisha nyumba zote ambazo ziko katika hatua
mbalimbali za utekelezaji.
(l) Huduma za Maktaba
(i) Kusimamia utekelezaji w a Sera ya Maktaba ya Zanzibar
na kukamilisha ujenzi wa jengo l a Maktaba Kuu Pemba,
kuanzisha M aktaba za Jamii katika maeneo wanayoishi
pamoja na kuendeleza uhamasishaji wa wananchi
kupenda kutumia maktaba ; na
(ii) Kuendeleza mafunzo ya Ukutubi na kuongeza idadi ya
vitabu katika maktaba zote.
Afya
101. Kwa kutambua umuhimu wa afya kwa wananchi, CCM imeendelea
kusimamia Utekelezaji wa lengo la kufikisha huduma za afya karibu na
wananchi wote mijini na vijijini. Huduma za afya zinapatikana katika kila
sehemu isiyozidi kilomiti 5 Unguja na Pemba. Aidha, katika kipindi cha
miaka mitano iliyopita (2010 -2015) , Sekta ya Afya imepata mafanikio
yafuatayo: –
(a) Utekelezaji wa Sera ya Afya:
Sera ya Afya ya mwaka 1999 imefanyiwa mapitio na Sera mpya
ya mwaka 2011 imeandaliwa na kuanz a kutumika. Aidha, Sheria
ya Afya ya Jamii na Sheria ya Mkemia Mkuu wa Serikali
imepitishwa. Chini ya sheria hii, Maabara ya Mkemia Mkuu wa
Serikali imeimarishwa na kupewa nguvu za kisheria.
(b) Kuimarisha Huduma za Hospitali Kuu ya Mnazimmoja:
Ili kufikia l engo la kuifanya Hospitali Kuu ya Mnazimmoja kuwa
Hospitali ya Rufaa, hatua mbalimbali za kuimarisha huduma
katika Hospitali hiyo zimetekelezwa kama ifuatavyo: –
(i) Idadi ya madaktari (MD) imeongezeka hadi kufikia 82
wakiwemo madaktari bingwa sita. Mashine ya
uchunguzi wa moyo (ECG na Echocardiography)
157
imenunuliwa na daktari bingwa mzalendo wa maradhi
ya moyo amepatikana ;
(ii) Kwa mashirikiano na taasisi ya Maendeleo ya Elimu ya
Upasuaji wa Ubongo (Neurosurgical Education and
Development ) ya Spain, jengo jipya la K itengo cha
Upasuaji wa Uti wa Mgongo ( Neorosurgical Unit)
limejengwa pamoja na ununuzi wa vifaa vipya vya
upasuaji wa mgongo na vichwa maji. Aidha, tiba kwa
njia ya mawasiliano ya mtandao (telemedicine)
imeanzishwa ;
(iii) Idara zote muhimu za maabara (microbiolo gy,
parasitology, aematology , biochemistry ,
histopathology and blood trasfusion) zimefanyiwa
matengenezo makubwa na kufikia kiwango cha
utendaji kinacholingana na maabara nyingine za
Afrika Mashariki. Jumla ya vipimo 67 vinafanyika
ikilinganishwa na vipim o 30 vya hapo awali ;
(iv) Huduma ya uchunguzi wa maradhi ya Kifua Kikuu
kwa kutumia mashine ya kisasa (Gene expert) yenye
uwezo mkubwa wa kugundua vimelea vya maradhi
hayo kwa haraka zimeanza kutolewa ;
(v) Sehemu ya matibabu ya meno na macho
zimeimarishwa na kuweka vifaa vipya vya matibabu ;
(vi) Ukarabati mkubwa umefanyika katika Kitengo cha
Wagonjwa Mahututi (ICU), Chumba cha Upasuaji
(theatre) na Wodi ya Wazazi pamoja na kuwekewa
vifaa vya kisasa ; na
(vii) Ujenzi wa ghala jipya la kuhifadhia dawa (Bohari Kuu
ya Dawa) huko Maruhubi na Kituo cha Damu Salama
huko Sebleni umekamilika.
(c) Hospitali ya Kivunge:
Jumla ya nyumba 12 za wafanyakazi zimejengwa, Chumba cha
Upasuaji, Wodi za Watoto na Sehemu ya Wagonjwa wa Nje
(OPD) zimejengwa. Aidha, mashine za upasuaji na mashine y a
158
mionzi (Utra Sound) zimenunuliwa na Kitengo cha Huduma za
Dharura kimeanzishwa.
(d) Hospitali ya Wete:
Ili kuipandisha hadhi H ospitali ya Wete kuwa Hospitali ya Mkoa,
maabara mpya, wodi ya akina mama na sehemu ya kuhifadhia
maiti zimejengwa. Aidha, wodi ya wanaum e, kliniki ya watoto,
vyoo na ghala ya kuhifadhia dawa zimefanyiwa ukarabati
mkubwa na mashine ya mionzi (Utra Sound ) pamoja na
mashine ya kupimia moyo zimenunuliwa.
(e) Hospitali ya Mkoani:
Ili kuipandisha daraja Hospitali ya Abdalla Mzee -Mkoani na
kuwa Hosp itali ya Mkoa , mpango wa kuijenga upya hospitali
hiyo umeandaliwa. Katika kutekeleza mpango huo, malipo ya
fidia kwa wananchi wote waliyobomolewa nyumba zao ili
kupisha ujenzi wa majengo mapya tayari yamefanyika na kazi
ya ujenzi w a hospitali hiyo unaendel ea.
(f) Hospitali ya Micheweni:
Kazi ya utanuzi na m atengenezo ya majengo ikiwemo W odi ya
Wazazi, Chumba cha U pasuaji na Chumba cha Maabara mpya
ya kisasa umekamilika. Aidha, ujenzi wa Chumba cha Upasuaji
unaendelea.
(g) Kuimarisha Huduma za Kinga na Tiba:
(i) Uwiano wa daktari kwa kutoa huduma kwa wananchi
sasa umefikia daktari mmoja anahudumia watu 9,093
(1:9093) badala ya watu 31,836 (1:31,836);
(ii) Jumla ya madaktari wazalendo 37 wameajiriwa. Idadi
ya madaktari na wataalamu wa afya imeongezeka
kutoka 3,634 mwaka 2010 hadi 4,618 mwaka 2014.
Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 26 ;
(iii) Elimu ya A fya kwa Umma ime endelea kutolewa kwa
njia mbali mbali. Mkazo mkubwa umewekwa katika
kuelimisha wananchi kuhusu maradhi ya kuambukiza na
yasiyo ya kuambukiza. Jitihada maalumu zimechuku liwa
159
juu ya kinga na tahadhari kuhusu maradhi ya EBOLA ;
na
(iv) Jumla ya wafanyakazi 142 wa kada mbali mbali
wamepelekwa masomoni ndani na nje ya nchi
wakiwemo Madaktari 9, Wasaidizi Madaktari 12,
Wauguzi 96 na wengiene wasiokuwa wa kada za afya.
(h) Mapambano dhid i ya Malaria:
(i) Ili kuendeleza mapambano dhidi ya malaria, mradi wa
"Maliza Malaria Zanzibar" umeendelea kutekelezwa. Kupitia
mradi huo, nyumba 57,385 sawa na asilimia 96 ya lengo
lililowekwa zilipulizwa dawa ya kuua mbu wa malaria. Zoezi
hilo limefanyika katika Wilaya zote za Unguja na Pemba ;
(ii) Vyandarua 717,000 viligawiwa kwa wananchi (vitatu kwa
kila kaya) na v ingine 30,474 vilisambazwa kwa k upitia
katika vituo vinavyotoa H uduma za Afya ya M ama na Mtoto
Unguja na Pemba ; na
(iii) Jumla ya wagonjwa 28,982 (7,618 w akiwa chini ya umri wa
miaka 5 na 21,364 wakiwa zaidi ya miaka 5) walichunguzwa
katika vituo mbalimbali vya afya na asilimia 1.4
waligundulika kuwa na vimelea vya malaria na kutibiwa.
Jitihada hizo zimewezesha kiwango cha ugonjwa wa malaria
kuendelea kushu ka kutoka asilimia 0.06 mwaka 2010 hadi
asilimia 0.03 mwaka 2014 .
(i) Mapambano dhidi ya UKIMWI:
(i) Jitihada za kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kupima
afya zao na kupiga vita unyanyapaa dhidi ya watu
wanaoishi na Virusi vya Ukimwi ( VVU) zimeendelezwa.
Ili kue ndeleza jitihada hizo, jumla ya shilingi 51,471,765
zimetolewa kwa Jumuiya ya Watu wanaoishi na Virusi
vya UKIMWI (ZAPHA+) ;
(ii) Wahudumu wa afya 150 na waelimishaji rika 40
wamepatiwa mafunzo ya kuelimisha jamii mbinu za
kujikinga na UKIMWI, kupiga vita unyany apaa na
udhalilishaji wa kijinsia. Jumla ya wananchi 3,881
160
kutoka katika Shehia 118 za Unguja na Pemba
wamefikiwa na kupatiwa elimu hi yo. Vile vile vi jana 300
wamepatiwa mafunzo ya Stadi za M aisha;
(iii) Jumla ya wananchi 61,921 wamejitokeza kupima afya
zao (wa nawake 32,477 na wanaume 29,444). Kati yao
966, sawa na asilimia 1.56 waligundulika kuwa wanaishi
na Virusi vya UKIMWI (VVU) wanawake 520 (asilimia
54) na wanaume 446 (asilimia 46) ;
(iv) Idadi ya wagonjwa wanaopata huduma ya dawa za
ARVs, imeongezeka kutoka 2, 341 mwaka 2010 hadi
4,669 mwaka 2014 sawa na asilimia 99 ;
(v) Huduma za tiba na kuzuia maambukizi ya mama
kwenda kwa mtoto zimetekelezwa. Idadi ya vituo
vinavyotoa huduma ya ushauri nasaha na upimaji wa
VVU imeongezeka kutoka 87 mwaka 2012 , hadi 91
mwaka 2014 ; na
(vi) Matokeo ya jitihada hizo, kiwango cha maambukizi ya
VVU bado kimeendelea kuwa asilimia 0.6.
(j) Mapambano dhidi ya Kifua Kikuu na Ukoma:
(i) Ili kudhibiti ugonjwa wa Kifua Kikuu na Ukoma , matibabu
ya maradhi hayo kwa wananchi yameendelea kutolewa na
kampeni maalumu ya ulishaji dawa kwa jamii imeendelea
kutekelezwa. Vijiji 24 vya Unguja na Pemba vimefikiwa
kwa njia ya mikutano na wananchi 314 waligunduliwa
kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa K ifua Kikuu k ati yao
223 (asilimia 71) wanapatiwa dawa wakiwa nyumbani
kwao na chini ya uangalizi wa familia zao ; na
(ii) Jumla ya wananchi 97 waligundulika kuwa na maradhi ya
Ukoma kati yao sita (6) wakiwa na ulemavu wa daraja la
pili. Hatua ya kuwap atia mafunzo juu ya ugonjwa wa
Ukoma wananchi 169 ambao ni jamaa za wagonjwa hao
imetekelezwa.
(k) Huduma za Afya ya Mama na Mtoto:
161
(i) Jumla ya Vituo vya A fya 84 vinatoa huduma za ziada
ikiwemo kuzalisha, maabar a na huduma za meno.
Huduma ya Afya ya U zazi (kwa njia ya kawaida au
upasuaji) na Afya ya Mama na M toto hutolewa b ila ya
malipo katik a hospitali zote na Vituo vya Afya. Vituo vyote
hivyo vinafaidika na upatikanaji wa dawa chini ya mpango
maalum u (Zanzibar Integrated Logistic System) ; na
(ii) Juhudi za kuwapatia watoto chanjo zimeendelea
kutekelezwa ili kupunguza idadi ya vifo vya watoto
ambapo asilimia 96.75 ya watoto wote wenye umri chini
ya miaka 15 wamepatiwa chanjo hizo. Chanjo ya BCG
imefikia asilimia 148, Polio 95, Dondakoo, Kifaduro,
Pepopunda na Uti wa mgongo asilimia 101 na Surua
asimilia 77.
(l) Kuendeleza Huduma ya Tiba Asili
Baraza la Tiba Asili limeanzishwa na waganga 193
wamesajiliwa. Jumla ya maduka ya dawa za asili 39, kliniki za
tiba asili na tiba mbadala 18 zimeanzishwa na wasaidizi
waganga 125 wamesajiliwa.
(m) Chuo cha Sayansi ya Afya:
(i) Jumla ya wanafunzi 821 wa taaluma mba limbali za afya
wamehitimu mafunzo. Aidha, kwa kushirikiana na Chuo
cha MATANZAS cha Cuba, wanafunzi 38 (19 wanaume na
19 wanawake) wa kada ya udaktari wamehitimu na
kuongeza idadi ya madaktari wazalendo wanaotoa huduma
katika hospitali za Unguja na Pemba. Aidha, masomo ya
kujiendeleza kwa wafanyakazi wenye cheti kwa muda
mrefu na ambao hawakupata fursa ya kujiendeleza kielimu
katika fani zao yameanzishwa ; na
(ii) Jumla ya wanafunzi 183 wamejiunga na mafunzo hayo
kwa mwaka 2013/2014 na wanafunzi 11 wanaende lea na
mafunzo ya Elimu Masafa kupitia AMREF.
162
102. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015 -2020) , Chama Cha
Mapinduzi kitaielekeza SMZ kuiendeleza zaidi Sekta ya Afya
kwa kutekeleza yafuatayo: –
(a) Kuendeleza ushirikishwaji wa wananchi na Sekta Binafsi i li
kuchangia maendeleo ya afya kwa kuzingatia MKUZA na Dira
ya 2020 ;
(b) Kuendelea kuifanya Hospitali ya Mnazimoja kuwa ya Rufaa
kwa kuongeza huduma za matibabu ya saratani na kuimarisha
huduma za uchunguzi na ununuzi wa vifaa kama "Magnetic
Resonance Ima ging" (MRI), DNA na kuongeza idadi ya
madaktari bingwa wa fani mbalimbali ;
(c) Kujenga Hospitali ya kisasa ya Rufaa katika eneo la Binguni
Unguja, kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Abdalla Mzee na
kuimarisha Hospitali ya Wete -Pemba ili zifikie daraja na
kiwango cha Hospitali za Mkoa. Aidha, Hospitali za Vijiji
(Cottage Hospitals ) za Micheweni na Vitongoji (Pemba ) na
Makunduchi na Kivunge (Unguja ) zitaendelea kuimarishwa ili
zifikie daraja na kiwango cha Hospitali za Wilaya ;
(d) Kuendeleza jitihada za kui marisha Huduma ya Afya ya Mama
na Mtoto kwa kujenga majengo mapya ya Wodi ya Wazazi na
Wodi ya Watoto katika Hospitali Kuu ya Mnazimoja pamoja na
kuvifanyia ukarabati vituo 19 vya Afya ya Msingi na kuvipatia
vifaa vya kisasa Unguja na Pemba ili kupunguza k iwango cha
vifo vya mama na mtoto ;
(e) Kuendeleza mapambano dhidi ya UKIMWI, Kifua Kikuu na
Ukoma na ma radhi mengine ya kuambukiza na yasiyo ya
kuambukiza pamoja na kuimarisha jitihada za utoaji wa elimu
ya afya kwa wananchi ili kupunguza ongezeko la mar adhi ya
Saratani, Kisukari na Shinikizo la Damu ;
(f) Kuendelea kukiimarisha Chuo cha Taaluma za S ayansi ya Afya
na watumishi wa Sekta ya Afya kwa kuwapatia mafunzo ya
ndani na nje ya nchi wakiwemo madaktari wa fani ya Udaktari
Bingwa katika fani ya maradhi ya wanawake, mifupa, watoto,
maradhi ya moyo na usingizi ;
163
(g) Kuendelea kutambua umuhimu wa tiba asili na tiba mbadala
katika jamii na kuimarisha ushirikiano na Baraza la Tiba Asili
katika utendaji wake wa kazi ;
(h) Kuhamasisha upatikanaji wa chakula na lishe bora katika kila
kaya ili kupunguza utapiamlo mkali kwa watoto kutoka asilimia
24 mwaka 2014 hadi asilimia 12 mwaka 2020 ;
(i) Kuendeleza tafiti mbalimbali katika maeneo ya Af ya ya Mama
na Mtoto, maradhi ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza
pamoja na mifumo ya utoaji wa huduma za afya ;
(j) Kuimarisha huduma za matibabu kwa wagonjwa walioathirika
na madawa ya kulevya na afya ya akili na kujenga kituo
maalum u kwa waathirika wa madawa ya kulevya ;
(k) Kuimarisha upatikanaji, ugawaji, usambazaji na udh ibiti wa
dawa, vifaa tiba na vitendanishi (Reagents) vyenye ubora na
usalama katika ngazi zote ;
(l) Kuandaa Sheria ya Uanzishaji wa Mfuko wa Bima ya Afya na
kusimamia utekelezaji wa mfuko huo ; na
(m) Kuimarisha na kusimamia mfumo wa taarifa za Afya ili z iweze
kutumika katika kutoa maamuzi katika ngazi zote.
Maji
103. Katika kipindi c ha miaka mitano iliyopita (2010 -2015), SMZ chini ya
uongozi wa CCM imeimarisha huduma za usambazaji na ugawaji wa
maji safi na salama kwa wananchi ambapo ma fanikio yafuatayo
yame patikana: –
(a) Mradi wa maji Mkoa wa Mjini Magharibi, Awamu ya Pili
umetekelezwa. Ujenzi wa matangi makubwa mawili huko
Kinuni na Dole na uchimbaji wa visima vitano (Kizimbani (3)
na Msikiti Mzuri (2) pamoja na ulazaji wa mabomba yenye
urefu wa kilomi ta 21 ume kamilika. Aidha, kiwango cha
upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kimefikia
asilimia 87.7 ;
(b) Katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, kazi ya ujenzi wa matangi
ya maji Matemwe (lita 3,000,000) na Nungwi (lita 3,000,000)
164
pamoja na ulazaji wa mabomba kwenye m aeneo yote ya
mradi imekamilika. Kiwango cha upatikanaji wa huduma ya
maji safi na salama katika mkoa huo kimefikia asilimia 71.68 ;
(c) Kwa Mkoa wa Kusini Unguja, kazi ya ujenzi wa matangi ya
maji ya Machui (lita 1,500,000) na Tunguu (lita 1,200,000)
pamoja na ulazaji wa mabomba kwenye maeneo ya mradi
imekamilika. Aidha, kiwango cha upatikanaji wa huduma ya
maji safi na salama katika Mkoa huo kimefika asilimia 76.45 ;
(d) Kazi ya ujenzi wa matangi ya maji ya Ndagoni (lita
1,000,000), Vikunguni (lita 300,000), Vitong oji-Ali Khamis
Camp (lita 300,000), Kambini Bahanasa (lita 1,000,000) na
Wambaa (lita 500,000) pamoja na ulazaji wa mabomba katika
maeneo yote ya miradi ya Mkoa wa Kaskazini na Kusini
Pemba imekamilika. Aidha, kiwango cha upatikanaji wa
huduma ya maji safi na salama katika Mkoa wa Kaskazini
Pemba kimefikia asilimia 56.42 na Mkoa wa Kusini Pemba
asilimia 74.08 ; na
(e) Jumla ya mita 3,007 zimefungwa katika nyumba za makazi na
maeneo ya biashara Unguja na Pemba i li kupunguza kiwango
cha upotevu wa maji .
104. Ili kue ndeleza sekta ya maji na kuimarisha huduma za
usambazaji wa maji safi na salama kwa wananchi, katika
kipindi cha miaka mitano ijayo (2015 -2020) , CCM itaielekeza
SMZ kufanikisha yafuatayo: –
(a) Kuendelea kuimarisha usambazaji wa huduma ya maji safi na
salama kw a wananchi kutoka asilimia 87 mwaka 2015 hadi
asilimia 97 mwaka 2020 kwa Mijini na kutoka asilimia 70 mwaka
2015 hadi asilimia 85 kwa vijijini ;
(b) Kuendeleza utekelezaji wa mradi wa uimarishaji wa
miundombinu ya maji katika Mkoa wa Mjini Magharibi na
ufunga ji wa mita kwa wateja ili kudhibiti upotevu wa maji ;
165
(c) Kuendeleza jitihada za kuhuisha miundombinu ya maji ili
kupunguza upotevu wa maji, kuhifadhi, kutunza na kulinda
vyanzo vya maji pamoja na maeneo ya hifadhi ya maji ; na
(d) Kuendelea kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu wa uhifadhi,
utumiaji na uchangiaji wa huduma ya maji safi na salama na
kufanya utafiti wa matumizi ya Nishati ya Jua katika visima na
vyanzo vya maji.
Makazi
105. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa CCM imefanya
juhudi kubwa za k uendeleza ujenzi wa nyumba bora kwa ajili ya makazi
ya wananchi Unguja na Pemba. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita
(2010 -2015) , huduma za makazi zimeboreshwa na kupatikana mafanikio
yafuatayo: –
(a) Katika kutekeleza Sera ya Taifa ya Nyumba, Sheria ya
kuanzisha Shirika la Nyumba la Zanzibar ya mwaka 2014
imepitishwa ili kuwapa fursa wananchi waliopangishwa
nyumba za maendeleo mijini na vijijini kuuziwa sehemu ya
majengo hayo ;
(b) Kazi ya kuu fanyia mapitio Mpango Kabambe (Master Plan) w a
mji wa Zanzibar ili k uanzisha maeneo maalumu ya ujenzi wa
nyumba za ghorofa hususan katika maeneo ya mijini na
kuwashajihi sha wawekezaji kuwekeza katika S ekta ya
Nyumba imefikia katika hatua za mwisho ; na
(c) Ujenzi wa Nyumba ya M aendeleo huko Bambi (Mpapa)
umekamilika. Jumla ya nyumba (fleti) 24 zimekabidhiwa kwa
wananchi wakati wa maadhimisho ya S herehe za Miaka 50 ya
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
106. Ili kuendelea kuwawezesha wananchi kupata nyumba na
makazi bora, CCM katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015 –
2020) , itahakikis ha kuwa SMZ inasimamia utekelezaji wa Sera
ya Taifa ya Nyumba na Sheria "Condominium " pamoja na
166
kuhamasisha S ekta Binafsi kuanzisha miradi ya makazi kwa
njia ya ubia (PPP).
Mamlaka ya Mji Mkongwe
107. Katika kuendeleza Mji Mkongwe, Mamlaka imefanya ukaguzi w a
kitaalamu ili kubaini nyumba zilizo katika hali mbaya ya uchakavu na
kuziingiza katika kanzidata (database) pamoja na kuwashauri wamiliki
au wapangaji wa nyumba hizo kuzifanyia ukarabati unaohitajika ambapo
majengo 267 yamefanyiwa ukarabati bila kubadili uhalisia wake.
108. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015 -2020), CCM
itahakikisha kuwa, SMZ inaendelea kuchukua hatua za
uhifadhi wa Mji Mkongwe ili uendelee kuwa kivutio cha utalii
na chanzo cha ajira kwa wananchi kwa kutekeleza yafuatayo: –
(a) Kuhifadhi na kuuendeleza Mji Mkongwe wa Zanzibar ili
uendelee kubaki katika uasili wake na katika orodha ya Miji ya
Urithi wa Dunia ;
(b) Kuendelea kuyahifadhi na kuyafanyia ukarabati majengo yote
ya kihistoria ndani ya eneo la Mji Mkongwe kwa kushirikiana
na Sekta Binafsi;
(c) Kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu na
thamani ya kuulinda, kuuhifadhi na kuendeleza Mji Mkongwe
kwa maslahi ya kizazi cha sasa na cha baada ye; na
(d) Kuendelea na usimamizi wa ujenzi wa ukuta wa ukingo wa
bahari katika eneo la Mizingani.
Maeneo mengine ya kipaumbele
Utamaduni na Michezo
109. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010 -2015) , Sekta ya
Utamaduni na Michezo imepata mafanikio makubwa.
Michezo
110. Michezo ni nyenzo muhimu katika kulinda na kudumisha mila na silka
njema za jamii. Michezo huimarisha afya na kujenga udugu na
167
mashirikiano miongo ni mwa wananchi na Mataifa mbali mbali. Katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita, yamepatikana mafanikio yafuatayo: –
(a) Mabaraza ya Michezo ya Wilaya yameimarishwa na kupatiwa
mafunzo juu ya usim amizi wa shughuli za michezo ;
(b) Timu ya Taifa na vilabu mbalimbali vimepata fursa ya kushiriki
katika mashindano mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa ;
(c) Timu ya vijana wenye ulemavu wa akili imeshiriki katika
mashindano ya olimpiki (Special Olympics) yaliyofanyi ka nchini
Ugiriki ;
(d) Uwanja wa Amani umewekewa nyasi bandia. Aidha, studio ya
kisasa ya kurekodia filamu/muziki imeanzishwa huko Rahaleo na
pia Kitu o cha Michezo huko Dole (Dole Academy ) kimejengwa
ambapo zaidi ya vijana 3,000 wameanza kukitumia na kupata
fursa ya kushiriki katika mashindano ya ndani na nje ya nchi ; na
(e) Uwanja wa mpira wa Gombani Pemba nao umeimarishwa kwa
kuwekewa taa, kujengwa paa jipya, njia ya kukimbilia (running
track) pamoja na kiwanja cha michezo ya ndani.
111. Ili kuiendeleza Sekta ya M ichezo, katika kipindi cha miaka
mitano ijayo (2015 -2020), CCM itaielekeza SMZ kutekeleza
yafuatayo: –
(a) Kuhamasisha jamii kushiriki katika michezo kwa lengo la
kuimarisha afya zao na kuendeleza Michezo ya Asili hususan
mchezo wa Ng'ombe na mashindano ya resi za ngalawa na
kutumia sanaa za aina mbalimb ali ili kujiajiri wao wenyewe
kwa lengo la kupambana na umasikini ;
(b) Kukiimarisha Kituo cha Michezo cha Dole (Dole Academy ) ili
kuendeleza michezo ya aina mbalimbali kwa vijana na
kuanzisha mfumo wa michezo ya kulip wa na kushiriki
mashindano ya Kimataifa ;
(c) Kujenga viwanja vya michezo katika Wilaya tano (5) na
kuwapatia mafunzo na vifaa vya kisasa vijana ili kuwaongezea
ujuzi na uzoefu wa michezo kwa kutumia walimu wa ndani na
nje ya nchi ;
168
(d) Kukifanyia matengennezo makub wa kiwanja cha michezo cha
"Mao Tse Tung" ili kiweze kutumika kwa shughuli za michezo
na sherehe za kitaifa ; na
(e) Kuvipatia vyama vya michezo vya watu wenye ulemavu fursa
stahiki ili waweze kushiriki kikamilifu katika kuendeleza
michezo ik iwemo michezo ya ku lipwa.
Utamaduni
112. Utamaduni ni nyenzo muhimu katika kulinda na kudumisha mila na silka
njema za jamii. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010 -2015) ,
yamepatikana mafanikio yafuatayo :-
(a) Sera na Sheria zinazoongoza Utamaduni zimefanyiwa mapitio
ili kukidhi matarajio na mahitaji ya wakati na sheria mpya ya
Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu na Utamaduni
imetungwa. Chini ya sheria hiyo, Bodi ya Sensa ya Filamu na
Baraza la Sanaa la Zanzibar vimeunganishwa ;
(b) Utafiti wa Urithi wa Utamaduni usioshikika umef anyika na
matokeo ya utafiti huo kuhifadhiwa Kimataifa na kuingizwa
katika orodha ya UNESCO ya tamaduni zinazohifadhiwa.
Sambamba na hatua hiyo, matokeo ya utafiti huo pia
yamerejeshwa kwa wananchi wa maeneo husika ili kuzitumia
kama sehemu ya ajira na kup ambana na umasikini ; na
(c) Hatua ya ukaguzi wa kazi za sanaa ili kulinda na kuhifadhi
mila, desturi na silka za Mzanzibari imetekelezwa. Aidha,
Kamusi za lahaja za Kipemba, Kimakunduchi na Kitumbatu
zimechapishwa na kusambazwa kwa wananchi.
113. Ili kuendeleza S ekta ya U tamaduni, katika kipindi cha miaka
mitano ijayo (2015 -2020) , CCM itaielekeza SMZ kutekeleza
mambo yafuatayo: –
(a) Kuandaa Sera ya Urithi wa Utamaduni na kufanya utafiti
maalumu katika visiwa visivyoishi watu ili kubaini aina ya utalii
unaoweza ku fanyika na kuongeza fursa za ajira kwa
wananchi ;
169
(b) Kuimarisha lugha ya Kiswahili na kuzifanya lahaja za Kiswahili
za Zanzibar kuwa chimbuko la Kiswahili fas aha. Jumla ya
machapisho mapya 10 ya vitabu na majarida 15 ya
kuimarisha lugha ya Kiswahili yata tolewa kwa lengo la
kuwawezesha watumiaji wenyeji na wageni kukitumia
Kiswahili fasaha katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii ;
(c) Kuihamasisha jamii ili kuuenzi, kuulinda na ku udumisha
utamaduni wa Mzanzibar i na kushiriki katika uandaaji wa
matam asha 50 ya utamaduni ;
(d) Kuwapatia mafunzo walimu 150 wa utamaduni na wasanii 500
ili kuwawezesha kutumia sanaa zao kwa mambo yenye
manufaa kwa wananchi na yenye kuzingatia maadili ya jamii ;
na
(e) Kuendeleza teknolojia za jadi kwa kutoa mafunzo kwa
mafundi 75 ili ziweze kuwanufaisha wananchi kiuchumi na
kuirithisha teknolojia hiyo kwa kizazi kipya.
Vyombo vya Habari
114. Vyombo vya habari vina jukumu kubwa la kutoa habari, kuburudisha na
kuelimisha jamii juu ya matukio na masuala mbalimbali yanayojiri nda ni
na nje ya nchi na kuchangia katika kukuza na kuimarisha demokrasia na
utawala bora. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010 -2015) ,
Sekta ya H abari imepata mafanikio yafuatayo: –
(a) Mageuzi makubwa ya kise ra na kisheria yamefanyika ili
kuiwezesha Zan zibar kuachana na mfumo wa matangazo ya
Analogi a na kuingia katika mfumo wa Dijitali. Aidha, Shirika la
Habari la Zanzibar (ZBC) limeanzishwa ambapo Redio,
Televisheni na Gazeti la Serikali (Zanzibar Leo)
vimeunganishwa. Hatua hizi zimeongeza ubora wa
matangazo na ufanisi katika vyombo vya habari ;
(b) Studio za Televisheni (Unguja na Pemba) zimepatiwa vifaa na
mitambo ya kisasa ya kurushia matangazo. Waandishi wa
habari 114 (wanawake 78 na wanaume 36) wamepatiwa
170
mafunzo ya Shahada ya U zamivu (PhD), Shahada ya Uzamili,
Shahada ya Kwanza, Stashahada na A stashahada ;
(c) Jumla ya vituo vipya tisa (9) vya Radio za FM na Televisheni
sita (6) vimeanzishwa ;
(d) Chuo cha Uandishi wa Habari kimepatiwa jengo jipya huko
Kilimani pamoja na vifaa vya kisasa, walimu wenye ujunzi na
kuanzisha mafunzo ya lugha ya Kichina. Idadi ya wanafunzi
wanaojiunga na Chuo hiki imeongezeka kutoka 75 mwaka
2010 hadi 180 mwaka 2014 ; na
(e) Kiwanda cha Upigaji Chapa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali
kimehamish wa kutoka eneo la zamani la Saateni na
kupelekw a katika majengo mapya h uko Maruhubi. Aidha,
kiwanda kimepatiwa mitambo mipya na ya kisasa ya uchapaji
(Digital Printing Machine) na kuanza kutekeleza majukumu
yake kwa ufanisi mkubwa.
115. Kwa kutambua uzito wa jukumu la Vyombo vya H abari, katika
kipindi cha miaka mitano ijayo (2015 -2020), SMZ chini ya
uongozi wa CCM itahakikisha kuwa Uhuru wa Vyombo vya
Habari unaendelea kuimarishwa na vyombo hivyo vinatekeleza
wajibu wake kwa weledi na kuzingatia maadili ya kazi zao kwa
kutekeleza yafuatayo: –
(a) Kuimarisha matu mizi ya TEHAMA na kuendeleza mageuzi katika
Sekta ya Habari ili kuongeza ufanisi na weledi katika tasnia hii ;
(b) Kuendelea kuliimarisha Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC)
kwa kulipatia mitambo, vifaa vya kisasa na vitendea kazi
pamoja na fursa za mafunzo nd ani na nje ya nchi kwa
wafanyakazi 600 wa kada mbalimbali ;
(c) Kuendeleza jitihada za kukiimarisha Chuo cha Uandishi wa
Habari ili kiwe chachu ya kuendeleza tasnia ya habari na
chimbuko la kuibua na kuendeleza vipaji vya uandishi ; na
(d) Kuimarisha mfumo wa uende shaji wa Kiwanda cha Upigaji
Chapa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kwa kukiongezea
mitambo na vifaa vya kisasa na wataalamu.
171
Huduma za Uokoaji
116. Huduma za Uokoaji ni muhimu kwa jamii hasa pale yanapozuka maafa
na majanga mbalimbali. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010-
2015) mafanikio yafuatayo yamepatikana: –
(i) Sera ya Maafa ya mwaka 2011 imeandaliwa na Mpango wa elimu
ya kukabiliana na Maafa kwa wananchi umetekelezwa ;
(ii) Kamati ya Maafa ya Zanzibar, Wilaya na Shehia 277 zimeendelea
kuima rishwa na kupatiwa mafunzo ya msingi ya kukabiliana na
maafa ; na
(iii) Kikosi Maalumu cha Uzamiaji kimeanzishwa na wan anchi
wamehamasishwa kuanzisha Vikosi na Jumuiya za Uokozi katika
maeneo yao.
117. Ili kuimarisha Huduma za U okoaji, katika kipindi cha miak a
mitano ijayo (2015 -2020) , CCM itahakikisha kuwa SMZ
inatekeleza yafuatayo: –
(a) Kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Kukabiliana na Maafa na
kuanzisha Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa ;
(b) Kuanzisha na kusimamia Mfuko wa Kukabiliana na Maafa
pamoja na kuimarisha juhudi za kuelimisha jamii katika
kukabiliana nayo ; na
(c) Kurahisisha uratibu na upatikanaji wa rasilimali fedha na
mawasiliano ya moja kwa moja na asasi nyingine za ndani na
nje ya nchi katika shughuli za uokoaji.
Madawa ya Kulevya
118. Madawa ya kulevya ni moja ya changamoto kubwa zinazowakabili
wananchi wengi hasa vijana. Madawa ya kulevya yameathiri sana afya
za watumiaji na kudhoofisha nguvu kazi na uchumi wa Taifa letu. Aidha,
utafiti umethibitisha kwamba upo uhusiano mkubwa kati ya matumizi ya
madawa ya kul evya na maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) . Katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita, mapambano dhidi ya madawa ya
kulevya yameendelezwa na mafanikio yafuatayo yamepatikana: –
172
(a) Mpango maalumu wa utekelezaji wa Sheria ya Dawa za Kulevya
(Road Map) umeanda liwa;
(b) Hali ya usalama katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha
Abeid Amani Karume imeimarishwa. Vifaa vya kisasa ikiwemo
"scanner", Kikosi cha Mbwa pamoja na choo maalumu kwa ajili
ya washukiwa wa madawa ya kulevya vimewekwa ;
(c) Kwa kushirikiana na taasisi zisizokuwa za kiserikali (NGOs), kazi
ya kuhamasisha wananchi kupima afya zao na kuwapitia
ushauri nasaha imetekelezwa ; na
(d) Jumla nyumba 13 za kurekebisha tabia za vijana walioathirika
na madawa ya kulevya (Sober Houses) zimeanzishwa na
kuhudumia jumla ya vijana 1,020 Unguja na Pemba.
119. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015 -2020) , SMZ chini
ya uongozi wa CCM, itaendeleza mapambano dhidi ya madawa
ya kulevya kwa kutekeleza yafuatayo: –
(a) Utekelezaji wa Sheria ya Madawa ya Kulevya kwa kuandaa
mazingira bor a ya utendaji kazi kwa vyombo husika ili
kudhibiti uingiaji na usafirishaji wa Dawa za kulevya ;
(b) Kuendeleza mafunzo na elimu kwa jamii juu ya athari za
madawa ya kulevya na kuandaa mkakati wa kuwasaidia
waathirika na madawa hayo ili kuachana na utumiaji. Aidha,
kitajengwa kituo maalumu cha kurekebisha vijana
walioathirika na madawa ya kulevya ;
(c) Kuendeleza na kuimarisha mashirikiano miongoni mwa
vyombo vinavyosimamia mapambano dhidi ya madawa ya
kulevya kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ; na
(d) Kushirikiana na Taasisi za Kimataifa zinazoendesha
mapambano dhidi ya madawa ya kulevya ili kudhibiti
usafirishaji na biashara haramu ya madawa hayo bila kujali
mipaka ya nchi.
Demokrasia na Utawala Bora
173
120. Demokrasia na U tawala Bora ni moja ya nyenzo muhimu katika ujenzi
wa jamii yenye umoja, mshikamano, uadilifu na uwajibikaji. Katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010 -2015) , mafanikio yafuatayo
yamepatikana: –
(a) Programu maalumu ya elimu ya uraia juu ya Sera ya Utawal a
Bora na Haki za Binaadamu imeandaliwa na kutekelezwa ;
(b) Sheria ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi pamoja na
Mamlaka ya Kuzuia Rushwa imeanzishwa na kuanza kazi.
Aidha, Kanuni za kudhibiti Rushwa na Uhujumu wa Uchumi
zimeandaliwa na kuanza kutumika ;
(c) Mafunzo juu ya mapambano dhidi ya rushwa yametoelewa
kwa wafanyakazi na viongozi mbalimbali wa Serikali ;
(d) Ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka,
Ofisi Ndogo ya Wanasheria (Mwera ) na nyumba za
waendesha Mashtaka wa Mahakama za Wilaya ya Makun duchi
na Mkokotoni (Unguja ); na Madungu na Chake Chake
(Pemba ) umekamilika ;
(e) Ujenzi wa jengo jipya la Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa
Hesabu za Serikali lilioko Unguja na lile la Wete Pemba
umekamilika. Aidha, mafunzo ya ukaguzi kwa kuzingatia
thamani na mazingira yametolewa kwa wafanyakazi.
Kutokana na juhudi hizo, ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali sasa imefikia kiwango kinachokubalika
Kimataifa ;
(f) Jengo la Mahakama Kuu Unguja na Pemba , majengo ya
Mahakama za Wilaya na Mahakama ya Kadhi yamefanyiwa
matengenezo makubwa. Mahakimu wapya 10 wameajiriwa
kati yao , saba (7) ni wanawake na watatu (3) ni wanaume ;
(g) Mafunzo juu ya matumizi ya Teknolojia ya Habari, uendeshaji
na usimamizi wa kesi pamoja na uandishi wa Sheria
yametoelewa kwa Ma jaji, Mahakimu na Waendesha
Mashtaka ;
(h) Sheria ya kuanzisha Mahakama ya Biashara Zanzibar
imepitishwa na matengenezo ya jengo la Mahakama hiyo
174
yamekamilika. Aidha, Mahakama ya W atoto imeanzishwa na
kuanza kufanya kazi ; na
(i) Ujenzi wa jengo jipya la Ukumbi wa B araza la Wawakilishi
huko Chukwani umekamilika na kuanza kutumika kwa ajili ya
mikutano na vikao vyote vya Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
121. Ili kuendeleza Demokrasia na U tawala Bora, katika kipindi cha
miaka mitano ijayo (2015 -2020) , CCM itahakikisha kuwa, SMZ
inatekeleza yafuatayo: –
(a) Utekelezaji wa kazi na majukumu ya Serikali unazingatia misingi
ya Demokrasia na Utawala Bora kama ilivyoainishwa katika
Katiba za nchi na kuimarisha uwazi na uwajibikaji kwa
wananchi ;
(b) Kuandaa na kupitisha Sheria ya Maadili ya Viongozi na
kuimarisha mafunzo na elimu ya uraia kwa viongozi wa taasisi
za umma na binafsi pamoja na wananchi juu ya misingi ya
Demokrasia na Utawala Bora ;
(c) Kuimarisha Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi
kwa kuiongezea rasilimali watu, mafunzo na v ifaa vya kisasa ;
(d) Kuimarisha mfumo wa Sheria kwa kufanya mabadiliko katika
utendaji kazi wa Mahakama, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka,
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Jeshi la Polisi, Vyuo vya Mafunzo
na wadau wengine wa Sheria ili kuwajengea uwezo katika utoaji
wa haki;
(e) Kuandaa Sera ya Msaada wa Kisheria ili kutoa fursa kwa
wananchi na makundi maalumu ya jamii kupata haki zao kwa
urahisi na kuanzisha mfumo wa kitaasisi wa masaada wa
kisheria ;
(f) Kuimarisha Ofisi ya Mrajis i Mkuu wa Serikali na mifumo ya
usajili wa Nyara ka, Biashara, Mali na Hakibunifu na kudhibiti
wizi na uharamia wa sanaa ; na
(g) Kuimarisha huduma za ukaguzi wa Hesabu za Serikali ili
kuhakikisha kwamba miradi inayotekelezwa ina thamani sawa
175
na fedha zilizotumika. Aidha, mafunzo ya kada mbalimbali
yatatolewa kwa watumishi ili kuongeza ufanisi.
Serikali za Mitaa
122. Serikali za Mitaa ni chombo muhimu cha kuwashirikisha wananchi katika
kusimamia shughuli za utawala na maendeleo yao. Serikali za Mitaa zina
mchango mkubwa katika kukuza maendeleo ya wananchi mijini n a
vijijini na kuendeleza demokrasia na utawala bora. Katika kipindi cha
miaka mitano iliyopita (2015 -2020) , mafanikio yafuatayo
yamepatikana: –
(a) Sheria za Serikali za Mitaa na Sheria ya Mamlaka ya Mikoa
zimefutwa na kutungwa Sheria mpya y a Tawala za Mikoa na
Sheria ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa ;
(b) Wananchi wamehamasishwa kuunda Kamati za Maendeleo za
Shehia na Majimbo ili kusukuma kasi ya maendeleo ya
kiuchumi na kijamii. Jumla ya Kamati za Maendeleo za She hia
339 katika majimbo yote Unguja na Pemba zimeanz ishwa ;
(c) Mabaraza ya Miji na Halmashauri za Wilaya yameendelea
kupatiwa ruzuku, vitendea kazi pamoja na watendaji wenye
ujuzi. Jumla ya wafanyakazi saba (7) wamepatiwa mafunzo
ndani n a nje ya nchi katika fani mbali mbali. Wajumbe wa
Kamati za Kudumu za Serika li za Mitaa nao wamepa tiwa
mafunzo juu ya masuala ya F edha, Afya na S heria;
(d) Mradi maalumu wa Huduma za Jamii (ZUSP) umeanzishwa ili
kuimarisha mazingira ya Manispaa ya Zanzibar, hifadhi ya
eneo la urithi wa Mji Mkongwe na miji ya Chake Chake, Wete
na Mkoan i huko Pemba. Mradi huo umekamilisha kazi ya
uwekajiwa taa za barabarani pamoja na taa za kuongoza
magari zinazotumia umeme wa jua (solar) katika maeneo ya
Mji Mkongwe ; na
(e) Baraza la Manispaa la Zanzibar limeanzisha utaratibu wa
kuingia mikataba na vikundi vya kijamii kwa ajili ya kufanya
usafi katika maeneo ya masoko, bustani, barabara, mitaro na
kuondoa taka ngumu ili kuimarisha usafi wa mazingira ya mji.
176
123. Ili kuziendeleza Serikali za Mitaa, katika kipindi cha miaka
mitano ijayo (2015 -2020) , CCM itahakiki sha kwamba, SMZ
inatekeleza yafuatazo: –
(a) Kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya
Halmashauri za Wilaya, Mabaraza ya Miji na Manispaa kwa
kuibua vyanzo vipya vya mapato na kuimarisha ubora wa
huduma kwa wananchi na usafi wa mazingira ya maeneo ya
miji;
(b) Kusimamia, kuratibu na kusaidia utendaji kazi wa Kamati za
Maendeleo katika maeneo mbalimbali ili kusukuma kasi ya
maendeleo na kudhibiti vitendo viovu katika jamii na kusaidia
juhudi za wananchi katika kuimarisha huduma za kijamii na
kuwapatia misaada ya aina mbalimbali ; na
(c) Kuendeleza utekelezaji wa mradi maalumu wa kuimarisha
mazingira ya Manispaa ya Zanzibar, hifadhi ya eneo la urithi
wa Mji Mkongwe na miji ya Chake Chake, Wete na Mkoani
Pemba. Aidha, ujenzi wa jengo la Ofisi y a Halmashauri ya
Wilaya ya Wete utakamilishwa.
Idara Maalumu za SMZ
124. Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni vyombo muhimu
katika utekelezaji wa Sera za CCM kuhusu Ulinzi na Usalama hususan
dhana ya ulinzi wa umma ambao unawashirikisha wananchi wote.
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010 -2015) , SMZ chini ya
uongozi wa CCM imeimarisha mazingira ya utendaji ka zi na maslahi ya
wapiganaji wa Idara Maalum u za SMZ kwa kutelekeza yafuatayo: –
(a) Kikosi Maalum Cha Kuzuia Magendo (KMKM)
Jumla ya wapiganaji 83 wamepatiw a mafunzo ndani na nje ya
nchi katika fani mbalimbali pamoja na kuwapatia vyombo vipya
vya usafiri na vifaa vya kisasa. Aidha, ujenzi wa Hospitali ya
Kibweni umekamilika na kuanza kutumika.
(b) Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU)
177
Jumla ya wapiganaji 86 wamepatiwa mafunzo ya aina
mbalimbali. Vijana 2,000 wamepatiwa mafunzo ya uzalendo,
uzalishaji mali pamoja na mafunzo ya amali kila mwaka. Aidha,
jumla ya vijana 900 wamepatiwa Mafunzo ya Stadi mbalimbali za
ufundi katika Chuo cha A mali cha JKU.
(c) Chuo Cha Mafunzo
Kazi ya ujenzi wa bweni la kulala wanafunzi huko Kinumoshi
imekamilika. Aidha, utaratibu wa wahalifu kutumikia adhabu zao
katika jamii badala ya Chuo cha Mafunzo umeanza kutekelezwa
ili kupunguza msongamano wa wanafunzi.
(d) Kikosi cha Zima Moto na Uokozi (K ZU)
Jumla ya wapiganaji 68 wamepatiwa mafunzo ya zimamoto nje
ya nchi. Huduma za Zimamoto na Uokozi zimefikishwa katika
wilaya zote za Unguja na Pemba. Aidha, huduma za Zimamoto
na Uokozi zimeanza kutolewa katika Bandari za Malindi (Unguja )
na Mkoani (Pemba).
(e) Kikosi Cha Valantia Zanzibar (KVZ)
Ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Kikosi hicho huko Mtoni
(Unguja) umekamilika na ujenzi wa nyumba ya maafisa na
makaazi ya wapiganaji wa Kikosi hicho huko Kisiwani P emba
umeanzishwa.
125. Katika kipindi cha miaka mit ano ijayo (2015 -2020) , CCM
itaielekeza SMZ kuendelea kuziimarisha Idara Maalum za SMZ
kwa kutekeleza yafuatayo: –
(a) Kuimarisha zaidi mazingira ya kazi na utendaji wa wapiganaji
wa KMKM, JKU, K ZU na KVZ kwa kuwapatia mafunzo, vifaa vya
kisasa, maslahi na mahi taji mengine muhimu ili kuwawezesha
kutekeleza majukumu yao ya ulinzi kwa weledi na ufanisi
mkubwa ;
(b) Kukamilisha ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya JKU Mtoni na
kukiendeleza Kituo cha Amali cha JKU kwa kupanua wigo wa
mafunzo ya Amali kwa vi jana wanaojiunga n a kituo hicho kwa
178
kuzingatia mahitaji ya soko la ajira na kuwawez esha vijana
kujiajiri wenyewe ; na
(c) Kukamilisha ujenzi wa nyumba za maafisa na makaazi ya
wapiganaji wa KVZ Kisiwani Pemba.
Kuwaunganisha Wananchi wa Zanzibar
126. Hoja ya kuwaunganisha wananchi w a Zanzibar imetokana na Sera ya
CCM ya kujenga umoja wa kitaifa, amani na utulivu. Bila ya kuwepo
mazingira ya amani na utulivu nchi haiwezi kupata maendeleo na
hakuna mwekezaji atakayekuba li kuwekeza. Aidha, wananchi
watashindwa kuendesha shughuli zao za kiuchumi, kijamii na
utamaduni. Katika kipindi cha 2010-2015, Serikali chini ya uongozi wa
CCM, imeifanyia mabadiliko Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1985
(Mabadiliko ya 10 ) na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010,
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye muun do wa Umoja wa Kitaifa
chini ya uongozi wa Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi imeundwa na kufanikiwa kutimiza
malengo yake kwa ufanisi.
127. Ili kuendeleza Sera ya kuwaunganisha wananchi wa Zanzibar,
katika kipin di cha 2015 -2020 , CCM itandelea kuwa muumini wa
kweli wa amani, utulivu na kuwaunganisha wananchi wa
Zanzibar kwa kuimarisha mafanikio yaliyokwisha kupatikana
na kuielekeza SMZ kutekeleza yafuayo: –
(a) Kuendeleza jitihada za kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa
amani, umoja na mshikamano ili kujenga mazingira ya
kuaminiana, kuvumiliana na kushirikiana katika masuala
mbalimbali ya kijamii ;
(b) Kuendelea kupiga vita na kudhibiti vitendo vya ubaguzi
vinavyojitokeza katika sehemu za utoaji wa huduma za kiuchumi,
kisiasa na kijamii miongoni mwa wananchi ; na
(c) Kuimarisha mifumo ya taasisi za uratibu na kushughulikia
malalamiko na kero za wananchi kwa wakati, haki na uadilifu.
179
Kuyaendeleza Makundi Mbalimbali
Watoto
128. Watoto kama Taifa la kesho wanayo haki ya kulindwa kwani nd io
chanzo cha rasilimali watu na mrithi wa Taifa la kesho. Watoto wanayo
haki ya kuishi, kutoa mawazo, kupata lishe bora, malezi na ulinzi,
kupewa elimu na kutobaguliwa kwa kwa namna yoyote. Katika kipindi
cha miaka mitano iliyopita (2010 -2015) , Serikali chini ya uongozi wa
CCM imeend elea kusimamia maendeleo ya watoto na mafanikio
yafuatayo amepatikana: –
(a) Sheria ya Mtoto pamoja na Kanuni saba za kusimamia
utekelezaji wa sheria hiyo zimepitishwa ikiwemo miongozo ya
uanzishaji na uendeshaji wa nyumba za kulel ea watoto. Aidha,
ujenzi wa Kituo cha Kulelea Watoto cha Mazizini umekamilika ;
(b) Jumla ya Mabaraza ya Watoto 239 yameanzishwa Unguja na
Pemba ili kupiga vita ajira kwa watoto na kazi ya usajili na
kuwatambua watoto wanaoishi katika mazingira magumu
imetekele zwa na watoto 12,453 (Unguja 7,711 na Pemba
4,742) wamesajiliwa na kutambuliwa mahitaji yao. Aidha,
kampeni maalumu ya kupiga vita vitendo vya udhalilishaji dhidi
ya wanawake na watoto imeanzishwa ; na
(c) Kiwanja cha kufurahishia watoto cha Uhuru Kariakoo (Unguja)
na Tibirinzi (Pemba ) vimejengwa upya ili kuwapatia watoto
maeneo ya kucheza yenye mandhari nzuri na kuvutia.
129. Katika kipindi cha miaka 2015 -2020 , CCM itaendelea
kuimarisha haki na maendeleo ya watoto na kuhakikisha
kwamba SMZ inatekeleza hatua zifuataz o:-
(a) Kusimamia uanzishaji na uendelezaji wa Mabaraza ya Watoto na
Kamati za Wazazi katika Shehia, Wilaya na Mikoa yote ya
Zanzibar ili kupiga vita vitendo vya udhalilishaji dhidi ya watoto ;
(b) Kuendelea kupiga vita ajira za watoto na kusimamia utekelezaji
wa Sheria na mikataba ya Kimataifa inayohusu Haki, Usa wa na
hifadhi ya mtoto; na
180
(c) Kuratibu na kutathmini huduma inazotolewa na vituo binafsi vya
kulelea watoto ili kuhakikisha vinaendeshwa kwa mujibu wa
Sheria.
Vijana
130. Vijana walioandaliwa vyema na kujipanga vi zuri wanao mchango
mkubwa katika kukuza uchumi na maendeleo ya jamii. Changamoto
kubwa inayowakabili vijana mijini na vijijini ni ukosefu wa ajira, kukosa
ujuzi na maarifa ya kisasa pamoja na mitaji hivyo kushindwa
kujiendeleza na kutekeleza wajibu wao wa kushiriki katika ujenzi wa
uchumi wa kisasa. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010 –
2015) , SMZ chini ya uongozi wa CCM, imechukua hatua mbalimbali za
kuwaendeleza vijana na kupata mafanikio yafuatayo: –
(a) Baraza la Taifa la Vijana limeanzishwa na ju mla ya asasi za
vijana 158 zilipatiwa mafunzo ya aina mbalimbali ;
(b) Jumla ya vikundi 258 (Unguja 203 na Pemba 55) vyenye
wanachama 2,285 (Unguja 2,015 na P emba 270) vimeanzishwa
na kupatiwa mafunzo ya ujasiriamali na stadi mbalimbali za
maisha. Vile vile , vyama viwili ( 2) vya SACCOS za vijana
vimeanzishwa ;
(c) Mfuko Maalumu umeanzishwa ili kutoa mikopo yenye riba na
masharti nafuu kwa Vijana. Mikopo yenye thamani ya Shilingi
813,800,000 (Unguja Shilingi 700,000,000 na Pemba Shilingi
113,800,000) imetolewa ;
(d) Kwa kupitia mifuko mingine ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi,
jumla ya Shilingi 318,600,000 zimetolewa kwa vikundi 130 vya
vijana Unguja na Pemba. Kati ya fedha hizo Shilingi 206,950,000
zimetolewa kwa vikundi 99 vya vijana wa Unguja, na Shilingi
111,700,000 zi metolewa kwa vikundi 31 vya vijana wa Pemba ;
(e) Jumla ya shilingi milioni 100 zimewekwa katika Benki ya CRDB
kama dhamana ya Serikali ili kuiwezesha Benki hiyo kutoa
mikopo kwa vijana ; na
(f) Jumla ya Vyama vya U shirika vinne (4) vyenye wanachama 72
(wanawake 42 na wanaume 30) ambao ni vijana waliohitimu
181
vyuo na vyu o vikuu vimeanzishwa na kuweza ku jiajiri wenyewe
kupitia kilimo na usindikaji ; na kutoa mafunzo na ukaguzi
kwenye vikundi vya ushirika. Pia vikundi vitatu ( 3) vya vijana
(Unguja 2 na Pemba 1) vinajishug hulisha na kilimo cha mboga
mboga kwa kutumia teknolojia ya umwagiliaji ( Drip Irrigation)
vimeanzishwa na kupatiwa msaada wa vifaa vya umwagiliaji maji
vyenye thama ni ya Dola za Kimarekani 21,000 kutoka Shirika la
Kazi Duniani (ILO).
131. Katika kipindi cha m waka 2015 -2020, SMZ chini ya uongozi wa
CCM, itaendelea kuzipatia ufumbuzi changamoto za vijana kwa
kuchukua hatua zifuatazo: –
(a) Kuandaa Programu za Elimu na Malezi Bora kwa Vijana ili
kuwawezesha jumla ya vijana 235,817 kupata mafunzo ya stadi
mbalimbali za maisha pamoja na kujiajiri ;
(b) Kuliendeleza Baraza la Taifa la Vijana ili kuongeza ushiriki wa
vijana katika ngazi mbalimbali za maamuzi ;
(c) Kuendelea kuimarisha Mfuko Maalum u wa Vijana ili kutoa mikopo
kwa vijana wengi zaidi na kujiajiri katika kilimo cha kisa sa na
kuanzisha "Green House" moja katika kila wilaya ;
(d) Kuhamasisha vijana 5,000 waliomaliza vyuo na vyuo vikuu
kuanzisha vikundi vya uzalishaji mali na utoaji huduma , kuvipatia
mafunzo na mikopo ili waweze kujiajiri. Aidha, taasisi za Serikali
na zisizo za Serikali zitahamasishwa kutoa zabuni za kazi na
huduma kwa vijana hao ; na
(e) Kuandaa mikakati ya malezi bora kwa vijana ili kujenga moyo wa
uzalendo, ari ya kujitolea na kuipenda nchi yao na kuimarisha
mahusiano y a vijana ndani na nje ya nchi .
Wanawake
132. Chama Cha Mapinduzi kinatambua uwezo na nguvu kubwa ya
wanawake katika kusukuma kasi ya maendeleo na kuleta mageuzi ya
kiuchumi, kijamii na kisiasa. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita
(2010 -2015) , SMZ chini ya uongozi wa CCM, imechukua hatua
mbalimbali za kuwaendeleza wanawake ili kuwajengea uwezo na
182
uthubutu wa kutumia fursa za kujiendeleza kiuchumi, kijamii na kisiasa
na kupata mafanikio yafuatayo: –
(a) Jumla ya vikundi 551 (Unguja 209 na Pemba 362) na SACCOS 53
(Unguja 24 na Pemba 29) za wanawake zimeanz ishwa. Aidha,
wajasiriamali wanawake 129 wamepatiwa mafunzo juu ya ubora
wa bidhaa na masoko ;
(b) Kwa kushirikiana na Chuo cha Barefoot College Tilonia cha India,
kituo cha kuwafundisha wanawake kute ngeneza vifaa vya
umeme wa jua kimeanzishwa huko Kibokwa Mkoa wa Kaskazini
Unguja ;
(c) Waratibu 40 na M akatibu watano ( 5) wa vikundi vya wanawake
wamepatiwa mafunzo ya uongozi, umuhimu wa Hati miliki,
UKIMWI, Sheria na jinsia. Pia wanawake 98 wamepatiwa
mafunzo juu ya mbinu za kubaini vitendo vya udhalilishaji na
kuepuk ana navyo ;
(d) Katika jitihada za ku piga vita udhalilishaji wa wana wake na
watoto, Nyumba Salama kwa ajili ya kuwahifadhi na
kuwahudumia waathirika wa vitendo hivyo, imeanzishwa. Jumla
ya waathirika 26 wa vitendo hivyo wamepatiwa huduma hizo ; na
(e) Skuli z a Benbe lla (Unguja ) na Uta ani (Pemba ) zimeteuliwa kuwa
Skuli Maalumu za Sayansi kwa Wanawake ili kuwashajiisha
wanaf unzi wa kike kupenda masomo ya Sayansi na Hisabati.
133. Ili kuendeleza juhudi za kuwawezesha wanawake kiuchumi
kijamii na kisiasa, CCM katika kipindi cha (2015 -2020) ,
itahakikisha kwamba SMZ inatekeleza yafuatazo: –
(a) Kuendelea kusimamia upatikanaji wa Haki za W anawake na
kupiga vita mila na desturi zinazowabagua au kudhalilisha
wanawa ke na kusimamia utekelezaji wa Sheria na M ikataba yote
ya Kimataifa ina yohusu ustawi wa mwanamke ;
(b) Kuendeleza juhudi za kuhamasisha wanawake na kuwajengea
uwezo na uthubutu ili kushiriki kikamilifu katika mabaraza ya
maamuzi ya ngazi mbalimbali za uongozi ; na
183
(c) Kuanzisha jumla ya vikundi vya kiuchumi 500 vya wanawake na
kupatiwa mafunzo ya ujasiriamali na mikopo ili kujiajiri wao
wenyewe.
Wazee
134. Wazee ni hazina na chemchem ya busara katika jamii kwa kuwa
mchango wao katika ujenzi wa Taifa letu ni wa kutukuka na wa
kupigiwa mfano. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010 -2015) ,
SMZ chini ya CCM imeendeleza jududi za kuwaendeleza wazee na
kupata mafanikio yafuatayo: –
(a) Jumla ya wazee 91 wameendelea kupatiwa huduma ya makazi
na mahitaji mengine muhimu katika Nyumba za Wazee za
Serikali (Unguja na Pemba). Aidha, jumla ya wazee 149
wameendelea kupatiwa msaada wa fedha kwa ajili ya kuweza
kujikimu kimaisha kila mwezi ; na
(b) Majengo matatu ya Nyumba za Wazee Sebleni zikiwemo nyumba
mbili na ukumbi wa mikutano yamefanyiwa matengenezo
makubwa. Miundombinu ya maji na umeme katika majengo hayo
pia yameimarishwa.
135. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015 -2020) , CCM
itahakikisha kwamba SMZ inaendelea kuchukua hatua thabiti
za kuwatunza na kuwaendeleza wazee kwa kutekeleza
yafuatayo: –
(a) Kuimarisha huduma za kijamii na mahitaji muhimu kwa wazee
wanaotunzwa katika nyumba za wazee ; na
(b) Kuanzisha na kusimamia uendeshaji wa programu maalumu ya
malipo ya pensheni na huduma nyingine muhimu kwa wazee
wote wa Zanzibar zikiwemo huduma za usafiri na matibabu bure.
Watu wenye ulemavu
136. Watu wenye ulem avu wanayo haki kwa mujibu wa Katiba ya
kutambuliwa utu wao, kuendelezwa, kuheshimiwa na kulindwa dhidi ya
vitendo vinavyoshusha utu wao ikiwemo ubaguzi, uonevu, ukatili na
mila potofu. Kwa kutambua uwezo mkubwa walionao watu wenye
184
ulemavu katika kujiendel eza na kuchangia uchumi na maendeleo ya
Taifa letu , katika kipindi cha 2010-2015, SMZ chini ya uongozi wa CCM
imewaendeleza watu wenye ulemavu ambapo pamoja na mambo
mengine imeanzisha Mfuko Maalumu na kuupatia jumla ya Shilingi
Milioni 167.6. Aidha, usaj ili wa watu wenye ulemavu umefanyika katika
wilaya zote za Unguja na Pemba ili kufahamu idadi yao kwa lengo la
kuwapatia visaidizi pamoja na dawa.
137. Ili kuwaendeleza watu wenye ulemavu, katika kipindi cha
miaka mitano ijayo (2015 -2020) , CCM itahakikisha kuw a SMZ
inaendeleza jitihada za kuimarisha ustawi wa watu wenye
ulemavu kwa kutekeleza yafuatayo: –
(a) Kuendelea kusimamia utekelezaji wa mipango na programu
mbalimbali zenye lengo la kuwaendeleza watu wenye ulemavu
na kuwapatia haki zao za msingi bila vikwazo ;
(b) Kuimarisha Mfuko wa Watu wenye Ulemavu na kuwapatia
huduma ya visaidizi pamoja na dawa bila malipo ; na
(c) Kuendeleza mafunzo na elimu kwa wazazi, walezi na walimu juu
ya makuzi ya mtoto mwenye ulemavu.
Wafanyakazi
138. Wafanyakazi wanao mchango mkubwa katika kuku za uchumi na
maendeleo ya nchi. Ili kuhakikisha kwamba mchango wa wafanyakazi
unaongezeka, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010 -2015),
SMZ imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha maslahi yao na kupata
mafanikio yafuatayo: –
(a) Sheria ya Ajira imefan yiwa mapitio na Kanuni kumi (10)
zimetayarishwa na kuanza kutumika. Kanuni hizo zinahusu
maslahi ya wanafanyakazi wa Sekta Binafsi, usajili na utendaji
kazi wa vyama vya wafanyakazi, mikataba, likizo bila ya malipo
na makundi maalumu ya wafanyakazi. Aidh a, Kanuni za
Utumishi wa Umma zimeandaliwa na kusambazwa kwa
wahusika ;
185
(b) Mashirikiano ya utatu kati ya Shirikisho la Vyama Huru vya
Wafanyakazi, Waajiri na Serikali yameimarishwa na majadiliano
ya pa moja yameendelezwa. Kwa kushiri kiana na Shiri ka la Kazi
Duniani (ILO), Toleo M aalumu la Sheria za Kazi kwa lugha
nyepesi ikiwemo Sheria ya Ajira, Sheria ya Uhusiano Kazini,
Sheria ya Usalama na Afya Kazini, Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii, Sheria ya Fidi a na Sheria ya Usafiri Baharini
limetayarishwa na kuanza kutumika ;
(c) Jumla ya wananchi 19,758 wamepatiwa ajira. Kati yao 5,667,
wameajiriwa katika Taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma na
7,256 Sekta Binafsi na 6,835 walipata ajira kupitia Vyama vya
Ushirika. Aidha, wananchi 3,400 walijiajiri wenyewe baada ya
kupatiwa mikopo na wengine 4,000 wamepata ajira zisizokuwa
za moja kwa moja ;
(d) Ili kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa ajira hasa kwa
vijana, Kituo M aalumu cha Kutoa Taarifa za Soko la Ajira
kimeanzishwa. Jumla ya vijana 2,473 wameorodheshwa na 1,978
kati yao wamefanikiwa kuajiriwa nje ya nchi kupitia Kituo hicho ;
(e) Maslahi ya Watumishi wa Umma yameimarishwa kwa
kuwaongezea mshahara pamoja na posho katika mwaka 2011 na
2014; na
(f) Kwa kuzingatia Sheria ya Usalama na Afya Kazini , Sehemu za
Kazi 351 zimesajil iwa na taarifa zake kuhifadhiwa katika daftari la
usajili wa sehemu za kazi. Aidha, taasisi 1,067 za kazi
zimefanyiwa ukaguzi (Unguja na Pemba ) na kupatiwa ushauri na
maelekezo ya kisheria.
139. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015 -2020) , CCM
itahakikis ha kuwa SMZ inaendelea kuimarisha maslahi ya
wafanyakazi kwa kutekeleza yafuatayo: –
(a) Kuendeleza mashirikiano ya utatu kati ya Serikali , Waajiri na
Wafanyakazi kupitia chombo chao (Shirikisho la Vyama Huru vya
Wafanyakazi) ili kuimarisha mahusiano mema ;
186
(b) Kusimamia utekelezaji wa Mpango wa Ajira kwa Vijana na
kuimarisha utendaji kazi katika Utumishi wa U mma kwa kuandaa
programu mbalimbali za mafunzo na upatikanaji wa rasilimali
watu wenye sifa, kuongeza maslahi ya watumishi ili kuongeza
ufanisi na tija ; na
(c) Kufanya ukaguzi katika maeneo 180 na kusajili taasisi za kazi 140
pamoja na programu mbalimbali zinazohusu masuala ya kazi.
Hifadhi ya Jamii
140. Katika kuhakikisha kwamba huduma za Hifadhi ya J amii zinaimarika,
katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010 -2015), mafanikio
yafuatayo yamepatikana: –
(a) Jumla ya wanachama waajiri wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
(ZSSF) kutoka Serikali Kuu imefikia 295, Mashirika ya Serikali 80
na Taasisi Binafsi ni 3,472. Idadi ya wanachama waajiriwa wa
Serikali Kuu ni 133,337, Mashirika ya Serikali ni 10,613 ;
(b) Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF) umeanzisha mfumo wa
uchangiaji wa hiari ili kutoa fursa kwa wananchi wengi zaidi
kunufaika na matunda ya Mfuko huo. Jumla ya wanachama
4,970 kutoka vikundi vya ushirika vya uzalishaji mali,
ujasiri amali, watu binafsi na Wazanzibari wanaofanyakazi nje ya
nchi wamesajiliwa chini ya mfumo huo na jumla ya shilingi
Milioni 122 zimekusanywa ;
(c) Ili kutunisha mapato yake na kuongeza fursa za ajir a kwa
wananchi, Mfuko ume wekeza katika miradi mbalimbali ya
kiuchumi. Miongoni mwa miradi hiyo, ni ujenzi wa Kiwanja cha
kufurahishia watoto cha Umoja – Kariakoo (Unguja ) na Kiwanja
cha Watoto cha Uhuru – Tibirinzi (Pemba ) pamoja na ujenzi wa
Mnara wa K umbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mfuko pia umeweza kutoa mikopo kwa taasisi mbalimbali za
Serikali na Binafsi. Mfuko pia umenunua jumla ya nyumba 10
katika eneo la Mbweni Unguja ambazo zimepangishwa kwa
taasisi za Serikali na watu binafsi ; na
187
(d) Mfuko umeimarisha mafao ya wanachama wake wanaostaafu
kwa kuonge za kiwango cha malipo ya kiinua mgongo na
pensheni.
141. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2015 -2020) , CCM
kitaielekeza SMZ kuimarisha zaidi huduma za Hifadhi ya Jamii
kwa kufanya mambo yafuatayo: –
(a) Kusimamia Utekelezaji wa Sera na Sheria ya Hifadhi ya Jamii;
(b) Kuimarisha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ili uendelee kuwekeza
katika miradi mbalimbali ya kiuchumi inayozalisha faida kubwa na
kukuza mapato ya mfuko huo ; na
(c) Kuhakikisha kwamba Mfuko wa Hifadhi ya Jamii unaendelea
kuboresha malipo ya pensheni na kuanzish a mafao mbalimbali
kwa wanachama wake.
188
SURA YA SABA
MAENEO MENGINE MUHIMU
Kuimarisha Muungano
142. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa mwaka 1964 ambao
umedumu kwa kipindi cha miaka 51 sasa, umekuwa daraja lisilotetereka
la kuwafikisha Watanzania katika azma yao ya kupata maendeleo ,
amani na ustawi. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010 -2015) ,
Chama Cha Mapinduzi kimeendelea kuzisimamia Serikali katika jitihada
za kuimarisha Muungano kwa kuta futa ufumbuzi wa changamoto
mbalimbali zinazouk abili kwa lengo la kudumisha amani, utulivu na
maendeleo.
143. Katika kipindi cha utekelzaji wa Ilani hii ya 2015 – 2020,
Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kizisimamia Serikali zake ili
zitekeleze majukumu yake ki kamilifu kwa lengo kuhakikisha
Muungano wetu unak uwa imara zaidi na kwamba amani na
utulivu vinaendelea kuwepo kwa kufanya yafuatayo: –
(a) Kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ;
(b) Kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika kuz ipatia ufumbuzi
changamoto zilizokuwepo kwa kuweka utaratibu wa kikatiba na
kisheria wa kutatua changamoto zitakazojitokeza ;
(c) Kuendelea kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha uchumi
katika pande mbili za Muungano hususan katika kubuni na
kutekeleza miradi ya maendeleo kwa manuafaa ya pande zote ;
na
(d) Kuendeleza harakati za kuulinda na kuutetea muungano kwa
kuzishirikisha asasi zisizo za Serikali kuimarisha utoaji wa elimu
ya uraia mashuleni, vyuoni na vyuo vikuu pamoja na makundi
mengine.
Utawala Bora na Demo krasia
144. Utawala Bora na Demokrasia ni moja ya nyenzo muhimu katika
kuhakikisha Taifa l inakuwa na utawala unaozingatia Sheria, Uwazi na
189
Uwajibikaji ili kutoa huduma bora kwa wananchi na kutok omeza
udikteta na umasikini katika jamii . Malengo mbalimbali ya ki uchumi na
kijamii hayataweza kufikiwa iwapo hak i, usawa, uwazi na uwajibikaji
vitakosekana . Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010 -2015),
mafanikio yafuatayo yamepatikana: –
(a) Uchaguzi huru na wa haki umeendelea kufanyika katika ngazi
mbalimbali za u ongozi ;
(b) Hatua z imeendelea kuchukuliwa katika kukuza, kulinda na
kuhifadhi Haki za Binadamu na Utawala B ora katika jamii ;
(c) Serikali zimeendelea kusimamia u tekelezaji wa Mpango wa
Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi (Open Government
Partnership – OGP). Aidha, Serikali imeandaa Rasimu ya Mu swada
wa Marekebisho ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(d) Mfumo wa Takwimu Huria u meanzish wa ambao utakuwa na
Tovuti Kuu ya Takwimu Huria, ili kuwezesha wananchi na wadau
wengine kupata taarifa za uendeshaji wa Serikali kwa urahisi na
kuzitumia katika shughuli na malengo mbalimbali; n a
(e) Mchakato wa kutungwa kwa Katiba mpya umeendeshwa na
umefikia hatua ya Katiba Inayopendekezwa iliyopitishwa na
Bunge Maalumu la Katiba ambayo itapigiwa K ura ya Maoni na
wananchi;
(f) Mfumo wa Kujitathmini katika Masuala ya Utawala Bora (APRM)
umeandaliwa na umeanza kufanya kazi;
(g) Katika kupanua demokrasia, Vyama vya Siasa vyenye usajili wa
kudumu vimeongezeka kutoka 17 mwaka 2005 hadi vyama 22
mwaka 2015;
(h) Mamlaka ya Vitambulisho vya Tai fa imeanza zoezi la kusajili na
kutoa vitambulisho vya uraia ambapo hadi Machi 2015 jumla ya
wananchi milioni 5 Tanzania Bara na 600,000 Tanzania Zanzibar
wameshapata vitambulisho.
145. Ili kuendeleza Utawala Bora, Demokrasia na Uwajibikaji , katika
kipindi cha miaka mitano ijayo (2015 -2020), CCM itahakikisha
kuwa, S erikali inatekeleza yafuatayo: –
190
(a) Kuendele za jitihada za kukuza, kulinda na kuhifadhi Haki za
Binadamu na Utawala wa Sheria katika ngazi zote za uongozi ;
(b) Kuifanyia mapitio Sheria ya Maadili ya Viongoz i wa Umma kwa
lengo la kuiboresha na pia kutunga Sheria mpya
itakayotenganisha shughuli za uongozi wa umma na biashara;
(c) Kuimarisha Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
Nchini (TAKUKURU) ili iweze kufanya kazi zake kwa ufanisi na
pia kuanzisha Mahakama Maalumu ya Makosa ya Rushwa na
Uhujumu Uchumi kwa lengo la kuharakisha uchunguzi na utoaji
hukumu kwa makosa hayo ;
(d) Kuimarisha mfumo wa utoaji haki kwa kufanya maboresho
katika utendaji wa vyombo vya maamuzi ikiwemo Mahakama,
Ofisi ya Mwendesha Mash itaka na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu;
(e) Kuimarisha Ofisi ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za
Serikali ili itekeleze majukumu yake kwa ufanisi zaidi ;
(f) Kuendelea na kukamilisha zoezi la uandikishaji na utoaji wa
vitambulisho vya uraia;
(g) Kukamilisha mchakato wa kutunga K atiba mpya na kuanza
kuitekeleza kwa mujibu wa Sheria ya M abadiliko ya Katiba; na
(h) Kuendelea kuimarisha Mfumo wa Kuji tathmini Kiutawala Bora
(APRM) na kutekeleza mapendekezo yaliyomo katika ripoti zake
za mara kwa mara;
Vyombo vya Ulinzi na Usalama
146. Kwa kutambua kazi kubwa iliyofanywa na vyombo vya ulinzi na
usalama katika kudumisha amani, usalama na utulivu nchini na kwa
kuzingatia umuhimu wa kuendeleza mafanikio haya, katika kipindi cha
Ilani hii (2015 -2020), CCM itazielekeza Serikali zake kuviimaris ha
vyombo vya ulinzi na usalama kwa kufanya yafuatayo: –
(i) Kuviwezesha vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuviongezea
raslimali watu na raslimali fedha kwa kadri uchumi
utakavyoruhusu.
(ii) Kuendelea kuboresha maslahi ya watendaji katika vyombo vya
ulinzi na usalama ikiwemo: makazi, mafunzo na zana za kazi za
kisasa.
191
(iii) Kuendelea kuweka mazingira yatakayowezesha Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT) kuimarisha mafunzo kwa vijana
wanaojiunga kwa hiari na wale wanaojiunga kwa mujibu wa
Sheria.
(iv) Kuendelea kushirikiana na Umoja wa Ma taifa (UN) na Umoja
wa Afrika (AU) katika kupeleka askari wetu kushiriki majukumu
ya ulinzi wa amani kwenye nchi mbalimbali duniani ili majeshi
yetu yaendelee kupata uzoefu na mbinu za kisasa za ulinzi wa
amani.
(v) Kuendeleza na kuimari sha mpango wa ulinzi sh irikishi na
kuwashirikisha wadau mbalimbali nchini kutoa elimu kwa
umma dhidi ya imani potofu zinazosababisha mauaji ya
vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi (Albin o). Aidha,
hatua kali na za haraka za kisheria zitachukuliwa kwa wote
watakaobainika kujih usisha na uhalifu wa aina hii, ujambazi na
vitendo vyenye mwelekeo wa ugaidi.
(vi) Kuendel ea kushiriki ana na Mataifa mengine na Asasi za
Kimataifa katika kupambana na makosa yanayovuka mipaka
hasa ugaidi, uharamia, utakatishaji wa fedha haramu (money
laundering ), biashara haramu ya madawa ya kulevya na
usafirishaji wa binadamu.
(vii) Kuimarisha uwezo wa vikosi vya Zimamoto na Uokoaji kwa
kuvipatia mafunzo na zana za kisasa za kupambana na
matukio ya moto , ajali na majanga mengine ya asili .
Serikali za Mitaa
147. Serikali z a Mitaa zimeundwa kwa ajili ya kupeleka madaraka na huduma
karibu na wananchi na kuhakikisha wananchi wanashirikishwa katika
uandaaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo mijini na vijijini.
Katika kipindi cha 2010-2015, mafanikio yafuatayo yamepatikana: –
(a) Sheria na Kanuni za uendeshaji wa Halmashauri za Wilaya, Miji na
Majiji zimefanyiwa mapitio kwa lengo la kuboresha mifumo ya
usimamizi wa mamlaka hizo ;
192
(b) Kiwango cha ruzuku ya Serikali Kuu kinachopelekwa katika
Halmashauri zote kimeongezeka kutoka Shilingi bilioni 950 mwaka
2010/2011 hadi Shilingi t rilioni 2.4 mwaka 2014/2015 ;
(c) Katika usimamizi wa matumizi sahihi ya fedha, ukaguzi wa mara
kwa mara umefanyika na hatua za kisheria na kinidhamu dhidi ya
watendaji wa Halmashauri waliojihusisha na vitendo vya
ubadhirifu na wizi wa fedha na rasilimali za wananchi zimeendelea
kuchukuliwa.
148. Ili kuziendeleza Mamlaka za Serikali za Mitaa, katika kipindi
cha 2015 -2020 ya Utekelezaji wa Ilani hii, CCM itahakikisha
kwamba, Serikali inatekeleza yafuatazo: –
(a) Kuendelea kuzif anyia mapitio Sheria zote zinazohusiana na
Serikali za Mitaa na Mamlaka ya Tawala za Mikoa ili kuharakisha
mchakato wa kugatua madaraka kwa lengo la kuziwezesha kutoa
huduma bora zaidi kutoka ngazi ya Kitongoji/ Kijiji hadi Kata;
(b) Kuendelea kuzijengea uwezo Serikali za Vijiji kwa kuzipatia
raslimali watu na fedha ili ziweze kupanga na kusimamia kwa
ukamilifu miradi yao ya maendeleo ;
(c) Kuendelea kuongeza kiwango cha ruzuku kuto ka Serikali Kuu
kinachopelekwa kwenye Halmashauri zote nchini kupitia Bajeti ya
Serika li ya kila mwaka kwa kadri ya uchumi utakavyokua;
(d) Kuendelea kuzihamasisha Halmashauri zote nchini kubuni vyanzo
vipya vya mapato ya ndani (own sources) pamoja na kuimarisha
mifumo ya ukusanyaji na udhibiti wa mapato ;
(e) Kuimarisha ubora na upatikanaji wa hud uma za kijamii hususan
afya, elimu, maji na miundombinu ya kiuchumi katika
Halmashauri zote nchini pamoja na kuongeza idadi ya wataalamu
wa fani mbalimbali ; na
(f) Kuendelea kuchukua hatua kali za kinidhamu na kisheria dhidi ya
watendaji wa Halmashauri za wila ya watakaobainika kuhusika na
vitendo vya ubadhirifu na wizi wa mali ya umma pamoja na
matumizi mabaya ya madaraka.
Mambo ya Nje
193
149. Ili kuimarisha mahusiano baina ya nchi yetu na nchi nyingine
duniani, Chama Cha Mapinduzi kitaihimiza Serikali kufanya
mambo y afuatayo katika kipichi cha utekelezaji wa Ilani hii ya
2015 – 2020: –
(a) Kuendelea kushiriki kwenye utengamano wa kikanda na
kuendeleza Diplomasia ya Uchumi kwa kuzingatia maslahi
muhimu ya nchi yetu ili kunufaisha Watanzania wote;
(b) Kuendelea kuimarisha uhusi ano wa Tanzania na mataifa mengine
na taasisi za kimataifa;
(c) Kuendelea kupigania mfumo wa haki wa utawala , siasa na
uchumi duniani;
(d) Kuendelea kuunga mkono jitihada za kulinda amani na utulivu
duniani;
(e) Kuendelea kupigania Diplomasia ya Uchumi na Siasa; na
(f) Kuendelea k ujenga au kununua majengo kwa ajili ya balozi za
Tanzania kwenye nchi ambazo kwa sasa yanakodishwa ili
kupunguza gharama.
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
150. Ili kuimarisha mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,
katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2015 -2020, Chama
Cha Mapinduzi kitaihimiza Serikali kufanya mambo yafuatayo: –
(a) Kutekeleza Mpangokazi wa miaka kumi wa kuelekea katika eneo
la Sarafu moja la Afrika Mashariki;
(b) Kutekeleza ujenzi wa mitandao ya reli na barabara
zinazou nganisha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki;
(c) Kuendelea na utekelezaji wa hatua za awali za mtangamano wa
Afrika Mashariki za Umoja wa Forodha na Soko la Pamoja ili
kuhakikisha Watanzania wanaendelea kunufaika na fursa za
kibiashara, uwekezaj i na ajira zitokanazo na utekelezaji wa hatua
hizo;
194
(d) Kuendelea kushirikiana na wadau kutoa elimu kwa wananchi
kuhusu fursa zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ili
wazitumie na kunufaika nazo; na
(e) Kuendelea na majadiliano na utekelezaji wa Ubi a wa Biashara na
uwekezaji baina ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na
Marekani, Mkataba wa Ubia wa Kiuchumi kati ya Nchi za Jumuiya
ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya (EAC -EU Economic
Partnership Agreement – EPA) na Kuanzisha eneo Huru la
Biashara la Utatu wa EAC -COMESA -SADC.
Kuhamia Makao Makuu Dodoma
151. Chama Cha Mapinduzi kinatambua jitihada zilizofanywa na
Serikali za kuunganisha mji wa Dodoma na mikoa mingine kwa
njia ya barabara za lami. Aidha, baadhi ya majengo ya Serikali
yameendelea kujengwa Dodoma likiwemo jengo la Bunge,
Benki Kuu, Hazina, Chuo Kikuu cha Dodoma na Shirika la
Nyumba la Taifa limejenga nyumba kwa ajili ya makazi ya
wananchi. Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2015 –
2020, Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza Serikali ku fanya
yafuatayo: –
(a) Kutunga Sheria itakayoutambua mji wa Dodoma kuwa Makao
Makuu ya nchi;
(b) Kusimamia azma ya Serikali ya kuhakikisha majengo yote ya
Wizara za Serikali yanajengwa Dodoma badala ya Dar es Salaam;
na
(c) Kuongeza kasi ya kupima viwanja kwa ajili ya makazi, viwanda
na taasisi ; na kuendelea ku boresha miundombinu ikiwemo maji,
umeme na barabara.
195
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) wakipima
viwanja kwa kutumia vifaa vya kisasa
196
Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi
152. Kupunguza na kuk abiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi
ni jambo muhimu katika kufikia maendeleo endelevu. Pamoja
na jitihada ambazo zimekuwa zikichukuliwa katika kukabiliana
na uchafuzi wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi, bado
zipo changamoto nyingi. Ili kuba biliana na changamoto hizo,
Chama Cha Mapinduzi katika kipindi cha Ilani hii ya 2015 -2020,
kitaielekeza Serikali kufanya yafuatayo: –
(a) Kupanga na kuendelea kutekeleza miradi ya upandaji miti ili
kuondokana na hatari ya Taifa kugeuka kuwa jangwa kwa
kuhakikis ha kila Halmashauri inapanda na kutunza miti
isiyopungua milioni 1.5 kila mwaka;
(b) Kuhakikisha Halmashauri zote nchini zinaweka na kusimamia
Sheria ndogo za hifadhi ya mazingira;
(c) Kuweka utaratibu wa kuwaelimisha na kuwashirikisha wananchi
kuhusu usimamizi na utekelezaji wa Sheria ya Utunzaji wa
Maeneo ya Fukwe na rasilimali zilizopo;
(d) Kuendelea kufanya tathmini ya vyanzo vya maji
vilivyohifadhiwa, kuongeza vyanzo vipya na kufufua vilivyopotea
ama kuharibika ili kuwa na uhakika wa upatikanaji wa maji safi
na sa lama;
(e) Kuweka utaratibu wa kupunguza bei ya gesi na majiko yake na
kuhamasisha jamii kutumia umeme na nishati mbadala ili
kuongeza idadi ya watumiaji wa nishati hizo kutoka asilimia 36
mwaka 2015 hadi asilimia 50 mwaka 2020 ili kupunguza
matumizi ya kuni na mkaa kwa lengo kupunguza kasi ya
uharibifu wa mazingira; na
(f) Kuimarisha ukaguzi na usimamizi wa shughuli za viwanda ili
zisiharibu mazingira.
Kujenga uwezo wa kukabili majanga
153. Majanga ni matukio yanayojitokeza na yenye uwezo mkubwa
wa kuleta maafa yanay ohatarisha maisha ya watu na mali zao,
miundombinu na huduma mbalimbali za jamii. Katika kipindi
197
cha miaka mitano ijayo (2015 -2020), katika kukabiliana na
maafa, Chama Cha Mapinduzi kitazielekeza Serikali kufanya
yafuatayo: –
(a) Kusimamia kikamilifu Utekelezaj i wa Sheria mpya ya Kukabiliana
na Maafa katika ngazi zote kuanzia Taifa hadi Vijijini; na
(b) Kujenga Kituo cha Menejimenti ya Maafa na Mawasiliano ili
kuongeza uwezo wa nchi katika kukabiliana na maafa.
Mapambano Dhidi ya VVU/UKIMWI
154. Katika kipindi cha miaka mitano ya Ilani hii ya 2015 -2020,
Chama Cha Mapinduzi kitazielekeza Serikali zake kuendeleza
kwa nguvu zaidi mapambano dhidi ya UKIMWI kwa kutekeleza
yafuatayo: –
(a) Kupunguza au kuondokana kabisa na utegemezi wa wafadhili
kwa kuanzisha Mfuko Maalumu wa UKIM WI (AIDS Trust Fund)
ukiwa na lengo la kuongeza rasilimali kwa ajili ya kuboresha
huduma za UKIMWI zinazotolewa ;
(b) Kufanya jitihada za kupunguza kasi ya maambukizi katika jamii
kutoka asilimia 5.1 mwaka 2015 hadi asilimia 3.0 ifikapo 2020 ;
(c) Kuimarisha huduma za elimu ya UKIMWI kwa njia ya
mawasiliano baina ya wanafamilia, watu mashuhuri, programu za
mahali pa kazi na viongozi wa dini ;
(d) Kuongeza usambazaji wa taarifa zinazohusu kubadili tabia
hatarishi na upatikanaji wa huduma bora kwa waathirika wa
UKIMWI kupit ia Vyombo vya Habari;
(e) Kuendeleza tafiti za UKIMWI na kutathmini vipaumbele kwa ajili
ya kufanya maamuzi na kuandaa programu za UKIMWI ; na
(f) Kutoa elimu kwa umma juu ya uhusiano uliopo kati ya utumiaji
wa dawa za kulenya na maambukizi ya VVU.
Mapambano Dhidi ya Dawa za Kulevya
155. Matumizi ya madawa ya kulevya ni tatizo linaloongezeka si
hapa Tanzania tu, bali duniani kote. Madhara ya matumizi ya
madawa ya kulevya ni makubwa hususan kwa vijana kwani
yanapunguza nguvukazi ya Taifa na kuongeza gharama za
198
kuwatibu n a kuwatunza waathirika. Katika kipindi kijacho,
Chama kitaielekeza Serikali kuongeza jitihada za kupambana
na madawa ya kulevya kwa kutekeleza yafuatayo: –
(a) Kuanzisha Mamlaka ya Kudhibiti na Kuzuia Dawa za Kulevya ;
(b) Kuongeza utoaji wa dawa na matibab u pamoja na kuanzisha
vituo vya kuhudumia wananchi walioathirika na matumizi ya
dawa za kulevya ;
(c) Kushirikiana na asasi za kijamii na kuziwezesha ili kuinua uwezo
wa kushiriki katika kutoa elimu juu ya athari ya matumizi ya
dawa za kulevya katika jamii zinazowazungu ka; na
(d) Kusimamia kwa ukamilifu s heria mpya ya kudhibiti madawa ya
kulevya.
Vyombo vya Habari
156. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010 -2015) , Sekta ya Habari
imeimarishwa zaidi na kupata mafanikio yafuatayo: –
(a) Serikali imeweka mazingira bora yaliyow ezesha kuanzishwa kwa
vyombo vingi vya habari nchini ;
(b) Matangazo ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) :-
(i) TBC imeendelea kuimarisha usikivu wa Radio na
Televisheni katika maeneo yenye miinuko ;
(ii) TBC imefunga mitambo ya kisasa ya idhaa ya TBC Taifa
na TBC FM yenye uwezo wa kusikika kwa ufasaha bila
mikwaruzo katika mikoa mbalimbali nchini ; na
(iii) Shirika limejenga mitambo ya kurushia matangazo ya
Televisheni katika mfumo wa kidijitali katika maeneo
mbalimbali nchini.
(iv) Mitandao mingi ya kijamii imeanzishwa na kuwa moja ya
njia kuu za upashanaji wa habari kwa haraka.
157. Ili kuendelez a Tasnia ya Habari na Uhuru wa Vyombo vya
Habari, katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2015 –
2020, Chama kitaielekeza Serikali ku endelea kuboresha
mazingira ya Uhuru wa Vyombo vya Habari kwa kufanya
mambo yafuatayo: –
199
(a) Kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa kwa urahisi na kwa
wakati kwa mujibu wa Sheria;
(b) Kuharakisha mchakato wa kupitisha na kuanza kutekeleza Sheria
kuhusu uhuru wa W ananchi kupata habari na uhuru wa Vyombo
vya Ha bari kupata na kutoa habari;
(c) Kuhakikisha kwamba matangazo ya Shirika la Utangazaji la Taifa
(TBC) yanasikika nchini kote kwa ku lipatia uwezo wa rasilimali
watu, fedha na vifaa vya kisasa ;
(d) Kuimarisha uwezo wa Idara ya Habari (MAELEZO) kama msemaji
Mkuu wa Serikali ;
(e) Kuanzisha Mfuko wa kuwaendeleza Wanahabari Kitaaluma ;
(f) Kuhakikisha kwamba kunakuwepo Uhuru wa Vyombo vya H abari
ili vitekeleze wajibu wake inavyopasa kwa mujibu wa Sheria ; na
(g) Kujenga ushirikiano wa Kizalendo baina ya Vyombo vya Habari
vya Umma na vya Binafsi katika kuitangaza Tanzania nchi za nje
hasa katika eneo la Vivutio vya Utalii na kujenga Taswira ya nchi.
Utamaduni
158. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010 -2015) , Sekta ya
Utamaduni imeendelea kuimarishwa zaidi ambapo maeneo yote muhim u
yanayohusu historia hasa ya mapambano ya ukombozi ya nchi yetu na
Kusini mwa Afrika yameendelea kutunzwa na kutangazwa kama vivutio
vya utalii.
159. Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2015 -2020,
Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza Se rikali kuimaris ha na
kuboresha Sekta ya Utamaduni nchini ili ichangie kikamilifu
katika kudumisha utamaduni wa Mtanzania kwa kutekeleza
mambo yafuatayo: –
(a) Kuhakikisha lugha ya Kiswahili inaendelezwa ndani na nje ya
nchi na kutumika kama bidhaa ya soko na chanzo cha ajira
kwa wataalamu na wapenzi wa Kiswahili. Aidha, kupanua
wigo wa misamiati na istilahi za lugha za Kiswahili kwa
kufanya utafiti wa Lugha za Kijamii;
200
(b) Kuandaa Sera ya Utamaduni wa Taifa kuhusu masuala ya
Lugha ya Taifa, Filamu, Muziki, Ngoma za Asili na Sanaa;
(c) Kusimamia Utekelezaji wa Sheria zinazohusu shughuli za
Filamu, Michezo ya Kuigiza, Muziki, Ubunifu kwa lengo la
kulinda haki na Maslahi ya Makundi hayo; na
(d) Kuhamasisha na kuimarisha ushiriki wa Sekta Binafsi katika
kuboresha Miundombinu ya Kiutamaduni ik iwemo ya Tasnia
ya Filamu, Michezo, Sanaa ya Muziki na Ubunifu kwa lengo
kulinda haki na Maslahi ya Makundi hayo.
Michezo
160. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010 -2015) , Sekta ya Michezo
imeimarishwa zaidi na kupata mafanikio yafuatayo: –
(a) Ukarabati w a miundombinu ya michezo nchini umefanyika
ukiwemo uwanja wa Uhuru (Dar es Salaam), Nyamagana
(Mwanza) na Sokoine (Mbeya) ;
(b) Sekta binafsi imehamasishwa ambapo kampuni binafsi ya AZAM
imeanzisha Kituo cha Michezo na kujenga Uwanja wa kisasa wa
Michezo ;
(c) Jumla ya Vituo vya Michezo 75 vimeanzishwa kwa lengo la
kuongeza fursa kwa watoto na vijana kuonesha vipaji vyao ili
viweze kutambuliwa na kuendelezwa ;
(d) Mashindano ya Michezo ya Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na
Sekondari (UMISSETA) imerudishwa na yanafanyika ki la mwaka ;
na
(e) Mradi wa majaribio wa kufundisha riadha kwa watoto (KIDS
ATHLETICS) umeanzishwa na unashirikisha shule 98 katika
Mikoa minne ya Tanzania Bara na skuli 18 za Zanzibar.
161. Katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa Ilani hii ya
2015 – 2020, Chama Cha Mapinduzi kitazielekeza Serikali
kuimarisha Sekta ya Michezo ili kuinua kiwango cha michezo
nchini ikiwa ni pamoja na kuifan ya Sekta ya Michezo kutoa
201
fursa za ajira husasan kwa vijana kwa kutekeleza mambo
yafuatayo: –
(a) Kujenga na kuimarisha miun dombinu ya michezo nchini ;
(b) Kupanua wigo wa vyanzo endelevu vya fedha z a uendeshaji na
ugharamiaji wa maendeleo ya m ichezo hapa nchini kwa kuanzisha
Bahati Nasibu ya Michezo ;
(c) Kuhamasisha na kusisimua Maendeleo ya Michezo katika ngazi
zote hapa nchini kwa ku endeleza matamasha ya Michezo kuanzia
ngazi za Vijiji, Kata, Wilaya, Mkoa hadi Taifa ;
(d) Kuweka vivutio vya kuwavutia wawekezaji na washiriki wengine
kuwekeza na kugharamia shughuli mbalimbali za michezo nchini ;
(e) Kulinda maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya michez o na burudani
kwa kushirikiana na makundi ya wanamichezo, jamii na mamlaka
nyingine zilizopo ;
(f) Kwa kushirikiana na Sekta B inafsi, kuanzisha Kituo cha
Kuendeleza Vipaji vya Wanamichezo M ahiri na kutumika kama
kituo cha maandalizi ya wanamichezo wanaoiwakilis ha Tanzania
katika michezo ya Kimataifa (Olympic village) ;
(g) Kuendelea kufundisha wataalam wa michezo na kuhakikisha
wanapatikana katika ngazi zote ;
(h) Kuwahamasisha wanamichezo kujiunga na kunufaika na fursa
zitolewazo na Mifuko ya Hifadhi ya J amii kwa ustawi na maisha
yao ya baadaye ; na
(i) Kuendeleza shughuli za michezo mashuleni ili kuibua vipaji vya
michezo mbalimbali nchini.
Tasnia ya Sanaa
162. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2010 -2015), Serikali
imeendelea kuwatambua na kuthamini kazi za sanaa na w asanii
nchini.
163. Tasnia ya Sanaa ikiwemo filamu, muziki, michezo ya kuigiza
inayo nafasi kubwa ya kupanua soko la ajira na kukuza pato la
202
mtu mmoja mmoja na Taifa kama ilivyo kwa nchi nyingi
duniani. Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii (2015 –
2020) Cha ma Cha Mapinduzi kitaielekeza Serikali yake kufanya
yafuatayo: –
(a) Kuendelea kuimarisha uwezo wa Bodi ya Filamu nchini ili
isimamie kwa ukamilifu maendeleo ya tasnia ya Filamu kwa
kuendeleza ujuzi katika sekta hii;
(b) Kuanzisha na kuratibu Mfuko wa Maendeleo ya Tasnia ya Sanaa
utakaowezesh a upatikanaji wa mikopo ya masharti nafuu kwa
wazalishaji, watengenezaji, wawekezaji wakubwa, wa kati na
wadogo wa tasnia hii nchini;
(c) Kuwekeza katika mradi wa Ujenzi wa Jumba Changamani la
Uzalishaji wa Filamu (Multipurpose Fil amu Complex) ;
(d) Kuendeleza programu z a Ujasiriamali kwa vijana n a makundi
mbalimbali kwa kutoa ushauri, mafunzo, mitaji na huduma za
kiufundi kwa wajasiriamali w alio katika tasnia ya sanaa na
kuweka msukumo mkubwa katik a maendeleo ya tasnia ya
sanaa;
(e) Kuwe ka mikakati ya kuhakikisha kuwa Sekta ya Filamu inakuwa
na bidhaa zenye ubora, wataalamu wenye weledi na
kuondokana na uharamia wa bidhaa za filamu ;
(f) Kuhakiksha kazi za wasanii zinalindwa ili zisighushiwe wala
kuibiwa;
(g) Kuhakikisha wasanii wanapata maslahi wanayostahili kutokana
na kazi zao kwa kuboresha mazingira ya kisheria;
(h) Kuweka msukumo katika kuhakikisha kwamba shughuli na
biashara za sanaa zikiwemo filamu, muziki, ngoma za asili,
michezo ya kuigiza na kazi nyingine za ubunifu zinarasimishwa
ili kuende leza tasnia hii na wasanii wenyewe;
(i) Kuanzisha maeneo changamani ya shughuli za utamaduni nchini
kwa kujenga miundombinu ya kisasa;
203
(j) Kuweka kumbukumbu na kuhimiza matumizi ya mila na desturi
dhidi ya utandawazi kwa kufanya utafiti wa mila na desturi za
jamii ya Kitanzania; na
(k) Kuhifadhi kumbukumbu ya ushiriki na mchango wa Tanzania
katika harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika kwa kuendeleza
utekelezaji wa Programu ya Urithi wa Ukombozi.
Kuendeleza Makundi Maalum
Wazee
164. Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuwaenz i wazee kutokana na
michango yao katika kulijenga Taifa letu.
165. Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2015 – 2020,
Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza Serikali kufanya yafuatayo: –
(a) Kuhakikisha wazee wanatambuliwa na kupatiwa huduma za
matibabu bila mal ipo;
(b) Kuhakikisha wazee wanapata haki zao za kisheria na kupa ta
fursa sawa katika ngazi zote;
(c) Kulindwa dhidi ya vitendo vya ukatili vikiwemo mateso na
mauaji;
(d) Kuwawekea miundombinu na mazingira bora
yatakayowawezesha kwenda wanapotaka na kutumia vyombo
vya usafiri wa umma kwa gharama nafuu; n a
(e) Kuweka utaratibu na vigezo vitakaowezesha wazee wote nchini
kulipwa pensheni.
Watu Wenye Ulemavu
166. Chama Cha Mapinduzi kinaamini kwamba: “Binadamu wote ni
sawa na kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na
kuthamin iwa utu wake”. Kwa imani hii, katika kipindi cha
miaka mitano ijayo, Chama Cha Mapinduzi kita zielekeza
Serikali kuhakikisha kwamba: –
(a) Walemavu wote nchini wanaendelea kutambuliwa na kulindwa
na vitendo vinavyoshusha utu vikiwemo ubaguzi, uonevu, ukatili
na mila potofu;
204
(b) Kuhakikisha kwamba watu wenye u lemavu wa ngozi (albino )
wanalindwa dhidi ya ukatili na ubaguzi wa aina yoyote;
(c) Kuhakikisha wanapata elimu kwa kutumia vifaa maalumu na
kushiriki katika nafasi za uwakilishi na shughuli za kijamii;
(d) Kuwawekea m iundombinu na mazingira rafiki
yatakayowawezesha kwenda wanapotaka, kutumia vyombo vya
usafiri na kupata habari;
(e) Kuboresha mahitaji maalumu ya watu wenye ulemavu kwa
kuwawezesha kupata taarifa mbalimbali kwa urahisi kwa
kutumia lugha ya alama, alama mguso, maandishi ya nukta
nundu, maandishi yaliyokuzwa au njia nyingine zinazofaa;
(f) Kuhakikisha wanapata ajira na kufanya kazi; na
(g) Kupata huduma bora za afya, uzazi salama, marekebisho na
utengemao .
Wanawake
167. Kwa kutambua kwamba wanawake wanao uwezo mkubwa wa ku leta
mabadiliko makubwa katika jamii, ipo haja ya kuendelea kuwathamini,
kuwalinda na kuwaendeleza ili waweze kushiriki kikamilifu katika
mchakato wa maendeleo ya Taifa letu.
168. Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2015 – 2020,
Chama kitaielekeza Serikali kufanya yafuatayo: –
(a) Kuendelea kuweka utaratibu wa kikatiba na kisheria
utakaowawezesha wanawake kushika nafasi sawa (50/50) za
uongozi katika vyombo vya maamuzi katika ngazi zote;
(b) Kuhakikisha wa nawake wanapata haki zao za kisheria na kupata
fursa sawa katika ngazi zote;
(c) Kupata haki ya kulindwa dhidi ya ubaguzi, udhalilishaji,
dhuluma, unyanyasaji, ukatili wa kijinsia na mila potofu; na
(d) Kuhakikisha kuwa ajira za wanawake zinalindwa wakati wa
ujauzito na pale wanapojifungua.
Watoto
205
169. Kila mtoto ana ha ki ya kuishi, kukua na kulelewa kikamilifu ili Taifa kwa
siku za baadaye lipate raia wema na waadilifu.
170. Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii ya 2015 – 2020,
Chama kitaielekeza Serikali kuende lea kutekeleza mambo
yafuatayo: –
(a) Kuhakisha watoto wanali ndwa dhidi ya uonevu, ukatili,
udhalilishaji, utumikishwaji na mila potofu;
(b) Kuhakikisha watoto wanapata lishe bora, huduma ya afya,
makazi na mazingira yanayomjenga kimwili, kiakili na kimaadili;
(c) Kuwapatia haki ya kushiriki katika shughuli zinazolingana na
umri, kuhakikisha kwamba wanapata malezi na ulinzi kutoka
kwa wazazi, walezi, jamii au mamlaka ya nchi bila ubaguzi
wowote; na
(d) Kuboresha viwanja vya kuchezea watoto katika ngazi za mitaa,
vijiji na vitongoji.
Vijana
171. Vijana ni chach u ya maendeleo ya nchi k atika n yanja zote kwani ndiyo
nguvu kazi ya Taifa na yenye fikra ya ubunifu endelevu. Kwa
kutambua uwezo na mchango wao jitihada kubwa zimefanywa na
Serikali katika kipindi kilichopita kuwashirikisha vijana katika shughuli
za maendeleo ya kijamii, kiuchum i na kisiasa.
172. Katika kipindi cha utekele zaji wa Ilani hii (2015 -2020), CCM
itaielekeza Serikali kufanya yafuatayo: –
(a) Kuendelea kuwashirikisha vijana kwa kuwapa nafasi za
maamuzi katika ngazi zote kutegeme ana na sifa, weledi na
uadilifu;
(b) Kuwaandaa n a kuwawezesha vijana kushiriki kwa ukamilifu
katika s hughuli zote za Baraza la Taifa la Vijana ;
(c) Kuendelea kutoa elimu kwa vijana kwa kuwatumia wadau
mbalimbali ili kuwajenga kuwa wazalendo na kuepuka
vishawishi vitakavyow aharibia malengo yao ya baadaye ;
206
(d) Kuvitambua na kuviendeleza vipaji vya vijana katika nyanja za
michezo, s anaa, elimu, ubunifu na uongozi; na
(e) Kuanzisha uraghibishi kwa vijana waweze kujiajiri kwa
kuthamini kazi nyingine za mikono na utaalamu kama vile
kilimo, ufundi, michezo, s anaa na kazi nyingine za kitaaluma .
Wafanyakazi
173. Chama Cha Mapinduzi kwa asili yake ni chama cha Wakulima na
Wafanyakazi. Wafanyakazi kwa tafsiri pana ni waajiriwa na waliojiajiri.
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, jitihada zimeendelea
kuchukuliwa il i kuboresha maslahi ya wafanyakazi ambapo mafanikio
yafuatayo yamepatikana: –
(a) Mishahara ya Wafanyakazi:
(i) Bodi za Kurekebisha Mishahara katika Sekta Binafsi
zimeongezeka kutoka nane mwaka 2010 hadi 12 mwaka
2013 ambapo kima cha chini cha mshahara katika sekta
hiyo kimeongezeka mara mbili. Aidha, nyongeza ya
mwaka 2013 ya kima cha chini cha mshahara
imeongezeka kati ya asilimia 21 hadi 65 ya viwango vya
mishahara vya mwaka 2010;
(ii) Kodi ya Mapato ya Wafanyakazi (PAYE) imepunguzwa
kutoka asilimia 18 mwaka 2005 had i asilimia 1 1 mwaka
2015;
(iii) Kima cha chini cha mshahara katika sekta ya umma
kimeongezeka kutoka Shilingi 65,000 mwaka 2005 hadi
Shilingi 300,000 mwaka 2015; na
(iv) Sheria za Kazi zimeendelea kufanyiwa mapitio ili
kuwawezesha wafanyakazi kujiunga katika vyama h uru
vya wafanyakazi kwa hiari yao.
(b) Afya na Usalama Mahala pa Kazi:
(i) Jumla ya kaguzi 220,350 zimefanyika ikiwa ni wastani wa
kaguzi 40,000 kwa mwaka kwa lengo la kuhakikisha
waajiri wanafuata Sheria za Kazi ipasavyo;
(ii) Jumla ya kaguzi za kawaida 26,412 na kag uzi maalumu
53,807 kuhusiana na Afya na Usalama kazini zimefanyika.
207
Aidha, wafanyakazi 136,076 walipimwa afya zao ili kubaini
matatizo na athari za kiafya zitokanazo na maeneo
wanayofanyia kazi;
(iii) Maafisa 4,931 wamepatiwa mafunzo mbalimbali kuhusu
Usalama na Afya Mahali pa Kazi;
(iv) Jumla ya sehemu za kazi 5,595 zilisajiliwa na kupewa
vyeti vya usajili; na
(v) Jumla ya sehemu za kazi 398 zilipewa leseni za kukidhi
viwango vya chini vya Sheria Na. 5 ya mwaka 2003 ya
Usalama na Afya Mahali pa Kazi .
(c) Migogoro Sehemu za K azi:
(i) Migogoro 10,281 imesuluhishwa ambapo uamuzi ulitolewa
kwa migogoro 6,057 na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi
(CMA);
(ii) Wastani wa muda wa kusikiliza na kusuluhisha migororo
ya wafanyakazi umepungua kutoka siku 30 hadi siku 12
wakati muda wa kusikiliza na kua mua umepungua kutoka
siku 90 hadi siku 85;
(iii) Wafanyakazi wapatao 1,908,000 na waajiri 6,890
wamepewa elimu kuhusu Sheria za Kazi;
(iv) Jumla ya Mabaraza ya Wafanyakazi 265 yameundwa
katika Taasisi za Umma ikiwa ni sawa na asilimia 86.6 ya
lengo;
(v) Jumla ya vyama sa ba vya wafanyakazi na shirikisho moja
la vyama vya wafanyakazi vimesajiliwa kati ya mwaka
2010 na 2015 kwa lengo la kuongeza na kuboresha wigo
wa ushiriki, majadiliano na utetezi wa haki za wafanyakazi
na waajiri katika sehemu za kazi;
(vi) Vyama vya Wafanyakaz i vilivyosajiliwa vimeongezeka
kutoka vyama 24 mwaka 2009 hadi 31 mwaka 2015; na
(vii) Waajiri wameendelea kushirikisha wafanyakazi katika
hatua za maamuzi kwa lengo la kuongeza ufanisi katika
maeneo ya kazi.
(d) Sheria ya Ajira kwa Wageni: –
208
Sheria ya Ajira kwa wa geni imetungwa mwaka 2015 na kuweka
mamlaka moja ambayo ni Wizara ya Kazi na Ajira kuwa
msimamizi wa utoaji wa vibali vya ajira kwa wageni ili kulinda
ajira za Watanzania zisichukuliwe na wageni.
(e) Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
(i) Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii
(SSRA) imeanzishwa mwaka 2010;
(ii) Sheria za mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii zimefanyiwa
marekabisho ili kuipa SSRA mamlaka ya kusimamia na
kudhibiti Mifuko ya Hifadhi ya Jamii;
(iii) Kanuni za kukokotoa mafao ya pensheni zimerekebishwa
mwaka 20 14 ili kupunguza tofauti ya malipo ya mafao ya
pensheni kwa wanachama miongoni mwa Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii pamoja na kuanzisha mafao mapya kwa
wanachama;
(iv) Marekebisho ya Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
kupitia Sheria Na. 5 ya mwaka 2012 yameruhusu
wanachama kujiunga na mfuko wowote wanaoupenda.
Aidha, marekebisho hayo yametoa fursa kwa Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii kusajili wanachama kutoka katika sekta
isiyo rasmi; na
(v) Katika mwaka 2014/2015 Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi wanaougua au kuumia kazini umea nzishwa.
174. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Chama Cha Mapinduzi
kitaielekeza Serikali yake kuendelea kulinda na kuboresha haki
na maslahi ya wafanyakazi kwa kufanya mambo yafuatayo: –
(a) Kuhakikisha kwamba mfanyakazi atalipwa kima cha chini cha
mshahara kinachokidhi mahitaji muhimu ya maisha kwa
kuzingatia uwezo wa kiuchumi wa Taifa;
(b) Kuwapunguzia wafanyakazi mzigo wa Kodi ya Mapato (PAYE)
kufikia tarakimu moja (single digit);
209
(c) Kuboresha na kulinda afya na usalama wa wafanyakazi
wakiwa sehemu za k azi;
(d) Kuridhia mikataba ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) yenye
maslahi kwa wafanyakazi;
(e) Kuboresha mazingi ra ya utendaji wa wafanyakazi wa Sekta
Binafsi ikiwemo kupewa mikataba kwa mujibu wa Sheria;
(f) Kuweka utaratibu wa kupunguza pengo la mapato kati ya
wafanyakazi wa ngazi ya chini na juu;
(g) Kuhakikisha kwamba wizi, ubadhirifu, utoro na rushwa
vinakomeshwa kwa lengo la kuongeza tija sehemu za kazi; na
(h) Kuweka utaratibu maalumu wa kutoa motisha kwa
wafanyakazi wanaofanyakazi katika mazingir a magumu.
(i) Hifadhi ya Jamii:
(i) Kuendelea kutekeleza mikakati mbalimbali kwa lengo
la kuimarisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ili iendelee
kutoa huduma bora na endelevu kwa wanachama
wao; na
(ii) Kuhamasisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuanzisha
mfuko mkubwa kwa a jili ya kutoa mikopo kwa
wafanyakazi na wajasiriamali wadogo kwa masharti
nafuu.
SURA YA NANE
CHAMA CHA MAPINDUZI
175. Ilani hii ya Chama Cha Mapinduzi ya kipindi cha mwaka 2015 -2020
imejikita katika kupambana na changamoto kubwa nne ambazo ni:
umaskini, ukose fu wa ajira hasa kwa vijana, rushwa na
ubadhirifu wa mali za umma ; na jukumu la kudumisha amani
na utulivu . Hii ndiyo ahadi na nadhiri kubwa ambayo Chama Cha
Mapinduzi kinaweka kwa wananchi endapo watakichagua na kuunda
Serikali.
176. Kwa muktadha huo katik a kipindi cha Utekelezaji wa Ilani hii, Serikali
zote mbili zitakazoundwa na CCM yaani Serikali ya Jamhuri ya
210
Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, zitatumia nguvu zote
na kwa kushirikisha Sekta Binafsi zitasimamia mambo yafuatayo: –
(a) Kuongeza uweke zaji katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
ambayo inategemewa na wananchi walio wengi nchini ;
(b) Kuweka msukumo katika uanzishaji wa viwanda vya kusindika
mazao ya kilimo, ufugaji na uvuvi ;
(c) Kuweka mipango madhubuti ya kuwawezesha wananchi
kiuchumi na matoke o ya utekelezaji yawe dhahiri ;
(d) Urasimishaji wa raslimali za wanyonge na h asa upimaji wa ardhi
na utoaji H atimiliki za Kimila kwa kuwek a mfumo madhubuti wa
kitaasisi, kifedha na kisheria.
(e) Kuongeza wigo wa kukusanya mapato ya ndani yatayotosheleza
Bajeti ya Serikali zetu kwa lengo la kuendelea kupunguza
utegemezi wa misaada ya kibajeti kutoka mataifa ya nje ;
(f) Kuongeza uwekezaji katika kukuza Sekta ya Sayansi na
Teknolojia ambayo ndiyo muhimili wa kuendesha uchumi wa
kisasa wenye tija ;
(g) Kuboresha miundombinu ya Barabara, Reli, Bandari, Nishati,
Vyombo vya Majini na Usafiri wa A nga;
(h) Kuimarisha huduma za kijamii, hasa Elimu, Maji na A fya;
(i) Kuimarisha usimamizi katika S ekta zinazokuwa kwa haraka kama
Utalii, Madini, Mawasiliano, H uduma ya Fedha na Biashara ; na
(j) Kuviimarisha V yombo vya Ulinzi na Usalama, Vyombo vya Kutoa
Haki, na Vyombo vya Udhibiti na N idhamu.
Kusimamia Utekelezaji wa Ilani
177. Wajibu wa CCM hauishii katika kutoa ahadi kwa wananchi kupitia Ilani
ya Uchaguzi na kuzikabidhi Serikali zake kwa utekelezaji, bali pia ina
wajibu mkubwa wa kufuatilia utekelezaji wa ahadi hizo. Hivyo, ni
muhimu kwa CCM kuzingatia utaratibu iliyojiwekea wa namna ya
kusimamia na kukagua utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi.
178. Tukirejea uzoefu wa mia ka ya nyuma, jukumu hili la CCM kusimamia
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi katika ngazi mbalimbali kuanzia Vijijini
211
hadi Taifa, limetekelezwa kwa kiwango cha wastani, hasa katika ngazi
ya Vijiji, Kata na Majimbo.
179. Kwa utaratibu wa sasa, ufuatiliaji wa ute kelezaji wa Ilani ya Uchaguzi
katika ngazi ya Taifa unafanywa na Wabunge na Wawakilishi kupitia
Kamati zao za Kudumu na pia kwa Wabunge na Wawakilishi kuwauliza
maswali mawaziri ndani ya Bunge na Baraza la Wawakilishi. Wabunge
na Wawakilishi wanaotokana n a CCM wanatakiwa kutoa taarifa za
utekelezaji wa Ilani katika vikao vya CCM, yaani kwenye vikao vya
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kupitia Wenyeviti na Makatibu wa
Kamati za Wabunge na Wawakilishi wote wa CCM. Utaratibu huu
unatekelezwa kwa kiwango cha kur idhisha.
180. Vikao vya Halmashauri Kuu za Wilaya, Kata, Wadi, Jimbo, na Matawi
vinapaswa kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi katika maeneo
hayo kupitia taarifa kutoka kwa Wabunge na Wawakilishi wa majimbo
husika, na pia kutoka kwa Madiwani kwa upande wa ngazi ya Kata,
Wadi, Jimbo na Matawi. Katika ngazi za Kata na Matawi, utekelezaji wa
utaratibu huu ni wa wastani.
181. Katika kipindi cha Ilani hii (2015 -2020), utaratibu wa vikao vya CCM
kupokea taarifa za utekelezaji wa Ilani kutoka kwa wahusika
utazing atiwa kwa ukamilifu. Utaratibu huu utakiwezesha Chama Cha
Mapinduzi kufanya tathmini ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi katika
ngazi mbali mbali kila baada ya miezi mitatu kwa mujibu wa vikao vya
kikatiba vya CCM.
182. Njia nyingine ya kufuatilia utekelezaji wa ahadi za Ilani ya Uchaguzi
unaotekelezwa na Serikali zake, ni kwa viongozi wa CCM kutembelea
miradi inayotekelezwa katika maeneo yao ili kujiridhisha juu ya
maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo. Utaratibu huu wa viong ozi wa
CCM wa Matawi, Kata, Wadi na Majimbo ambako miradi mingi ndiko
iliko, utekelezaji wake bado upo chini.
212
183. Katika kipindi cha utekelezaji wa ahadi zilizomo katika Ilani hii, viongozi
wa ngazi zote za CCM ni muhimu wajiwekee ratiba za kutembelea na
kukagua miradi inayotekelezwa katika maeneo yao. Endapo watakuta
utekelezaji unahitilafu, viongozi hao watoe taarifa haraka kwa viongozi
wa Serikali wa ngazi ya juu yao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana (kulia) akishiriki
katika shughuli za kilimo katika moja ya ziara za kuka gua Uhai wa
Chama na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi alizofanya katika Wilaya
zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano Mkuu
184. Kama ambavyo Serikali za CCM zinavyowajibik a kutekeleza maelekezo
yaliyomo katika Ilani ya U chaguzi ya Chama, vile vile CCM inawajibu wa
kutekeleza maelekezo yanayotolewa na Mikutano Mikuu. Mkutano Mkuu
213
wa CCM wa Taifa wa mwaka 2012 ulitoa maelekezo mengi
yanayotakiwa kuzingatiwa.
Kwa hiyo, kupitia Ilani hii, CCM ina jukumu la kutekeleza maeleke zo
yaliyotolewa na Mkutano Mkuu wa Taifa mwaka 2012. Utekelezaji
makini wa maelekezo hayo utakipatia Chama Cha Mapinduzi uhai na
nguvu thabiti ya kuzisimamia Serikali zake ili zitekeleze kwa ufanisi Ilani
hii. Tukumbuke kaulimbiu isemayo ; “Chama madhubut i huzaa
Serikali madhubuti” ; na “Chama legelege huzaa Serikali
legelege” (…Mwongozo wa CCM wa 1981).
Maazimio ya Mkutano Mkuu wa Nane
185. Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM wa Taifa uliofanyika mjini Dodoma
tarehe 11 -13 Novemba , mwaka 2012 ulipitisha maazimio me ngi yenye
umuhimu mkubwa katika kudumisha uhai wa Chama chetu i li kiendelee
kuwa na nguvu na uhalali wa kushika dola. Baadhi ya maazimio hayo ni
kama ifuatavyo: –
(a) Kudumisha Muungano
Mkutano Mkuu wa Taifa ulielekeza kuwa hatua ziendelee
kuchukuliwa za kuuenz i na kuuimarisha Muungano wetu wa
kihisitoria wa Tanganyika na Zanzibar wenye muundo wa Serikali
mbili. Aidha, changamoto za Muungano huu zitafutiwe majawabu
kila zinapojitokeza ili kuimarisha, kudumisha na kuendeleza
udugu, umoja na mshikamano uliopo bai na ya pande mbili za
Muungano.
Katika kutelekeza azimio hili, CCM imeridhishwa na hatua
zilizochukuliwa na Serikali zote mbili katika kusim amia mchakato
wa kupata Katiba I nayopendekezwa na ambayo hatimaye
itazaa Katiba mpya ya nchi yetu.
Aidha, Chama Cha Mapinduzi ki naamini kwamba ndani ya Katiba
Inayopendekezwa, kero nyingi za Muungano zimepatiwa
214
majawabu ya kuridhisha. Hivyo, iwapo Katiba Inayopendekezwa
itapitishwa hapana shaka itaimarisha Muungano wetu.
(b) Uimarishaji wa Chama
Mkutano Mkuu wa Taifa ulielekeza kwamba jitihada ziendelezwe
za kujenga na kuimarisha Chama Cha Mapinduzi, na kwamba
Viongozi wa Chama wa ngazi zote waongeze jiti hada za kuwa
karibu na wananchi na kuwasemea na kuwatetea. Aidha ,
mikutano baina ya Viongozi wa Chama na wananchi ya kufafanua
na kueleza mambo mbali mbali ifanyike mara kwa mara.
Kwa hiyo, katika kipindi hiki viongozi wa ngazi zote wanawajibika
kufanya ziara za mara kwa mara katika ngazi zote ili kukutana na
wananchi, kusikiliza matatizo yao na kuyatafutia majawabu.
(c) Maadili na Miiko ya Uongozi
Mkutano Mkuu wa Taifa ulikemea tabia ya baadhi ya viongozi wa
umma wanaotumia nafasi zao kuji limbikizia mali isivyo halali hali
inayosababisha madhara makubwa ya kimaadili na kiuongozi
katika nchi yetu. Mkutano Mkuu uliiagiz a Serikali kuchukua hatua
za kuondoa migongano ya kimaslahi inayojitokeza, kwa
kusimamia kwa ukamilifu Sheria ya Miiko ya Uongozi. Pia
iharakishe hatua ya k utunga sheria itakayotenganisha mtu kuwa
kiongozi wa umma na mf anyabiashara kwa wakati mmoja. Lengo
ni kurejesha dhamira ya kuwa na viongozi wanaoutumikia
umma kwa maslahi ya umma na si viongozi wanaotumia ofisi
za umma kwa maslahi yao binafsi.
Kwa hiyo, katika kipindi hiki, Chama Cha Mapinduzi kitazitaka
Serikali zake kutekeleza maagizo hayo ya Chama k uhusu
kuimarisha utekelezaji wa Sheria ya Miiko ya Uongozi na kutunga
sheria mpya itakayotenganisha mtu kuwa kiongozi wa umma na
mfanyabiashara kwa wakati mmoja. Aidha, katika kipindi hiki,
Chama Cha Mapinduzi kitaendeleza utaratibu wa kuwafuatilia na
215
kuwachukulia hatua viongozi wake wanaokiuka maadili ya
uongozi.
(d) Mapambano dhidi ya Rushwa
Mkutano Mkuu wa Taifa ulilaani tabia ya baadhi ya wagombea wa
uongozi kutoa rushwa nyakati za uchaguzi, na uliagiza
Halmashauri Kuu ya Taifa kuchukua hatua kali dhidi y a
watakaothibitika kujihusisha na tabia hii. Kwa hivyo, Chama Cha
Mapinduzi kinaziagiza Kamati za Usalama na Maadili na Kamati za
Siasa za kila ngazi kuwafuatilia kwa karibu wagombea uongozi
katika maeneo yao ili watakaobainika kutoa rushwa wachukuliwe
hatua kwa mujibu wa Kanuni za Chama na Sheria za nchi.
Kukua kwa tofauti kubwa ya kimapato katika Jamii
186. Mkutano Mkuu wa Taifa ulibainisha tatizo na hatari ya kukua kwa kasi
pengo la mapato baina ya walionacho na wasio nacho, na kwamba
Serikali zote mbili z iliagizwa kuchukua hatua za kurekebisha hali hii
mapema kwani ikiachwa iendelee itajenga chuki na uhasama baina ya
matabaka haya mawili na kuathiri amani, utulivu na umoja wa Taifa
letu.
Kwa hiyo, Chama Cha Mapinduzi kitazielekeza Serikali zake kuchukua
hatua thabiti zenye lengo la kupunguza pengo l a mapato kwa kutumia
njia mbali mbali kama kuziba mianya ya wanaokwepa kulipa kodi,
kuimarisha utaratibu wa Bima ya Afya ili iwafikie wananchi walio wengi
na hasa wanyonge, kuongeza ajira, kuwapunguzia wananchi m zigo wa
ada mbalimbali na hasa wa kipato cha chini.
Chama Kujitegemea Kimapato
187. Uendeshaji wa shughuli za Chama hutumia gharama kubwa , hivyo moja
ya vigezo vya uimara wa Chama ni kuwa na vyanzo vya mapato
vinavyotosheleza mahitaji.
216
Kwa kuzingatia ukwel i huu, katika kipindi hiki, Chama Cha Mapinduzi
kinawaagiza viongozi katika ngazi zote wabuni miradi itakayokiingizia
Chama mapato kwa ajili ya kugharamia shughuli za uendeshaji.
Aidha, Chama Cha Mapinduzi kinasisitiza suala la ubunifu wa miradi ya
kukiingizia Chama mapato; kwani zipo fursa nyingi za uanzishaji miradi
na kinachohitajika ni ubunifu na uthubutu kwa kila ngazi. Kwa mfano,
mikoa, wilaya, kata na matawi wanayo majengo na viwanja vyenye
Hatimiliki ambazo zinaweza kutumika kama dhamana ya kupata mitaji
kutoka benki ili kuanzisha miradi.
Mafunzo kwa Makada na Viongozi wa Chama
188. Mafunzo kwa makada na viongozi wa Chama ni nyenzo muhimu katika
ujenzi wa Chama na njia sahihi ya kuandaa viongozi bora. Hivyo , katika
kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii, CCM kwa kushirikiana na vyama vya
kidugu itaongeza kasi ya ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Makada cha
Ihemi (Iringa ) na kuanzisha ujenzi wa Chuo cha Tunguu (Unguja ) kwa
lengo la kutekeleza azma hiyo.
Jukumu la CCM
189. CCM ina jukumu la kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa Ilani hii kwa
kupata taarifa za kila baada ya miezi mitatu, na pia kwa viongozi
kufanya ziara za kutembelea miradi inayotekelezwa katika maeneo yao.
Ili Chama Cha Mapinduzi kiendelee kuku balika na kuaminiwa na
wananchi ni muhimu v iongozi wake wawe karibu na wananchi kwa
kuwatembelea, kusikiliza kero zao na kuzitafutia majawabu. Ni muhimu
kabisa Chama Cha Mapinduzi kuendelea kuwa msemaji na mte tezi mkuu
wa mwananchi na hasa wanyonge kwan i kwa asili yake, CCM ni Chama
Cha Wakulima na Wafanyakazi.
217
Ndugu John Pombe Magufuli akiwa na Mgombea
Mweza wakiwa katika ziara ya kujitambulisha kwa
wanachama mara baada ya kuchaguliwa na
Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kuwa Mgombea wa
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Copyright Notice
© Licențiada.org respectă drepturile de proprietate intelectuală și așteaptă ca toți utilizatorii să facă același lucru. Dacă consideri că un conținut de pe site încalcă drepturile tale de autor, te rugăm să trimiți o notificare DMCA.
Acest articol: Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiwatambulisha [600807] (ID: 600807)
Dacă considerați că acest conținut vă încalcă drepturile de autor, vă rugăm să depuneți o cerere pe pagina noastră Copyright Takedown.
